Nonda, tatizo kubwa ni kuwa kwa mfano uchaguzi mkuu wa 2015 upinzani uliweka mkazo mkubwa sana katika Urais kiasi kwamba walipojichoma wenyewe mkuki hawakujua wamejidhuru kiasi gani. Sheria zinabadilishwa Bungeni. NIngekuwa na uwezo ningewaambia sahauni urais kwa sasa wekeni mkazo kwenye Ubunge kwa sababu ni rahisi kushinda Ubunge kuliko Urais. Kumbuka matokeo ya Ubunge yanatangaza pale pale kwenye Halmashauri na mbunge mteule anajulikana. Kama mwaka 2015 wangetusikiliza sisi wengine na wangejipanga vizuri hata 2/3 ya Bunge naamani upinzani ungeweza kuchukua (na hapa namaanisha CHADEMA). Sasa ukishakuwa na wabunge wengi maana yake - unatoa Spika, na unatoa Waziri Mkuu (technically). Na hivyo unaweza kubadilisha sheria ambazo zilikuwa zinakusumbua; Rais anaweza kukataa kwa veto lakini wabunge wenu wanaweza kuoveride veto hiyo au kwenda tena kwenye uchaguzi. Siasa ni mikakati siyo matamanio tu.