Tumshukuru MUNGU kwa haya

Tumshukuru MUNGU kwa haya

Niweke wazi mimi ni muumini.
Lakini desturi ya kusema mabaya yanayowafika watu eg wangapi wamekufa, hawana chakula, wamepata ajali na kupoteza viungo, wako hoi hospitali nk kisha kukumbusha watu kumshukuru Mungu kwasababu yeye sio miongoni mwao siielewi/siipendi. Na wengine hata katikati ya maombi wanataja hayo Baba kuna wengine wamefikwa na hiki na kile lakn mimi umeniepusha nashukuru...whaaat?
Hivi tunajua tunaposema hayo inaeza kua tupo kati ya kijana aliyepoteza wazazi wake recently yuko devastated anatafuta faraja katika uwepo wa Mungu au mtu aliyefikwa na baya lolote jingine? tunampa ujumbe gani mtu huyo? Ni Mungu aliacha kumuangalia yeye ndio maana akafikwa na hayo?
Kifupi nachotaka kusema ni kweli tunapaswa kumshukuru Mungu kwa mengi anayotutendea lakini bila kuhusisha na madhila yanayowapata wengine lakini sisi tukaepushwa nayo
Mkuu umewaza vyema ndugu
 
Back
Top Bottom