Ni hivi;
Siyo kwamba sieleweki. Ni kwamba wewe na wenzako walio kama wewe ndo hamnielewi na sidhani kama mna uwezo wa kuelewa.
Mmeshazifunga akili zenu. Mnadhani ni lazima mtu awe na upande mmoja tu, basi.
Mimi sipo hivyo. Siangalii wala siegemei upande.
Nasimamia kile ninachokiamini na ninachokiona kuwa ndicho kilicho sahihi bila kuangalia rangi wala itikadi za vyama.
Hakuna ugumu wowote hapo katika kuuelewa msimamo wangu.
Kuhusu upokewaji wa ndege, ni ama umesahau au hujui. Kitendo hicho nilikiponda.
Sasa sijui hukuona au umeamua tu kuifunga akili yako.