Sakata la Bandari: Hekima na busara itatuvusha, historia ni Mwalimu mzuri, tujikumbushe haya

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Mwaka 2014 Tamko la Maaskofu Wakatoliki TEC,Tasisi ya Waadventist Wasabato na Baraza la Kikrito Tanzania lilisitisha Bunge la Katiba Mpya baada ya kuona CCM imepora mjadala na kutaka kufanya wanavyotaka wao huku wakipuuza maoni ya wananchi.

Rais Kikwete akatumia hekima na busara za Walaka ule akaachana na mchakato ule uliokuwa unaenda kinyume na Malengo.

"...... Sisi tunaona mchakato wa mabadiliko ya katiba unapokwa na wanaCCM wenye wabunge wengi huku Spika akitumia nguvu na ubabe kupitisha maoni binafsi nje ya yaliyotolewa na wananchi,. Pia tunaona vijembe na matusi vikiendelea bungeni na Serikali kufunga tovuti ya kamati ya kukusanya maoni ni dalili mbaya kuwa Serikali haina nia njema kwa Taifa la Tanzania....". Ilisema sehemu ya Waraka huo.

Rais Kikwete alitumia busara kuusitisha mchakato huo wa Katiba Mpya Mwaka 2014,tukumbuke nani alikuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo la kutafuta Katiba Mpya,ni Rais wa Sasa,Mh Samia Suluhu Hassan

Tukumbuke pia Rais Mwinyi alipotaka kuingiza Tanzania kwenye Jumuiya ya kiislamu na kutumia Sharia,Japo Mwalimu Nyerere alikuwepo lakini mgogoro huo wa OIC mwaka 1994 ulikuwa mkubwa ukamfanya Rais Mwinyi aamue kuachana nao kwani ulikuwa unaenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sasa hili la DPW akiachana nalo yeye sio wa kwanza kikubwa maslahi ya Taifa kwanza@Chawa@Kupe@Nyuki@Itikadi kali@Waliokula hela@Waandishi wa habari@Waliopitisha huo mkataba wa kimangungo.

Mwisho kabisa,nawakumbusha kuuzwa kwa Loliondo mwaka 1992,mgogoro wake ulifika Duniani hata leo ukigoogle Loliondo Gate itakuja,waandishi wa habari walikufa RIP Stan Katabalo,nikikumbuka habari hii ya Hayati Mrema namkumbuka pia Jenerali Imran Kombe (RIP) yeye alihusishwa kuungana na Hayati Augustine Lyatonga Mrema, lakini zaidi ya yote mgogoro huo ulimuinua na kumpa umaarufu Hayati Augustine Lyatonga Mrema ambapo kila alipoitisha mkutano alisukumwa kwenye gari yake,wananchi waliojaa kwenye malango ya kuingilia kila Mkoa kama pale msamvu Morogoro na Ubungo Dar es Salaam,Wananchi walimwambia zima gari Mzee,usimalize mafuta,tutakusukuma,

Wananchi walimbeba Mh Mrema,wakamkumbatia wakamrudisha tena kwenye gari wakamwambia kaa humo humo Mzee tutakusukuma hadi uwanja wa mkutano na mikutano yake ilivunja rekodi ya kujaza watu na kwa mara ya kwanza Ndugu Mrema aliujaza uwanja wa Jangwani peke bila nguvu ya CCM bila nguvu ya Serikali bila nguvu ya Mwalimu Nyerere na Mwalimu Mwalimu Nyerere kwa busara na hekima aliwaambia polisi wasimguse kabisa wamuache afanye mikutano yake,watu walienda kusikiliza Kashfa ya Loliondo na Kashfa ya Mkonge iliyomhusu Chavda,uwanjani alikuwa na staili yake kama anatangaza mpira, nawakumbusha ndugu zangu hili la bandari nalo linakwenda kuvunja rekodi nyingine kabisa ambayo haijawahi kuvunjwa na mtu yeyote.

Nimalizie kwa tafakuri jadidi,hivi ukipewa dola elfu mbili uuze nchi utakubali? Je ukipewa dinari 4,000,000 je ukipewa AED 2,000,000 je uko tayari kuuza ndugu zako kwa ujira wa thumuni? Je upo tayari kuitwa mzungu au mwarabu wakati wewe ni mweusi tii ilimradi tu uambatane nao utatoa vyako vyote,je heshima yako utaiweka wapi? Naamini hakuna Mtanzania wa kufanya haya yote, Watanzania tumelelewa vyema kwa malezi na makuzi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,sisi ni Wazalendo kwa Taifa letu,sisi ni Watanzania.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Hizo Masters na bachelors ulizoandika hapo chini ni kujaribu kutisha watu au kujiongezea kuheshimika kutoka kwa msomaji wa andiko lako?.

DPW anakwenda kuongeza pato la bandari kutoka trilioni 7 mpaka trilioni 18 kwa mwaka kama makusanyo ya TRA, hizo pesa zinakwenda kugusa sekta mbalimbali za Tanzania kuanzia afya mpaka michezo.

Pia DPW sio mwekezaji wa mwisho kuja kuwekeza katika bandari yetu yupo mwekezaji mwingine anayetegemewa kupewa mageti matatu hapo TPA, kwa hiyo tupunguze siasa kwenye masuala ya uchumi moja kwa moja.
 
Hizo Masters na bachelors ulizoandika hapo chini ni kujaribu kutisha watu au kujiongezea kuheshimika kutoka kwa msomaji wa andiko lako?.

DPW anakwenda kuongeza pato la bandari kutoka trilioni 7 mpaka trilioni 18 kwa mwaka kama makusanyo ya TRA, hizo pesa zinakwenda kugusa sekta mbalimbali za Tanzania kuanzia afya mpaka michezo.

Pia DPW sio mwekezaji wa mwisho kuja kuwekeza katika bandari yetu yupo mwekezaji mwingine anayetegemewa kupewa mageti matatu hapo TPA, kwa hiyo tupunguze siasa kwenye masuala ya uchumi moja kwa moja.
Watetezi wa DPW Wana lugha tamu sijapata ona.
Kweli rushwa hupofusha macho
 
Back
Top Bottom