Waziri Stergomena Tax ashiriki hafla ya uzinduzi wa boti ya doria katika bahari na maziwa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
829
524
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA ASHIRIKI HAFLA YA UZINDUZI WA BOTI YA DORIA KATIKA BAHARI NA MAZIWA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax, April 21, 2024 ameshiriki katika halfa ya Uzinduzi wa boti ya kisasa ya doria katika bahari na maziwa makuu Tanzania uliofanyika katika Bandari ya Dar - es - Salaam, ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi na makabidhiano ya boti hiyo alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Boti hiyo ya kisasa ya doria itasaidia kuongeza mapambano dhidi vitendo vya kihalifu vinavyofanyika katika bahari ya Tanzania, na itakuwa uwezo wa kudhibiti wa matukio ya uvunjifu wa usalama yanayofanyika majini Tanzania. Boti hiyo itakuwa pia na uwezo wa kutoa msaada pindi kutakapotokea maafa ya mafuriko, mapambano dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya, kufanya doria za mara kwa mara katika bahari ya Tanzania na maziwa makuu. Aidha uwepo wa boti hiyo ya kisasa ya doria majini, itasaidia katika operesheni mbalimbali za kuokoa maisha ya watu na kutumika katika uokoaji wakati wa ajali za majini na kuzima moto.

Hafla hiyo ya uzinduzi na makabidhiano ya boti hiyo ya doria ya kuzuia uhalifu wa majini ilihudhuriwa na viongozi kadhaa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na Balozi wa Japani nchini Tanzania, Yasushi Misawa, na Mwakilishi mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Bw. Shigeki Komatsubara.
 

Attachments

 • IMG-20240422-WA0032.jpg
  IMG-20240422-WA0032.jpg
  362.1 KB · Views: 1
 • IMG-20240422-WA0031.jpg
  IMG-20240422-WA0031.jpg
  362 KB · Views: 1
 • IMG-20240422-WA0029.jpg
  IMG-20240422-WA0029.jpg
  358.3 KB · Views: 2
 • IMG-20240422-WA0030.jpg
  IMG-20240422-WA0030.jpg
  156.2 KB · Views: 1
 • IMG-20240422-WA0026.jpg
  IMG-20240422-WA0026.jpg
  193.6 KB · Views: 1
 • IMG-20240422-WA0027.jpg
  IMG-20240422-WA0027.jpg
  336.1 KB · Views: 1
 • IMG-20240422-WA0028.jpg
  IMG-20240422-WA0028.jpg
  334.3 KB · Views: 1
 • IMG-20240422-WA0025.jpg
  IMG-20240422-WA0025.jpg
  239.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom