Tresor Mandala
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 43,241
- 90,417
Mlisoma Uzi humu una kwenda kwa jina LA utata kifo cha Dr Omar? Mule kuna code iko inahusu tuko hili LA EL kwenda ikulu
Jamaa Uko vizuri sana up stairs!Toka nazaliwa mpaka leo sijapeleka kura yangu popote untill nitakapogombea mwenyewe
Hakuna haki na uhuru kwenye hizi chaguzi wala upinzani wa kweli mpaka kizazi chetu cha wanafiki kiishe kabsaJamaa Uko vizuri sana up stairs!
Mshana Jr, umeandika vizuri mno. All in all, Lowasa kuja CDM kwa watu, wenye akili , philosophical ones, tulijua kuwa huyu mtu ana mapungufu mengi tu kuwa Rais, ila kwa wakati ule ilikuwa inalipa kupata wabunge wengi. Na hilo lilifanikiwa. Alikuwa na wafuasi wengi sana, usingeliweza kumwacha mtu kama huyo. Kwa siasa za ujima kama za kwetu, maamuzi ya kumchukua yalikuwa muafaka.Kesho tarehe 10.01.2018 inaweza kuwa siku nyingine mbaya kwa wale wapenda wabadiliko. Kesho kuna kulia ama kucheka kama ni kweli kutakuwa na mkutano Serena hotel.
Mchana wote wa leo mpaka mida hii huku mitandaoni hakufai ni mitifuano na speculations za kila aina kuhusu siku ya kesho na kile kitachasemwa. Kila upande umejiandaa vilivyo na madongo ama vilio ama shangwe za kutosha.
Kama ilivyo kwa mechi ngumu za Simba na Yanga kila upande Unahitaji ushindi. Chochote kitakachotokea kesho kitakuwa na hasara kubwa kwa upande mmojawapo.
Kama hahami furaha shangwe nderemo na vifijo vitakuwa vingi mno... Nchi italipuka kwa kushangilia. Na wale wa upande wa pili watakuwa wamepigwa mweleka mkubwa.
LAKINI ikitokea akasema anahama au hata kusema anastaafu harakati upande wa pili patakuwa hapatoshi japo si kwa kushangilia sana bali vijembe na dhihaka kwa wingi wake.
Huku kwingine kutakuwa ni simanzi kubwa na nchi itakuwa kama iko msibani
Kuna viashiria vya kutisha kidogo.
-Kwanini kaenda peke yake? Pengine ni haki yake
-Kwanini hakushirikisha viongozi wenzake? Kizungumkuti kiko hapa
-Alichoongea mbona kinapingana na uhalisia? Ngoja tutaona...
Itoshe tu kuamini kwamba hatatonesha makovu ya vidonda vinavyopona.. Hatasahau fadhila. Hatawageuka wale wote waliompenda na kumwamini sana.
Hatawavunja moyo na kuwaumiza kihisia wale wote walioumia na kuumizwa kwa ajili yake.
Inawezekana kabisa ukawa ni mwanzo mpya wa kutufanya tusonge mbele pale tulipokwamishwa.
Naikumbuka ile code. Jamaa alitabiri.Mlisoma Uzi humu una kwenda kwa jina LA utata kifo cha Dr Omar? Mule kuna code iko inahusu tuko hili LA EL kwenda ikulu
Mwananke anapobeba mimba hutegemea kuzaa mtoto mzuri asiye na kasoro na mara zote ni aidha wa kike au wa kiume ama mapacha wa jinsia mbili tofauti au zinazofanana... Hii huwa furaha ya wazazi ndugu na jamaaHi yo kesho ikiwa tofauti utasema nini
Nimegundua JF ,kn wengine bado sana,zile code zimemaliza kila kitu hadi 2025 hukooNaikumbuka ile code. Jamaa alitabiri.
hyo video imenichoma sana
Mshana, likelihood ya kuwa tofauti ni ndogo. Kitendo cha kwenda huko KINYEMELA bila kumfahamisha mwenyekiti wake, kina uhaini mkubwa sana. Walikuwa pamoja kumwona Kingunge, waliongea sana, walijadiliana. Kwa nini alimficha ziara kama hiyo ambayo ni sensitive. Let him go, na Magufuli alivyo, atampa hata cheo kikubwa kuukomoa upinzani. Kuna mtu amesema kuwa agenda kubwa ya Magufuli ni kupambana na wapinzania/upinzani, KUUA UPINZANI/WAPINZANI. Yuko tayari kufanya LOLOTE, NASEMA LOLOTE, kuona upinzani unaumia.Mwananke anapobeba mimba hutegemea kuzaa mtoto mzuri asiye na kasoro na mara zote ni aidha wa kike au wa kiume ama mapacha wa jinsia mbili tofauti au zinazofanana... Hii huwa furaha ya wazazi ndugu na jamaa
Lakini si mara zote matokeo huja kama matarajio ya wazazi.. Sometimes kuna vifo ama kuzaa mlemavu... Matokeo yakiwa na tofauti hii utafanya nini? Tafakari!
ccm ni cancer kwa taifa.Kabisa Mkuu nchi iliyojaaliwa utajiri wa hali ya juu badala ya kukaa na kujadili mikakati ya kuleta maendeleo kwa Watanzania bado tunajadili upatikanaji wa demokrasi nchini. Kuna chama kimeamua kung'ang'ania madarakani kwa gjarama yoyote ile pamoja na kujifanya kinaunga mkono mfumo wa vyama vingi nchini.
Miaka 56 waliyokaa madarakani hakuna cha kujivunia zaidi ya ufisadi wa kutisha miaka nenda miaka rudi kusaini mikataba ambayo haina maslahi kwa Watanzania. Kikundi cha watu wachache ambao hawafikii hata 100K wanafaidi keki ya Taifa na kuwa mabilionea kwa njia haramu wakati Watanzania kwa mamilioni hawajui mlo mmoja tu kwa siku wataupata wapi, wakiugua hawana dawa, maji yao ya kunywa ni shida tupu! Wakilima wanalaliwa bei ya mazao yao na mengine kuozea mashambani, mashule mengi nchini hayana hadhi ya kuitwa choo achilia mbali kuitwa shule.
Kweli Tanzania na labda Afrika yote tuna laana kubwa sana. Ndiyo sababu nchi zetu nyingi na Bara letu zinashindwa/linashindwa kuwa na maendeleo ya kweli miaka nenda miaka rudi.
Leo ndio yamekuwa haya dah Poleni sanaLowassa amekuwa gamba chadema kama alivyokuwa gamba ccm. Arudi huko ccm hatuna mahaba nae tena.