Tumewekwa njia panda

Tumewekwa njia panda

hizi mambo ndio zinafanya TZ izidi na kuendelea kuwa maskini, waTZ watu wa matukio hasa yasiyo na kichwa wala miguu..

saa hizi watu wanawaza innovations za kukabiliana na baridi/winter ili lisidhuru utendaj kaz na uzalishaji....waTZ badala ya kuwaza cha kufanya kutatua matatzo yenu hasa hayo ya mafuriko wanabaki kununuana na kuhamahama vyama tuu,

yaani its too rubish...media coverage zimejaa huo upuuzi tu!
aibu sana kwakweli.
 
Umepangilia hoja zako vizuri.... Je nikisema tena wakati utaamua kutakuwa na ubaya wowote? I mean nimeandika nawe umeandika! Ni haki yetu sote so long hatuvunji sheria na taratibu za JF na tunabishana kwa hoja.. Ni wakati sasa wa kusubiri kuona muda utatuletea nini
Hoja zako hakika ni fikirishi. Wengi wetu humu tutashangilia au kuhuzunika kwa uamuzi wowote wa Lowassa. Lakini ukweli unabaki kwamba ni maisha yake Lowassa kama Lowassa, ambayo katu hayagusi maisha yetu na familia mmoja mmoja.

Lakini yatagusa Taifa kwa kuwa viongozi wa kisiasa, kwenye nchi changa za demokrasia ya vyama vingi vya siasa, viongozi wa kisiasa wanatumia uelewa wa wananchi kwa faida yao binafsi.

Lakini mimi binafsi mshana jr, naamini CCM inapitia mabadiliko makubwa kisera, kiitikadi na hata kiuongozi kama lilivyo jina lake Mapinduzi. Hivyo basi wanaohamia CCM wanapaswa kujitafakari kwa kina kuhusu maisha yao kisiasa. Humu JF na vyombo vya habari tutawajadili tu kujiridhisha.
 
Nasikitika kuona kwamba mpaka leo wengi wetu hatujui maana ya siasa ndio maana tubakuwa vibaraka wa vyama flani.
Kama uko smart na unawaza mbali huwezi kuchezewa kama mpira, niliona haya mambo miaka 2 ilopita na sasa nachekelea tu ninavoona yakitimia, sina kihoro kabisa japo nawasikitikia watanzania wengi ambao bapo gizani bawana utashi juu ya maisha yako wanadhani kiongozi flan anaweza kuwapa faraja.

Ushauri wangu think beyond what u see with ua normal eyes.
 
Siasa ni mchezo mchafu! Hakuna msafi awezae kushiriki mchezo huo
 
Labda ataongea kati ya haya:

  • Hatuwezi kuwa tunapinga kila kitu
  • Nimegundua Chadema haiwezi kuchukua dola
  • Magu anafanya kazi nzuri sana (bila ufafanuzi wa kina)
  • Nimeamua kurudi baada ya kuona kasi ya maendeleo nchini ili kumuunga mkono Magu
  • Mie na Mama Ngina wote tunarudi nyumbani
Sidhani kama atagusia kuanguka kwa demokrasi nchini, kununua Wabunge na Madiwani kwa kuwapa rushwa ya pesa au vyeo, upinzani kuzuiwa kufanya shughuli zao hadi 2020, shambulizi la Lissu na Nassari, kupotea kwa Saanane na Mwandishi wa Mwananchi, kudharauliwa kwa katiba, Bunge, mahakama, sheria za nchi na taratibu za pesa Serikalini na kupora ushindi katika uchaguzi wa Madiwani kwa mapanga marungu visu na bunduki.
Anaweza kujibu maswali ya kirahisi mawili au matatu kwa kubabaisha kutoka kwa waandishi wa kupandikizwa au asitoe nafasi ya kuulizwa maswali.
 
Kama kuna kitu ambacho kinagharimu upinzani hivi sasa ni kutoambiana ukweli. Badala ya kumlaumu Mbowe kwa kuwaingiza mkenge hakuna anayerudi nyuma kutadhimini ahadi zake na jinsi alivyopuuza ushauri wa katibu mkuu hatua za kuchukua kwa hawa wageni wanaohamia kabla ya kuwapa nafasi walizopewa. Mnajadili tukio la sasa! Kwanini CCM wasiendelee kutawala kwa hizi akili? Mlipigwa ganzi wakati ule na mnapigwa ganzi nyingine. Hivi kuna ugumu gani kuona Dr Slaa alikuwa sahihi na nyie hamkuwa sahihi mkajisahihisha ili mfute makovu mambo yasonge? Inafikia mahali hadi viongozi wakubwa wanasema Lissu tu akiondoka ndio watasikitika ila takataka zingine ziende!!!! Lissu akiondoka Chadema ndio ife? Kuna taasisi hapo? Mkiendelea kushipaza shingo mnaenda kubaki na Chadema kama NCCR ya Mbatia! Akina Lissu wametokea NCCR iliyokufa ....wao watapata platform nyingine siasa ziendelee .....tutajenga upinzani mpya hadi lini? Mbona mnasahau haraka?
 
Wakati ule mnaimba mabadiliko kuletwa na mtu badala ya chama bila kujali nini kitatokea kesho hamkutaka kusikia la mtu. Wafuasi wenye nia njema ni wale wanaohoji pale viongozi wao wanapotenda kinyume na ahadi zao. Acheni kujadili tukio linalotokea sasa bali safari nzima inayotufikisha hapa ili makosa yasijirudie.
 
MTAZAMO ,
Mkuu,
Umeandika vizuri sana. Tatizo, wenzio wanaangalia matumbo yao kwanza.

Ujenzi wa upinzani imara siyo tija kwao, kwa sababu, wanaamini kuwa watapata watanzania wenzentu wasio kuwa na uelewa wa siasa na kuwaburuza tena ili wawasaidie.

Mfano, tu hadi sasa CDM ikiomba michango huko mitaani kama walivyokuwa wanaomba kwa wananchi wa kawaida miaka 2005 hadi 2014 hawatapata kabisa kwani watu wamegundua kuwa nao ni majanga.

Any way, siasa ni usela na kujifanya mwanasesere.
 
Kama kuna kitu ambacho kinagharimu upinzani hivi sasa ni kutoambiana ukweli. Badala ya kumlaumu Mbowe kwa kuwaingiza mkenge hakuna anayerudi nyuma kutadhimini ahadi zake na jinsi alivyopuuza ushauri wa katibu mkuu hatua za kuchukua kwa hawa wageni wanaohamia kabla ya kuwapa nafasi walizopewa. Mnajadili tukio la sasa! Kwanini CCM wasiendelee kutawala kwa hizi akili? Mlipigwa ganzi wakati ule na mnapigwa ganzi nyingine. Hivi kuna ugumu gani kuona Dr Slaa alikuwa sahihi na nyie hamkuwa sahihi mkajisahihisha ili mfute makovu mambo yasonge? Inafikia mahali hadi viongozi wakubwa wanasema Lissu tu akiondoka ndio watasikitika ila takataka zingine ziende!!!! Lissu akiondoka Chadema ndio ife? Kuna taasisi hapo? Mkiendelea kushipaza shingo mnaenda kubaki na Chadema kama NCCR ya Mbatia! Akina Lissu wametokea NCCR iliyokufa ....wao watapata platform nyingine siasa ziendelee .....tutajenga upinzani mpya hadi lini? Mbona mnasahau haraka?
Sijui kama comment hii itaonwa, kusomwa na kueleweka. Pengine ndiyo comment bora na yenye uhalisia kuliko zote hapa. Asante sana mkuu !!!
 
mshana jr, Hoja ya pili, niliyonukuu hapo, juu ni dhaifu kwa kuwa dhana yake ni kwamba Lowassa ndiye mwamuzi wa mwisho wa siasa za nchi hii

mshana jr kumbuka kuwa jina la Lowassa lilipokatwa CCM, ikafiatutiwa na sekeseke mkutano wa NEC wengi, nadhani na wewe, uliamini CCM ndiyo mwisho, mbendembende kifo cha mende. Matokeo unayajua.

mshana jr, hoja ya mwisho, nukuu hapo juu, nakubaliana na wewe ila nakukumbusha kuwa, nje ya ndani ya uongozi wa CCM (kwa maana ya vikao vyake), kila mwanachama ana nguvu. Lakini ndani ya chama, nguvu ya mwanachama mmoja mmoja haipo. Mwanachama anakihitaji chama kuwa na nguvu na chama hakimhitaji mtu mmoja mmoja kuwa na nguvu.

Hitimisho ni kwamba kurejea au kutokurejea kwa Lowassa CCM kuna tija/hasara kwa Lowassa kama Lowassa, BASI. Rejea hotuba zake zote ndani na nje ya CCM. Ila nina uhakika CHADEMA itaathirika sana akirejea CCM na sababu ziko nyingi km amewezesha kupata wabunge wengi - na Team Lowassa. Lakini CCM mpya, kama Lowassa hakujipanga vizuri jinsi ya kurejea, Team Lowassa itasambaratIka.

NI MAONI YANGU TU

Mwengeso nimeangalia hoja zako zote. Sipendi kuzijadili zote bali napenda kujadili hiyo ya mwisho kwamba ndiye aliyeleta wabunge wengi. Hili dhana nipingana nayo na nitaendelea kupingana nayo. Nakuhakikishia Lowassa alifaidika na cdm kama chama kuliko cdm ilivyofaidika na Lowassa. Wanaoweza kusema walifaidika na Lowassa ni viongozi wachache na sio chama.

Msingi wa cdm kupata kura nyingi ilikuwa ni operation zake za nchi nzima za 2010-2015 ambazo Lowassa hakushiriki hata moja. Watu wengi wa cdm walijiandikisha kupiga kura ili kuipiga ccm chini kwani ilionekana kabisa ccm lazima imchague Lowassa kugombea urais kupitia ccm. Hapo ndipo kitambulisho cha kura kilipoitwa kichinjio. Kilichopelekea Lowassa kukatwa huko ccm ni nguvu iliyokuwa nayo cdm kabla ya huo uchaguzi, na yote hayo yalikuwa bila nguvu ya Lowassa. Ni kweli kuna kura cdm walipata kwa ajili ya uwepo wa Lowassa japo mimi niliziita kura za ushabiki. Lakini naamini kabisa cdm ilipoteza kura nyingi kwa hiyo gia ya angani kwani si kila mtu alikuwa mjinga au mwenye ushabiki wa kijinga.

Ni kweli Lowassa akiondoka cdm kutakuwa na mabadiliko lakini sio madhara kama wengi wanavyongopeana. Uwepo wa Lowassa ndani ya cdm niliuchukulia kama mafanikio hewa, kwani ukiachia ukubwa wa jina lake ambao kitengo chake binafsi cha propaganda ndio kililikuza hakuwa na mchango wa maana katika kukikuza. Lowassa ndani ya miaka mitatu kabla ya 2015 alipita kwenye taasisi mbalimbali hasa za dini akiitisha michango mikubwa kwa ajili ya ujenzi kwenye taasisi hizo. Je alivyoingia cdm aliwahi kujenga ofisi popote nchi hii? Ni kipi alichofanya Lowassa baada ya uchaguzi ambacho kimeongeza wanachama cdm?

Nakuhakikishia Lowassa akiondoka cdm tegemea cdm kuwa nzuri na bora zaidi na hii itafikisha mwisho wa uenyekiti wa Mbowe ndani ya cdm pamoja na wote waliokuwa nyuma yake. Nitoe muda huku nikiomba Lowassa aondoke cdm ili mageuzi ndani ya cdm yatokee.
 
Kabisa Mkuu nchi iliyojaaliwa utajiri wa hali ya juu badala ya kukaa na kujadili mikakati ya kuleta maendeleo kwa Watanzania bado tunajadili upatikanaji wa demokrasi nchini. Kuna chama kimeamua kung'ang'ania madarakani kwa gjarama yoyote ile pamoja na kujifanya kinaunga mkono mfumo wa vyama vingi nchini.

Miaka 56 waliyokaa madarakani hakuna cha kujivunia zaidi ya ufisadi wa kutisha miaka nenda miaka rudi kusaini mikataba ambayo haina maslahi kwa Watanzania. Kikundi cha watu wachache ambao hawafikii hata 100K wanafaidi keki ya Taifa na kuwa mabilionea kwa njia haramu wakati Watanzania kwa mamilioni hawajui mlo mmoja tu kwa siku wataupata wapi, wakiugua hawana dawa, maji yao ya kunywa ni shida tupu! Wakilima wanalaliwa bei ya mazao yao na mengine kuozea mashambani, mashule mengi nchini hayana hadhi ya kuitwa choo achilia mbali kuitwa shule.

Kweli Tanzania na labda Afrika yote tuna laana kubwa sana. Ndiyo sababu nchi zetu nyingi na Bara letu zinashindwa/linashindwa kuwa na maendeleo ya kweli miaka nenda miaka rudi.

hizi mambo ndio zinafanya TZ izidi na kuendelea kuwa maskini, waTZ watu wa matukio hasa yasiyo na kichwa wala miguu..

saa hizi watu wanawaza innovations za kukabiliana na baridi/winter ili lisidhuru utendaj kaz na uzalishaji....waTZ badala ya kuwaza cha kufanya kutatua matatzo yenu hasa hayo ya mafuriko wanabaki kununuana na kuhamahama vyama tuu,

yaani its too rubish...media coverage zimejaa huo upuuzi tu!
aibu sana kwakweli.
 
Sijui kama comment hii itaonwa, kusomwa na kueleweka. Pengine ndiyo comment bora na yenye uhalisia kuliko zote hapa. Asante sana mkuu !!!
Mkuu vijana wengi wanaojifanya wapambanaji kama upo JF muda kidogo utagundua tatizo kubwa kwao. Inatugharimu mno! Wao wanarukia kila tukio na hawahoji viongozi wao. Ndio maana ni rahisi kuchezewa kijinga na siasa za kutiana moyo while viongozi wamefanya blunders. Haina tofauti na Simba na Yanga ....umebaki ushabiki tu hadi kwa viongozi! Nafikiri umeona comment ya Meya wa Chadema bwana Boniface Jacob ....huoni tatizo hapo la kukemea? Wao kazi yao wamefundishwa kumsema Rais aliye madarakani tu!!!
 
Akatayetaka kuondoka aondoke tu ...hakuna jinsi tunajua wapinzani wanapitia wakati mgumu sana,tumeona mikutano ya siasa kuzuiwa kufanyika laiti wao. Wanafanya,tumeona kamatakamata ya wapinzani....
Mm binafsi ishu ya Lowasa kwenda ikulu hainiumizi Hata kidogo maana amekwenda Kwa Kwa ajili yake zaidi syo Kwa ajili ya chama cdm

Ova
 
Ndiyo tabia za wapenda hela na watoa rushwa
 
Back
Top Bottom