Tume ya Haki Jinai: Rais asipoidhinisha Adhabu ya Kifo baada ya Miaka 3, Mfungwa apewe Kifungo cha Maisha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Othman Chande amependekeza kuwa endapo itapita miaka 3 bila Rais kutoa Idhini katika Adhabu ya Kifo, Wafungwa wenye Hukumu hiyo waweze kubadilishiwa adhabu kuwa Kifungo cha Maisha.

Hata hivyo, Tume imesema kuna malalamiko kuhusu Adhabu ya Kifungo cha Maisha kuwa hakitoi nafasi ya Mfungwa kujirekebisha. Hivyo kuna mapendekezo kuwa Kifungo cha Maisha kipewa muda maalumu.

Kuhusu adhabu Kifo amesema Tume imebaini kuna maoni ya Kufutwa adhabu hiyo kwasababu ni ya kikatili na isiyozingatia Haki za Binadamu pamoja, kutotekelezeka kwa muda wa miaka 28 na kuwatia hofu Wafungwa.
 
In my opinion Kifo sio adhabu ni inevitablity na wote tutakufa...; Kwahio hawa watu waliokosa kwa manufaa ya jamii iliyobaki wafungwe maisha yao yote na kupewa suluba ya kazi ngumu na wanachozalisha kije kufidia jamii as a whole ya sisi waliotukosea kitaa...

Yaani kama kuna kazi hatarishi za maisha hawa ndio waende huko; au kuna sayansi tunahitaji specimen na hatuna uhakika kama itafanya kazi hawa ndio wawe guinea pigs (Its the price they have to pay kwa kosa walioitendea jamii) Huku kujidanganya kwamba nimemkomoa mtu kwa kumuua ni kama wewe unamcheka mzee eti amezeeka wakati eventually na wewe ndipo unapoelekea
 
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Othman Chande amependekeza kuwa endapo itapita miaka 3 bila Rais kutoa Idhini katika Adhabu ya Kifo, Wafungwa wenye Hukumu hiyo waweze kubadilishiwa adhabu kuwa Kifungo cha Maisha.

Hata hivyo, Tume imesema kuna malalamiko kuhusu Adhabu ya Kifungo cha Maisha kuwa hakitoi nafasi ya Mfungwa kujirekebisha. Hivyo kuna mapendekezo kuwa Kifungo cha Maisha kipewa muda maalumu.

Kuhusu adhabu Kifo amesema Tume imebaini kuna maoni ya Kufutwa adhabu hiyo kwasababu ni ya kikatili na isiyozingatia Haki za Binadamu pamoja, kutotekelezeka kwa muda wa miaka 28 na kuwatia hofu Wafungwa.
Asipoidhiniaha si atakuwa amevunja katiba aliyoapa kuielinda
 
Inabidi swala la kunyonga liondolewe kwa Rais, liachwe kwa Majaji wa Mahakama kuu maana kama wanatoa hizo adhabu basi wao ndo watekeleze
 
Futa hii death sentence ,haileti tija yeyote, hii adhabu imejionyesha haipunguzi watu kuua, a long sentence in jail ndio njia sahihi, hapa nchini tuna 30 yrs in jail kwa rapists, lakini bado kuna matukio mengi ya rape, hii adhabu haipunguzi matukio haya kutokea hapa nchini, we need to go to drawing board, peleka jela bila kupewa parolee
 
Wauwaji waachie huru tuje kuwashughulikia uraiani
Jitu limeuwa tena kwa kuskusudia lijambazi au limeuwa kisa lipate mirathi au mapenzi halafu mnalihukumu kifo ambacho hakipo

Leta huku tumalizane kijeshi
 
Back
Top Bottom