Tumia hekima na busara kwenye makosa ya wenzio

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
6,476
11,627
Hakuna kitu kisichofaa kama kuwa "mbogo" pale mwenzio anapokosea ama kukukosea. Tambua binadamu hajakamilika ila muumba pekee, kukosea ni sehemu ya maisha yetu, kuna kukosea kwa bahati mbaya na kuna makusudi.

Sasa naongelea unapokosewa, tumia hekima na busara katika kulitambua kosa ulotendewa sio kukurupuka tu kuhukumu.

Kuna baadhi ya watu wako very harsh wanapokosewa. Mke akiunguza chakula bahati mbaya unamwasha kofi au kachelewa kurudi nyumbani basi unatoa kipigo alikua kwa hawara wake, anajitetea humsikilizi.

Housegirl kapasua sahani bahati mbaya wala huulizi, unamparamia na makonde na unamkata mshahara kabisa, lakini hebu jiulize we hufanyi makosa?

Kosa alolifanya mwenzio hata we utakuta umewahi kulifanya. Je, response yako ilikuaje?
au sababu huyo alofanya kosa leo yupo chini yako we hukuwa chini ya mtu?

Ni rahisi "kuitazama" sura ya mwenzio lakini ni vigumu "kuuona" uso wako.
Ni rahisi "kuliona" kosa la mwenzio lakini ni vigumu "kulitambua" kosa lako
Ni rahisi kumuhukumu mwenzio na kuona mapungufu yake lakini ni vigumu kujikosoa mwenyewe na kutambua mapungufu yako..

Unapokosea. Hukumu kwa haki hekima na busara vikikuongoza. Sababu hata we pia una yako..jiulize "nnachomfanyia huyu mtu nikgekuwa mie nafanyiwa ningejiskiaje?

Siku njema!

Aggy
 
Tatizo la baadhi ya wanawake ni kwamba wanapokuwa wamekosea hawapo tayari kukiri kosa na kuwa wapole! Na hii hupelekea kukutana na wakati mgumu ikiwa ni pamoja na kuchezea kichapo kidogo ili mambo yakwende sambamba!
 
Tatizo la baadhi ya wanawake ni kwamba wanapokuwa wamekosea hawapo tayari kukiri kosa na kuwa wapole! Na hii hupelekea kukutana na wakati mgumu ikiwa ni pamoja na kuchezea kichapo kidogo ili mambo yakwende sambamba!
ila kuna wengine wakp humble

kwahyo dawa ya kutuliza huo mdomo ni mkong'oto?
 
Ujumbe mzuri sana my dada. Ila kiukweli haka kaugonjwa kwa asilimia kubwa kapo sana kwetu wanawake ni wachache wenye kufanya maamuzi baada ya kufikiria kwanza, tulio wengi huwa tunafanya maamuzi papo kwa hapo na hiyo inasababisha saa nyingine tuwe ni wenye kujuta na hata kupoteza vitu ambavyo vilikuwa na msaada mkubwa kutokana na maamuzi ya pasi kufikiria mara mbili.

Cha muhimu tuwe na tabia yakufikiria kabla ya kufanya maamuzi nadhani huenda ikawa ndio suluhu ya yote hayo najua ni ngumu ila tujitahidi kwa kweli.
 
Ujumbe mzuri sana my dada. Ila kiukweli haka kaugonjwa kwa asilimia kubwa kapo sana kwetu wanawake ni wachache wenye kufanya maamuzi baada ya kufikiria kwanza, tulio wengi huwa tunafanya papo kwa hapo na hiyo inasababisha saa nyingine tuwe ni wenye kujuta na hata kupoteza vitu ambavyo vilikuwa na msaada mkubwa kutokana na maamuzi ya pasi kufikiria mara mbili.

Cha muhimu tuwe na tabia yakufikiria kabla ya kufanya maamuzi nadhani huenda ikawa ndio suluhu ya yote hayo najua ni ngumu ila tujitahidi kwa kweli.
asante kwa kiongezea emmy
tufikiri ksbla ya kutenda
 
asante kwa kiongezea emmy
tufikiri ksbla ya kutenda
Haswaaaa. Mie nina mifano hai kwa jirani yangu yeye akiwa na msichana wa kazi hamalizi mwezi yaani kama ulivyosema asiunguze maharage, asivunje chombo yaani inapotokea hivyo kwake ni kipigo na masimango juu. Hii imesababisha hadumu na wasichana hata kama unamuona anamwelekeo kiasi gani basi kwake akikaa sana miezi miwili sababu anavumilia hadi anaona cha kufia nini bora niondoke.

Saa nyingine najisemea angekuwa anawaza kwamba kuna bahati mbaya nadhani angedumu nao ila ndio hivyo tena.
 
Haswaaaa. Mie nina mifano hai nina jirani yangu yeye akiwa na msichana wa kazi hamalizi mwezi yaani kama ulivyosema asiunguze maharage, asivunje chombo yaani inapotokea hivyo kwake ni kipigo na masimango juu. Hii imesababisha hadumu na wasichana hata kama unamuona anamwelekeo kiasi gani basi kwake akikaa sana miezi miwili sababu anavumilia hadi anaona cha kufia nini bora niondoke.

Saa nyingine najisemea angekuwa anawaza kwamba kuna bahati mbaya nadhani angedumu nao ila ndio hivyo tena.
aisee..
 
Mimi huwa nina hekima na busara sana! ila akipitiwa na shetani sijui hizo hekima na busara zinaendaga wapi nakuwa km vampire..
 
Mm nimekuelewa zaid mtoa mada, ume gusa mambo mengi na watu wa kila aina hasa umemgusa huyu boss wng huku ambae jana alinikalipia na kunilima barua kwa sababu ya kutosimama nikiwa nimenyoka kama mti wkt wimbo wa taifa ukiimbwa, mm nilikua nawaza maisha yng huku mshahara uchwara umeisha kabla tar 15! Boss kichefu chefu
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom