Tumshukuru MUNGU kwa haya

Tumshukuru MUNGU kwa haya

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2010
Posts
15,145
Reaction score
5,574
Nimetafakari haya maisha nikagundua kuna ulazima wa kumshukuru MUNGU. Mwaka huu pekee 2013 watu wengi sana tunaowafahamu na tusiowafahamu wamepoteza maisha kwa sababu mbalimbali. Kuna watu wengi mahospitalini na majumbani ni wagonjwa mahututi wengine ni ndugu zetu, marafiki na hata tusiowajua. MWANA MMU MWENZANGU PITA HAPA USEME ASANTE MUNGU KWA WEMA WAKO NA KUMUOMBA REHEMA ZAIDI.
 
huwezi kuwa serious, yaani tumshukuru mungu kwenye thread! Eiyer tuonane jioni kwa ajili ya ibada ya shukrani.
 
Last edited by a moderator:
Thank You GOD for all Your blessings for me and my family. T
Thank You for fulfilling my needs and desires in expected and unexpected ways.
I am grateful
Ameni, hakika anastahili kushukuriwa bila kujali dini au dhehebu
 
Ee mwenyezi MUNGU yote tunayaweka mikononi mwako,maana bila wewe sisi si kitu
 
huwezi kuwa serious, yaani tumshukuru mungu kwenye thread! Eiyer tuonane jioni kwa ajili ya ibada ya shukrani.

Binafsi nafikiri kumshukuru Mungu ni popote, hata barabarani, nyumbani, kazini, vitani nk ili mradi tu shukrani zako na maombi yako yawe yanatoka ndani ya moyo wako na hufanyi hivyo ili kuwaonyesha watu kuwa wewe ni mtu wa Mungu.

Kwa kweli mimi nina mengi sana ya Kumshukuru Mungu na namuomba sasa apokee shukran zangu kwa yote aliyonitendea mpaka leo. Namshukuru sana.
 
Ni kweli Mokoyo
Ni jambo jema kumshukuru Mungu kwa mema mengi aliyotutendea na kutupa kibali chake kuiona siku njema ya leo
Wenzetu wengi tumeachana nao katika maisha haya wengine ni wagonjwa mahospitalini kwa muda mrefu na wengine walipata ajali ambazo zilichukua baadhi ya viungo vyao ila shukrani kwake kwa ulinzi wake na kutuwezesha kuiona siku hii na kufikia muda kama huu
asante sana Mwenyezi Mungu kwa wema wako na baraka zako kwangu na kwa familia yangu na namuomba azidi kutupa ulinzi wake kwangu na kwa familia yangu.
 
Last edited by a moderator:
Mahali popote pale Mungu ashukuriwe....

Mkienda kwenye ibada mtuombee......hivi hamna huduma ya kutuma sadaka kwa tigo pesa na Mpesa?

unataka kutuma sadaka nikupe namba ya baba paroko Eiyer? lol
 
Last edited by a moderator:
Mahali popote pale Mungu ashukuriwe....

Mkienda kwenye ibada mtuombee......hivi hamna huduma ya kutuma sadaka kwa tigo pesa na Mpesa?

Tumegongana mawazo, Shukran ni popote, si lazima kwenye majumba ya ibada!

Nimefikiria kipuuzi, hiyo ya kutuma sadaka kwa njia ya tigo pesa au mpesa, mwisho wa siku sister, utaishia kufuatilia ibada kwa njia ya twitter, facebook, youtube nk na interest ya kwenda kuungana kwenye majamba ya ibada na wenzako ili kutengeneza umoja katika imani moja itaisha kabisa!
 
Mkuu Mokoyo nadhani ni jambo jema kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
 
Last edited by a moderator:
Ee Mwenyezi Mungu, wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, Mwenye mamlaka ya kila kitu dunia na mbinguni, Mungu Uliyetuumba sisi wanadamu, sisi ni watu wako Nawe ni Mungu wetu.
Mungu wetu Utuhurumie sisi wakuchao'
"Unastahili kuaabudiwa..."
 
Asante Bwana Yesu kwa Damu yako Takatifu yenye Thamani ....Damu Yako Ee Yesu... Imenitendea Mambo Makuu.
I Praise Your Name Jesus...
Thank You LORD!...
 
Back
Top Bottom