Desire Dizaya
JF-Expert Member
- Feb 16, 2015
- 6,476
- 11,628
Hakuna kitu kisichofaa kama kuwa "mbogo" pale mwenzio anapokosea ama kukukosea. Tambua binadamu hajakamilika ila muumba pekee, kukosea ni sehemu ya maisha yetu, kuna kukosea kwa bahati mbaya na kuna makusudi.
Sasa naongelea unapokosewa, tumia hekima na busara katika kulitambua kosa ulotendewa sio kukurupuka tu kuhukumu.
Kuna baadhi ya watu wako very harsh wanapokosewa. Mke akiunguza chakula bahati mbaya unamwasha kofi au kachelewa kurudi nyumbani basi unatoa kipigo alikua kwa hawara wake, anajitetea humsikilizi.
Housegirl kapasua sahani bahati mbaya wala huulizi, unamparamia na makonde na unamkata mshahara kabisa, lakini hebu jiulize we hufanyi makosa?
Kosa alolifanya mwenzio hata we utakuta umewahi kulifanya. Je, response yako ilikuaje?
au sababu huyo alofanya kosa leo yupo chini yako we hukuwa chini ya mtu?
Ni rahisi "kuitazama" sura ya mwenzio lakini ni vigumu "kuuona" uso wako.
Ni rahisi "kuliona" kosa la mwenzio lakini ni vigumu "kulitambua" kosa lako
Ni rahisi kumuhukumu mwenzio na kuona mapungufu yake lakini ni vigumu kujikosoa mwenyewe na kutambua mapungufu yako..
Unapokosea. Hukumu kwa haki hekima na busara vikikuongoza. Sababu hata we pia una yako..jiulize "nnachomfanyia huyu mtu nikgekuwa mie nafanyiwa ningejiskiaje?
Siku njema!
Aggy