Tume huru ya uchaguzi

Tume huru ya uchaguzi

Tume huru ni kwamba wahusika wanapaswa kuomba kazi sifa kutokuwa mwanachama wa chama chochote na jaji mstaafu baada ya hapo kamati inayompitisha ni kamati ya wajumbe kutoka vyama vyote vyenye usajili kama sikosei baada ya kupendekezwa ndipo rais anapelekewa jina kulitangaza katika wajumbe sijui idadi kila chama husika kitateua wajumbe wawakilishi sasa kila wilaya pia inatakiwa kuwe na wasimamizi wa tume walioajiriwa kwa kuomba kazi siyo wateule wa raisi kama ilivyo sasa wakurugenzi makada wa ccm ndiyo wasimamizi wa uchaguzi hata hiyo 2020 hatutakatiza kama mfumo utakuwa haujabadilika
 
Mkuu umeleta mjadala mzuri sana

Naamini ndugu zetu kina Nguruvi3 na The Boss watatoa mawazo yao pia.

Muundo wa tume ambayo ni huru ni ile ambayo wadau wa chaguzi watakuwa wanakubaliana nayo kimuundo kwamba ni muundo sahihi unaoweza kutoa haki kwa pande zote..Muundo wenyewe upate ridhaa ya wadau wote.

Kuna watu wanapendekeza tume iwe na wawakilishi wa vyama vya siasa na makundi mengine ya jamii....Watendaji wakuu wa tume wasipatikane kwa kuteuliwa ..Wapitishwe katika usaili ambao pia utaridhiwa na 2/3 ya wabunge wa kila kambi Pale Bungeni.

Rais au awaye yote asiwe na mamlaka ya kuwawajibisha watendaji wakuu wa tume.Bunge na mahakama viwe ni vyombo vya kimaadili pale inapotokea wanavuruga.


Kuwe na mfumo imara wa kitaasisi utakaowafanya wawe huru katika maamuzi yao...Bajeti yao isichezewe na Executive ilazimishwe kupeleka pesa hizo kadri ilivyopangwa...

Kuhusu kwamba kila mtendaji anaweza kuwa na political affiliation yake..hilo linaweza kudhibitiwa na code of ethics and conduct
 
Kule Kenya baada ya Raila kushindwa akadai tume haiko huru licha ya yeye mwenyewe kushiriki kikamilifu katika kuiunda.

Hizi siasa bana...hususan hizi za Kiafrika ni za ajabu kweli kweli.

Na ndo maana nahisi hata tukija kuipata hiyo tume huru [binafsi sidhani kama hata kuna kitu kama hicho] bado tu watu watahamisha magoli.

Sawa; lakini tuipate kwanza hiyo tume huru halafu ndo tutashuhulika na hilo tatizo unalolifikiria la wanasiasa kuja kuhamisha magoli huko mbeleni.
 
Zanzibar waliunda tume huru iliyoshirikisha vyama vyote vya kisiasa. Kilichotokea kila mtu anayefuatilia masuala ya kisiasa anafahamu.

Kenya waliunda tume huru ya Uchaguzi ikishirikisha wadau wote wa siasa. Kilichotokea kila anayefuatilia masuala ya kisiasa anafahamu.

Nirejee kwenye swali lako, hiyo tume itakuwa huru kiasi gani?

Kumbuka hizi ni siasa za nchi za Afrika.
"Tukumbuke hizi ni siasa za nchi za Africa " una maana gani?
 
Tatizo la Tanzania sio tume huru ya uchaguzi , tatizo hatuna upinzani madhubuti ambao umevaa ngozi ya upinzani na uzalendo yaani mvua inyeshe. Jua liwake

Pia , agenda za maana , yaani wanapenda siasa za matusi na kumsema rais au CCM

Badala waje na siasa za kisasa kitafiti

Mfano unapofanya research lazima uwe na source of problem , then una kuwa na Specific objectives zako , alafu unakuja na Solution ya Problem , na unamaliza na methodology utakayotumia

Sasa wao mwanzo mwisho matusi matusi hakuna mbadala wa jawabu kwamba mkitupa nchi tutafanya hivi kwa kutumia mbinu hizi na mifano mingi

Ila wao ni siasa za mitaroni

Masikini Upinzani Tanzania
Mkuu hapa labda nieleze basi hili suala tusiwavike wapinzani. Hili tatizo la watanzania wenyewe .
Wananchi wa Tanzania either bado hawajauamini upinzani au somo la siasa bado halijatuingia vizuri vichwani mwetu.
 
Kuna jambo watu wengi hasa Waafrika hatulielewi, nalo ni hili, Katiba zote Duniani huundwa kuwanufaisha wale wanaoiunda, na hii ni USA, Ulaya, Ujapani au sijui Ghana, hivyo hata hapa Tanzania hata hiyo inayoitwa Katiba mpya ikiundwa, maadamu CCM ndiyo wako wengi Bungeni hawawezi kupitisha Katiba ambayo haitakuwa upande wao kwa namna moja au nyingine, huo ndiyo ukweli, hivyo ni kupoteza muda tu!

Na mfano mzuri ni Kenya Raila Odinga na wenzake waliipigania sana hii wanaoiita Katiba mpya kwa maana walifikiri kwamba ingeweza kupunguza nguvu ya Wakikuyu na kumuingiza Raila madarakani ikashindikana sasa hivi hawaitaki, na kwa nini? Ni kwa sababu imeshindwa kutimiza lengo, lkn kwa Kenya hili liliwezekana tu kwa sababu Chama cha Odinga kilikuwa na Wabunge wengi Bungeni!

Na ndiyo maana siku zote nasema kama Wapinzani wangekuwa na akili wangepigania kuwa na Wabunge wengi Bungeni, wangeachana uraisi na kuwekeza zaidi huku chini, hiyo ndo game changer lkn hilo haliwezekani kwa maana wanajindanganya kwamba wanashinda Uraisi lkn wanaibiwa kura, hapo sasa kila mtu Kambale!
Barbarosa tangu nikufahamu hapa JF leo umeamua kuongea fact. Nakupongeza kwa hilo mkuu tuwe wakweli siku zote ili kusaidia nchi yetu msema ukweli ni mpenzi wa Mungu
 
Tume haina tatizo , hasa katika mapinduzi ya teknolojia kama haya

Tatizo ni Upinzani wenyewe ,hawajawa tayari kushika dola

Tume hata isipokuwa presidential appointee , bado hao watakaopatikana kwa mfumo wanaoupenda wao bado , elements za uvyama kwa hao members wa tume itakuwamo

Tatizo sio tume
Mkuu kama tume siyo tatizo tujaribu kuwateua makada wa chadema wakina tundu lisu waiongoze tume ya uchaguzi.
 
Tume Huru Ni Dhana Tu Ya Kuukwepa Ukweli Sometimes.

- Siku Zote Kama Tume Haitatangaza Sisi Ndo Tulioshinda Basi Tume Hiyo Siyo Huru Na Haki Haijatendeka, Yaani Tumeibiwa Kura

- Nchi Za Afrika Siku Zote Wapinzani Hawajawahi "Kushindwa" Uchaguzi Bali Wao Huwa Wanaibiwa Tu Kura " Dhana Iliyopo Na Iliyojengwa Na Wapinzani

- Mfano: Hata Kama Tanzania, Mwenyekiti Wa Tume Atakuwa Mbowe, Lowassa Au Mtei Na Akasimamia Uchaguzi Na Mshindi Akawa Siyo CHADEMA Basi Hiyo Tume Siyo Huru
Lakini mkuu kwa siasa za afrika mtu kama Yahya Jammeh juzi anaondoka Banjul na ndege ya mizigo iliyojaa magari ya kifahari na dola zaidi ya milioni 10 zikipotea katika akaunti ya hazina juu ya serikali unataka tusemeje?
Miaka ya nyuma hapa utawala wa JK watu walichota fedha za umma kwenye account ya escrow kwenye mifuko ya sandarusi na hakuna aliyechuka hatua mpaka leo ni history je unaona ni fair?
 
Tume huru ambayo itafanya kazi bila woga wala vitisho kutoka kwa yule anayewateua wajumbe wa Tume hiyo kuanzia Mwenyekiti wa Tume. Kama tunavyojua Jecha alikuwa tayari kutangaza ushindi wa Urais kwa chama cha CUF kule Zanzibar lakini akaingiliwa na Kikwete na katika mazingira ya kutatanisha akashinikizwa afute matokeo yale.

Uchaguzi wa 2015 kama tutakumbuka kura zilikamatwa sehemu mbali mbali nchini zikiwa zote zimeshapigwa kwa Wagombea wa CCM tu lakini cha kushangaza Tume ya uchaguzi haikutia hata neno kuhusu kura zile zilizokamatwa au kuokotwa katika baadhi ya maeneo nchini.
1) Hapo juu kwenye bold, hizi ni tetesi (hearsay), kwakuwa si Jecha wala Kikwete walishathibitisha hilo pamoja na kuongea na vyombo vya habari mara kadhaa tangu uchaguzi.

2) Hapo chini kwenye red, ndipo linakuja suala la umuhimu wa mawakala makini kwenye kila kituo cha kupigia kura. Hivi inawezekanaje kura zilizopigwa nje ya kituo na kutiwa kwenye box lisilo kwenye kituo ziingizwe kwenye hesabu ya kituo wakati mawakala wote wapo.

Mkuu Nyani Ngabu hoja yako ni ya msingi sana. Tume huru ni ipi? Hata ile ya Zanzibar ilirekebishwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015, tena kwa "maridhiano" hata ikabatizwa kwa kauli moja kwamba ni "Tume Huru ya Uchaguzi". Lakini bado iliyoyafanya yalifanyika. Huko Kenya vivyo hivyo waliunda Tume Huru ya Uchaguzi kwa mbinu shirikishi, lakini bado ililalamikiwa na walewale walioshiriki kuiunda. Nina uhakika hata wakiletwa European Union kwenye nafasi hiyo watalalamikiwa tu. Anyway, this is Africa.
 
Kwamfano kwa sasa ukichilia TBC clouds FM ni tawi jingine la CCM unategemea nini general election 2020?
 
Kwa hii tunayoitumia kama mbadala wa katiba inayompa huyu bwana mkubwa madaraka makubwa namna hii, hiyo tume huru labda tuiazime kutoka kanda nyingine ya dunia...
 
Kuna jambo watu wengi hasa Waafrika hatulielewi, nalo ni hili, Katiba zote Duniani huundwa kuwanufaisha wale wanaoiunda, na hii ni USA, Ulaya, Ujapani au sijui Ghana, hivyo hata hapa Tanzania hata hiyo inayoitwa Katiba mpya ikiundwa, maadamu CCM ndiyo wako wengi Bungeni hawawezi kupitisha Katiba ambayo haitakuwa upande wao kwa namna moja au nyingine, huo ndiyo ukweli, hivyo ni kupoteza muda tu!

Na mfano mzuri ni Kenya Raila Odinga na wenzake waliipigania sana hii wanaoiita Katiba mpya kwa maana walifikiri kwamba ingeweza kupunguza nguvu ya Wakikuyu na kumuingiza Raila madarakani ikashindikana sasa hivi hawaitaki, na kwa nini? Ni kwa sababu imeshindwa kutimiza lengo, lkn kwa Kenya hili liliwezekana tu kwa sababu Chama cha Odinga kilikuwa na Wabunge wengi Bungeni!

Na ndiyo maana siku zote nasema kama Wapinzani wangekuwa na akili wangepigania kuwa na Wabunge wengi Bungeni, wangeachana uraisi na kuwekeza zaidi huku chini, hiyo ndo game changer lkn hilo haliwezekani kwa maana wanajindanganya kwamba wanashinda Uraisi lkn wanaibiwa kura, hapo sasa kila mtu Kambale!

Haya ndio maneno ambayo wapinzani hawataki kuyasikia. Ukweli huu ni mchungu lakini dawa. Muda mwingine inashangaza sana kuona watu wenye akili timamu wakidhani wanachama wa CCM tena wabunge wataenda bungeni kutengeneza katiba ya kuwatoa madarakani. Wakifanya hivyo lengo lao litakuwa nini hasa? CCM kuna mtego imeweka nao ni ruzuku ipatiakanayo kutokana na idadi ya kura za urais. Vyama vyetu vya upinzani vimekuwa vikiona huu ni mtaji kwao ndio maana akitokea mgombea mwenye wanaodhani ana mvuto na anaweza kuwapa kura nyingi humpachia bila kujali mipango ya awali ya chama. Wananchi wakipima na wakiwaona wanafanya mchezo hawawapi kura, wakishindwa wanajidai wameibiwa, viongozi wa juu wanafurahi ruzuku imeongezeka. Siasa za ulaghai na ghiliba ndicho kilichobaki
 
Lakini mkuu kwa siasa za afrika mtu kama Yahya Jammeh juzi anaondoka Banjul na ndege ya mizigo iliyojaa magari ya kifahari na dola zaidi ya milioni 10 zikipotea katika akaunti ya hazina juu ya serikali unataka tusemeje?
Miaka ya nyuma hapa utawala wa JK watu walichota fedha za umma kwenye account ya escrow kwenye mifuko ya sandarusi na hakuna aliyechuka hatua mpaka leo ni history je unaona ni fair?
Hoja Yako Nini ?
 
Kwanini ccm,na taasisi za dini hazitaki tume huru ya uchaguzi?wakati ccm ,na taasisi za dini wanajua fika kabisa,wananchi bado wanaimani kubwa sana,na chama tawala ccm?pamoja na maombi yote hayo ya maskofu,wanayoombea taifa viongozi wa dini,na ccm bado wanaogopa tume huru ya uchaguzi tu?
 
Back
Top Bottom