Tumuweke Membe kiporo

Tumuweke Membe kiporo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,472
Reaction score
872,175
Kwa sasa agenda kuu ni kushinda uchaguzi mkuu ili tukipumzishe chama chawala...Benard Membe asiwe agenda kwasasa ...haitatupa manufaa yoyote.

Membe ana historia yake na heshima yake ndani ya ccm na Tanzania kwa ujumla...maisha na historia yake yote ni ndani ya ccm na serikali ya ccm...hajawahi kuwa mpinzani nje ya ccm...labda mpinzani ndani ya ccm kama wengine wote.

Membe hakuwa tayari kutoka ccm bali alifukuzwa...Membe hakugombana na ccm bali na mtu mmoja....Ujio wake kwenye mageuzi ulikuwa ni uamuzi wa haraka kwa ajili ya kugombea urais wa Tanganyika kulipa kisasi cha aliyemfukuza chamani
ACT ni chama kichanga bado kinakuwa ..ujio wa Membe pale ni njia Ile ile waliyopita CHADEMA 2015 kwa Lowassa...Nafasi yenye hadhi ndani ya ACT kwa Membe ni ya mgombea urais.

Projection iko wazi huku Tanganyika kuwa Membe hawezi kuwa rais wa awamu ya sita kupitia ACT...Je ninini hatima yake baada ya uchaguzi? Mvurugano mkubwa sana unakuja...yaliyotokea NCCR 1995 pale Tanga yanaweza kutokea kwa ACT Tanganyika

Agenda ya Maalim Seif iko wazi..kushinda urais wa Zanzibar kupitia ACT ..huyu ni mpinzani tangu enzi na enzi...ana historia iliyotukuka huko...kwahiyo kutoka kwake CUF na kuingia ACT ni kama kutoka chumba hiki na kuingia chumba kile kwenye nyumba hiyohiyo

Zitto bado anajijenga...bado ana ndoto za kuja kuwa rais wa Tanganyika...ni kwenye mchakato huu wa kujijenga anatumia kila malighafi inayofaa kumjenga...ujio wa Membe ACT ulichagiza hamasa mpya iliyoletwa na maalim... Tofauti za kimaono kati ya Membe na Zitto ni ushindani serious wa nafasi ya urais.

Membe hapaswi kulaumiwa bado ni mchanga sana na mgeni kabisa kwenye siasa za upinzani...CHADEMA iliona mbali kumkataa kwakuwa tayari ilishapata uzoefu huko nyuma...Membe ni kama mwana mkiwa ndani ya ACT..Hata kama halisemwi popote lakini unaona wazi kuna kundi la Membe na watu wake halafu kuna kundi la Zitto na watu wake.

ACT kwasasa isihangaike na Membe bado ni mgeni na bado ana taharuki ya kilichomkuta ccm...inawezekana kabisa ana kundi kubwa nyuma yake lakini walau angeondoa kigugumizi cha kutamka kama walivyotamka wenzake chamani kumuunga mkono mgombea wa CHADEMA.

Neno NAMUUNGA MKONO LISSU kwenye nafasi ya urais...Membe ameshindwa kabisa kulitamka...Tuko hatua ya lala salama kuelekea uchaguzi wa kihistoria tuweke nguvu zetu huko...lakini kuna baadhi yetu ndani ya ACT vifua vimejaa vinakaribia kupasuka...TUWAWEKE KIPORO!
 
Tuliwaonya ACT kuwa these CCM defectors kwa vile wamekosa maslahi yao na si kwa vile CCM haitendi haki, wasipokelewe. Ona sas anavyoleta sintofahamu!
Wanahama CCM kwa vile wamekosa matarajio yao na si kwa vile wamekerwa na dhuluma ndani ya CCM!
 
Tuliwaonya ACT kuwa these CCM defectors kwa vile wamekosa maslahi yao na si kwa vile CCM haitendi haki, wasipokelewe. Ona sas anavyoleta sintofahamu!
Wanahama CCM kwa vile wamekosa matarajio yao na si kwa vile wamekerwa na dhuluma ndani ya CCM!
Sahihi kabisa
 
Nikiona mtu wa Chadema anajifanya kushtuka kuhusu Lowasa au Membe wakati huu namuona mpumbavu tu,!

Kwa sababu suala la Lowasa watu walionywa wakaziba masikio.
Suala la Membe, hili ndio kituko na upumbavu mwingie wa upinzani nchi hii maana tulionya tukaitwa sie buku saba tunyamaze Membe anaenda kumuangusha jiwe na ccm.

Ni upumbavu kujifanya eti ndio unashtuka kuhusu Membe wakati huu wakati hadi wana ccm wenyewe waliwaonya.
 
Membe ni takataka kama zingine ndani ya CCM
Baada ya huu uchaguzi ataunda chama kitakachokuwa chama kikuu cha upinzani most likely anaweza kukimegua ACT bara kama atakosa nafasi kwenye baraza jipya la mawaziri
 
Viongozi wengi wa Upinzani kuna kitu ambacho karibia wote wanachangia nacho ni low IQ, ukisikia wanavyofanya chokochoko utafikiri wamejipanga kweli kweli, kumbe hamna kitu, Membe ni kama tundu tu hakuna kitu, wote siyo intelligent men, sasa Zito Kabwe na yeye kwa akili yake anaamini kabisa kwamba 2025 chadema itampendekeza kugombea Uraisi kama yeye alivyofanya kwa tundu? Kwa akili yake ni kwamba ana deni na chadema?
 
Back
Top Bottom