Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 5,094
- 11,328
Ni ukweli usiopingika kwamba chama cha mapinduzi ndio chama ambacho kina historia kubwa hapa barani africa,,na hii ni kutokana na historia ya viongozi wake kuwa mstari wa mbele kutoka enzi za kupigania uhuru kupambana katika harakati za kuona nchi nyingine za Afrika zinapata uhuru pia.
Lakini hata hapa Tanzania pamoja na mapungufu ya hapa na pale bado chama hiki kimekuwa mhimili mkubwa wa amani na maelewano ambayo sisi wananchi tunajivunia
Natambua kama chama kina mapungufu yake kwasababu kitu chochote ambacho kinasimamiwa na wanadamu lazima hakikosi kasoro,lakini kimekuwa kinajihimarisha na kuendana na nyakati tulinazo hivi sasa.
Na kubwa zaidi kimekuwa na sera ambazo zinatekelezeka kitu ambacho kinawapa wananchi wengi matumaini makubwa ya kuendelea kukiamini,,natumaini chama hiki kikiendelea kujitathimini na kuondoa mapungufu yanayo jitokeza kitaendelea kuaminiwa na wananchi na kitazidi kushika hatamu.
Kama zilivyo nchi nyingine za Afrika ziliingia katika siasa za vyama vingi kutokana na mabadiliko ya dunia kwasasa na hivyo Tanzania nayo haikubakia nyuma
Katika baadhi ya nchi tumeshuhudia vyama vya upinzani vikishika hatamu za uongozi na kuvibwaga vyama tawala lakini kwa hapa Tanzania bado hakijaonekana chama cha upinzani chenye mlengo wa kimapinduzi,vyama vyote ambavyo vimewahi kuwa maarufu na kuonekana tishio kwa chama tawala baada ya mda huonekana ni dhaifu na havina dira
Ndani ya vyama vyao hakuna demokrasia ingawa kwa nje vinaonekana kana kwamba vinafuata demokrasia,ulafi wa madaraka umetamalaki,hakuna kuaminiana miongoni mwa viongozi wao,na ufisadi ni sehemu ya mambo yao ndani ya vyama,je kwa stahili hii vinastahili kuaminiwa kweli?
Hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya viongozi wao wakitoka katika vyama hivi na kuenda kujiunga na chama tawala kwa kile kinachoonekana kukosekana kwa demokrasia katika vyama vyao,madaraka ya chama kuhodhiwa na mtu mmoja na ndio mwenye maamuzi ya mwisho.
Lakini kama haitoshi vyama hivi vimekuwa havina sera madhubuti badala yake vinafanya siasa zake kutokana na matukio,,yaani wanasubiri chama tawala kiboronge ndio wao waendani na tukio hilo,,kibaya zaidi chama tawala kwasasa kinakidhi mahitaji ya wananchi kwasasa kwa kuweka miundo mbinu rafiki katika nyanja zote kuhakikisha wananchi wanajikwamua katika umaskini
Natambua bado kuna mambo hayajakaa sawa katika namna ya kuwaridhisha wananchi lakini walau kuna matumaini huko mbeleni mambo yatakuwa sawa,,kwani nia wanayo na lengo lao ni kuwafanya watanzani wafikie mahali wajivunie matunda ya nchi hii.
Ni mategemeo yangu kwamba chama cha Mapinduzi kina dhamira kubwa ya kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kuifanya iwe nchi ya maziwa na asali
Ni hayo tu!