Tumemchoka sasa Mtangazaji wa TBC1 na TBC Taifa Enock Bwigane abadilike upesi na huu ushamba!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Nilidhani ni Kitendo tu cha siku moja labda alikikosea lakini sasa naona kama ni Kitendo ambacho amekibariki na anakifanya sasa bila hata aibu au kujishtukia kuwa anachokifanya kiukweli ni kinyume kabisa na maadili ya Utangazaji na nashangaa kwanini Uongozi wake kupitia kwa Mwalimu wangu Kipenzi Dkt. Ayub Ryoba ambaye ndiyo Mkurugenzi Mkuu wa hivyo Vyombo bado hawajamwonya.

Ni kwamba kila anapokuwa anatangaza mipira hasa hii ya Ligi Kuu ya Tanzania bara VPL huyu Mtangazaji Enock Bwigane amekuwa na tabia ya kuudhi kama si ya kukera kabisa ya kupenda kutangaza huku akiweka maneno ya lugha yake ya Kinyakyusa kila mara kitu ambacho kiukweli nisimfiche kinatukera wengi na pengine ndiyo maana kwa udhaifu wake huu Watu wengi sasa hawasikilizi tena matangazo yao ya moja kwa moja ya mpira na badala yake sasa tumekimbilia SIKUKA fm na Radio One ambapo Watangazaji wake wanajua maadili yao.

Kila mara tu utamsikia sijui ' ndaga fijo ' akitangaza tu kidogo sijui ' kukoya ' hatujakaa sawa utasikia tena anaongea kilugha chake cha Kinyakyusa na akisema tena sijui ' ndaga fijo ' yaani ni full ' kutuboa '.

Kama vipi TBC1 na TBC Taifa hebu anzisheni haraka sana idhaa ya Lugha ya ' Kinyakyusa ' halafu mpeni Mtangazaji Enock Bwigane awe ' anatiririka ' nayo mwenyewe kila siku na Wanyakyusa wenzake ila huku TBC1 na TBC Taifa mtuachie tu akina ' Poti ' Chacha Maginga na Bingwa wa Utangazaji wa mipira kwa sasa Tanzania nzima Kamarada Jesse John.

Atakayepata ujumbe huu ' murua ' kabisa na akijua yupo karibu na huyo Mtangazaji Enock Bwigane basi amfikishie na tunamtaka abadilike haraka kama siyo upesi sana na asitake kupandikiza mbegu ya ukabila hasa katika Chombo kikubwa cha Habari ambacho ni cha Kitaifa kama hicho anachokifanyia.

Kama kawaida yangu GENTAMYCINE huwa silei ' upuuzi ' na kazi yangu siku zote ni ' kunyoosha ' tu ili Watu wakae sawa katika mstari na hatimaye twende sawa. Tanzania official language ni Kiswahili na siyo sijui Kinyakyusa au Kizanaki au Kimakuwa au Kinyarwanda.

Nawasilisha.
 
Gentamycine! Kipi bora kati ya Kinyakyusa na Kiingereza? Mpira ni burudani. Mpira una vionjo vingi. Ingekuwa anatangaza Taarifa ya habari tungemkanya.
Mwl Kashasha anaweka maneno ya kiingereza na kunogesha matangazo.
Outer pass, snake ball, cross shots, mpira burudani
 
Hivi kuna mimtu inaangalia tbc hivi sasa?
Limkituo lenyewe linatangaza habar za uongo...
Yaani natamani nilifute hilo limsteshen kwenye king'amuzi nisilione kabisa!
Binadamu mwenzio unawaita Mimtu! Hii chuki unaitoa wapi?
Mie hapa nilipo matangazo ya mpira nasikiliza TBC .Vituo vingine havioni umuhimu na coverage yao sio kubwa.
 
TBC niliacha kusikiliza na kutazama toka mwaka 2010 kumbe kuna watu bado wanatazama na kusikiliza radio hizi?? Umenishangaza sana
 
Hata naniliu huwa aniboaga sana kupenda kuongea kisukuma hasa anapokuwa kwenye ziara za mikoa ya kanda ya ziwa. Nilidhani ataishia kipindi cha kampeni tu lakini naona ni kama utaratibu wake, na kama ingekuwa ni amri yake angetangaza kuwa kisukuma kiwe ndio lugha ya Taifa badala ya Kiswahili
 
Back
Top Bottom