Tume huru ya uchaguzi

Tume huru ya uchaguzi

*RC kada, RAS kada,DC kada, DAS kada, DED kada, NEC ya kwao!UKAWA mnatwanga maji*

1. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) anateuliwa na rais ambaye kwa upande wa pili wa shilingi rais ni Mwenyekiti wa moja ya Chama kinachoshindana na vyama vingine.
2. Wakurugenzi ambao ni sehemu ya wasimamizi wa Uchaguzi katika maeneo wanayoyasimamia wanateuliwa na rais ambaye kwa upande wa pili wa shilingi ni Mwenyekiti wa moja ya Chama kinachoshindana na vyama vingine.
3. Jeshi la Polisi ambalo linasimamia usalama wa mali na raia katika Chaguzi zote nchini liko chini ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ambao ni wenyekiti wa Kamati ya Usalama wa maeneo (Mkoa & Wilaya) husika. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote wanateuliwa na rais. Ikumbukwe kwamba Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wengi ni makada watiifu wa Chama husika ambacho rais ni mwenyekiti wao.
Je, katika uhalisia kuna yeyote ambaye atakuwa tayari kuona chama cha boss wake aliyemwajiri kikishindwa kirahisi katika uchaguzi?!
Katika aina hii ya mfumo na uongozi hatuoni kama kuna haja kubwa ya kuwa na Katiba mpya itakayotupa Tume Huru ya Uchaguzi sambamba na kupunguza madaraka ya rais?!
Ni dhahiri athari za uteuaji wa makada kwenye nafasi zote za utendaji zimeanza kujitokeza sasa.
Sio siri kwenye uchaguzi huu mdogo wa madiwani na mbunge wa Dimani kila DED alikuwa anahangaika kuhakikisha CCM inashinda, ili kulipa fadhila za uteuzi na kumfurahisha muheshimiwa sana.
Tukumbuke hawa MADED ndo wasimamizi wa uchaguzi kwa level ya kata na jimbo (udiwani na ubunge) na ndo wasimamizi pia wa kura za Raisi. Tangu juzi kwa mfano RC wa mkoa wa Arusha amekuwa akijitapa kuisambaratisha CDM huko Meru.
Katika mazingira kama haya ambapo RC kada, RAS kada,DC kada, DAS kada, DED kada, NEC ya kwao!UKAWA mnatwanga maji tu.
Anzeni na katiba mpya itakayozaa Tume mpya na huru ya uchaguzi.
Tz ya viwanda
ni ushauri mzuri sana, kwamazingira kama haya ambapo kila wilaya wamerundikwa makada na ndo wasimamia uchaguzi UKAWA kweli mnatwanga maji
Kinachonichanganya ni pale watu na 'utimamu' wao wanapoamua na kuhakikisha kuwa ni lazima mtu au chama fulani ndicho kishinde regardless matakwa ya wapiga kura! Na hilo swali ukienda mbali zaidi unawaona wabunge wa Gambia wakipitisha kwa kauli moja 'nyongeza' ya miezi mitatu kwa Yahya Jammeh. Ndipo unakuwa na mashaka na mtu mweusi!
It is very true.
It is next to impossible kwa mfumo uliopo nchini wa makada watupu wa Chama tawala kuwekwa kwenye zile posts zote zinazoamua washindi kwenye chaguzi mbalimbali hapa nchini, kutegemea upinzani uibuke washindi!
Hata ikitokea mpinzani amepata asilimia 80 ya kura, Usishangae kura hizo 'zikapinduliwa' na mpinzani akapewa asilimia 20 na mgombea wa Chama tawala 'akawezeshwa' na kupewa hizo asilimia 80!,
Huru, haki na halali! Haijawahi kuwepo Tanzania!
Katika mazingira ambayo wamezuiwa kufanya mikutano ya kisiasa, na kuzimiwa bunge live! ni hatari sana
Naunga mkono hoja.
*****TUME HURU NI LAZIMA****
 
Ieleweke kuwa katika dunia hii yenye nchi zenye Presidential system huwezi kuwa na mazingira ya kisiasa yaliyo sawa katika chaguzi ambapo kuna Rais anatetea kiti chake. Kile kitendo cha Rais kuendelea kuwa Rais wakati wa kampeni kinanyima fursa sawa katika kampeni. Kwa nchi za Afrika ambapo Rais wa nchi ana nguvu za kimungu, multiplier effect yake ni kubwa zaidi.

Msikilize hapa Tundu Lissu kuanzia dakika ya 19 anavyopinga kuhusu visingizio vya kuibiwa kura.

Ulichosema hapo ni kweli kabisa. Ni kitu kinachoitwa 'power of the incumbency'.

Na mara zote incumbent president anakuwa ana advantages kuzidi challengers wake.
 
Mjinga hasipo jielewa uwa mpumbafu!! mleta mada unatatizo hilo!! Kams umesoma, kwenda kwako shule ni hasara kw familia na taifa! Mungu akurehemu!!!

Imebidi nikucheke tu 😀😀😀😀😀
 
Sio lazima tuwe na tume huru kama serikali iliyoko madarakani inatimiza majukumu yake. Siku serikali ya ccm ikiweza kutimiza majukumu yake hatutakua na aja ya kuwa na upinzani.
Upinzani tunauhitaji ili kuikumbusha serikali na sio kuhitaji tu siku moja tufikie level za Democratic na Republican katika kubadilishana uongozi lakini je hili litawezekana , ???
 
Wapinzani inabidi watumie mbinu ya USA ilivyompandikiza Golberchiev na kumsaidia kugombea urais Urusi na hatimaye akashinda na akatekeleza kazi waliyomtuma.

Apandikizwe mtu ndani ya ccm ambaye atakuja kuwa rais na akatimiza malengo ya wapinzani.
 
Angalau kukupa msaada wa tofauti hizo .. Google Tume huru ya INDIA dhidi ya Tume huru ya Uchaguzi ya Tanzania. Alafu ulinganishe. ...
 
Zanzibar waliunda tume huru iliyoshirikisha vyama vyote vya kisiasa. Kilichotokea kila mtu anayefuatilia masuala ya kisiasa anafahamu.

Kenya waliunda tume huru ya Uchaguzi ikishirikisha wadau wote wa siasa. Kilichotokea kila anayefuatilia masuala ya kisiasa anafahamu.

Nirejee kwenye swali lako, hiyo tume itakuwa huru kiasi gani?

Kumbuka hizi ni siasa za nchi za Afrika.
Hata mchakato wa kupata katiba mpya wakasema kuna tume huru ila ccm ikafanya yasiyowezekana yawezekane marehemu wakapiga kura kukubali katiba ya ccm!
 
Hapana aisee.

Tume ya taifa ya uchaguzi kuundwa [hususan viongozi wake wa juu] na rais aliyepo madarakani ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala nalo ni tatizo.

Na ni tatizo kubwa. Ni tatizo la mgongano wa kimaslahi.

Ila, si tatizo pekee linalowakwamisha wapinzani, kwa mtazamo wangu.
Safii sana ,hii ni kwa siasa za Tanzania ,je unaweza kutusaidia mfano ya Gambia , Zambia , n.k ambako vyama tawala vilitolewa madarakani na Wananchi??

Je Kenya ambapo NARC ilishinda je tatizo ilikuwa tume na je mfumo wa upatikanaji wa wajumbe wa tume ilikuwaje ??

Je ulikuwa tofauti na Tanzania???

Msaada tafadhali
 
Mara nyingi hutasikia wapinzani wakipiga kelele pale inapotokea wameshinda!
 
Ulichosema hapo ni kweli kabisa. Ni kitu kinachoitwa 'power of the incumbency'.

Na mara zote incumbent president anakuwa ana advantages kuzidi challengers wake.
Mbaya zaidi kwenye vinchi vyetu hivi masikini na vichanga ambavyo jeshi ndio muhimili mkuu, huwezi kuruhusu serikali ya mpito wakati wa uchaguzi mkuu. Kufanya hivyo kuna athari kubwa kuliko kuendelea kuwa na Rais wakati wa kampeni.
 
Mjinga hasipo jielewa uwa mpumbafu!! mleta mada unatatizo hilo!! Kams umesoma, kwenda kwako shule ni hasara kw familia na taifa! Mungu akurehemu!!!
Utamtukanaje mtoa mada aliyeleta mada fikirishi

Nyie ndio mkishindwa uchaguzi mnakimbilia tume

Ustaarabu haununuliwi
 
Hakuna kitu kinachoitwa tume huru, yaani hai exist na haitakaa i exist, tume lazima itakuwa na bias tu, labda we tume amabayo ina uhuru kuliko ya sasa ila sio tume huru, huu msamiati uondoeni haufai kuwepo.
Achilia mbali tume, kwa system ya Tanzania ilivyo CCM inabebwa na vyombo vingi sana kuanzia media, majeshi, taasisi nyingine
Mambo ya upendeleo hapo kila mahali duniani, sio Tanzania pekee, mfano hao ni vile Trump alipokua akilalamika kua vyombo vya habari vilikua vikimpendelea Hilary! Hivyo kusema kwamba itakaa iwepo tume huru sahau! Time ni huru pale unapopata matokeo chanya tu!
 
Safii sana ,hii ni kwa siasa za Tanzania ,je unaweza kutusaidia mfano ya Gambia , Zambia , n.k ambako vyama tawala vilitolewa madarakani na Wananchi??

Je Kenya ambapo NARC ilishinda je tatizo ilikuwa tume na je mfumo wa upatikanaji wa wajumbe wa tume ilikuwaje ??

Je ulikuwa tofauti na Tanzania???

Msaada tafadhali

Mimi bado naamini kuwa kama wapiga kura wengi kupita kawaida wakipiga kura nyingi dhidi ya CCM, basi hata CCM yenyewe itaona haya kuchakachua matokeo.

Ila kwa sasa hilo sioni likitokea kwani CCM bado ina wafuasi wengi nadhani kushinda chama kingine chochote kile.
 
Kutoka gazeti la Mtanzania:

Dk. Lwaitama

Dk. Azaveli Lwaitama, alisema ni vigumu kusema CCM imeshinda ikiwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Alisema bila tume huru CCM itaendelea kushinda uchaguzi kwani imekuwa ikisaidiwa na dola.

“Katika hali ya kutokuwa na tume huru ya uchaguzi, mtu utaamini vipi kile kinachotangazwa ili ujue kweli kulikuwa na ushindani.

“Kwa hali kama hii ambayo Jeshi la Polisi linaenda kutanda kwenye jimbo la uchaguzi kama ilivyokuwa Dimani, lazima CCM iendelee kutawala, wala hatutafikia walipo wenzetu Kenya ambako chama kikishindwa kinakubali,” alisema Dk. Lwaitama.
 
You nailed it .

Hiyo ndio point ya msingi , upinzani usiwaze 2020 uwaze 2030 na kuendelea kwa kuweka plan kwa vijana wa miaka kuanzia 15 hadi 20 hawa ndio mtaji wao

Pia wajifunze kwa Nyerere aliwezaje kueneza CCM Tanzania nzima na wananchi wakamkubali hadi Leo CCM inaishi sababu ya misingi ya nyerere
 
Vilio upinzani uchaguzi mdogo

www.ippmedia.com/sw/habari/vilio-upinzani-uchaguzi-mdogo

Juma Ali Juma, aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, aliibuka na ushindi kwa kupata kura 4,860 dhidi ya mpinzani wake wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdulrazak Khatib Ramadhan, aliyepata kura 1,234.

Chama hicho tawala pia kiliibuka kidedea katika kata 21 kati ya 22, moja ikirejea kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kilikuwa kinaitetea.

Viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani, wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti jana kuhusu matokeo ya uchaguzi huo, walidai haukuwa huru na haki na haukufuata misingi ya kidemokrasia. Nipashe haikuweza kuthibitisha madai hayo ya vyama vya upinzani.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim, alisema uchaguzi huo wa marudio ulikuwa na kasoro nyingi ambazo alidai ndicho kiini cha upinzani kufanya vibaya.

Mwalimu alidai kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na idadi kubwa ya vyombo vya dola na silaha nzito hususani visiwani Zanzibar, hali iliyosababisha baadhi ya wapigakura kuingiwa na hofu na kushindwa kujitokeza kupiga kura.

"Vyombo vya dola vilimwagwa sana Zanzibar, kila unapogeuka unakutana na askari, mwanajeshi, sasa huko si kutisha wananchi? Na kwa hali hii baadhi wanaogopa hata kwenda kupiga kura. Niseme tu kwamba hicho wanachokifanya wanakijua," alisema Mwalimu.

Kiongozi huyo wa Chadema alisema jambo jingine lililotia doa katika uchaguzi huo ni kitendo cha kuondolewa kwa mawakala wengi wa vyama ya upinzani kusimamia uchaguzi huo.

"Mbali na dosari hiyo, daftari la wapigakura lililotumika katika uchaguzi wa jana (juzi) pia lilikuwa ni tofauti na lile ambalo mawakala walikuwa nalo," alisema.

"Mimi nilikuwapo Zanzibar, nilichokishuhudia kwa kweli siyo haki, mawakala wa CUF waliondolewa eti kisa wamehoji kwanini daftari lililoletwa ni jipya na ni tofauti na lile walilokuwa nalo mawakala na limehakikiwa ambalo vyama vyote vilishirikishwa katika uhakiki wake, sasa vitu kama hivyo huwezi kusema uchaguzi ulikuwa huru na haki."

*Imeandikwa na Elizabeth Zaya na Gwamaka Alipipi
 
Kwa mazingira haya katika chaguzi zetu CCM itatimiza ile ndoto yake ya kung'ang'ania madaraka nchini milele. Wapinzani KAMWE wasitegemee kushinda katika mazingira haya ya chaguzi ambazo si huru na wala si za haki zinazosimamiwa na kitengo cha MACCM AKA Tume ya uchaguzi.

Vilio upinzani uchaguzi mdogo

www.ippmedia.com/sw/habari/vilio-upinzani-uchaguzi-mdogo

Juma Ali Juma, aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, aliibuka na ushindi kwa kupata kura 4,860 dhidi ya mpinzani wake wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdulrazak Khatib Ramadhan, aliyepata kura 1,234.

Chama hicho tawala pia kiliibuka kidedea katika kata 21 kati ya 22, moja ikirejea kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kilikuwa kinaitetea.

Viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani, wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti jana kuhusu matokeo ya uchaguzi huo, walidai haukuwa huru na haki na haukufuata misingi ya kidemokrasia. Nipashe haikuweza kuthibitisha madai hayo ya vyama vya upinzani.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim, alisema uchaguzi huo wa marudio ulikuwa na kasoro nyingi ambazo alidai ndicho kiini cha upinzani kufanya vibaya.

Mwalimu alidai kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na idadi kubwa ya vyombo vya dola na silaha nzito hususani visiwani Zanzibar, hali iliyosababisha baadhi ya wapigakura kuingiwa na hofu na kushindwa kujitokeza kupiga kura.

"Vyombo vya dola vilimwagwa sana Zanzibar, kila unapogeuka unakutana na askari, mwanajeshi, sasa huko si kutisha wananchi? Na kwa hali hii baadhi wanaogopa hata kwenda kupiga kura. Niseme tu kwamba hicho wanachokifanya wanakijua," alisema Mwalimu.

Kiongozi huyo wa Chadema alisema jambo jingine lililotia doa katika uchaguzi huo ni kitendo cha kuondolewa kwa mawakala wengi wa vyama ya upinzani kusimamia uchaguzi huo.

"Mbali na dosari hiyo, daftari la wapigakura lililotumika katika uchaguzi wa jana (juzi) pia lilikuwa ni tofauti na lile ambalo mawakala walikuwa nalo," alisema.

"Mimi nilikuwapo Zanzibar, nilichokishuhudia kwa kweli siyo haki, mawakala wa CUF waliondolewa eti kisa wamehoji kwanini daftari lililoletwa ni jipya na ni tofauti na lile walilokuwa nalo mawakala na limehakikiwa ambalo vyama vyote vilishirikishwa katika uhakiki wake, sasa vitu kama hivyo huwezi kusema uchaguzi ulikuwa huru na haki."

*Imeandikwa na Elizabeth Zaya na Gwamaka Alipipi
 
Kutoka gazeti la Mtanzania:

Dk. Lwaitama

Dk. Azaveli Lwaitama, alisema ni vigumu kusema CCM imeshinda ikiwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Alisema bila tume huru CCM itaendelea kushinda uchaguzi kwani imekuwa ikisaidiwa na dola.

“Katika hali ya kutokuwa na tume huru ya uchaguzi, mtu utaamini vipi kile kinachotangazwa ili ujue kweli kulikuwa na ushindani.

“Kwa hali kama hii ambayo Jeshi la Polisi linaenda kutanda kwenye jimbo la uchaguzi kama ilivyokuwa Dimani, lazima CCM iendelee kutawala, wala hatutafikia walipo wenzetu Kenya ambako chama kikishindwa kinakubali,” alisema Dk. Lwaitama.

Sasa kama kweli hakuna tume huru, kwa nini wapinzani huwa wanashiriki chaguzi?

Haiingii akilini kabisa.

Yaani mtu unashiriki chaguzi ambazo mwisho wa siku unajua kabisa huwezi kushinda kwa sababu chombo kinachoendesha hizo chaguzi hakipo huru!!

That's lunacy!
 
Naomba nikukosoe. Toka 2010 upinzani haujawai kushindwa uchaguzi.
 
Zanzibar waliunda tume huru iliyoshirikisha vyama vyote vya kisiasa. Kilichotokea kila mtu anayefuatilia masuala ya kisiasa anafahamu.

Kenya waliunda tume huru ya Uchaguzi ikishirikisha wadau wote wa siasa. Kilichotokea kila anayefuatilia masuala ya kisiasa anafahamu.

Nirejee kwenye swali lako, hiyo tume itakuwa huru kiasi gani?

Kumbuka hizi ni siasa za nchi za Afrika.
Wewe tume huru ya kenya usiifananeshe na vitu vya kipuuzi apa TZ
 
Back
Top Bottom