Tume ya mabadiliko ya katiba


Ndyali,

Nafikiri hunijui mie muulize Joka Kuu atakuambia mie ni liberalist na ada ya maliberali kutetea haki ya mtu hata kama chungu vipi. Napigilia misumari kote na simfagilii mtu. Ngoja nikuambie hicho unachokifikiria ndio udini wenyewe why???

Ukishaanza kugeneralize kuwa waislamu ni fundamentalist utashangaa ukija kuona mafundamentalist wakristo vile vile. I strongly support Tanzania kujiunga na OIC kwasababu kuna more benefits to us kuliko hoja yenu dhaifu iliyojaa udini. Ndio maana niliwashinda hoja kule kwenye topic ya mahakama ya kadhi na OIC kwasababu hakuna hoja ya maana msomi yeyote anaweza kushawishiwa na nyie.

Hoja ya mtei haina nia dhati ya kujenga umoja bali inataka kuleta ubaguzi wa kidini nchini. Kama angelikuwa anataka kuleta umoja tunatakiwa kuwaamini waliopewa dhamana hiyo wafanye kazi na sio kuangalia kwa jicho la imani zao. Choko choko zinaanzishwa na watu wenye mtizamo hasi dhidi ya watu wa dini nyengine kwa kuwa wanawafikiria mambo mabaya tu wakati uislamu na waislamu ni vitu viwili tofauti!!! Uislamu ni dini na waislamu ni watu.
 
Bwana mdogo Pasco, ningekuwa karibu na wewe ningekunasa kibao, huna nidhamu hata kidogo wewe. Maana yake nini unapoanza kusema :

(1) Baba umeanza kuzeeka! Je, unataka kumaanisha nini hapo? Unataka kusema mzee Mtei sasa ameanza kupungukiwa na ufahamu? Akili? Haki ya kutoa mawazo yake? Heshima yake? Uraia wake?
(2) Wewe umesoma na mtoto wa Mtei.. kwahiyo hujuwi kwamba mzee Mtei ni mzee? Ya nini sasa kutangaza uzee wake wakati unajuwa fika kuwa yeye ni baba yako kwa mujibu wa maelezo yako? Huu ni utovu wa nidhamu Pasco. Hakika yake ningekunasa kibao Pasco…
(3) Umeendelea kumwandama kwa kumkumbusha .."kijanawako Tundu Lisu"..Je, wewe si kijana wake kumbe? Wewe ni kijana wa nani sasa? Sasa ya nini kurudiarudia kumwandama "baba yako"? …Ningekuzaba kibao..
Next time jifunze adabu, leo nakuonya tu kama kaka yako..uwe na nidhamu kijana Pasco

Mawazo yangu:
Hoja ya mzee Mtei si hoja dhaifu. Ni hoja muhimu sana kwa kila mtu, hasa wazee kama yeye, wanapojaribu kutafakari mstakabali wa hali ya nchi yetu katika siku za usoni. Wanaangalia viashiria mbalimbali katika kutafakari mambo yanavyoendelea katika siasa, uchumi na utamaduni wa taifa.

Wazee ni manabii wa taifa. Wamepewa umri huo ili kutahadharisha, kuonya na kufunda vizazi vipya. Tukianza kuwa-Pasco wazee hawa ni maafa ya taifa zima. Tusipuuze wasiwasi wa mzee Mtei.

Tukumbuke kuwa:

(1) Zanzibar imekuwa sehemu ya matatizo ya Katiba yetu pale walipoamua kurekebisha katiba yao kwa kuvuruga katiba ya Muungano
(2) Zanzibar wamejitambulisha kama nchi yenye mipaka yake wakati wakingali ndani ya Muungano
(3) Zanzibar wamekuwa na madai mengi yakiwemo ya kujitenga katika matumizi ya raslimali zao eg mafuta ya Zanzibar, kujiunga na OIC, uwezo wa kujiamulia mambo yao, wimbo wa taifa lao, bendera yao, kuwakilishwa katika UN kama nchi huru, kuwa na uwakilishi wa nchi katika EAC.. na kadhalika.

1] Je, kwa mtiririko huo huoni kuwa tatizo lipo upande wa Bara, kwa maana kuwa Katiba ya Muungano ni Katiba ya Bara, wakati huo ikitumika kuwabeba na wa-Zanzibar ?
2] Wa-Zanzibar ni 3% ya population ya Tanzania. Kwanini wapewe nguvu ya 50% katika Kamati ya Katiba yenye maslahi ya 97% ya watu wa-Bara?

Hapo haikuhitajika sharia bali hekima zaidi. Zingatia kuwa Zanzibar hawakuhitaji sharia kufanya mabadiliko ya katiba yao bali hekima yao na mabavutu.

Hoja ya pili, kuhusu dini, kweli hoja hii ni hatari. Lakini, kila mtu mwenye kumbukumbu na ufahamu hataacha kuzingatia kuwa, wa-Islam wamekuwa na madai mengi . Baadhi yake ni

(1) Kuwa na Mahakama ya Kadhi inayotambuliwa kisheria na ki-Katiba.
(2) Zamu katika uongozi wa ki-taifa, yaani rais mu-Islam akitoka mu-Krsto
(3) Idadi sawa ya viongozi wa ki-taifa, yaani mawaziri na viongozi waandamizi wa mashirika ya umma..nk

Kutokana na mambo hayo, baadhi ya watu wanaanza kuwa na wasiwasi na ratio ya wa-Islam katika Kamati ya Katiba. Katika Kamati hiyo utakuta kuwa wa-Islam ni 64%. Ratio hiyo inawapa uwezo wa ku=influence mawazo na utendaji kazi wa Kamati ya Katiba. Na mimi sioni kwa nini wasifanye hivyo kwa sababu ya historia iliyopo ya madai yao.

Hivyo mzee Mtei hana kosa kuwa na wasiwasi huo. Yeye katoa mawazo yake kama miongoni mwa wazee wa taifa hili. Hastahili kupuuzwa na kuambiwa nyamaza wewe "umezeeka"!

Mwisho mimi napendekeza kuwa..
[1] Tuvunje kwanza Muungano
[2] Tufufue taifa la Tanganyika na Katiba yake
[3] Tuziulize hizi nchi mbili kama zinataka kuungana ama kukutana katika Shirikisho la East Afrika

Naitwa Sungura na bahati mbaya sijuwi sharia kabisa …
 
Kwani katiba mpya ni ya Tanganyika ama ya Zanzibar?
Kuna ujinga mkubwa sana unaendelea na umekuwa ukiendelea kwa muda miongoni mwetu, huu ni wakati wa kuufutilia mbali once and for all!

Tunatafuta katiba ya Tanzania nimekutajia Tanganyika ili nieleweke vizuri basi ngoja nikutajie Tanzania Bara kuna Watanzania bara wanalalamika kuwa tume ya mabadiliko ya katiba imewapendelea Wakiristo.

Katika tume hiyo Wakiristo 11 Waislam 4 tu. Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba na msaidizi wake Jaji A. Ramadhan wote Wakiristo.

Mzee Mtei, kasema tume imejaa Waislam wengi kawatambua kwa majina yao lakini upande wa pili anasema kuna Wakiristo na wengine hawana dini sijui kajuaje.

Mie naongea kama Mtazania bara kuwa tume yetu imejaa Wakirsto wengi.
 

Mdondoaji,

..nijibu hoja yangu kama kweli unaamini Zanzibar hakuna Wakristo 7 wenye sifa za kuwa kwenye Tume ya Katiba.

..Zaidi nieleze kama huku Tanganyika u dont know of 4 more Muslimu who r qualified kuwa kwenye Tume ya Katiba.

..hizi ni nafasi za UTEUZI siyo kama wahusika wameomba wenyewe, au ni nafasi zinazohitaji mhusika awe ameanzia kwenye entry level.

..nimeyaona makosa ya Mzee Mtei, lakini nadhani kuna unafiki mkubwa sana miongoni mwa wale wanaomkosoa.
 

Nilikuwa nimekusudia kuwa mtazamaji lakini umenilazimisha kuingia uwanjani.

Ulichoandika hapa ni very low and out of context. Assuming kwamba ni kweli uliyoandika, lakini ukumbuke kwamba chadema wana utaratibu wao wa kufanya uteuzi wa mgombea wao wa uraisi.

Jaji waryoba na dr salim hawawezi kufanya maamuzi kwa niaba ya chadema.
 

Mkuu,

Nilishakujibu kamanda ila pengine hukunisoma. Kigezo cha uteuzi mie naamini ni competence na sio dini ya mtu. Mie ni mtanganyika mbona sijalalamika waislamu tuko kidogo katika composition ya tume ya katiba kutoka bara wakati population ya Tanzania Bara waislamu ni kama 36% ya population? Je unalionaje hilo?

Vile vile Zanzibar kuteuliwa mkristo mmoja vile vile tukiwa tunajadili in terms of demographic kama waislamu ni 99% of the population hata augustion Ramadhani hakutakiwa awepo kwasababu ni almost 100% ya population ya zanzibar ni waislamu. Je nayo waislamu kutoka zanzibar wakihoji uwepo wa Augustion Ramadhani itakuwaje?

Hakuna unafiki but huyu mzee amechemka yeye alitakiwa asupport watu kuteuliwa in terms of competence na sio dini yake kwani tukianza na hayo tutafika mbali ndugu yangu. Ndio nikauliza hoja ya siku nyingi ya waislamu kuwa je ile 70% ya wakristo kuwa wanaongoza serikali imekaaje nijibuni basi!!!
 
Mkuu Ndyali, ni kweli nilijipambanua kuwa mimi ni mnazi mkubwa wa EL, ila unazi wangu unaeleweka na ma great thinkers wa humu.

Bahati mbaya wewe ni miongoni mwa wale wenye uelewa duni kuhusu mchakato wa katiba mpya, ila pia lazima nikiri, sio kosa lako, Watanzania wengi zaidi wanahitaji kuelimishwa kuhusu mchakato huu. Kama CCM haiwezi kutengeneza katiba kwa Watanzania, na kwa mwelekeo ulivyo, Chadema ndio itachukua nchi 2015, jee ungeshauri mchakatoi huu wa katiba mpya tuuahirishe mpaka baada ya 2015 ili Chadema ndio watupatie katiba kwa manufaa ya Watanzania?.
 
mkuu Mwita, hisia zangu tu ndiyo zimekuondoa kutoka kwenye utazamaji wako na kuwa mchangiaji? unaonaje lakini wewe binafsi mlezi wa chama ambacho labda kitakuja kupata dhamana ya kuwaongoza watanzania anapoleta swala la udini?

 
bora muungano uvunjwe maana haki za waislam wa tanganyika zinamezwa sana na wazanzibar ktk mambo mengi yanayohusu serikali ya muungano!!!
 
mkuu Mwita, hisia zangu tu ndiyo zimekuondoa kutoka kwenye utazamaji wako na kuwa mchangiaji? unaonaje lakini wewe binafsi mlezi wa chama ambacho labda kitakuja kupata dhamana ya kuwaongoza watanzania anapoleta swala la udini?

Hakika mkuu mtazamo wako ndio umeniingiza uwanjani.

Hii issue ni very tricky, ndio maana niliamua kuwa mtazamaji. Kwa sasahivi sitatoa maoni yoyote juu ya mtazamo wa mzee mtei.
 

JK kaunda tume yenye harufu za udini, ila mtu akihoji anabatizwa kuwa mdini.
 
Hoja yasngu hapa siyo kuongelea ubaguzi wa kidini wala nini ila ni kutazama malengo ya kiudini yaliyojificha humu ndani.nafikirei hapa mahakama ya kadhi nchini tanzania inanukia.

tazama team hii hapa chini

angalizo-mimi nimetazama majina yao kuwapanga kidini.

Hata mtei kaandika hivi "Mfano wa pili ni kwamba, licha ya kwamba Tanzania siyo nchi inayozingatia dini katika maamuzi yake ya kisiasa, ni lazima tukubali kuwa madhehebu ya dini yana influence katika mchakato na hatimaye maamuzi. Nikihesabu Waislamu katika hii Tume kwa kuzingatia majina naona zaidi ya theluthi mbili ni Wao. Wengine ni Wakristo au watu wasiokuwa na dini yoyote.
"



wakiristo wapo 11
Waislam wapo 23

WALIOTEUA
1.Rais Kikwete -Mwislam
2.Rais Shein---Mwislam


1. Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA - Mwenyekiti-Mkiristo

2. Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino RAMADHANI - Makamu Mwenyekiti -Mwislam

WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - BARA
1. Prof. Mwesiga L. BAREGU--Mkiristo
2. Nd. Riziki Shahari MNGWALI--Mwislam
3. Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI--Mkiristo
4. Nd. Richard Shadrack LYIMO--Mkiristo
5. Nd. John J. NKOLO--Mkiristo
6. Alhaj Said EL- MAAMRY--Mwislam
7. Nd. Jesca Sydney MKUCHU--Mkiristo
8. Prof. Palamagamba J. KABUDI--Mkiristo
9. Nd. Humphrey POLEPOLE--Mkiristo
10. Nd. Yahya MSULWA--Mwislam

11. Nd. Esther P. MKWIZU--Mkiristo
12. Nd. Maria Malingumu KASHONDA--Mkiristo
13. Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)--Mwislam
14. Nd. Mwantumu Jasmine MALALE--Mwislam
15. Nd. Joseph BUTIKU-Mkiristo

WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - ZANZIBAR
1. Dkt. Salim Ahmed SALIM--Mwislam
2. Nd. Fatma Said ALI=-Mwislam
3. Nd. Omar Sheha MUSSA--Mwislam
4. Mhe. Raya Suleiman HAMAD--Mwislam
5. Nd. Awadh Ali SAID--Mwislam
6. Nd. Ussi Khamis HAJI--Mwislam
7. Nd. Salma MAOULIDI--Mwislam
8. Nd. Nassor Khamis MOHAMMED--Mwislam
9. Nd. Simai Mohamed SAID--Mwislam
10. Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA--Mwislam
11. Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN--Mwislam
12. Nd. Suleiman Omar ALI--Mwislam
13. Nd. Salama Kombo AHMED--Mwislam
14. Nd. Abubakar Mohammed ALI--Mwislam
15. Nd. Ally Abdullah Ally SALEH--Mwislam

UONGOZI WA SEKRETARIETI
1. Nd. Assaa Ahmad RASHID - Katibu --Mwislam
2. Nd. Casmir Sumba KYUKI - Naibu Katibu --Mwislam
 

Umendika mengi lakini mie takujibu yale ya muhimu..

Vyovyote utakavyosema lakini Zanzibar itabaki ni nchi huru, umetoa mifano dhaifu ya asilimia ili kujengo hoja yako lakini hamna kitu.

Udogo wa Zanzibar haifanyi kutokuwa nchi, Vatican City ina wakazi 800 na ina ukubwa wa eneo acres 110 ni nchi sembuse Zanzibar.
 

Aaaaah! Jamani. Mbona unafiki umetujaa hivi? Hapo kwenye red; sijui tafsiri yako ya "mtu" ni ipi ila kama ni ninayoifahamu mimi basi hebu muulize Sheikh Bassaleh na kundi lake, Radio Imaan, na magazeti ya Annuur na Al-Huda.

Yaani mkuu leo unajidai "inakuwaje" mtu anaanza kuhesabu dini fulani ni wangapi? Mbona hayo mambo ni kawaida sana katika jamii yetu na serikali imeyaendekeza yenyewe?
 
mmeanza mambo ya kidini,ulitaka wakiristo wawe wangapi? acheni hizo wewe
 
muungano ukivunjika, Tanganyika nayo igawanywe kwa kufuata dini, wakristo wapotelee bara waislam wabaki pwani, tatizo la hawa wakristo wanasukumwa na udini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…