Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi ya RC Paul Makonda

Samber Junior

Member
Nov 7, 2012
33
13

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Barua Pepe: chragg@chragg.go.tz
Tovuti: www.chragg.go.tz

Agosti 26, 2016​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yanayokiuka misingi ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati wa kuaga miili ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti 26, 2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike makao makuu ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi wa haki za binadamu.

Aidha, Tume imeona kuwa maagizo aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi la Polisi hayana msingi wa kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa Mkoa.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na (i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a) vya Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya Sheria za Tanzania 2002, THBUB ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa mtu au taasisi yoyote kuhusiana na utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka ya madaraka yake, ili kuchukua hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.

Imetolewa na:

(SIGNED)

Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo

Agosti 26, 2016
 
Afutwe tu kazi...ni msiigo mkubwa kwa Dar, jiji ni kubwa kuliko uwezo wake. Jiji sio kukutana na wasanii na kujidai dai clouds.
Maneno alosema ni hatari , na uchochezi mkubwa sana kuliko haya ya Ukuta.
Akili yake anadhani tupo kwenye police state....nadhani hafai
 
Hivi hawa haki za binadamu mbona hawazungumzii kuuwawa kwa hao askari wasiokuwa na hatia basi kama ni hivyo watusaidie waende kule msituni wakawatoe hawa watu wanaoua na kuvunja haki za binadamu wenzao za kuishi na wawapokonye hizo siraha zao
 
1472223783980.jpg
 
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Barua Pepe: chragg@chragg.go.tz
Tovuti: www.chragg.go.tz

Agosti 26, 2016​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yanayokiuka misingi ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati wa kuaga miili ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti 26, 2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike makao makuu ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi wa haki za binadamu.

Aidha, Tume imeona kuwa maagizo aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi la Polisi hayana msingi wa kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa Mkoa.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na (i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a) vya Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya Sheria za Tanzania 2002, THBUB ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa mtu au taasisi yoyote kuhusiana na utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka ya madaraka yake, ili kuchukua hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.

Imetolewa na:

(SIGNED)

Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Agosti 26, 2016
Kwa mtazamo wangu,kauli ya makonder ni muendelezo wa ile kaulu ya "kuwalaza chini" ambayo ilitolewa miez michache nyuma,makonder ameendelezea hapo.Nadhan tume inapaswa kuanza kule nyuma ilipaswa kuikemea ile KAULI ya kuwataka polisi "Kuwalaza chini" watuhumiwa................
 
Back
Top Bottom