Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,627
- 146,779
- Thread starter
- #101
Wewe kweli junya.Wewe kweli Nyani
Wewe kweli junya.Wewe kweli Nyani
precisely ngabu...ni ujinga wa kiwango cha phdSasa kama kweli hakuna tume huru, kwa nini wapinzani huwa wanashiriki chaguzi?
Haiingii akilini kabisa.
Yaani mtu unashiriki chaguzi ambazo mwisho wa siku unajua kabisa huwezi kushinda kwa sababu chombo kinachoendesha hizo chaguzi hakipo huru!!
That's lunacy!
Nawaza tu hapa....maana huenda tatizo la wapinzani kushindwa chaguzi ni zaidi ya uwepo au kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.....
Nani amekuambia waafrika hawahitaji utawala wa sheria?Unaleta porojo kwa kisingizio kwamba hii ni Afrika, kwa hio Waafrika hawahitaji utawala wa sheria? Au Waafrika hawahitaji kuheshimiwa maamuzi yao?Tume huru inawezekana sana na mfumo wa tume huru ni kufanywa iwe ni ajira kuliko kupeana maslahi ili alopewa maslahi nae arudishe fadhila, kwa mtindo huu wa kijinga wa kina Magufuli na wahuni wenzake kule Zanzibar iko siku tutazungumza kupitia shaba maana inaonekana wahuni wa ccm ndio lugha wanayoifahamu.
NN, tatizo kubwa siyo uhuru wa tume ya Uchaguzi. Tume yetu ya uchaguzi tangu hata wakati wa chama kimoja ilikuwa ina uhuru mkubwa. Hata hivi sasa bado upo uhuru mkubwa tu ambao unaweza kuwafanya wapinzani washinde. Tatizo kubwa siyo tume; ni sheria ya uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa. Kulalamikia kila wakati tume ya uchaguuzi ni kutokuwa wa kweli tatizo hasa ni nini.
Lakini wa kufanya kazi hiyo ni wana siasa wa upinzani wenyeweMkuu hapa labda nieleze basi hili suala tusiwavike wapinzani. Hili tatizo la watanzania wenyewe .
Wananchi wa Tanzania either bado hawajauamini upinzani au somo la siasa bado halijatuingia vizuri vichwani mwetu.
Wewe ndii usie na hoja unaongea nadharia tuuTume huru ambayo itafanya kazi bila woga wala vitisho kutoka kwa yule anayewateua wajumbe wa Tume hiyo kuanzia Mwenyekiti wa Tume. Kama tunavyojua Jecha alikuwa tayari kutangaza ushindi wa Urais kwa chama cha CUF kule Zanzibar lakini akaingiliwa na Kikwete na katika mazingira ya kutatanisha akashinikizwa afute matokeo yale.
Uchaguzi wa 2015 kama tutakumbuka kura zilikamatwa sehemu mbali mbali nchini zikiwa zote zimeshapigwa kwa Wagombea wa CCM tu lakini cha kushangaza Tume ya uchaguzi haikutia hata neno kuhusu kura zile zilizokamatwa au kuokotwa katika baadhi ya maeneo nchini.
Nimejaribu kuingia kwenye Tume ya uchaguzi kule Gambia kuona Tume yao inapatikana vipi lakini sikuona info zozote zile. Tunaweza kuangalia katika nchi za Afrika ambazo vyama vya upinzani vimewahi kushinda chaguzi mbali mbali kama vile Malawi na Zambia Tume zao za uchaguzi zinapatikana vipi na hivyo kuweza kuwa huru kufanya maamuzi yao ya haki na huru bila ya woga wa kuingiliwa na yoyote yule ukilinganisha na hapa kwetu. Si haki wala si sawa hata kidogo Tume ya uchaguzi wa vyama vingi nchini iteuliwe na Mwenyekiti wa CCM.
Tume hii ya uchaguzi tuliyonayo nchini ni kama kitengo cha MACCM tu, inatumika kuhakikisha wanatumia kila mbinu ili CCM waendelee kung'ang'ania madarakani huku wakisaidiwa na vyombo vya dola. Tume hii ni kikwazo kikubwa sana cha uchaguzi huru na wa haki nchini na kupitia tume hii KAMWE wapinzani hawawezi kushinda urais nchini au viti vingi Bungeni kutokana na njama kubwa zinazofanywa na Tume hii AKA kitengo cha CCM.
Wewe ndii usie na hoja unaongea nadharia tuu
ata hivi sasa bado upo uhuru mkubwa tu ambao unaweza kuwafanya wapinzani washinde.
Tatizo kubwa siyo tume; ni sheria ya uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa. Kulalamikia kila wakati tume ya uchaguuzi ni kutokuwa wa kweli tatizo hasa ni nini.
Mkuu upinzani unakandamizwa na CCM. Tutaongea mengi lakini kama CCM haitaamua Upinzani uingie ikulu ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Mbona hili linasemwa wazi hata na watu wa CCM.Lakini wa kufanya kazi hiyo ni wana siasa wa upinzani wenyewe
Hawawezi kushinda kama sandakalawe , Bali waweke misingi madhubuti ,
Hivi unafikiri mwalimu alipoachia u waziri mkuu na kuzunguka nchi nzima kueneza TANU hasa vijijini hakujua umuhimu wake ,
Upinzani uchukue mazuri ya CCM kuweka miziz ya vijijini na kuongeza mbinu zao ndipo watawrza
Lakini ni ngumu mbowe kaharibu kila kitu , Leo Chadema ina makundi 3
1. Chadema Maslahi - Mbowe na kundi lake
2. Chadema wakuja- Lowasa na kundi lake
3.Chadema Asili- Mnyika ,mdee na kundi lao wengine humu ni kina IDAWA,MTAZAMO n.k
Hapo ndipo chadema ilipo na ndio chama kikuu cha upinzani huku kikiwa na makundi 3 , ni ngumu kuitoa CCM hata tume itoke mbinguni .
Leo hii kundi la 3, chadema asilia limenywea na kimtindo wanamuunga mkono Rais Magufuli , hivyo tukubali ni kazi upinzani kuchukua nchi ,
Cha Msingi wameshakosea na walufanya kosa 2015 ,sasa wajirekebishe na wawe upinzani wa agenda na sio matukio ya chama tawala
Lakini je, wewe binafsi unaona ni sawa kwa marais [ambao wote mpaka hivi sasa wamekuwa ndiyo wenyeviti wa CCM] kuwa ndo wateuzi pekee wa viongozi wa hiyo tume?
Mfumo wetu wa uchaguzi unauhuru mkubwa sana na hata upo uwezekano wa upinzani kushinda nafasi zote. Kudhani kuwa upinzani unashindwa Urais kwa sababu tu ya Tume ya uchaguzi au kwa sababu ya CCM ni kukubali kushindwa kabla ya kuingia uwanjani. Hakuna nafasi iliyokuwa nzuri kama ya upinzani kushinda kama iliyokuwa mwaka jana. Tatizo wao wenyewe wakajivuruga na hadi leo hawataki kukubali walijivuruga. Hata hizi chaguzi za wiki iliyopita watu hawataki kuangalia mikakati na hoja za upinzani zilikuwa nini na kwanini hazikukubaliwa na wananchi. Ni rahisi zaidi kutukana giza kuliko kuwasha taa..Mkuu MMM katika mfumo wa sasa wa tume kujaa wateule wa Rais ,Mwenyekiti wa CCM na wakurugenzi ambao ni makada wa chama tawala kuwa wasimamizi wa chaguzi zinazoendeshwa na Tume...Ni uhuru upi unaouongelea?
Na labda ungefafanua...Tume inatoa uhuru kwa wapinzani kushhinda katika level ipi? Udiwani,Ubunge au Urais?
Nakubaliana na wewe kuwa kuna hilo tatizo lingine...Tatizo sio tume peke yake...Lakini tume ndio tatizo namba moja........
umemaliza maneno yoooote hakuna cha kuongeza hapo*RC kada, RAS kada,DC kada, DAS kada, DED kada, NEC ya kwao!UKAWA mnatwanga maji*
1. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) anateuliwa na rais ambaye kwa upande wa pili wa shilingi rais ni Mwenyekiti wa moja ya Chama kinachoshindana na vyama vingine.
2. Wakurugenzi ambao ni sehemu ya wasimamizi wa Uchaguzi katika maeneo wanayoyasimamia wanateuliwa na rais ambaye kwa upande wa pili wa shilingi ni Mwenyekiti wa moja ya Chama kinachoshindana na vyama vingine.
3. Jeshi la Polisi ambalo linasimamia usalama wa mali na raia katika Chaguzi zote nchini liko chini ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ambao ni wenyekiti wa Kamati ya Usalama wa maeneo (Mkoa & Wilaya) husika. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote wanateuliwa na rais. Ikumbukwe kwamba Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wengi ni makada watiifu wa Chama husika ambacho rais ni mwenyekiti wao.
Je, katika uhalisia kuna yeyote ambaye atakuwa tayari kuona chama cha boss wake aliyemwajiri kikishindwa kirahisi katika uchaguzi?!
Katika aina hii ya mfumo na uongozi hatuoni kama kuna haja kubwa ya kuwa na Katiba mpya itakayotupa Tume Huru ya Uchaguzi sambamba na kupunguza madaraka ya rais?!
Ni dhahiri athari za uteuaji wa makada kwenye nafasi zote za utendaji zimeanza kujitokeza sasa.
Sio siri kwenye uchaguzi huu mdogo wa madiwani na mbunge wa Dimani kila DED alikuwa anahangaika kuhakikisha CCM inashinda, ili kulipa fadhila za uteuzi na kumfurahisha muheshimiwa sana.
Tukumbuke hawa MADED ndo wasimamizi wa uchaguzi kwa level ya kata na jimbo (udiwani na ubunge) na ndo wasimamizi pia wa kura za Raisi. Tangu juzi kwa mfano RC wa mkoa wa Arusha amekuwa akijitapa kuisambaratisha CDM huko Meru.
Katika mazingira kama haya ambapo RC kada, RAS kada,DC kada, DAS kada, DED kada, NEC ya kwao!UKAWA mnatwanga maji tu.
Anzeni na katiba mpya itakayozaa Tume mpya na huru ya uchaguzi.
Tz ya viwanda
ni ushauri mzuri sana, kwamazingira kama haya ambapo kila wilaya wamerundikwa makada na ndo wasimamia uchaguzi UKAWA kweli mnatwanga maji
Kinachonichanganya ni pale watu na 'utimamu' wao wanapoamua na kuhakikisha kuwa ni lazima mtu au chama fulani ndicho kishinde regardless matakwa ya wapiga kura! Na hilo swali ukienda mbali zaidi unawaona wabunge wa Gambia wakipitisha kwa kauli moja 'nyongeza' ya miezi mitatu kwa Yahya Jammeh. Ndipo unakuwa na mashaka na mtu mweusi!
It is very true.
It is next to impossible kwa mfumo uliopo nchini wa makada watupu wa Chama tawala kuwekwa kwenye zile posts zote zinazoamua washindi kwenye chaguzi mbalimbali hapa nchini, kutegemea upinzani uibuke washindi!
Hata ikitokea mpinzani amepata asilimia 80 ya kura, Usishangae kura hizo 'zikapinduliwa' na mpinzani akapewa asilimia 20 na mgombea wa Chama tawala 'akawezeshwa' na kupewa hizo asilimia 80!,
Huru, haki na halali! Haijawahi kuwepo Tanzania!
Katika mazingira ambayo wamezuiwa kufanya mikutano ya kisiasa, na kuzimiwa bunge live! ni hatari sana
Naunga mkono hoja.
*****TUME HURU NI LAZIMA****
hakuna hata nchi moja ya afrika yenye mfumo kama Tanzani isipokuwa Zimbabwe tuSafii sana ,hii ni kwa siasa za Tanzania ,je unaweza kutusaidia mfano ya Gambia , Zambia , n.k ambako vyama tawala vilitolewa madarakani na Wananchi??
Je Kenya ambapo NARC ilishinda je tatizo ilikuwa tume na je mfumo wa upatikanaji wa wajumbe wa tume ilikuwaje ??
Je ulikuwa tofauti na Tanzania???
Msaada tafadhali
mzee umesahu ZanzibarMimi bado naamini kuwa kama wapiga kura wengi kupita kawaida wakipiga kura nyingi dhidi ya CCM, basi hata CCM yenyewe itaona haya kuchakachua matokeo.
Ila kwa sasa hilo sioni likitokea kwani CCM bado ina wafuasi wengi nadhani kushinda chama kingine chochote kile.
bila mapanga musitegemee chochote cha maana ni CCM mpaka kiamaTume huru ni kwamba wahusika wanapaswa kuomba kazi sifa kutokuwa mwanachama wa chama chochote na jaji mstaafu baada ya hapo kamati inayompitisha ni kamati ya wajumbe kutoka vyama vyote vyenye usajili kama sikosei baada ya kupendekezwa ndipo rais anapelekewa jina kulitangaza katika wajumbe sijui idadi kila chama husika kitateua wajumbe wawakilishi sasa kila wilaya pia inatakiwa kuwe na wasimamizi wa tume walioajiriwa kwa kuomba kazi siyo wateule wa raisi kama ilivyo sasa wakurugenzi makada wa ccm ndiyo wasimamizi wa uchaguzi hata hiyo 2020 hatutakatiza kama mfumo utakuwa haujabadilika