Mleta hoja una hoja nyingine zaidi ya hiyo?.Kama alivyosema mdau mmoja mbona mwenzake Mwalimu Kashasha anachanganya kiingereza kwenye maelezo na hujamsema?Enock ni mmoja wa Watangazaji bora wa mpira wa miguu redioni (kwangu ni namba 1).Mara nyingi huyatumia kama vionjo kwenye mechi zinazohusu timu za Mbeya City na Prison na hana nia yoyote ya Ukabila.Mtangazaji Charles Hilary wakati akiwa RTD alitumia vionjo hivi kwenye mechi za Tukuyu Stars au Mecco.Unajua hapa nchini kuna lugha za makabila fulani zinavutia masikioni mwa wasikilizaji ndiyo maana hutumika kama vionjo vya matangazo ya biashara redioni mfano:Aise Meku....,nitakuarrest Mura,namgambila inafu, nshomile bwana mpaka fomu six, ndaga fijo....nk.