Tumefikaje Hapa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,549
40,204
Je tumefika mahali ambapo tulitaka kufika kama Taifa? Je hapa tulipo ndipo wazazi wetu waliposimama kulilia uhuru na kuwa Taifa walitarajia ndipo tungekuwa? Je hapa tulipo ndipo kwa haki yote ndiyo hasa tumepaswa kuwa na siyo zaidi? Je kuna kitu ambacho tungekifanya ambacho kingetufanya tuwe zaidi ya hapa tulipo? Nazungumzia kitaifa katika nyanja zote; elimu, afya, miundo mbinu, huduma za jamii, n.k je tumefikia mahali bora zaidi na tuone fahari au kuna maeneo ambayo hatuna budi kujiuliza kwanini hatujafika mbali?

Ukiangalia changamoto zote tulizo nazo leo hii, bila ya shaka kuna makosa yamefanyika au mapungufu fulani ambayo yawezekana kabisa yametuzuia kufikia pale ambapo tungefikia kama tusingekuwa na makosa au mapungufu hayo. Unafikiri imekuwaje tumefikia hapa tulipo? Na tufanye nini ili tujinasue?
 
tumefika hapa kwasababu ya fikra bora za Mwalimu,Nadahni Miiko ya Uongozi aliyoiweka Mwalimu ilichangia kulinda Rasrimali nyingi za nchi yetu,alipokuja Mwinyi akacha Dira aliyoiweka MWalimu na Alikuja Namwelekeo wa chama kwa iaka 15 ijayo.hiyo ilikuwa 1990,Mampo chama kilianza kubadilika na kuacha kuwa cha wafanyakazi na wakulima,Mwalimu kwa huruma mwaka 1995 katika sherehe ya Mei Mosi akatukumbusha pale Mbeya,Tangu lini CCM imeacha kwa ya wafanyakazi na wakulima?
Mkapa alikuja na sera ya uwazi,Ubeapari ukaingia,Rushwa kubwa ndio ikashamili,Mashirika mengi yakauzawa..ila aliacha msingi mzuri katika Kutunza kiasi cha pesa hazina..ALiyepewa alikuwa naa Ari mpya ila na Nguvu mpya ya Kusaini mikataba ya kududmiza zaidi kama ya Richmond na Buzwagi.
Kwa kifupi tumefika hapa sababu ya jambo moja,Amani ya nchi yetu..
 
We need to have a sustained indignation going into next elections and the elections after, and on and on in order kujinasua from the current state
 
We need to re-examine and re-define our priorities. The problem at the moment is that we dont know what are our major priorities.

Tupunguze warsha, makongamano, semina, mashangingi, etc. Tuache ubabaishaji. Tufanye kazi kwa bidii. Tutangulize mbele maslahi ya taifa kuliko maslahi binafsi. There is no quick fix solution.

bila Semina Wafanyakazi wa serikali hawawezi kuishi,hizi ndizo posho zao..wewe kwa mshahara wa TGS D. unadhani utaenda wapi??
hili siliungi mkono

Warsha ziwepo ila ziwe zinapimwa kutokana na mafanikio yake!!
 
Serikali kutangaza Wiki ya Kuondoa Umaskini

2007-11-19 17:20:04
Na Usu-Emma Sindila, Jijini

Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji ikishirikiana na wadau mbalimbali wa kupambana na umaskini inatarajiwa kuadhimisha `Wiki ya Kuondoa Umaskini` ambapo mbali na mambo mengineyo, washiriki wataweza kuzielewa sera mbalimbali za kupambana na umaskini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa wizara hiyo, Dk. Juma Ngasongwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Amesema maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam yamelenga kutoa fursa kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kuelimishana, kujadiliana na kubadilishana ujuzi kuhusu hali ya mapambano dhidi ya umaskini.

Amesema pia imelenga kuangalia hali ya utekelezaji na mafanikio yanayopatikana katika michakato ya utekelezaji wa jitihada za kupambana na umaskini.

Aidha amesema pia ni nafasi muafaka kwa Serikali kuwafahamisha wananchi juu ya utekelezaji wa mikakati ya kupambana na umaskini, mafanikio na kujadili kwa pamoja kuhusu changamoto na vipaumbele kwa siku zijazo.

Amesema kuwa pia wadau hao watapata nafasi yakutoa maoni yao ambayo yatakayozingatiwa na kuchangia kuboresha mipango katika bajeti ya Serikali ya mwaka ujao.

Amesema mijadali hiyo imelenga kuwatia ari wakereketwa wa maendeleo kusiriki katika michakato mbalimbali katika kubuni na kutekeleza miradi ili kujiongezea kipato na kupunguza tatizo la kitaifa kuhusu ajira.

Amesema wiki hiyo ya sera za kuondoa umaskini imebebwa na kauli mbiu isemayo ``Ubunifu na bidii ya kazi ndiyo nguzo ya mapambano dhidi ya umaskini``.

Amesema wadau mbalimbali wanatarajiwa kutoa mada, wakiwemo wa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, ESRF, Taasisi ya Utafiti Kuhusu Umaskini, REPOA na asasi ya NSA.

Amesema maadhimisho hayo yantarajiwa kufanyika kati ya Novemba 19 hadi 22 mwaka huu.

SOURCE: Alasiri

Tuma Maoni Yako

Hebu tazama huyu waziri sijui anaongea kitu gani hapa??? Someni huyo waziri anachoongea hapo juu, mtaelewa nilikuwa namaanisha nini katika posti yangu iliyopita.
 
Je tumefika mahali ambapo tulitaka kufika kama Taifa? Je hapa tulipo ndipo wazazi wetu waliposimama kulilia uhuru na kuwa Taifa walitarajia ndipo tungekuwa? Je hapa tulipo ndipo kwa haki yote ndiyo hasa tumepaswa kuwa na siyo zaidi? Je kuna kitu ambacho tungekifanya ambacho kingetufanya tuwe zaidi ya hapa tulipo? Nazungumzia kitaifa katika nyanja zote; elimu, afya, miundo mbinu, huduma za jamii, n.k je tumefikia mahali bora zaidi na tuone fahari au kuna maeneo ambayo hatuna budi kujiuliza kwanini hatujafika mbali?

Ukiangalia changamoto zote tulizo nazo leo hii, bila ya shaka kuna makosa yamefanyika au mapungufu fulani ambayo yawezekana kabisa yametuzuia kufikia pale ambapo tungefikia kama tusingekuwa na makosa au mapungufu hayo. Unafikiri imekuwaje tumefikia hapa tulipo? Na tufanye nini ili tujinasue?

Ni dhahiri ndugu MWKJJ kwamba hali tuliyokuwa nayo, ni hali mbaya na inatisha sana

kwa uchache wa niliyoyagudua hali yetu ni mbaya kwa sbabu zifuatazo.

1:Bado Watanzania hatujazitumia nguvu zetu ipasavyo
Nikiwa nimeishi katika mikoa ya pembezoni mwa ziwa victoria ,nimeshuhudia jinsi mikoa hiyo ilivyokuwa na mvua nyingi na ya kutosha, lakini jiulize ni kwa namna gani tunazitumia mvua hizo?. almost ni mara moja tu kwa mwaka mtu analima kwa nguvu, na siku zilizobaki anakula alivyovitunza kwenye ghala au kuuza ,misimu mingine ya mvua mtu wala halimi .ghafla ikitokea msukosuko akiba haitoshi, laiti tungekuwa tunalima kisawasawa ,tungepata chakula cha kutosha na pia tungeuza vile vya kuuzwa.

2:Kuiga mfumo wa Elimu wa Wazungu
Chukulia pale mlimani Kozi kama ya Computer Engineering, Computer engineer anaweza kudesign na kutengeneza computer/component zake, lazima ziwepo lab za nguvu na vifaa kiujumla, Wazungu wanavimudu vitu hivyo na nchi zao zina makampuni kibao ya wanafunzi wao kufanyia field, sisi kwetu mwanafunzi wa computer engineering anakwenda kufanya Field Celtel/TTCL, jiulize wapi na wapi tutaweza kupata maengineer walioiva kikweli kweli?

3:Mazingira mazima ya Ukuaji wa Mtoto ni Utatanishi
hatuna sera ya kuelezea tufanye nini kwa mtoto wetu kila anapopiga hatua ya ukuaji.
Jukumu la namna gani mtoto alelewe limeachiwa mzazi peke yake, hatuna sera ya kitaifa yenye kutoa muongozo wa kumsaidia mzazi kuonyesha kwamba kila mtoto akifikia hatua fulani basi afundishwe vitu kadhaa, au mtoto katika hatua hiyo ya ukuaji awe anajua vitu kadhaa, mathalani kuna viwango standard kwamba mtoto akiwa na miezi kadhaa lazima awe na uzito fulani.lakini hakuna viwango vilivyowekwa kumsaidia mzazi kumuongoza katika kukuza viwango vya ufahamu vya watoto wao. Yaani imekuwa kila mzazi/mlezi na lwake. sasa mtoto huyu ambaye kutokana na kutokupewa mwongozo imara wa ufahamu bora(ukiondoa elimu ya darasani ambayo ni dhahiri peke yake haitoshi)anakuwa hajaandaliwa kuwa askari mahiri wa kupambana ipasavyo katika challenge nyingi za maisha, maana kuna mambo mengi, kujiajiri, kujilinda na maradhi ya maambukizi, kuepuka uvunjaji wa sheria, ndoa, n.k

4:Uongozi kugeuka kuwa ni biashara
Mtu haiingii katika siasa kutokana na uchungu wa Wananchi, mtu anaingia katika siasa kwa utashi kwamba akipata uongozi aitumie nafasi yake kujinufaisha, kwa kujipa tenda, kuvizia posho na luxury nyingine, kuingia mikataba mibovu ili mradi awe amekula, n.k

hayo ni baadhi tu
 
Hiki ni kiini macho cha CCM na sirikali! Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya na Maisha bora kwa kila Mtanzania sasa wamekuja na mpya wakati zile zilizotangazwa kwenye kampeni ya 2005 hatujui zimeishia wapi!
 
Nitarudi na kuangalia hoja zenu na hapa tuchambua kwa kina nataka niandike in few weeks makala of the same title na mawazo yenu mengi nitayatumia... la msingi ni kujibu swali, "what went wrong".. na "tufanye nini tujinasue"..
 
Dr. Ngasongwa na timu yake.. can I say something please kwenye hilo kongamano katika kuwachochea watu.. ? au ni kwa wale walio nyumbani tu?
 
bila Semina Wafanyakazi wa serikali hawawezi kuishi,hizi ndizo posho zao..wewe kwa mshahara wa TGS D. unadhani utaenda wapi??
hili siliungi mkono

Warsha ziwepo ila ziwe zinapimwa kutokana na mafanikio yake!!

Mshahara ni matokeo ya tija. Sasa kama nyie mishahara yenu inatokana na warsha, semina na makongamano, No wonder we are where we are now.
 
I think we have given too much importance to political leadership at the expense of other sectors. Mtu yeyote haoni kama anafanikiwa kama hajashika madaraka ya kisiasa. Hata wale wanaofanya kazi vizuri katika sector zingine wakionekana tu kuwa ni wachapa kazi wanaanza kuchochewa wewe unafaa kuwa mbunge, waziri, n.k. So politics has become the measure indicator of a successful person in our country. Tukaharibu zaidi pale tulipoamua kuwapa mishahara mikubwa zaidi wanasiasa kuliko watumishi wengi wote wa serikali. Hapa UK, Waziri Mkuu anashika namba 148 katika watumishi wa serikali wanaopokea mishara mikubwa; wa juu ni watumishi wa mashirikia ya umma kama Posta. Kwetu, sijui hata mshahara wa Rais ni shilingi ngapi,lakini nasikia hakatwi hata kodi!

As result: hata wasio na sifa na hawastahili kuwa viongozi wanakimbilia huko na wale wenye sifa na wanastahili hawapati nafasi. Kama alivyosema Plato: "philosophers alone are fit to govern a country, because they have two important qualities: 1) they have the ability to govern, and 2) they do not want to do so"! So, you need to identify philosophers and convince them to seek leadership positions. After their tenure they will happily relinguish power and go back to their philospophical work.

So there we go, something is wrong with our system of getting leadership, this is where we messed up. We have to sort out this mess first and foremost, mengine yataongezewa tu!
 
Mzee Kitila hapo umesema jambo moja kubwa sana na nyongeza yake ni kuwa kuna sababu ya watu kuingia kwenye siasa.. it seems that it pays more! Wakati huku kwa mjomba Bush anayegombea Urais basically anachukua a big pay cut kutoka sekta binafsi. NI kwa sababu hiyo watu kama kina Mengi kuingia kwenye siasa it'll be a major paycut.. lakini mkufunzi wa Chuo Kikuu akiingia Ubunge.. it is a major pay boost.. !
 
Je tumefika mahali ambapo tulitaka kufika kama Taifa? Je hapa tulipo ndipo wazazi wetu waliposimama kulilia uhuru na kuwa Taifa walitarajia ndipo tungekuwa? Je hapa tulipo ndipo kwa haki yote ndiyo hasa tumepaswa kuwa na siyo zaidi? Je kuna kitu ambacho tungekifanya ambacho kingetufanya tuwe zaidi ya hapa tulipo? Nazungumzia kitaifa katika nyanja zote; elimu, afya, miundo mbinu, huduma za jamii, n.k je tumefikia mahali bora zaidi na tuone fahari au kuna maeneo ambayo hatuna budi kujiuliza kwanini hatujafika mbali?

Ukiangalia changamoto zote tulizo nazo leo hii, bila ya shaka kuna makosa yamefanyika au mapungufu fulani ambayo yawezekana kabisa yametuzuia kufikia pale ambapo tungefikia kama tusingekuwa na makosa au mapungufu hayo. Unafikiri imekuwaje tumefikia hapa tulipo? Na tufanye nini ili tujinasue?

ingekuwa uzuri ungeuliza ,tumefikishwaje hapa? , hatukufika wenyewe bali tumefikishwa , na nani? tumsakeni mchawi.ila pia kumbuka kwamba tanzania haijawahi kuwa ni sehemu bora ya kuishi tangu tupate fahamu zetu,ukitoa amani na utulivu ambayo ndiyo ngonjera tunayojivunia.hatujawahi kuwa na maendeleo ya kujitapa mbele za watu.hivyo tusiseme tulifikaje hapa? wakati hata hiyo safari ya maendeleo mpaka leo kwa taifa la tanzania ni ndoto.
ni mzee wa porojo, under age
 
kama tulifikishwa basi tundio tumefika.. so tumefikaje hapa aidha kwa kufikishwa au kwa kuacha tufikishwe..
 
I think we have given too much importance to political leadership at the expense of other sectors. Mtu yeyote haoni kama anafanikiwa kama hajashika madaraka ya kisiasa. Hata wale wanaofanya kazi vizuri katika sector zingine wakionekana tu kuwa ni wachapa kazi wanaanza kuchochewa wewe unafaa kuwa mbunge, waziri, n.k. So politics has become the measure indicator of a successful person in our country. Tukaharibu zaidi pale tulipoamua kuwapa mishahara mikubwa zaidi wanasiasa kuliko watumishi wengi wote wa serikali. Hapa UK, Waziri Mkuu anashika namba 148 katika watumishi wa serikali wanaopokea mishara mikubwa; wa juu ni watumishi wa mashirikia ya umma kama Posta. Kwetu, sijui hata mshahara wa Rais ni shilingi ngapi,lakini nasikia hakatwi hata kodi!

As result: hata wasio na sifa na hawastahili kuwa viongozi wanakimbilia huko na wale wenye sifa na wanastahili hawapati nafasi. Kama alivyosema Plato: "philosophers alone are fit to govern a country, because they have two important qualities: 1) they have the ability to govern, and 2) they do not want to do so"! So, you need to identify philosophers and convince them to seek leadership positions. After their tenure they will happily relinguish power and go back to their philospophical work.

So there we go, something is wrong with our system of getting leadership, this is where we messed up. We have to sort out this mess first and foremost, mengine yataongezewa tu!

kwa kuongezea kidogo,
Swala la maamuzi makubwa ya maendeleo na mstakabali wa Taifa letu kufanyika/kuamuliwa kisiasa badala ya utaalamu! (decision maker)

Hili nitatizo kubwa lilo tufikisha hapa tulipo, mfano swala la |Rada.. ilipo pingwa waziri husika akipata veto ya raisi akasema hata kama tunakula nyasi lazima inunuliwe!

Mfano wa 2, swala la mfumuko wa bei wa sasa, wataalamu wa HAZINA walipo shauri mafuta yasiguswe kwani yataleta shida ya mfumuko wa bei.. Muungwana na Zakhia, kwa mamlaka yao na maamzi ya kisiasa badala ya kufata ushauri wa kitaalamu wakasema hapo ndo pakuleta hela haraka kwani kila mtu lazima atumie mafuta!

Nyote ni mashahidi kutozingatia utaalamu kulipotufikisha, achilia mbali mikataba mibovu kama wa IPTL ambayo wataalamu wetu wamekuwa wakiipinga ( Mfano Rutabanzibwa?) lakini wanaishia kudharauliwa na kutupeleka kusiko na hakika ndiko walikotufikisha!
 
Hata wale wanaofanya kazi vizuri katika sector zingine wakionekana tu kuwa ni wachapa kazi wanaanza kuchochewa wewe unafaa kuwa mbunge, waziri, n.k. So politics has become the measure indicator of a successful person in our country. QUOTE]

Mfano mzuri ni Keenja alifanya vizuri ktk kukusanya mapato na kuliendesha jiji lakini akaingia ktk siasa na kuharibu kabisa
 
mbali na mifano mliyotoa hapo juu, vile vile hapa JF nyie mpo hapa kwa ajili ya politics (NA MTAHARIBU TU KAMA KEENJA)( na itawafikisha pabaya *kama mlivyosema), wengi hushinda humu na ninaamini kama kila member angekuwa kwenye sector fulani, basi each angeweza kutoa magunia 20 ya mpunga kwa wiki na kulisha raia tanzania !

tusiseme waliopo bongo, na sie tuliomo JF je ???????????
 
Kwa kweli sisi tumefanya makosa ambayo bado tunayarudia,kwa mfano Suala la uzawa katika kumiliki na kuendesha biashara halipewi kipaumbele na sekta ya Viwanda na Biashara.Tuchukulie mfano wa Asian Tigers mfano Singapore au India,hpa huwezi kuja mwekazaji kutoka nje ukainvest zaidi ya asilimia 50 na kumiliki kampuni,wanachofanya ni kumpa maximum 50 percent foreigner na wao kumiliki asilimia zilizobaki hat kama mwananchi huyo hana uwezo wa kuinvest kufikia asilimia hizo serikali itaingilia kati na kumuwezesha huyo mzawa kwa mkataba maalum na serikali.

Ndio maana hata ukiangalia matajiri wakubwa wa huku kama akina Anil Ambani,Mahindra na akina Ratan Tata wamesaidiwa kwa kiasi kikubwa na serikali yao hata pale inapotokea kuna ushindani wa kizabuni na makampuni makubwa ya nje kama.

Suala la Elimu,
Ukiangalia nchi nyingine kama Kenya wanapiga hatua kubwa kimaendeleo na wanazidi kutuacha kila kukicha kwa sababu suala la elimu linapewa kipaumbele sana ndio maana ukiangalia Kenya leo hii hakuna state utakayoenda huku India bila kukuta wanafunzi wa Kikenya waliojazana kwenye vyuo vikuu mbalimbali kwa sababu kipindi cha nyuma hawa watu walikua wanaleta wanafunzi wao hujku India na wanafunzi walipofika wakatengeneza mazingira ya kuwavuta wengine kuja kusoma huku kwani kuna vyuo vya bei rahisi sana.Hata wale ambao gharama za maisha zinakua ngumu huku huwa kuna utaratibu maalum kwenye ubalozi wao wa kusaidia wanafunzi walioelemewa kitu ambacho ni tofauti kabisa na hapo kwetu

Pia ,hatujawa na uwezo wa kusimamia na kuendesha raslimali zetu kikamilifu kwa sababu ya kuwa na uongozi mbovu usiokuwa na dhamira za dhati katika kuleta mabadiliko ya haraka katika sekta ya mali asili.Kwa mfano hatujawa na taasisi madhubuti za kutangaza raslimali zetu kama Milima,hifadhi nk. katika nyanja za kimataifa.Kama kwenye mashirika ya Ndege kama KLM,British airways,Singapore na kushirikiana na mawakala wengine wa kimataifa ndio maana Kenya wanatumia udhaifu huo kutuibia watalii wetu etc
 
mbali na mifano mliyotoa hapo juu, vile vile hapa JF nyie mpo hapa kwa ajili ya politics (NA MTAHARIBU TU KAMA KEENJA)( na itawafikisha pabaya *kama mlivyosema), wengi hushinda humu na ninaamini kama kila member angekuwa kwenye sector fulani, basi each angeweza kutoa magunia 20 ya mpunga kwa wiki na kulisha raia tanzania !

tusiseme waliopo bongo, na sie tuliomo JF je ???????????

Ndo maana walioko hapa JF wanajadili ni wapi tulipokosea ili tutafute suluhisho la kudumu kama kila member atatoa constuctive opinions bila kukaa kiudaku udaku na kuleta mzaha.

Pia ndio maana tukajadili kwa kina list ya mafisadi 11 wa nchi kuliko yule aliyepoteza muda kukaa chini na kuja kiudaku udaku kuleta ishu ya mafisadi wa JF katika jamvi serious kama hili.Pia mind kama hizo ndizo zilipotufikisha hapa tulipo.

Naam baadhi ya watu wamekataa tamaa na hawajali tena kupoteza muda wao amabao wangeweza kufanya kitu muhimu kwa taifa kama kutoa michango ya maana kwenye mada kama hii bila kuleta unazi wa kisiasa na mizaha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom