Tumezidi ushamba

Pole nilikuwa nataka kueleza kuwa gadhabu za watu wa nchi moja huonesha kwa kuandamana katika ubalozi wao. Wanaija walifanya huko kwao kuonesha kusikitishwa na mauaji ya wanaija na sie vijana wapo Sawa maana ndege yao imeshikiriwa sauzi hivyo kuandamana mbele ya ubalozi wa sauzi ni kutoa ujumbe (voice of the voiceless). Una jengine?
Mkuu ule ulikuwa ni uhalifu, kwa hiyo ni sawa waandamane kulaani vitendo hivyo vya kihalifu. Hivi unafikiri wangekuwa ni watu waliokutwa na hatia na kustahili adhabu ya kifo hao wanaigeria wangeandamana?? Suala la ndege kukamatwa ni la kisheria, tunadaiwa na anayedai alishinda kesi ya madai dhidi ya serikali yetu. Sasa hao walioandamana wanataka serikali ya SA itengue uamuzi/hukumu ya mahakama!!. Nchi za wenzetu wanaheshimu utawala wa sheria.
 
KKunaweza kuwa na sababu mbalimbali zilizosababisha kushindwa kulipa deni kwa wakati,tuna madeni mengi tu kama nchi,si hilo tu la huyo mkulima wa kizungu, but kuzuia ndege sidhani kama ni sahihi,labda tu kama sheria za huko south zinaruhusu kukamata mali za mdaiwa,hii sio poa.
Hata hapa TZ sheria inaruhusu kukamatwa mali za mdaiwa. Umesahau yaliyompata Mbowe?
 
Mkuu ule ulikuwa ni uhalifu, kwa hiyo ni sawa waandamane kulaani vitendo hivyo vya kihalifu. Hivi unafikiri wangekuwa ni watu waliokutwa na hatia na kustahili adhabu ya kifo hao wanaigeria wangeandamana?? Suala la ndege kukamatwa ni la kisheria, tunadaiwa na anayedai alishinda kesi ya madai dhidi ya serikali yetu. Sasa hao walioandamana wanataka serikali ya SA itengue uamuzi/hukumu ya mahakama!!. Nchi za wenzetu wanaheshimu utawala wa sheria.

Hapa Tz katiba inaruhusu watu au vyama ya siasa kuandamana kupinga au kuishinikiza serikali jambo fulani, lakini ni nani anaweza leo kuandamana kwa mujibu wa katiba??!!, kinyume chake Watz wanaandamana kupinga hukumu ya Mahakama wakati jambo hilo ni lazima lipingwe kwa kufuata taratibu za ki-mahakama. Ni ujinga mkubwa wameuonyesha.
 
Naangalia kichwa cha thrd yako na maelezo uliyotoa, hakuna uhusiano. Ushamba una uhusiano gani na maandamano, na ununuzi wa ndege? Kwa maoni yangu walioandamana wanatuamusha tunaojidai kupiga kelele hapa JF bila kujulikana. Africa kusini haikustahili kabisa kukamata ndege ya TZ kwa kisingizio cha mahakama, wakati walishindwa kumkamata Al Bashir bila kujali amri ya mahakama. Ukishatazamia kufanya tukiola aina hiyo, tegemea matatizo ya kidiplomasia maana hiyo siyo ndege ya muuza gongo.

Tunaojidai kujua mbinu za kuendesha serikali, tuko bize mtandaoni kwa matusi na kuzomea, wakati wachuuzi wanajaribu hata kuandamana.
Hoja yako ya Al Bashiri na ndege yetu ina mambo mawili. Moja linafanana na jingine ni tofauti kabisa. Linalofanana ni hukumu ya mahakama, KUKAMATA. La pili ambalo linaleta tofauti hapo ni kwamba Al Bashiri ni Binadamu na ile ndege yetu ni Asset. Kesi ya Al Bashiri na ya Ndege yetu hazifanani. Moja ni kesi ya jinai na nyingine ni kesi ya madai.
 
Kwa kweli sisi tumezidi ushamba sasa!

Yaani huko kushikiliwa kwa ndege moja tu ndo imekuwa nongwa hadi majitu yanaenda kuandamana?

Kushikiliwa kwa ndege kumekuwa ndo gumzo la taifa sasa! Mengine yote yamesahaulika!

Mimi si mshabiki sana wa haya mashirika ya ndege ya taifa. Najua yapo dunia nzima. Napendelea zaidi mashirika binafsi ndo yafanye hizo biashara za anga kama ilivyo Marekani.

Hii ya ndege moja kukamatwa na watu kuanza kutoa mapovu hadi kufikia kuandamana mbele ya ubalozi wa nchi inakoshikiliwa ndege hiyo ni ushamba.

Nishawahi kusema humu kuwa maamuzi ya kununua hayo madege yalikuwa ni ya papara. Na haya yaliyotokea ndo ushahidi wa papara yenyewe sasa.

Yaani ndege moja tu kukamatwa ndo ifanye watu wazima waache shughuli zao waende kuandamana mbele ya ubalozi?? Hawana shughuli za kufanya au?

Tumezidi ushamba.
Na jamaa yangu huwa hueleweki kabisa, mara umsifie Magu na kuponda upinzani, unashangaa watu kuandamana? Mbona hukushangaa walipoipokea ndege kwa ngoma?
Mikononi mwa CCM, hutaona Tanzania iliyoendelea isipokuwa Tanzania iliyochakaa.
Serikali huwa haifanyi Biashara, zaidi ya kukusanya kodi, US hata Lockheed Martin ni ya watu binafsi na serikali ya US hununua silaha zake hapo
Ili nchi iendelee ni lazima uchumi uwe mikononi mwa watu na siyo serikali.
 
Hii nchi bhana
IMG_20190815_200543.jpeg
 
Wasukuma /wakazi wa kanda ya ziwa na ushamba ni sawa na pipa na mfuniko
 
Na jamaa yangu huwa hueleweki kabisa, mara umsifie Magu na kuponda upinzani, unashangaa watu kuandamana? Mbona hukushangaa walipoipokea ndege kwa ngoma?
Mikononi mwa CCM, hutaona Tanzania iliyoendelea isipokuwa Tanzania iliyochakaa.
Serikali huwa haifanyi Biashara, zaidi ya kukusanya kodi, US hata Lockheed Martin ni ya watu binafsi na serikali ya US hununua silaha zake hapo
Ili nchi iendelee ni lazima uchumi uwe mikononi mwa watu na siyo serikali.

Ni hivi;

Siyo kwamba sieleweki. Ni kwamba wewe na wenzako walio kama wewe ndo hamnielewi na sidhani kama mna uwezo wa kuelewa.

Mmeshazifunga akili zenu. Mnadhani ni lazima mtu awe na upande mmoja tu, basi.

Mimi sipo hivyo. Siangalii wala siegemei upande.

Nasimamia kile ninachokiamini na ninachokiona kuwa ndicho kilicho sahihi bila kuangalia rangi wala itikadi za vyama.

Hakuna ugumu wowote hapo katika kuuelewa msimamo wangu.

Kuhusu upokewaji wa ndege, ni ama umesahau au hujui. Kitendo hicho nilikiponda.

Sasa sijui hukuona au umeamua tu kuifunga akili yako.
 
Mkuu na wewe si umeongeza ukubwa wa kundi la washamba? Mpaka ukakaa na wewe ukaanzishe thread ya ndege una tofauti gani na hao 'washamba' walioandamana?
 
Hapo walimaanisha watupe ndege bure bure bila kufuata sheria kwa kuwa tumewasaidia sana enzi za kupigania haki yao..kwa kweli huu ushamba unazidi kutuaibisha kimataifa tunaonekana ni nchi ya wapumbavu
Ushamba Gani HAPO Sasa Acha Kutuaminisha Ujinga,, Kama Wewe Ndiye Mjanja Hamia Kwa Wajanja Wenzako Kwani Umelazimishwa Kuishi Hapa Tz
 
Back
Top Bottom