Tumshauri Zitto...

Tumshauri Zitto...

Status
Not open for further replies.
kamshauri mbowe...ondokeni tu zzk ni kipenzi cha waTZ

Kuwa kipenzi cha watu ni vizuri ukatumia nafasi hiyo vizuri lakini kunaweza kukuponza kama kutakuondolea busara. Mamba siku zote nguvu zake ziko majini.
 
rubbish...this is childish,i didnt knw kumbe wazee wa buku 7 wapo kote kote
 
Namshauri Zito aanzishe chama na hao wafuasi wake na yeye atakua bora kuliko chama hicho....
 
Zitto anajiharibia mwenyewe, huwezi kupokelewa kwa mabango yanayokashifu viongozi wako na chama chako huku ukiangalia tu, zitto hana mapenzi ya dhati na chama, labda ni unafiki tu, mdomoni anajifanya ni mwanachama mtiifu huku akiongoza na kuhutubia mikutano inayodhalilisha viongozi na chama chake, chadema kuweni makini sana na watu kama hawa!

Hata mimi nimeshangaa sana. Ndio maana nasema huyu dogo kategeshewa kingi kaingia mwenyewe mzimamzima hadi makalio. Wallahi kwa ushahidi ule kazi imekuwa nyepesi kuliko maelezo. LB7 njooni hapa mumtetee mwenzenu.
 
Hata mimi nimeshangaa sana. Ndio maana nasema huyu dogo kategeshewa kingi kaingia mwenyewe mzimamzima hadi makalio. Wallahi kwa ushahidi ule kazi imekuwa nyepesi kuliko maelezo. LB7 njooni hapa mumtetee mwenzenu.

Mkuu ndo maana nimesema Dogo Zito kajinyonga mwenyewe huku akijona. Kwa maneno mengine kajikaanga kwa mafuta yake.
 
Anajua kuwa political career yake iko mashakani, anajua amechafua sana, anajua kuwa sababu za kumvuruga na uwezo upo! Ndiyo maana speech yake inaomba huruma ya kuvumiliwa! sasa hivi ni mdogo kama piriton, ukimkunja anaingia kwenye chupa ya soda...dhambi ya usaliti na dhamira vina msuta sana...
 
Nimejaribu kufuatilia mijadala mbali mbali humu ndani, nimejiuliza swali hilo hapo juu. Je, Chadema itakufa Zitto akifukuzwa uanachama? Katika mijadala mingi ukiisoma unaona kwamba kuna mgongano tu wa mawazo kwa vyama hivi viwili vinavyokimbizana kwenye siasa zetu hapa nchini, CHADEMA na CCM. Wale wa CCM mijadala yao yote inamtetea ZITTO na kumuona kwamba bila Zitto hakuna CDM. Wale wa CHADEMA bado wana msimamo wao wa kwamba Zitto ni msaliti katika chama.

Hebu sasa tuache bias zote za vyama hivi viwili, hebu tuingie akilini sasa tujiulize kwa fikra pevu, ni kweli bila Zitto Chadema haipo?

Watu wameegemea kwenye misafara ya viongozi wawili walioenda Kigoma, Dr. Slaa na Zitto, lakini tukumbuke kwamba mmoja hajaitembelea Kigoma, ni mwenyeji wa Kigoma, ni mbunge kutoka Kigoma. Dr. Slaa alipata mapokezi makubwa, Zitto amepata mapokezi makubwa, nani anakubalika zaidi? Mgeni au mwenyeji?

Kwangu mimi ili nione kwamba CDM ni Zitto, aende Mwanza, Arusha, Moshi, Dar, Mbeya, Iringa nk. apate mapokezi makubwa hivi.
 
kwasababu humjui zitto ndiyo maana unaongea haya lakini wakati utatuambia tu.
 
Zito anachofanya sasa kule kigoma sidhani kama kitamsaidia in long term .. angekuwa amefanya jambo jema kukaa kimya huko akisubiria maamuzi ya cc.. kwa haraka haraka inaonekana ni mtu wa kupenda sana media attention... mwisho wa siku peak itafika na nawatu watamchoka na wataendelea na shughuli zao mwisho wake utakuwa umewadia... inaingia akilini tu kama kufafanya hivi kunalenga kuisaidia CCM kama watu wanavyo hisi na sio kujenga CDM.hadi hadi sasa Kitila anaonekana kuwa mwenye utimamu kuumpita Zito
 
Sasa ana haraka hadi kashindwa sema chuki zake kwa wachaga km gia ya kujilinda...kesho kwa haraka ataongelea uislam tena.Then atakuwa keshakuja around km kawaida yake.

Ana sema kuna baadhi ya wachaga..inamaana anasema kuna wachaga wengi...hao baadhi ni exceptional
 
ZZK si chochote si lolote nje ya CDM. Ndo maana hataki kukihama chama hiki anachokidharau.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom