Tumebaki na Rais wa Uzinduzi, Safari na Misiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumebaki na Rais wa Uzinduzi, Safari na Misiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Sep 15, 2012.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Yule Rais tuliyemchagua kwa kishindo mwaka 2005 amepotea, Rais tuliyemtegemea - aboreshe uchumi na kuondoa umasikini, aongeze nidhamu kwa watendaji serikali, apambane na Rushwa, aboreshe huduma za jamii kama afya na elimu, akuze demokrasia nchini - hayupo tena.

  Huyu tulienae

  1. [*=1]Ameshindwa kukuza uchumi na kuondoa umasikini - angalia mfumuko wa bei, angalia thamani ya shilingi inavyoporomoka, angalia deni la taifa linavyoongezeka, angalia jinsi idadi ya masikini inavyokua kwa kasi. n.
   [*=1]Ameshindwa kusimamia nidhani kwa watendaji wake - kila mtu serikalini anafanya la kwake, hakuna tena utendaji wa pamoja, malumbano kati ya mawaziri achia mbali huko kwenye chama chao yeye akiwa mwenyekiti, kila mmoja ni chukua chako mapema, uwajibikaji haupo tena.
   [*=1]Ameshindwa kupambana na rushwa - hapa ndio ameshindwa kabisa, na anakuja hadharani kwa jinsi asivyo na aibu na kuanza kutetea wala rushwa, mara Richmond ni ajali ya kisiasa, mara hakuna rushwa kwenye sakata la rada, simama barabarani uone polisi wanavyofanya rushwa kama haki yao, nenda mahakamani, nenda mahospitalini utalia jinsi rushwa ilivyohallalishwa,ameunda Takukuru isiyo na meno au iliyo na meno ya mtoto kung'ata vidagaa na kushindwa kuuma mapapa.
   [*=1]Ameshindwa kuporesha huduma za msingi za jamii - kipindi chake kimeshuhudia kuporomoka vibaya kwa kiwango cha elimu cha ngazi zote, wanafunzi wakifaulu darasa la saba bila kujua kusoma wala kuandika, sekondari ni wizi wa mitihani ndio order of the day, vyuo vikuu imekuwa ni uchakachuzi na madesa, sijui tunakwenda wapi. Afya ndio usiseme, watanzania wengi wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kirahisi, hakuna vifaa tiba wala madawa kwenye vituo vya afya, wataalamu hawapo, kama wapo hawana ari ya kufanya kazi kwa ujira duni, watanzania wakimbilie wapi? Kipindi chake kimeshuhudia migawo ya umeme ambayo haijawahi kutokea toka nchi hii ipate uhuru.nk.
   [*=1]Demokrasia ndio imemshinda kabisa - angalia jinsi anavyofanya hila za kunyima watu uhuru wa kufanya siasa, ameamua badala ya kushindana kwa sera, sasa ni kushindana kwa ubavu wa nani ana majeshi, ameamua kunyima watu uhuru wa kupata habari kwa kufungia vyombo vya habari vinayoibua madudu ya serikali na kufikia hata kuua waandishi wa habari wanaohoji mwenendo mbaya wa ukosefu wa demokrasia nchini, ameamua kutumia vyombo vya habari vya umma kama TBC kuendesha propaganda chafu dhidi ya vyama vya upinzani vyenye nguvu.

  Baada ya kushindwa yote haya, sasa atoke vipi?

  • [*=1]Ameamua kutoka kwa staili ya uzinduzi wa majengo, nyumba za kulala wageni (labda hotels - Arusha nakumbuka), vyuo nk., kazi ambayo ilikuwa ya Makamu wake ambaye hatujui wajibu wake hasa ni nini, lakini tulidhani hii ndio kazi yake.
   [*=1]Pia ameamua atoke kwa staili ya kuhudhuria misiba popote pale itakapotokea duniani.
   [*=1]Na pia anatoka kwa staili ya Vasco da Gama, hii haihitaji maelezo.

  Rais wetu tafadhali sana, hatukuchagua kwa ajili ya kuhudhuria misiba na uzinduzi au safari, tulikuchagua kwa ajili ya mambo hayo matano juu. Utamaliza muda wako, utaondoka lakini ujue kama si sheria kukuhukumu basi historia itafanya hivyo.
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Raisi hawezi kufanya hayo yote bila msaada wako! Je wewe umechukuwa hatua gani..? Mfano kupambambana na rushwa je ushawahi kugoma kutoa rushwa!? Traffic amekukamata ushawahi kugoma kutoa kitu kidogo!

  JK anaangushwa na watendaji na baadhi ya wananchi ambao wanatumika kisiasa..

  Kipindi cha jk madudu mengi yaliofanywa utawala wa nyuma yaliibuliwa na kuwekwa hadharani!

  Misiba ya kitaifa! Mlitaka aende nani???!
   
 3. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Wewe kama mtanzanaia umeifanyia nini nchi yako? Jk kuwa rais wa nchi haimaaniishi wewe kwenda likizo na kuacha kuijenga nchi yako.
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mwanangu umenena vyema. Kikwete hana analojua wala kufanya zaidi ya kusafiri, kuzindua kila upuuzi na kushiriki misiba hata isiyokuwa na umuhimu. He is but a political and historical accident to our country.
   
 5. Chimbuvu

  Chimbuvu JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 4,403
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kikwete akibaki ndani ikulu utaongezwa mshahara?paye itapungua?akienda asiende kila mtu na staili yake ya maisha as long as ni rais wetu.b concernd na maisha yako ya familia yako,au unataka kikwete akuletee gari?hakuna serikali duniani inayomsaidia mtu afanikiwe if ur waiting for that am sorry ur in a wrong place.nakumbuka sunday school tulikuwa tunaimba kila mtu atabeba msalaba wake ....wako unataka umbebeshe kikwete,,mbona watoto wako nao wanakulalamikia oohh baba cku hizi atulii nyumbani?kwa nini hutulii nyumbani?oohh huna ela..sawa na presida nae ndo ivo kama wewe unavyowafanyia ktk familia yako kurudi watoto wamelala
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  So hatuna sababu ya kuwa na rais, is this what u mean? Kwa Kikwete is like hatuna rais. Na unayosema ndio yanayotokea, kila mtu anafanya analoweza
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kama umenipata vyema nazungumzia majukumu ya Rais, mimi nafanya wajibu wangu kama mtanzania, nilotaja ni majukumu yake ambayo ameshindwa kuyafanya
   
 8. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Jk alifaa awe kiongozi wa kidini, ana huruma sana !! He is a ceremonial leader.
   
 9. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Alikuwaje Rais kama hawezi kukuza uchumi na kupambana na Rushwa, anasubiri nini?Alijua urais ni kusafiri

  Kwa nini anawatetea walaji wakubwa wa rushwa? anafikiaje kusema hakuna rushwa kwenye kesi ya rada, wakati kila kitu kiko wazi, au nae alishiriki?
  Ni kwa sababu ameshindwa kusimamia nidhamu ya watendaji wake!

  Amechukua hatua gani kwa hayo madudu? Lakini hata kipindi cha nyuma si alikuweko kwenye serikali alifanya nini kuzuia hayo madudu? Kifupi alinufaika na bado ananufaika na hayo madudu.

  Achague misiba ya kwenda, sio kila msiba yeye, yuko makamu wa rais, waziri mkuu na hata waziri wa mambo ya nje anaweza kumwakilisha. Kwani marais wote huwa wanakuwa kwenye hiyo misiba ya kitaifa.
   
 10. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kitufe cha like kiko wapi?
   
 11. m

  masabo Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 12. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mnyang`anyeni mkasi w kukatia utepe.lol!
   
 13. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Huruma? Kama alivyomuhurumia Babu Seya, sio?

  Ni cold-blood killer/assassin.
   
 14. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Kapotolo,

  Kama uliyoainisha kwa uchache sana hapo juu, ni wazi kuwa JK sio rais na wala hajaitendea haki taasisi hiyo kubwa na muhimu.

  Hasara ya udhaifu wake tunalipa sisi wananchi, kila siku na popote tulipo ndani ya JMT. Ameshindwa jumla, he's a proper and complete failure!

  Muda huu ni vema Watanzania tukajipanga kuanza maisha upya kabisa akiondoka. Inaweza kuwa mwaka huu, mwakani au 2015 lakini tunayo kazi kubwa sana ya kujijenga kama nchi.

  JK ameshindwa hata kwenye vitu basic kabisa kama teuzi. Hivi hao watendaji ambao vipofu na mashabiki wake sikuzote hudai eti ndio wanaomwangusha je nani aliyewachagua? Si ni yeye na prince Riz ndio wanaowachagua, sasa iweje asibebe mzigo wa uwajibikaji kwa utendaji mbovu?
   
 15. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,381
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Huruma gani mbona hata ubani kwa Mwangosi hakutoa wala kusabai familia kama kwa Kanumba???
  Huyu ni Dhaifu tu.
   
 16. mukizahp2

  mukizahp2 JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 635
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  jk aombe kuwa mufti mpya,hiyo kazi itamfaa sana lakini sio uraisi,na siku moja yeye na vibaraka wake tutawaburuza mahakamani kwa mauaji ya watanzania wasio na hatia ,one day hata kama ni miaka 50 ijayo
   
 17. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Mimi naona JK tunamuonea maana kinachotuumiza ni mfumo wa serikali yetu ambao unazidi kutuletea umaskini. Tuanze kuiondoa CCM madarakani tuanze kutengeneza nchi upya, mfumo usukwe upya. 2015 tuseme basi na kauli mbiu iwe hivi ''Change we need''
   
 18. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Inviroment is not condusive to make me do something for my country.
  Please dont be diplomatic fool!!!!
   
 19. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Kati ya vitu vinavyoniudhi hii ni namba moja. Kama watendaji wanamwangusha amechukua hatua gani? Yeye ndie aliwateua hao wabovu lakini ajabu hajapata kufukuza hata Mtendaji wa Kata tu. Miaka 10 nchi haina Rais, Makamu wa Rais wala Waziri Mkuu. Wanaosikika ni Magufuli na Mwakyembe basi na yule Sitta anayewapiga vijembe wenzake. President yuko likizo ya Uzeeni (kama ipo)
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wewe huja jua kipaji cha Kikwete alipaswa awe promoter au afisa michezo kule Gamboshi...
   
Loading...