Tume huru ya uchaguzi

Tume huru ya uchaguzi

Tume huru itapatikana pale mtakapokubaliana hiyo tume iundwe na watu wa EU na US na UN. Ha ha ha ha
Lakini utakapomchagua Mtanzania hakuna tume huru hapo. Otherwise tutakuwa tunajidanganya tu wabongo. Watanzania wako so corrupt, na pia siyo wakweli na pia hawakubaliani hata na uhalisia halisi. Hata ukichagua CCM na CHADEMA namba sawa mmoja akishindwa atarusha ngumi hakubali kushindwa japo anaona ameshindwa.
 
Kwanini ccm,na taasisi za dini hazitaki tume huru ya uchaguzi?wakati ccm ,na taasisi za dini wanajua fika kabisa,wananchi bado wanaimani kubwa sana,na chama tawala ccm?pamoja na maombi yote hayo ya maskofu,wanayoombea taifa viongozi wa dini,na ccm bado wanaogopa tume huru ya uchaguzi tu?
Iyo tume huru inafananaje labda???
ebu toa maelezo mazur tukuelewe maana kila siku ni kelele kelele za tume huru!!
au unataka tume iajiri wamarekani ndio ulizike???
 
Kwa muda mrefu sasa baadhi yetu humu tumekuwa tukizungumzia juu ya umuhimu wa uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Hiyo ni kwa sababu hii iliyopo sasa hivi baadhi yetu hatuioni kama ipo huru.
Lakini sina uhakika kama tulio wengi tunajua hata hiyo tume huru inapaswa iweje. Hivi kuna kitu kama tume huru ya uchaguzi kweli? Na ni huru kiasi gani hasa?

Hivi kweli kabisa katika mazingira yaliyopo sasa hivi uwepo wa tume huru ya uchaguzi unawezekana? Hao watu watakaounda hiyo tume huru watatoka wapi?

Na kweli watakuwa huru au watakuwa na upendeleo waliouficha na siku ya siku ikifika ndo wanazionyesha rangi zao za kweli?
Hakuna njia au namna nyingine zaidi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi?

Na tuseme tunaipata hiyo tume 'huru'. CCM ikiendelea kushinda chaguzi kisingizio cha upinzani kushindwa itakuwa nini?
Kwamba bado hiyo tume 'huru' haipo huru?

Nawaza tu hapa....maana huenda tatizo la wapinzani kushindwa chaguzi ni zaidi ya uwepo au kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.....
Kama Taifa ikiwa tumekosa watu waadilifu wa kusimamia chaguzi zetu kwa kuanzia tunaweza kuomba msaada wa Jumuia ya Madola au UN kusimamia uchaguzi mkuu mmoja, kuanzia A to Z.
Baada ya uchaguzi huo, ndio tuchukue hatua , tuunde Tume mpya ya uchaguzi, watakaofanya kazi huko waombe na sio wateuliwe, wafanyiwe vetting na ithibitishwe si wanachama wa chama cha siasa, tunao watu wengi tu ambao wanaweza kufanya kazi hiyo.

Lakini la msingi sana ni Katiba ya wananchi ambayo itatandika misingi ya kujenga Taasisi zinazojitegemea(huru). Wapo watanzania wengi tu ambao hawashabikii chama na ambao wanataka kuitumikia Tanzania kama Taifa bila kujali vyama vya siasa.

Kikwazo siku zote ni Chama dola katika kuweka mambo ya msingi ya kitaifa. Kwao chama na kung'ang'ania madaraka ndio kila kitu na siku zinavyosonga mbele ndio hofu ya kupoteza madaraka inawafanya wafanye mambo ya ajabu kama ile kitu JWTZ, Polisi na Jecha walifanya kule Zanzibar.

Au kama walivyo-uintarahamwe mchakato wa Katiba Mpya huku wakiendelea kuwagawia wadanganyika umasikini kwa mwendokasi.
 
Freeland #46 kuna sehemu kuu mbili za mada ya Nyani Ngabu

B
1. Kwamba yapo madai tume ya sasa si huru. Kuna ukweli juu ya hili kwa ushahidi
Jaji mkuu ambaye alikuwa mwenyekiti wa tume alitaka kugombea Urais kwa CCM
Lini alijiunga na CCM? Hakuna jibu. Je, wenye shaka na hili wamekosea?

2. Vyombo vinavyopaswa kuwa huru hata nje ya tume si huru.
Yupo mtu anaongoza taasisi aliulizwa Marufuku ya mikutano yapo katika sheria ipi?

Hakuwa na jibu. Mtu huyo ni mteuliwa wa Rais.
Hata sheria zilipokiukwa hakuweza kusimama kwa kukosa uhuru

3. Vyombo vya dola na vingine havipo huru katika kutoa haki.
Hili ni mwendelezo wa tu wa taasisi kama tume ya uchaguzi kutokuwa huru

B. Tume ya uchaguzi inakuwaje ili kuwa huru?

Uhuru wa tume si watu. Tume inaweza kuwa na maaskofu na masheikh,haki isitendeke.

Hatuhitaji kusema mifano ya jinsi gani wanaodhaniwa ni waadilifu kumbe ni wahalifu

Wala uwepo wa wanasiasa au watu wa makundi ya jamii hautoi haki

Mfano, tulikuwa na wajumbe wa Tume ya Warioba kutoka taasisi na mashirika

Leo tunajua yule wa UDSM ni kada, na mwingine wa NGO sasa ni kinara wa makada

Tuliaminishwa wanawakilisha taasisi, kumbe mioyoni mwao wamebeba uchama

C. Uhuru wa Tume:
Tunapotaka kuwa na tume huru tunapaswa kuangalia haya
1. Maridhiano ya jamii nani awepo nani asiwepo na kwanini
2. Tume kupatikana nje ya uteuzi wa mtu au kikundi cha watu bali kwa mfumo mahususi
3. Kuweka taratibu za kuiwajibisha tume bila ruhusa ya mtu au kikundi cha watu
5. Kuweka watch dog kama mahakama kuweza kuiwajibisha tume bila kuingiliwa
6. Kuweka misingi ya wajumbe kutokuwa na masilahi wakishachaguliwa
7. Kuweka ukomo, kwamba mwisho wa kazi yao wasijihusishe na shughuli za umma tena

Lakini hayo hapo juu hayatoshi na hayana maana kama mfumo mzima hautafumuliwa

1. Mahakama iwe huru , majaji wapatikane kwa mfumo usiotegemea mtu
2. Vyombo vya dola viwajibishwe na eneo jingine (mfano Polisi)
3.Kuondoa taasisi kama msajili wa vyama, ziwe chini ya Mahakama au Bunge
4. Kuondoa mamlaka ya Rais au mkuu wa chama katika shughuli za uchaguzi
 
Tume huru ambayo itafanya kazi bila woga wala vitisho kutoka kwa yule anayewateua wajumbe wa Tume hiyo kuanzia Mwenyekiti wa Tume. Kama tunavyojua Jecha alikuwa tayari kutangaza ushindi wa Urais kwa chama cha CUF kule Zanzibar lakini akaingiliwa na Kikwete na katika mazingira ya kutatanisha akashinikizwa afute matokeo yale.

Uchaguzi wa 2015 kama tutakumbuka kura zilikamatwa sehemu mbali mbali nchini zikiwa zote zimeshapigwa kwa Wagombea wa CCM tu lakini cha kushangaza Tume ya uchaguzi haikutia hata neno kuhusu kura zile zilizokamatwa au kuokotwa katika baadhi ya maeneo nchini.

Nimejaribu kuingia kwenye Tume ya uchaguzi kule Gambia kuona Tume yao inapatikana vipi lakini sikuona info zozote zile. Tunaweza kuangalia katika nchi za Afrika ambazo vyama vya upinzani vimewahi kushinda chaguzi mbali mbali kama vile Malawi na Zambia Tume zao za uchaguzi zinapatikana vipi na hivyo kuweza kuwa huru kufanya maamuzi yao ya haki na huru bila ya woga wa kuingiliwa na yoyote yule ukilinganisha na hapa kwetu. Si haki wala si sawa hata kidogo Tume ya uchaguzi wa vyama vingi nchini iteuliwe na Mwenyekiti wa CCM.

Tume hii ya uchaguzi tuliyonayo nchini ni kama kitengo cha MACCM tu, inatumika kuhakikisha wanatumia kila mbinu ili CCM waendelee kung'ang'ania madarakani huku wakisaidiwa na vyombo vya dola. Tume hii ni kikwazo kikubwa sana cha uchaguzi huru na wa haki nchini na kupitia tume hii KAMWE wapinzani hawawezi kushinda urais nchini au viti vingi Bungeni kutokana na njama kubwa zinazofanywa na Tume hii AKA kitengo cha CCM.
Zanzibar iliundwa tume ambayo CUF waliridhia na kushiriki kwa kuteua baadhi ya wajumbe. Kilichotokea kwenye uchaguzi uliopita wote tunajua. Kenya waliunda tume huru tena baada ya mabadiliko ya katiba. Ni tume ambayo hata kina Laira Odinga waliiona huru. Lakini waliposhindwa uchaguzi wakaibebesha lawama za kulazimisha hadi ikavunjwa.
Anachosema mtoa mada je tatizo kubwa ni kukosekana kwa tume "huru" au kuna sababu nyingine?
Mimi naamini CHDEMA ilifanya Kosa kubwa sana kwa kumtema mtu ambaye aliijenga CHADEMA na kumkumbatia mgombea urais asiyekubalika na wengi. Ikawa ni pamoja na kutupa kapuni sera zilizoiinua CHADEMA.
Kosa hili ambalo linaendelea mpaka leo ni sababu moja kubwa ya kuporomoka kwa upenzi na imani(trust) kwa CHADEMA, japokuwa chama bado hakitaki kuona kuwa hili ni tatizo!
 
wanaodai tume huru kupatikana haiwezekani wanasahau kuwa tume ya Warioba (katiba mpya) ilifanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa sana bila kuegemea upande wa establishment.

common sense.....borrow a leaf from that!
 
Tume huru katika Afrika ni ya Taifa la Gambia.uchaguzi ulifanyika kwa kutumia groli(mable vote) -Naomba tusome na tujue ukweli wa tume ya uchaguzi.Ghana wanapenda nchi yao na wako huru nchi zilizobaki ni wasanii.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jecha alikuwa yuko tayari kumtangaza mshindi kama ni Seif Maalim. Kikwete akasafiri usiku ule ule siku ya uchaguzi kwenda kuhakikisha matokeo yale yanafutwa. Unadhani kama ile ingekuwa ni tume huru wangekubali kufuta matokeo kirahisi namna ile baada ya kushinikizwa na Kikwete? Na baadhi ya wajumbe wa Tume ile ambao ilibidi wakutane ili wafikie maamuzi kama tume hawakushirikishwa ni Jecha ndiye aliamua kutangaza matokeo kufutwa bila kuwashirikisha wenzie. Je, uhuru wa hiyo tume uko wapi? Uchaguzi wa Tanzania hauko huru wala si wa haki na kwa mantiki hiyo hakuna uwezekano wa wapinzani kushinda Urais au kuchukua viti vingi Bungeni.

CUF hawakumsimamisha yoyote zaidi ya Maalim na bado wakaporwa ushindi wao. Kama tume ingekuwa ni huru yule Mwenyekiti wa Tume Jecha asingekubali kushinikizwa na Kikwete na MACCM na pia asingekubali kutangaza kufuta matokeo katika uchaguzi ambao matokeo yake alikuwa anakaribia kuyatangaza na kumpa ushindi Maalim kama walivyoamua Wazanzibari.

Zanzibar iliundwa tume ambayo CUF waliridhia na kushiriki kwa kuteua baadhi ya wajumbe. Kilichotokea kwenye uchaguzi uliopita wote tunajua. Kenya waliunda tume huru tena baada ya mabadiliko ya katiba. Ni tume ambayo hata kina Laira Odinga waliiona huru. Lakini waliposhindwa uchaguzi wakaibebesha lawama za kulazimisha hadi ikavunjwa.
Anachosema mtoa mada je tatizo kubwa ni kukosekana kwa tume "huru" au kuna sababu nyingine?
Mimi naamini CHDEMA ilifanya Kosa kubwa sana kwa kumtema mtu ambaye aliijenga CHADEMA na kumkumbatia mgombea urais asiyekubalika na wengi. Ikawa ni pamoja na kutupa kapuni sera zilizoiinua CHADEMA.
Kosa hili ambalo linaendelea mpaka leo ni sababu moja kubwa ya kuporomoka kwa upenzi na imani(trust) kwa CHADEMA, japokuwa chama bado hakitaki kuona kuwa hili ni tatizo!
 
Nchi zote Mkuu hata za Afrika ambazo kuna Tume huru za uchaguzi wapinzani wanashinda. Tumeona hivyo Ghana, Nigeria, Gambia hivi karibuni, Zambia, Malawi etc lakini hapa kwetu miaka 20 sasa ya mfumo wa vyama vingi lakini hakuna uwezekano wa upinzani kushinda kutokana na uchaguzi kutokuwa huru na wa haki kwa sababu hatuna tume huru ya uchaguzi na pia vyombo vya dola vinaingilia uchaguzi ili kuhakikisha ushindi wa MACCM.

Kama MACCM wanajiamini wanapendwa sana na Watanzania kwanini wanaogopa katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi!? Warioba ni CCM, SAS ni CCM na wajumbe wengi katika ile Tume ya Warioba walikuwa ni MACCM waliweka maslahi ya nchi mbele badala ya MACCM na kuandika rasimu nzuri sana. Kwanini CCM hawaitaki rasimu ile!?

Tume huru katika Afrika ni ya Taifa la Gambia.uchaguzi ulifanyika kwa kutumia groli(mable vote) -Naomba tusome na tujue ukweli wa tume ya uchaguzi.Ghana wanapenda nchi yao na wako huru nchi zilizobaki ni wasanii.
 
Yaani Mkuu tulikuwa karibu tupate katiba mpya na ile rasimu ilikuwa poa sana ni kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania. Haikuwa kwa ajili ya maslahi ya CCM, CHADEMA, CUF au UKAWA. Cha kushangaza MACCM wakaikana!

wanaodai tume huru kupatikana haiwezekani wanasahau kuwa tume ya Warioba (katiba mpya) ilifanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa sana bila kuegemea upande wa establishment.

common sense.....borrow a leaf from that!
 
Tatizo la Tanzania sio tume huru ya uchaguzi , tatizo hatuna upinzani madhubuti ambao umevaa ngozi ya upinzani na uzalendo yaani mvua inyeshe. Jua liwake

Pia , agenda za maana , yaani wanapenda siasa za matusi na kumsema rais au CCM

Badala waje na siasa za kisasa kitafiti

Mfano unapofanya research lazima uwe na source of problem , then una kuwa na Specific objectives zako , alafu unakuja na Solution ya Problem , na unamaliza na methodology utakayotumia

Sasa wao mwanzo mwisho matusi matusi hakuna mbadala wa jawabu kwamba mkitupa nchi tutafanya hivi kwa kutumia mbinu hizi na mifano mingi

Ila wao ni siasa za mitaroni

Masikini Upinzani Tanzania

...siasa za kisasa za kitafiti ndio zipi??...hivi ccm wanafanya siasa gani kwa mtazamo wako?...hivi anaewatukana wenzake ni ccm ama wapinzani...kusema la ukweli!.....mara nyingine tuache unafiki....hivi kwa mtizamo wako unateema wapinzani wafanyeje siasa wakati hata platform ya kufanyia siasa hawana?....mahali pa kufanya siasa na kuuza sera ni kwenye mikutano ya hadhara na hata bungen...hivi kwa akili yako hali halisi iliyopo...kwa maana ya kutoruhusiwa kufanya siasa kupitia platform hizi unategemea wapinzani wafanyeje??...tuache unafiki kwa kujifanya vipofu wasioona status quo....
 
...kuwa na tume huru kunawezekana...lakini kwa ccm hii na uongozi wake hawatoruhusu...maana itakua ndio mwisho wao kutawala taifa hili....mifano ni mingi pale vyama dhalimu na vikongwe viliposhindwa na upinzani baada ya kukubali tume huru...mfano latest ni kule gambia...ambapo Jammer alifanya kosa(kwa mtazamo wa maamuzi yake baadae)kukubali tume huru iliyomtangaza mshindi halali toka upinzani...na alipogundua alichofanya akang'ang'ania madarakani....mfano mwingine kenya...na malawi.....Hapa TZ kwa utawala huu uliopo sioni tume huru ikikubalika....na kwa maana hiyo sioni ccm hii ya mabavu ikiondoka madarakani...

...njia pekee kwa mtazamo wangu..ili kuitoa ccm hii madarakani itahitaji zaidi ya tume huru..na jibu ni nguvu ya umma...pale ambapo kila mtu na dalili zote zitaonyesha ccm kukataliwa kwenye kura..watu wanaweza wote kuingia barabarani kudai haki....ni kwa njia hii tu ccm itaondoka madarakani...kutoka njiani kwa amani huku tukishuhudiwa na dunia nzima....hadi watawala waone aibu na kupata mashinikizo ya nje...
 
Jecha alikuwa yuko tayari kumtangaza mshindi kama ni Seif Maalim. Kikwete akasafiri usiku ule ule siku ya uchaguzi kwenda kuhakikisha matokeo yale yanafutwa. Unadhani kama ile ingekuwa ni tume huru wangekubali kufuta matokeo kirahisi namna ile baada ya kushinikizwa na Kikwete? Na baadhi ya wajumbe wa Tume ile ambao ilibidi wakutane ili wafikie maamuzi kama tume hawakushirikishwa ni Jecha ndiye aliamua kutangaza matokeo kufutwa bila kuwashirikisha wenzie. Je, uhuru wa hiyo tume uko wapi. Uchaguzi wa Tanzania hauko huru wala si wa haki na kwa mantiki hiyo hakuna uwezekano wa wapinzani kushinda Urais au kuchukua viti vingi Bungeni.

CUF hawakumsimamisha yoyote zaidi ya Maalim na bado wakaporwa ushindi wao. Kama tume ingekuwa ni huru yule Mwenyekiti wa Tume Jecha asingekubali kushinikizwa na Kikwete na MACCM na pia asingekubali kutangaza kufuta matokeo katika uchaguzi ambao matokeo yake alikuwa anakaribia kuyatangaza na kumpa ushindi Maalim kama walivyoamua Wazanzibari.
Hiyo ya Zanzibar unayosema haikuwa tume huru, iliridhiwa na Maalim Seif kama tume huru baada ya kushiriki kuiunda upya, kama ilivyofanyika Kenya. Hiyo ni moja ikukae kichwani. Tafsiri yake ni kwamba uhenda tunaweza tusiwe na "tume huru" in the near foreseable future, sababu tutaingia kwenye uchaguzi tukiwa tumekubaliana kwamba ni tume huru, lakini mara baada ya matokeo, chama kinachoshindwa kinageuza kauli na kusema tume haikuwa huru!
Pili pointi yangu ilikuwa pamoja na Hali ya tume, tunasahau sababu nyingine za msingi zinazoweza kusababisha chama Kishinde. Nimeeleza Kama chama kina sera zinazokubalika na mass, na kikaaminika na watu wengi na makundi mbalimbali ya kijamii, inawezekana kushinda uchaguzi. Sababu hata kama tume haiko huru, lakini mbele ya wananchi wengi walioamua mabadiliko na kuyasimamia kwa dhati chini ya uongozi wanaouamini, si serikali wala tume inayoweza kuzuia ushindi. Mifano iko wazi kwenye nchi nyingi tu.
Swali ambalo tunalikwepa au kulipa majibu ya uongo, je chama chetu sasa hivi kinaaminika na watanzania kwamba ni mkombozi wao kama ilivyokuwa mwanzo?
 
Sahau mambo ya chama kushinda au kutoshinda. Nchi yenye mfumo wa vyama vingi ni LAZIMA iwe na tume huru ya uchaguzi FULL STOP. Huwezi ukasema sisi nchi yeyu ina mfumo wa vyama vingi halafu ukagomea kuwepo kwa Tume huru ya uchaguzi na Mwenyekiti wa chama kimoja kuendelea kuteua wajumbe wa Tume ya kusimamia uchaguzi. Kwanini CCM haitaki uwepo wa Tume huru ya uchaguzi inaogopa nini? Jibu hili swali acha kulikimbia?

Mambo chungu nzima yanatokea wakati wa uchaguzi ambayo yanaonyesha wazi kwamba uchaguzi si huru na wala wa haki lakini hiyo Tume fake haitii neno iko kimyaaa.

watakuita mchochezi. maDAS na maDED kuwa maka ni jambo baya sana katika ukuwaji wa demokrasia katika taifa letu.

ni bora tuwe na chama kimoja, maana tanzania demokrasia ni kama tunalazimisha japo tusilo liweza.
 
C. Uhuru wa Tume:
Tunapotaka kuwa na tume huru tunapaswa kuangalia haya
1. Maridhiano ya jamii nani awepo nani asiwepo na kwanini
2. Tume kupatikana nje ya uteuzi wa mtu au kikundi cha watu bali kwa mfumo mahususi
3. Kuweka taratibu za kuiwajibisha tume bila ruhusa ya mtu au kikundi cha watu
5. Kuweka watch dog kama mahakama kuweza kuiwajibisha tume bila kuingiliwa
6. Kuweka misingi ya wajumbe kutokuwa na masilahi wakishachaguliwa
7. Kuweka ukomo, kwamba mwisho wa kazi yao wasijihusishe na shughuli za umma tena

Lakini hayo hapo juu hayatoshi na hayana maana kama mfumo mzima hautafumuliwa

1. Mahakama iwe huru , majaji wapatikane kwa mfumo usiotegemea mtu
2. Vyombo vya dola viwajibishwe na eneo jingine (mfano Polisi)
3.Kuondoa taasisi kama msajili wa vyama, ziwe chini ya Mahakama au Bunge
4. Kuondoa mamlaka ya Rais au mkuu wa chama katika shughuli za uchaguzi

Yote hayo uliyoyaorodhesha yamefanyika nchini Kenya, na bado wale ambao ni Upinzani hawaitaki hiyo Tume unayoiita huru, Raila Odinga ameshasema kwamba hataenda Mahakamani tena kama asiporidhika na matokeo, sasa ataenda wapi?
Umeandika kinadharaia tu yaani jinsi inapaswa kuwa lkn utekelezaji wake ni mgumu sana karibu unaweza kusema kwamba haiwezekani, kwa maana mwisho wa siku ni lazima Binadamu apitishe, labda msubiri artificial intelligence ambapo maamuzi yatakuwa yafanywa na algorithm tu, lkn hata hivyo bado utahitaji binadamu kuiandika hiyo algorithm!!
 
Sahau mambo ya chama kushinda au kutoshinda. Nchi yenye mfumo wa vyama vingi ni LAZIMA iwe na tume huru ya uchaguzi FULL STOP. Huwezi ukasema sisi nchi yeyu ina mfumo wa vyama vingi halafu ukagomea kuwepo kwa Tume huru ya uchaguzi na Mwenyekiti wa chama kimoja kuendelea kuteua wajumbe wa Tume ya kusimamia uchaguzi. Kwanini CCM haitaki uwepo wa Tume huru ya uchaguzi inaogopa nini? Jibu hili swali acha kulikimbia?

Mambo chungu nzima yanatokea wakati wa uchaguzi ambayo yanaonyesha wazi kwamba uchaguzi si huru na wala wa haki lakini hiyo Tume fake haitii neno iko kimyaaa.
Kwa hiyo wewe utaishia kuimba ngonjera tume siyo huru! Mpaka lini?
 
Marais wa Afrika waliopo madarakani ukiwambia tume huru au katiba ziwapunguzie madaraka watasema wewe ni kibaraka wawa zungu Unakumbuka Rasimu ya jopo la Warioba kama ulisoma ilikua inampunguzia madaraka Rais wanafuta RAS na DC ilikua inapunguza kubebana sasa mtu Kwa Mfano kama Makonda ataipenda Rasimu ya Warioba?
 
Hata hayo madaraka yakipunguzwa bado utakuja tu kulalamika hapa, hakuna kitu kama Tume huru Dunia hii, hata hao Wazungu mnaowaiga ni kwamba tu hamuwaelewi, hata wao hawana mifumo huru kama mnavyofikiria!
 
Back
Top Bottom