Tumebaki na Rais wa Uzinduzi, Safari na Misiba

salute! mkuu njiwa nakubaliana na wewe 100%
Raisi hawezi kufanya hayo yote bila msaada wako! Je wewe umechukuwa hatua gani..? Mfano kupambambana na rushwa je ushawahi kugoma kutoa rushwa!? Traffic amekukamata ushawahi kugoma kutoa kitu kidogo!

JK anaangushwa na watendaji na baadhi ya wananchi ambao wanatumika kisiasa..

Kipindi cha jk madudu mengi yaliofanywa utawala wa nyuma yaliibuliwa na kuwekwa hadharani!

Misiba ya kitaifa! Mlitaka aende nani???!
 
Happy Makuku sijui mabata ni wewe anayepaswa kutumia kichwa badala ya masaburi. Kikwete si rais wako peke yako. Isitoshe issue ya CDM imeingiaje hapa. Nyinyi manepi ya kusafishia uchafu wa mafisadi jaribu kuwa na strategies na ideas zinazoingia akilini badala ya kila kitu kutupia CDM. Sikatai Kikwete anazindua yale yaliyofanywa na chama chake na serikali. Je yanalingana na hadhi yake? Isijekuwa siku moja akakaribishwa kuzindua choo nanyi mshangilie kuwa CCM imefanya mengi. Stop gerrymandering start ruling justly and equitably.
 
naam maafa makubwa kwa miaka 10 ya umri wa taifa na kila mtanzania atakayeimaliza hii 10!yaani kama tunapiga mark time kurudi UJIMA
 
Raisi hawezi kufanya hayo yote bila msaada wako! Je wewe umechukuwa hatua gani..? Mfano kupambambana na rushwa je ushawahi kugoma kutoa rushwa!? Traffic amekukamata ushawahi kugoma kutoa kitu kidogo!

JK anaangushwa na watendaji na baadhi ya wananchi ambao wanatumika kisiasa..

Kipindi cha jk madudu mengi yaliofanywa utawala wa nyuma yaliibuliwa na kuwekwa hadharani!

Misiba ya kitaifa! Mlitaka aende nani???!

Chini ya utawala wa huyu rais huwezi kumkatalia police mdai rushwa au kutoa taarifa za ufisadi/wizi/rushwa kunako husika na ukabaki salama, unaweza kuokotwa kwenye mtalo nusu mfu au kama unabahati utatekwa nyara na familia yako itadaiwa kulipa hela za kukugombolea. huyu raisi wa sasa ni maafa ya kitaifa
 
Big up JK, kama nchi imekushinda kwa nini usitulie ule nchi, taliii mwaya miaka 3 ni muda mfupi sana..!
 
Kikwete akibaki ndani ikulu utaongezwa mshahara?paye itapungua?akienda asiende kila mtu na staili yake ya maisha as long as ni rais wetu.b concernd na maisha yako ya familia yako,au unataka kikwete akuletee gari?hakuna serikali duniani inayomsaidia mtu afanikiwe if ur waiting for that am sorry ur in a wrong place.nakumbuka sunday school tulikuwa tunaimba kila mtu atabeba msalaba wake ....wako unataka umbebeshe kikwete,,mbona watoto wako nao wanakulalamikia oohh baba cku hizi atulii nyumbani?kwa nini hutulii nyumbani?oohh huna ela..sawa na presida nae ndo ivo kama wewe unavyowafanyia ktk familia yako kurudi watoto wamelala
ndio uwezo wako wa kufikiri unaanzia hapo au ndo unaishia hapo?Rais ndiye anayetakiwa kujua nakupanga safu nzuri itakayowasaidia wananchi wake kujikwamua kiuchumi kwa kupanga mikakati mizuri ya kukuza uchumi na kuboresha maisha yao.lakini kama bado anasimamia kodi za bia na vileo wakati mashimo ya dhahabu ni makubwa kama kreta ya ngorongoro na hali ya maisha ni ngumu hafai.wenzetu wenye raslimali kama hizi ghana ,botswana ,namibia wamepiga hatua kusimamia uzalishaji wa madini .sisi tunampa waziri jukumu la kusaini mikataba.na amesafiri kuliko rais yeyote duniani,je unahitaji kuambiwa kuwa hafai wewe huoni.Acha hizo ndugu yangu,ukweli utakuweka huru.Au ulipata 10% ya kupandisha twiga kwenye ndege?
 
Kikwete akibaki ndani ikulu utaongezwa mshahara?paye itapungua?akienda asiende kila mtu na staili yake ya maisha as long as ni rais wetu.b concernd na maisha yako ya familia yako,au unataka kikwete akuletee gari?hakuna serikali duniani inayomsaidia mtu afanikiwe if ur waiting for that am sorry ur in a wrong place.nakumbuka sunday school tulikuwa tunaimba kila mtu atabeba msalaba wake ....wako unataka umbebeshe kikwete,,mbona watoto wako nao wanakulalamikia oohh baba cku hizi atulii nyumbani?kwa nini hutulii nyumbani?oohh huna ela..sawa na presida nae ndo ivo kama wewe unavyowafanyia ktk familia yako kurudi watoto wamelala

Chimbuvu: Mleta mada alikuwa anatoa mtazamo wake kuhusu a national figure (Mr. President) na akilinganisha ahadi alizotoa na jisji ambavyo hazijatimia. Hili kila mtu hata wewe unaliona. Sasa kuhusu maisha ya kapotolo na familia yake unayajuaje hadi kuyaweka hapa JF ilhali yeye si nationall figure in any sense? Kwa wana JF wengi tunahitaji nguvu ya hoja ili tujiongezee maarifa na si kushambuliana kwa mtazamo binafsi.
 
"William B. Mkapa, Jakaya
M. Kikwete, Nazir Karamagi, Andrew
Chenge, Yusuf Makamba, Edward
Lowassa, Rostam Aziz, Yusuf Manji,
Ridhiwani Kikwete, Mohamed Dewji,
Bernard Membe, Paul Chagonja , Zitto
Kabwe, Said Mwema, Abdulrahman
Shimbo, Edward Hosea, Daudi T.S Balali,
Basil Mramba, Mustapha Mkullo, January
Makamba, Abdalla Kighoda, Nimrod
Mkono, Grey Mgonja, Patrick
Rutabanzibwa, Tanil Somaiya, Jeetu
Patel, Onoko Okesukwu, Awadh
MohamedSubhash Patel pamoja na
Reginald Mengi.
 
"William B. Mkapa, Jakaya M. Kikwete, Nazir Karamagi, Andrew Chenge, Yusuf Makamba, Edward Lowassa, Rostam Aziz, Yusuf Manji, Ridhiwani Kikwete, Mohamed Dewji, Bernard Membe, Paul Chagonja , Zitto
Kabwe, Said Mwema, Abdulrahman Shimbo, Edward Hosea, Daudi T.S Balali, Basil Mramba, Mustapha Mkullo, January
Makamba, Abdalla Kighoda, Nimrod Mkono, Grey Mgonja, Patrick Rutabanzibwa, Tanil Somaiya, Jeetu Patel, Onoko Okesukwu, Awadh MohamedSubhash Patel pamoja na Reginald Mengi.
Mkuu hawa ndio wala nchi au, sijakusoma
 
Niliwahi kumwambia rafiki yangu mmoja kuwa kama ungekuwa uwezo wangu JK angekuwa mjumbe wa nyumba kumi. nadhani kwa uwezo wa huyu jamaa ndiyo kazi anaweza. Mara nyingi huwa simlaumu maana najua tatizo ni uwezo wake mdogo ni bahati mbaya tu kuwa watanzania tunakosa umakini kwenye mambo muhimu. Kitendo tu cha mtu mweledi kupiga kura kwa JK lazima ujiulize na wewe huko sawa kichwani.
 
Uliyoandika ni yale ambayo wengi tunayashuhudia na kuyatafakari mioyoni. Kwa mtazamo wangu naona kama Rais Kikwete ameelemewa na uozo ulioko ndani ya mfumo wa serikali na chama tawala. Mambo mabaya tunayoshuhudia kama vile, rushwa, ufisadi, kutowajibika, wizi wa mali ya umma, uvunjaji wa sheria nk. nk. ni matokeo ya muda mrefu na si wakati wa Rais Kikwete tu. Wana historia watuambie kwa kuangalia utendaji wa mahakama, watumishi wa umma, majeshi na wanasiasa tangu miaka kumi kabla ya kung'atuka Baba wa Taifa! Ubaya hata siku moja hauzai wema na una mwisho. Inawezekana basi mwisho umefikia kilele na kuonekana zaidi na yeye kuwa mhanga wa uovu uliojengeka miaka nenda rudi.
 
Yule Rais tuliyemchagua kwa kishindo mwaka 2005 amepotea, Rais tuliyemtegemea - aboreshe uchumi na kuondoa umasikini, aongeze nidhamu kwa watendaji serikali, apambane na Rushwa, aboreshe huduma za jamii kama afya na elimu, akuze demokrasia nchini - hayupo tena.

Huyu tulienae

  1. [*=1]Ameshindwa kukuza uchumi na kuondoa umasikini - angalia mfumuko wa bei, angalia thamani ya shilingi inavyoporomoka, angalia deni la taifa linavyoongezeka, angalia jinsi idadi ya masikini inavyokua kwa kasi. n.
    [*=1]Ameshindwa kusimamia nidhani kwa watendaji wake - kila mtu serikalini anafanya la kwake, hakuna tena utendaji wa pamoja, malumbano kati ya mawaziri achia mbali huko kwenye chama chao yeye akiwa mwenyekiti, kila mmoja ni chukua chako mapema, uwajibikaji haupo tena.
    [*=1]Ameshindwa kupambana na rushwa - hapa ndio ameshindwa kabisa, na anakuja hadharani kwa jinsi asivyo na aibu na kuanza kutetea wala rushwa, mara Richmond ni ajali ya kisiasa, mara hakuna rushwa kwenye sakata la rada, simama barabarani uone polisi wanavyofanya rushwa kama haki yao, nenda mahakamani, nenda mahospitalini utalia jinsi rushwa ilivyohallalishwa,ameunda Takukuru isiyo na meno au iliyo na meno ya mtoto kung'ata vidagaa na kushindwa kuuma mapapa.
    [*=1]Ameshindwa kuporesha huduma za msingi za jamii - kipindi chake kimeshuhudia kuporomoka vibaya kwa kiwango cha elimu cha ngazi zote, wanafunzi wakifaulu darasa la saba bila kujua kusoma wala kuandika, sekondari ni wizi wa mitihani ndio order of the day, vyuo vikuu imekuwa ni uchakachuzi na madesa, sijui tunakwenda wapi. Afya ndio usiseme, watanzania wengi wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kirahisi, hakuna vifaa tiba wala madawa kwenye vituo vya afya, wataalamu hawapo, kama wapo hawana ari ya kufanya kazi kwa ujira duni, watanzania wakimbilie wapi? Kipindi chake kimeshuhudia migawo ya umeme ambayo haijawahi kutokea toka nchi hii ipate uhuru.nk.
    [*=1]Demokrasia ndio imemshinda kabisa - angalia jinsi anavyofanya hila za kunyima watu uhuru wa kufanya siasa, ameamua badala ya kushindana kwa sera, sasa ni kushindana kwa ubavu wa nani ana majeshi, ameamua kunyima watu uhuru wa kupata habari kwa kufungia vyombo vya habari vinayoibua madudu ya serikali na kufikia hata kuua waandishi wa habari wanaohoji mwenendo mbaya wa ukosefu wa demokrasia nchini, ameamua kutumia vyombo vya habari vya umma kama TBC kuendesha propaganda chafu dhidi ya vyama vya upinzani vyenye nguvu.

Baada ya kushindwa yote haya, sasa atoke vipi?

  • [*=1]Ameamua kutoka kwa staili ya uzinduzi wa majengo, nyumba za kulala wageni (labda hotels - Arusha nakumbuka), vyuo nk., kazi ambayo ilikuwa ya Makamu wake ambaye hatujui wajibu wake hasa ni nini, lakini tulidhani hii ndio kazi yake.
    [*=1]Pia ameamua atoke kwa staili ya kuhudhuria misiba popote pale itakapotokea duniani.
    [*=1]Na pia anatoka kwa staili ya Vasco da Gama, hii haihitaji maelezo.

Rais wetu tafadhali sana, hatukuchagua kwa ajili ya kuhudhuria misiba na uzinduzi au safari, tulikuchagua kwa ajili ya mambo hayo matano juu. Utamaliza muda wako, utaondoka lakini ujue kama si sheria kukuhukumu basi historia itafanya hivyo.



Kama umefanikiwa kuiona ile list ya fedha uswiss usishangae kinachotokea sasa na kinachoendelea.
 
Haswaaa, tena ni baadhi ya misiba! Maana wa Daud Mwangosi aliupotezea!
 
Back
Top Bottom