Nimejaribu kufuatilia mijadala mbali mbali humu ndani, nimejiuliza swali hilo hapo juu. Je, Chadema itakufa Zitto akifukuzwa uanachama? Katika mijadala mingi ukiisoma unaona kwamba kuna mgongano tu wa mawazo kwa vyama hivi viwili vinavyokimbizana kwenye siasa zetu hapa nchini, CHADEMA na CCM. Wale wa CCM mijadala yao yote inamtetea ZITTO na kumuona kwamba bila Zitto hakuna CDM. Wale wa CHADEMA bado wana msimamo wao wa kwamba Zitto ni msaliti katika chama.
Hebu sasa tuache bias zote za vyama hivi viwili, hebu tuingie akilini sasa tujiulize kwa fikra pevu, ni kweli bila Zitto Chadema haipo?
Watu wameegemea kwenye misafara ya viongozi wawili walioenda Kigoma, Dr. Slaa na Zitto, lakini tukumbuke kwamba mmoja hajaitembelea Kigoma, ni mwenyeji wa Kigoma, ni mbunge kutoka Kigoma. Dr. Slaa alipata mapokezi makubwa, Zitto amepata mapokezi makubwa, nani anakubalika zaidi? Mgeni au mwenyeji?
Kwangu mimi ili nione kwamba CDM ni Zitto, aende Mwanza, Arusha, Moshi, Dar, Mbeya, Iringa nk. apate mapokezi makubwa hivi.