Tume huru ya uchaguzi

Tume huru ya uchaguzi

Wewe unaona ni ngojera, Ngojera zetu zilimfanya Kikwete akaunda tume ya Warioba, hatukumshikia bunduki. Unadhani ni kwanini wanataka mashetani kuifunga mitandao!? Unapokubali nchi iwe ya mfumo wa vyama vingi basi iwe ni 100% siyo useme tuna mfumo wa vyama vingi lakini Tume ya kusimamia uchaguzi nitaichagua mimi Mwenyekiti wa CCM. Hilo si sawa na halikubaliki.

Chama pendwa na Watanzania wa kila kona nchini kinahofia nini nchi kuwa na katiba mpya kupitia rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi? Kwanini wakubali mfumo wa vyama vingi nusu nusu na siyo 100%? Mfumo wa vyama vingi lakini Tume ya uchaguzi itachaguliwa na Mwenyekiti wa CCM! Kuna walakini hapa tena si mdogo.

Kwa hiyo wewe utaishia kuimba ngonjera tume siyo huru! Mpaka lini?
 
Mimi naona wananchi wa Tanzania walio wengi hawataki kuchagua vyama vingine. Wanataka CCM. Wakiwa tayari na wakitaka kuchagua chama kingine watafanya hivyo hata tume iweje.

Kuna maeneo ya Tanzania ambayo wananchi wameamua kuchagua vyama vingine pamoja na tume tuliyo nayo na wamefanikiwa.

Kwa hiyo ni suala la muda tu. Wananchi wakitaka chama kingine watakichagua tu.
 
Sahau mambo ya chama kushinda au kutoshinda. Nchi yenye mfumo wa vyama vingi ni LAZIMA iwe na tume huru ya uchaguzi FULL STOP. Huwezi ukasema sisi nchi yeyu ina mfumo wa vyama vingi halafu ukagomea kuwepo kwa Tume huru ya uchaguzi na Mwenyekiti wa chama kimoja kuendelea kuteua wajumbe wa Tume ya kusimamia uchaguzi. Kwanini CCM haitaki uwepo wa Tume huru ya uchaguzi inaogopa nini? Jibu hili swali acha kulikimbia?

Mambo chungu nzima yanatokea wakati wa uchaguzi ambayo yanaonyesha wazi kwamba uchaguzi si huru na wala wa haki lakini hiyo Tume fake haitii neno iko kimyaaa.

Tatizo ni kwamba mnaomba CCM wawakubalie, sasa haijawahi kutokea ktk Historia ya Dunia hii hilo likatokea, kama mnataka kupata mnachokita ni lazima mkilazimishe bila ya hivyo mtasubiri mpaka Yesu arudi!
 
Mimi naona wananchi wa Tanzania walio wengi hawataki kuchagua vyama vingine. Wanataka CCM. Wakiwa tayari na wakitaka kuchagua chama kingine watafanya hivyo hata tume iweje.

Kuna maeneo ya Tanzania ambayo wananchi wameamua kuchagua vyama vingine pamoja na tume tuliyo nayo na wamefanikiwa.

Kwa hiyo ni suala la muda tu. Wananchi wakitaka chama kingine watakichagua tu.
Hapo Umenena, kama na mimi nilivyotangulia kesema post za nyuma. Jambo muhimu sana ni chama kikubalike na kiaminike, mengine yatafuata
 
Mtatiro akipita humu atajifunza Kitu, sio kuweka mabandiko yake ya uongo Facebook kupata like nyingi, na kujiona ameshinda Ubunge
 
Utafiti uliufanya lini na wapi na kufikia hitimisho kwamba chama hakikubaliki? Ulitumia sample ipi? Hii ni dhana yako tu ambayo huwezi kuthibitisha chama hakikubaliki kwa kutumia dhana tu.

Hapo Umenena, kama na mimi nilivyotangulia kesema post za nyuma. Jambo muhimu sana ni chama kikubalike na kiaminike, mengine yatafuata
 
Yote hayo uliyoyaorodhesha yamefanyika nchini Kenya, na bado wale ambao ni Upinzani hawaitaki hiyo Tume unayoiita huru, Raila Odinga ameshasema kwamba hataenda Mahakamani tena kama asiporidhika na matokeo, sasa ataenda wapi?
Umeandika kinadharaia tu yaani jinsi inapaswa kuwa lkn utekelezaji wake ni mgumu sana karibu unaweza kusema kwamba haiwezekani, kwa maana mwisho wa siku ni lazima Binadamu apitishe, labda msubiri artificial intelligence ambapo maamuzi yatakuwa yafanywa na algorithm tu, lkn hata hivyo bado utahitaji binadamu kuiandika hiyo algorithm!!
Wewe maoni yako ni yapi?
 
Kutakuja kutafutwa visingizio vingine kwa mfano BVR inaweza kuja kulaumiwa sana au watu watadai mtandao wa tume huru umeingiliwa kwa kupitia ''safaricom'' akina Vicent nao watadai wana data zao maadamu sababu hazitakosekana ,maana jamaa wa upande ule kazi yao ni kulalamika tu badala ya kumwaga sera,ikifika siku ya kumwaga sera tutaambiwa tukasome sera mitandaoni au tutasubiri watu wamelalal ndio tutaenda kwenye vituo vya runinga kumwaga sera teh teh
 
Kwa muda mrefu sasa baadhi yetu humu tumekuwa tukizungumzia juu ya umuhimu wa uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Hiyo ni kwa sababu hii iliyopo sasa hivi baadhi yetu hatuioni kama ipo huru.
Lakini sina uhakika kama tulio wengi tunajua hata hiyo tume huru inapaswa iweje. Hivi kuna kitu kama tume huru ya uchaguzi kweli? Na ni huru kiasi gani hasa?

Hivi kweli kabisa katika mazingira yaliyopo sasa hivi uwepo wa tume huru ya uchaguzi unawezekana? Hao watu watakaounda hiyo tume huru watatoka wapi?

Na kweli watakuwa huru au watakuwa na upendeleo waliouficha na siku ya siku ikifika ndo wanazionyesha rangi zao za kweli?
Hakuna njia au namna nyingine zaidi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi?

Na tuseme tunaipata hiyo tume 'huru'. CCM ikiendelea kushinda chaguzi kisingizio cha upinzani kushindwa itakuwa nini?
Kwamba bado hiyo tume 'huru' haipo huru?

Nawaza tu hapa....maana huenda tatizo la wapinzani kushindwa chaguzi ni zaidi ya uwepo au kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.....
Tume huru ya uchaguzi peke yake haitasaidia kitu, cha msingi lazima kuwa na uhuru wa vyombo vyote, uhuru wa mahakama, na vyombo vyote vya inforcement viwe huru, kama police, intelligence, TAKUKURU,na usalama wa taifa wawe huru, na bunge liwe pia balanced, yaani hivyo vyombo vya uchunguzi waweze kumhoji yeyeto na kumchukulia sheria yoyote kama ameenda kinyume na katiba ya nchi. Hapa ndio kutakuwa na democrasia, kitu ambacho ni kigumu sana kwa taifa changa kama Tanzania. Sababu watawala ndio wanavitegemea kupindua pindua kila kitu. Mfano ni uchaguzi wa Zanzibari, vyombo vya inforcement ndio vilitumika kudhibiti wapinzani kwa kutenguliwa matokea ya uchaguzi. Hata ikipeleka kesi yako katika ile mahakama ya Afrika mashariki ukashinda, ile hukumu kuitekeleza ni ngumu sababu hawana inforcement tool, labda ile nchi ambayo ina jali sana utawala wa sheria inaweza kuiplement na kutii zile hukumu. Na hiyo sio tu kwa hapo kwetu, sababu nimesomea international business law, hata hapa Europe, European high court haina inforcement force ya kuilazimisha nchi ambayo ni member wake kutii hukumu zake, ila kwa kuwa wenzetu wanajali sana utawala wa sheria na mikakata waliyo ingia huwa wanachukulia kwa uzito hukumu hizo, lakini bado ni shida kwa nchi zile za balkani, yaani East Europe sababu bado zina harufu za ukomunist.
 
Kiuhalisia tume inaweza kuwa isiwe huru lakini ikawa na UTHUBUTU wa kumtangaza mshindi.

Sasa hii kwetu kwanza haiko HURU lakini pia haina UTHUBUTU wa kumtangaza mshindi ambaye hatokani na aliyewateuwa ie Chama Tawala. Refer uchaguzi wa Zanzibar ambapo Jecha badala ya kumtangaza mshindi yeye akaamua kufuta matokeo.

Pamoja na kwamba tume huru ya uchaguzi haiwezi kuwa huru persel kuna elements ya mambo inabidi yafanyike ambayo ndiyo road map ya kuelekea uhuru.

Kwanza tume huru ya uchaguzi isiteuliwe na Mwenyekiti wa Chama ambacho nacho ni mdau katika chaguzi. Itafutwe namna ya kuwapata wajumbe wa tume badala ya kuwa hand picked na mtu mmoja ambaye baadaye atakuja kuwa miongoni mwa wagombeaji.

Pili kama tume itaboronga basi matokeo ya uchaguzi yawe challenged mahakamani.

Lakini kama unafikiri kuna mtawala yoyote anaweza kufanya hivyo bila nguvu ya wananchi then think twice. Kwani kufanya hivyo anajuwa fika kabisa unauweke utawala wake rehani. Kwani amezoea kugombani na mabondia ambao wamefungwa kamba mikono yao kwa nyuma.
 
Ili tume iwe 'huru' ni lazima mgombea wa urais wa upinzani ashinde au?

Na vipi ikitokea tukaipata hiyo tume 'huru' halafu CCM ikaendelea kushinda kwenye chaguzi....hiyo tume itakuwa siyo huru hadi hapo mgombea wa upinzani atakaposhinda?

Just wondering.....
 
Kwa muda mrefu sasa baadhi yetu humu tumekuwa tukizungumzia juu ya umuhimu wa uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Hiyo ni kwa sababu hii iliyopo sasa hivi baadhi yetu hatuioni kama ipo huru.
Lakini sina uhakika kama tulio wengi tunajua hata hiyo tume huru inapaswa iweje. Hivi kuna kitu kama tume huru ya uchaguzi kweli? Na ni huru kiasi gani hasa?

Hivi kweli kabisa katika mazingira yaliyopo sasa hivi uwepo wa tume huru ya uchaguzi unawezekana? Hao watu watakaounda hiyo tume huru watatoka wapi?

Na kweli watakuwa huru au watakuwa na upendeleo waliouficha na siku ya siku ikifika ndo wanazionyesha rangi zao za kweli?
Hakuna njia au namna nyingine zaidi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi?

Na tuseme tunaipata hiyo tume 'huru'. CCM ikiendelea kushinda chaguzi kisingizio cha upinzani kushindwa itakuwa nini?
Kwamba bado hiyo tume 'huru' haipo huru?

Nawaza tu hapa....maana huenda tatizo la wapinzani kushindwa chaguzi ni zaidi ya uwepo au kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.....
Hakuna tume itakayokuwa na uhuru kamili. Cha muhimu ni kujenga utamaduni wa fair play, kukubali matokeo na kufuata sheria.
 
Kwa muda mrefu sasa baadhi yetu humu tumekuwa tukizungumzia juu ya umuhimu wa uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Hiyo ni kwa sababu hii iliyopo sasa hivi baadhi yetu hatuioni kama ipo huru.
Lakini sina uhakika kama tulio wengi tunajua hata hiyo tume huru inapaswa iweje. Hivi kuna kitu kama tume huru ya uchaguzi kweli? Na ni huru kiasi gani hasa?

Hivi kweli kabisa katika mazingira yaliyopo sasa hivi uwepo wa tume huru ya uchaguzi unawezekana? Hao watu watakaounda hiyo tume huru watatoka wapi?

Na kweli watakuwa huru au watakuwa na upendeleo waliouficha na siku ya siku ikifika ndo wanazionyesha rangi zao za kweli?
Hakuna njia au namna nyingine zaidi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi?

Na tuseme tunaipata hiyo tume 'huru'. CCM ikiendelea kushinda chaguzi kisingizio cha upinzani kushindwa itakuwa nini?
Kwamba bado hiyo tume 'huru' haipo huru?

Nawaza tu hapa....maana huenda tatizo la wapinzani kushindwa chaguzi ni zaidi ya uwepo au kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.....
Kama Viongozi wenyewe tunaoletewa tuwapigie kura upande wa Upinzani ni hawa, bora CCM itawale milele. Tume huru itakuwa na manufaa tu kama kuna Viongozi wazuri , wenye nia ya dhati na uchungu na maendeleo ya Nchi. Hawa wa kutaka waende Ikulu kwa manufaa yao na kwa gharama yoyote bora waendelee kukataliwa na wananchi
 
Tatizo la Tanzania sio tume huru ya uchaguzi , tatizo hatuna upinzani madhubuti ambao umevaa ngozi ya upinzani na uzalendo yaani mvua inyeshe. Jua liwake

Pia , agenda za maana , yaani wanapenda siasa za matusi na kumsema rais au CCM

Badala waje na siasa za kisasa kitafiti

Mfano unapofanya research lazima uwe na source of problem , then una kuwa na Specific objectives zako , alafu unakuja na Solution ya Problem , na unamaliza na methodology utakayotumia

Sasa wao mwanzo mwisho matusi matusi hakuna mbadala wa jawabu kwamba mkitupa nchi tutafanya hivi kwa kutumia mbinu hizi na mifano mingi

Ila wao ni siasa za mitaroni

Masikini Upinzani Tanzania
Pamoja na CCM kupigwa chini chaguzi zote za vyama vingi Zanzibar bado tu unamiani upinzani siyo madhubuti? Unaumwa seek medical attention haraka.
 
Ili tume iwe 'huru' ni lazima mgombea wa urais wa upinzani ashinde au?

Na vipi ikitokea tukaipata hiyo tume 'huru' halafu CCM ikaendelea kushinda kwenye chaguzi....hiyo tume itakuwa siyo huru hadi hapo mgombea wa upinzani atakaposhinda?

Just wondering.....
Wewe kweli Nyani
 
Inaonyesha tunaitazama Tume katika level ya Mwenyekiti, makamu na makamishna tuu na kusahau hawa Ma Returning Officers walioenea nchi nzima ambao ni Wakurugenzi wa miji na wilaya. Hawa ndio kiini cha uchaguzi wenyewe na wana impact kubwa katika kushinda au kushindwa. Ni waajiriwa wa serikali kwa kuteuliwa na wengi ni makada wa chama tawala walioteuliwa baada ya kukosa au kushindwa Ubunge kama kipozeo.
Hapo ndio tatizo la tume kutokuwa huru ndio linapo anzia. Iko wazi kuwa majimbo yote ambayo wapinzani wameshinda lazima ni kwa mapambano makali kuhakikisha kura haziibiwi, uhesabuji hauchakachuliwi na wakati mwingine hata kuuumizwa bila msaada wa hao ROs kwani sio kuwa hawako huru bali wapo na assignment maalum 'ushindi' or Out.
Hawa Returning officers wakitengwa na wakurugenzi na kuwa ni ajira inayotangazwa kwa sifa na kufuata mashart ya ajira yanasimamiwa na Tume hakika mabadiliko yataonekana
 
Dhana ya tume huru ni utopia. Hakuna tume ya uchaguzi iliyo huru.

Kila tume katika nchi zina matatizo ya hapa na pale.

Zanzibar waliunda ''tume huru'' iliyoshirikisha vyama vyote vya kisiasa. Kilichotokea kila mtu anayefuatilia masuala ya kisiasa anafahamu.

Kenya waliunda ''tume huru'' ya Uchaguzi ikishirikisha wadau wote wa siasa. Kilichotokea kila anayefuatilia masuala ya kisiasa anafahamu.

Tanzania wapinzani wakishindwa uchaguzi huleta hoja ya tume ya uchaguzi sio huru. Hizi kelele zimeanza mwaka 1995 lakini kinachoshangaza kila uchaguzi wanagombea.

Nirejee kwenye swali lako, hiyo tume itakuwa huru kiasi gani?

Je, wadau wa uchaguzi watakubaliana kubadilisha Katiba ya Tanzania?

Kumbuka hizi ni siasa za nchi za Afrika.
Unaleta porojo kwa kisingizio kwamba hii ni Afrika, kwa hio Waafrika hawahitaji utawala wa sheria? Au Waafrika hawahitaji kuheshimiwa maamuzi yao?Tume huru inawezekana sana na mfumo wa tume huru ni kufanywa iwe ni ajira kuliko kupeana maslahi ili alopewa maslahi nae arudishe fadhila, kwa mtindo huu wa kijinga wa kina Magufuli na wahuni wenzake kule Zanzibar iko siku tutazungumza kupitia shaba maana inaonekana wahuni wa ccm ndio lugha wanayoifahamu.
 
Back
Top Bottom