Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,490
- 119,355
Kwa muda mrefu sasa baadhi yetu humu tumekuwa tukizungumzia juu ya umuhimu wa uwepo wa tume huru ya uchaguzi.
Hiyo ni kwa sababu hii iliyopo sasa hivi baadhi yetu hatuioni kama ipo huru.
Lakini sina uhakika kama tulio wengi tunajua hata hiyo tume huru inapaswa iweje. Hivi kuna kitu kama tume huru ya uchaguzi kweli? Na ni huru kiasi gani hasa?
Hivi kweli kabisa katika mazingira yaliyopo sasa hivi uwepo wa tume huru ya uchaguzi unawezekana? Hao watu watakaounda hiyo tume huru watatoka wapi?
Na kweli watakuwa huru au watakuwa na upendeleo waliouficha na siku ya siku ikifika ndo wanazionyesha rangi zao za kweli?
Hakuna njia au namna nyingine zaidi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi?
Na tuseme tunaipata hiyo tume 'huru'. CCM ikiendelea kushinda chaguzi kisingizio cha upinzani kushindwa kitakuwa nini?
Kwamba bado hiyo tume 'huru' haipo huru?
Nawaza tu hapa....maana huenda tatizo la wapinzani kushindwa chaguzi ni zaidi ya uwepo au kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.....