Tumemchoka sasa Mtangazaji wa TBC1 na TBC Taifa Enock Bwigane abadilike upesi na huu ushamba!

Dah kwenye la liga huwa wanatangaza kwa kiswahili ,Charles na bwigane

Ebwana bwigane anachapia mno mpaka kero na huwa nachukizwa mno na utangazaji wao wa kiswahili wanatukosesha ladha ya mpira ,huyo bwigane anachanganya majina ya wachezaji ,hadi timu Mara nyingine anakosea


Nilitaka kutoa thread kuhusu huyu mtangazaji na kuhusu la liga chini ya azam

Kiukweli mpaka unaboeka ase
 
Hivi bado mtu unaangalia TBC hii TV ipo mahususi kwa ajili ya viongozi tu ndio wanaoweza kuangalia mm nina zaidi ya miaka 10 sijaangalia mpaka nimepandikiza chuki kwa watoto wangu waichukie kabisa na nimefanikiwa 100% halafu hata sijui kwanini naichukia
 
Maelezo meeeengi, umeandika gazeti zima kisa anaongea kinyakyusa? Eti maadili ya utangazaji we jamaa bhana, angeongea kiingereza ungemsifia.
 
Mimi sina shida na Lugha anayochangia tatizo langu kwake anaonyesha sana yeye ni Yanga tena usiombe Simba akawa ametanguliwa na Mbao FC yaani nilitamani kuzima redio, lakini kingine nilitaka kumuomba Mkurugenzi Mkuu wa TBC kumsafirisha mwl.Kashasha kwenye mechi za mikoani maana ni mwl.mzuri sana
 
Nilidhani ni Kitendo tu cha siku moja labda alikikosea lakini sasa naona kama ni Kitendo ambacho amekibariki na anakifanya sasa bila hata aibu au kujishtukia kuwa anachokifanya kiukweli ni kinyume kabisa na maadili ya Utangazaji na nashangaa kwanini Uongozi wake kupitia kwa Mwalimu wangu Kipenzi Dkt. Ayub Ryoba ambaye ndiyo Mkurugenzi Mkuu wa hivyo Vyombo bado hawajamwonya.

Ni kwamba kila anapokuwa anatangaza mipira hasa hii ya Ligi Kuu ya Tanzania bara VPL huyu Mtangazaji Enock Bwigane amekuwa na tabia ya kuudhi kama si ya kukera kabisa ya kupenda kutangaza huku akiweka maneno ya lugha yake ya Kinyakyusa kila mara kitu ambacho kiukweli nisimfiche kinatukera wengi na pengine ndiyo maana kwa udhaifu wake huu Watu wengi sasa hawasikilizi tena matangazo yao ya moja kwa moja ya mpira na badala yake sasa tumekimbilia SIKUKA fm na Radio One ambapo Watangazaji wake wanajua maadili yao.

Kila mara tu utamsikia sijui ' ndaga fijo ' akitangaza tu kidogo sijui ' kukoya ' hatujakaa sawa utasikia tena anaongea kilugha chake cha Kinyakyusa na akisema tena sijui ' ndaga fijo ' yaani ni full ' kutuboa '.

Kama vipi TBC1 na TBC Taifa hebu anzisheni haraka sana idhaa ya Lugha ya ' Kinyakyusa ' halafu mpeni Mtangazaji Enock Bwigane awe ' anatiririka ' nayo mwenyewe kila siku na Wanyakyusa wenzake ila huku TBC1 na TBC Taifa mtuachie tu akina ' Poti ' Chacha Maginga na Bingwa wa Utangazaji wa mipira kwa sasa Tanzania nzima Kamarada Jesse John.

Atakayepata ujumbe huu ' murua ' kabisa na akijua yupo karibu na huyo Mtangazaji Enock Bwigane basi amfikishie na tunamtaka abadilike haraka kama siyo upesi sana na asitake kupandikiza mbegu ya ukabila hasa katika Chombo kikubwa cha Habari ambacho ni cha Kitaifa kama hicho anachokifanyia.

Kama kawaida yangu GENTAMYCINE huwa silei ' upuuzi ' na kazi yangu siku zote ni ' kunyoosha ' tu ili Watu wakae sawa katika mstari na hatimaye twende sawa. Tanzania official language ni Kiswahili na siyo sijui Kinyakyusa au Kizanaki au Kimakuwa au Kinyarwanda.

Nawasilisha.
alijua zambia wanamuangalia mkuu. msamehe sana
 
Ni sehemu ya burudani mkuu!
Umesahau kuna mwingine hotuba za kitaifa kabisa lazima aweke kisukuma!
"Hiiiiiii bhangosha" na rais wa bank ya dunia yupo anasikiliza siku ile pale ubungo mataa!.Sembuse huyo tena kwenye michezo
Mwambie huyo
 
Mbona hujahama nchi kwa kusikia mkuu wa nchi anaongea Kikwao? aliyesema ni nyivu za kike hajakosea , kuongea lugha yako sio ukabila,ukabila ni ubaguzi kwa wasiokuwa kuwa wa kabila lako.
 
Hivi hiyo MEDIA mnaisikiliza ya nini kama na nyie hamtaki kukereka kwa kukusudia wenyewe
 
Back
Top Bottom