kapotolo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2010
- 3,727
- 2,214
Yule Rais tuliyemchagua kwa kishindo mwaka 2005 amepotea, Rais tuliyemtegemea - aboreshe uchumi na kuondoa umasikini, aongeze nidhamu kwa watendaji serikali, apambane na Rushwa, aboreshe huduma za jamii kama afya na elimu, akuze demokrasia nchini - hayupo tena.
Huyu tulienae
Baada ya kushindwa yote haya, sasa atoke vipi?
Rais wetu tafadhali sana, hatukuchagua kwa ajili ya kuhudhuria misiba na uzinduzi au safari, tulikuchagua kwa ajili ya mambo hayo matano juu. Utamaliza muda wako, utaondoka lakini ujue kama si sheria kukuhukumu basi historia itafanya hivyo.
Huyu tulienae
[*=1]Ameshindwa kukuza uchumi na kuondoa umasikini - angalia mfumuko wa bei, angalia thamani ya shilingi inavyoporomoka, angalia deni la taifa linavyoongezeka, angalia jinsi idadi ya masikini inavyokua kwa kasi. n.
[*=1]Ameshindwa kusimamia nidhani kwa watendaji wake - kila mtu serikalini anafanya la kwake, hakuna tena utendaji wa pamoja, malumbano kati ya mawaziri achia mbali huko kwenye chama chao yeye akiwa mwenyekiti, kila mmoja ni chukua chako mapema, uwajibikaji haupo tena.
[*=1]Ameshindwa kupambana na rushwa - hapa ndio ameshindwa kabisa, na anakuja hadharani kwa jinsi asivyo na aibu na kuanza kutetea wala rushwa, mara Richmond ni ajali ya kisiasa, mara hakuna rushwa kwenye sakata la rada, simama barabarani uone polisi wanavyofanya rushwa kama haki yao, nenda mahakamani, nenda mahospitalini utalia jinsi rushwa ilivyohallalishwa,ameunda Takukuru isiyo na meno au iliyo na meno ya mtoto kung'ata vidagaa na kushindwa kuuma mapapa.
[*=1]Ameshindwa kuporesha huduma za msingi za jamii - kipindi chake kimeshuhudia kuporomoka vibaya kwa kiwango cha elimu cha ngazi zote, wanafunzi wakifaulu darasa la saba bila kujua kusoma wala kuandika, sekondari ni wizi wa mitihani ndio order of the day, vyuo vikuu imekuwa ni uchakachuzi na madesa, sijui tunakwenda wapi. Afya ndio usiseme, watanzania wengi wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kirahisi, hakuna vifaa tiba wala madawa kwenye vituo vya afya, wataalamu hawapo, kama wapo hawana ari ya kufanya kazi kwa ujira duni, watanzania wakimbilie wapi? Kipindi chake kimeshuhudia migawo ya umeme ambayo haijawahi kutokea toka nchi hii ipate uhuru.nk.
[*=1]Demokrasia ndio imemshinda kabisa - angalia jinsi anavyofanya hila za kunyima watu uhuru wa kufanya siasa, ameamua badala ya kushindana kwa sera, sasa ni kushindana kwa ubavu wa nani ana majeshi, ameamua kunyima watu uhuru wa kupata habari kwa kufungia vyombo vya habari vinayoibua madudu ya serikali na kufikia hata kuua waandishi wa habari wanaohoji mwenendo mbaya wa ukosefu wa demokrasia nchini, ameamua kutumia vyombo vya habari vya umma kama TBC kuendesha propaganda chafu dhidi ya vyama vya upinzani vyenye nguvu.
Baada ya kushindwa yote haya, sasa atoke vipi?
[*=1]Ameamua kutoka kwa staili ya uzinduzi wa majengo, nyumba za kulala wageni (labda hotels - Arusha nakumbuka), vyuo nk., kazi ambayo ilikuwa ya Makamu wake ambaye hatujui wajibu wake hasa ni nini, lakini tulidhani hii ndio kazi yake.
[*=1]Pia ameamua atoke kwa staili ya kuhudhuria misiba popote pale itakapotokea duniani.
[*=1]Na pia anatoka kwa staili ya Vasco da Gama, hii haihitaji maelezo.
Rais wetu tafadhali sana, hatukuchagua kwa ajili ya kuhudhuria misiba na uzinduzi au safari, tulikuchagua kwa ajili ya mambo hayo matano juu. Utamaliza muda wako, utaondoka lakini ujue kama si sheria kukuhukumu basi historia itafanya hivyo.