Tumuweke Membe kiporo

Tumuweke Membe kiporo

JamiiForums-1078331197.jpg
 
Mshana turudi kwenye mastori yetu yale, uchaguzi umeisha.
Sasa nataka uje na topic ya levels za uchawi na nguvu zake. Pia ukiweza elezea kwa nini wachawi hawawezi kuiba bank.

Unitag kabisa.
 
Mshana Jr , kitu kilicho wazi ni kuwa CDM inashinda, sasa je Kaijage atamtangaza? Lisu aandae mapema what to do in that situation. Kuingia barabaran watanzania sidhani, tu waoga!

JF huwa Kuna watu wanaota mpaka unashangaa na kuwaombea waendelee kuota. Tuache mambo ya vyama mana Hata mie sio mpenzi wa Siasa za vyama Bali nampenda JPM kwa uthubutu Wake. Hivi huyo LISSU atashinda kwa Kura za kina Nani. Embu jikusanyeni kwa Siri mjihesabu.
 
Kwa sasa agenda kuu ni kushinda uchaguzi mkuu ili tukipumzishe chama chawala...Benard Membe asiwe agenda kwasasa ...haitatupa manufaa yoyote.

Membe ana historia yake na heshima yake ndani ya ccm na Tanzania kwa ujumla...maisha na historia yake yote ni ndani ya ccm na serikali ya ccm...hajawahi kuwa mpinzani nje ya ccm...labda mpinzani ndani ya ccm kama wengine wote.

Membe hakuwa tayari kutoka ccm bali alifukuzwa...Membe hakugombana na ccm bali na mtu mmoja....Ujio wake kwenye mageuzi ulikuwa ni uamuzi wa haraka kwa ajili ya kugombea urais wa Tanganyika kulipa kisasi cha aliyemfukuza chamani
ACT ni chama kichanga bado kinakuwa ..ujio wa Membe pale ni njia Ile ile waliyopita CHADEMA 2015 kwa Lowassa...Nafasi yenye hadhi ndani ya ACT kwa Membe ni ya mgombea urais.

Projection iko wazi huku Tanganyika kuwa Membe hawezi kuwa rais wa awamu ya sita kupitia ACT...Je ninini hatima yake baada ya uchaguzi? Mvurugano mkubwa sana unakuja...yaliyotokea NCCR 1995 pale Tanga yanaweza kutokea kwa ACT Tanganyika

Agenda ya Maalim Seif iko wazi..kushinda urais wa Zanzibar kupitia ACT ..huyu ni mpinzani tangu enzi na enzi...ana historia iliyotukuka huko...kwahiyo kutoka kwake CUF na kuingia ACT ni kama kutoka chumba hiki na kuingia chumba kile kwenye nyumba hiyohiyo

Zitto bado anajijenga...bado ana ndoto za kuja kuwa rais wa Tanganyika...ni kwenye mchakato huu wa kujijenga anatumia kila malighafi inayofaa kumjenga...ujio wa Membe ACT ulichagiza hamasa mpya iliyoletwa na maalim... Tofauti za kimaono kati ya Membe na Zitto ni ushindani serious wa nafasi ya urais.

Membe hapaswi kulaumiwa bado ni mchanga sana na mgeni kabisa kwenye siasa za upinzani...CHADEMA iliona mbali kumkataa kwakuwa tayari ilishapata uzoefu huko nyuma...Membe ni kama mwana mkiwa ndani ya ACT..Hata kama halisemwi popote lakini unaona wazi kuna kundi la Membe na watu wake halafu kuna kundi la Zitto na watu wake.

ACT kwasasa isihangaike na Membe bado ni mgeni na bado ana taharuki ya kilichomkuta ccm...inawezekana kabisa ana kundi kubwa nyuma yake lakini walau angeondoa kigugumizi cha kutamka kama walivyotamka wenzake chamani kumuunga mkono mgombea wa CHADEMA.

Neno NAMUUNGA MKONO LISSU kwenye nafasi ya urais...Membe ameshindwa kabisa kulitamka...Tuko hatua ya lala salama kuelekea uchaguzi wa kihistoria tuweke nguvu zetu huko...lakini kuna baadhi yetu ndani ya ACT vifua vimejaa vinakaribia kupasuka...TUWAWEKE KIPORO!
Haya kajiungeni muwe kiporo dabodabo maana wote mmeshakua viporo
 
Back
Top Bottom