Tuliwaambia lakini Ubishi tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuliwaambia lakini Ubishi tu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 9, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mongella: Sheria ya Gharama za Uchaguzi itekelezwe kwa umakini

  Mwandishi Wetu

  Mbunge wa Ukerewe, Dk. Getrude Mongella, ametaka busara itumike katika kutekeleza Sheria ya Gharama za Uchaguzi, vinginevyo wagombea watatengwa na jamii.
  Mongella alisema hayo baada ya Kamanda wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Ukerewe, Leonidas Rugemalila, na Msimamizi wa Uchaguzi wa wilaya hiyo, Dk. Leonard Masale, kuwasilisha mada zao kuhusu sheria hiyo katika kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Ukerewe.
  Alisema kifungu kinachokataza mgombea kukusanya watu popote na hata nyumbani kwake kitawanyima haki ya wagombea kutembelewa na kutembelea wananchi na hasa majirani kwa hofu ya kuadhibiwa na sheria hiyo.
  Akitoa mfano, Dk. Mongella alisema kwa kawaida anapokuwepo nyumbani kwake, watu humtembelea kwa ajili ya kusalimia na kwamba wakati mwingine unaweza kukuta zaidi ya mtu mmoja na kwamba wakati mwingine hula nao chakula hivyo, kwa hali ya sasa kitendo hicho kinaweza kutafsiriwa kuwa kinavunja sheria hiyo.
  Mbunge huyo alivitaka vyombo vinavyosimamia sheria hiyo hasa maafisa wa Takukuru kuwa makini na kutumia busara wakati wanatekeleza majukumu yao ili kuepuka kuwachukulia watu waio na makosa na kuongeza kuwa ni vyema elimu hiyo ikatolewa hadi ngazi ya chini ili wananchi waielewe.
  Akiwasilisha mada, Rugemalila alisema Takukuru imejiandaa kukabiana na vitendo vya rushwa katika uchaguzi mkuu ujao ikiwa ni pamoja na katika mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM na kuwataka wote wenye mipango hiyo kuachana nayo ili kuepuka mkono wa sheria.
  Kwa upande wake, Dk. Masale aliwataka wanachama wa vyama vya siasa kuwa makini na watu wanaodaiwa kupita maeneo tofauti nchini wakigawa kadi za vyama vya siasa hasa CCM.
  Alisema kamati yake itakuwa na watu wawili kila kata na kuwataka wagombea kusoma sheria hiyo na kuielewa ili kuepuka kufanya makosa na hatimaye kuondolewa katika uchaguzi.

  NIPASHE

  My Take:
  Mmezidi Ubishi, wabunge nyinyi, kulalamika mlalamike nyinyi.. tuliwaimbia na kuwapigia kelele hii sheria mbovu mkaizunguka kwa mbwembwe kama watu wanaomzunguka mganga wa kienyeji.. sasa wacha igeuke iwanyofoe ndio mkome. Inakuwaje mtunga sheria anailalamikia sheria ambayo alikuwa na uwezo wa kuifanyia mabadiliko!
   
 2. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji unashangazwa na hilo? nilishasema huko nyuma kuwa wabunge wengi wako pale ila hawajui wako pale kufanya nini zaidi ya sehemu ya mlo. Angalia vikao vinavyoendelea sasa hivi, hawapo ,viti vitupu, katika kikao muhimu kama hiki cha bajeti. Hawa sii wawakilishi wa wananchi,wanajiwakilisha wao na familia zao tuu.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  usishangae sheria hiyo ilipopitishwa hakuwa macho bungeni.................na hakujua hasa kuwa sheria kama hiyo imepitishwa.

  wabunge wetu ni vichekesho kwa kweli
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna sheria inayotekelezwa bila busara? Au hiyo busara ndio kuipindisha? Kupindisha na kuvunja sheria ni kule kule! Sheria ifuatwe kama ilivyo ili wabunge wa CCM wajue maana ya kutunga sheria bora, nzuri, na zenye kujenga na kulenga maisha bora kwa kila mtanzania. Wenyewe walifikiri wamewabana wapinzani na mahasimu wao! Na hakuna mtu aliyejuu ya sheria. JK mwenyewe kesha ijunja mara nyingi tu!!!
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Wakati wa kupitisha sheria hakuwa na mshiko........sasa ana cheki ya 80m ya mafao...........anataka kununua wapiga kura...kakabwa ndio maana analialia
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  yaani wananiudhi kweli..!! na bado we ngoja waanze kutoa ahadi wajikute wanavunja sheria..
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa upuuzi tuliouzoea nchini mwetu hawa wakuu wa Takukuru badala ya kutekeleza sheriawanaweza kuanza kutafuta compromise na CCM.
   
 8. m

  magee Senior Member

  #8
  Jul 9, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nnaloliona mm ni ufinyu wa fikra katika viongozi wetu.....Hv hawa watu wangekuwa makini ,wangetumia busara wakati wa kuitunga hii sheria na sio kulalamika sasa!!
  Nashangaa kitu kimoja why now??wakati sheria inasomwa bungeni walikuwa wapi kuitafakari??au ndio walikuwa majimboni kama sasa,jana nilikuwa naangalia bunge niliishia kushikwa na uchungu kwaajili ya wadanganyika wenzangu tunaojidanganya tunawawakilishi wakati ukweli hatuna......wabunge wanaosimama kama wawakilishi waliokuwepo ni wachache mno wengi hawakuepo na hawa ndio wanawakilisha matakwa yao binafsi na makundiflaniflani na usishangae baadae wakataka busara katika bajeti zilizopitishwa jana!!!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Halafu sheria ilisharudishwa tena kufanyiwa marekebisho kabla hata ya kuanza kutumika hawakusema lolote!
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sheria iko sawa tu. Tatizo ni kubadili mtazamo hasa kwa jinsi tulivyokuwa tumezoea kuenenda na kutenda kwenye chaguzi zetu. Hebu jaribu kufikiria watu kama RA, EL, Mramba, Yona, Manji, magwiji wa EPA,....wangetufanyia nini kwenye uchaguzi wa mwaka huu bila ya sheria angalau kuwepo.
   
 11. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Tatizo la wapunge wetu pamoja na Raisi hawasomi ndo maana wanapiga makofi na kupitisha vitu vya ajabu. sasa hili liko kwa upande wao ndo maana walalamika sasa. Nafikiri baada ya uchaguzi wabunge wengi watawekewa pingamizi kwa sababu ya rushwa.
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mama Mongella naona analalamika bure wakati huu. TAKUKURU wamepewa maelekezo ya kutosha juu ya nini ni rushwa na nini sio rushwa.

  Sio kweli kwamba mheshimiwa akitembelewa na marafiki nyumbani na kula nao chakula eti TAKUKURU wataingilia. Kuna mambo ambayo wameyapa uzito ikiwa ni pamoja na hilo la kugawa kadi kinyemela, kutoa zawadi kwenye mikutano ya hadhara, kutoa zawadi au michango makanisani na kukutana na wananchi au viongozi kwa lengo la kuwashawishi kukupigia kura na kisha kuwapa zawadi.

  Kwenye mikutano mingi ya wabunge sasa, kabla haijaanza, TAKUKURU humwaga makaratasi ya kuonya juu ya kutoa na kupokea rushwa. Wabunge wengi wamekimbia bungeni ili kuanza kampeni mapema kwa kisingizio cha kwamba wanatimiza majukumu yao jimboni. Huu ndio muda ambao walikuwa wanajiandaa kutoa misaada na zawadi nyingine mbalimbali. Kuwepo kwa hii sheria kunawabana na hata mikutano yao inaishia malalamiko tu maana wananchi wanategemea posho.

  Kwa mtu ambaye hana pesa za kutoa hii ni habari njema. Ukiwaita wananchi na kuwaacha waondoke bila posho unakuwa umejiletea maadui. Hivyo huko mbele wagombea wengi wataona bora wafuate ratiba za chama au tume ya uchaguzi ili wasilaumiwe kwa kuita wananchi kwenye mikutano yao na kuwanyima hata soda.

  Wacha tuone mwisho wake ila ni kweli TAKUKURU wapo kila sehemu wakikusanya ushahidi. Labda tatizo kwa Tanzania ni je huo ushahidi wanaoupata wanautumia vizuri kuhakikisha wenye makosa wanaadhibiwa? Kibaya ni pale wanapoamua kuchagua watu wa kuwashughulikia na kuwaacha wengine ambao huenda makosa yao hata ni makubwa zaidi.
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Jul 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Wabunge wooote waCCM akilizao za Hovyo, they dont read, wamekua mashabiki tu, na hata wakisoma , wakigundua kasoro hakuna anaejali, watakosoa wa dakika Thelasini, dakika tano watasifiana na kupeana pole, Dakika moja atatumia kusema kua naunga mkono hoja kwa aslimia mia.....stupid, utoto na ujinga ulioje.
  Sasa huyu Mongella anakuja kulalamika upuuzi na utumbo mtaani, wakati yeye hakuupinga huo mswaada wa sheria wazi wazi, alijidai kuunga mkono.
  Wito wangu kwa WaTz , wang'oeni hawa Wabunge wa Chama cha CCM , KIELELEZO CHA WATU DHALILI, WASIO NA MAADILI DHIDI YA UMMA, wanaotetea ujinga kwa gharama za maisha yetu, ni kundi wa wafujaji na waidhinisha ulaji kwa mafisadi .
  hawa ni genge la mabaka Uchumi.
   
 14. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  wabunge wetu woote sehemu kubwa ni 'shake well be for use' hawana wanalolijua kwa sababu wengi wao ni vilaza, but they are there for their own benefits and prostitusion practices
   
 15. doup

  doup JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  tumezoea mpaka tuguse kwanza kama Tomaso; ndio tujue; Sasa wanagusa wagundua kumbe ni moto tena unawarudiwa wao wenyewe. HATUTAKI ibadilishwe ibaki hivyo hivyo, tukutane kwenye viwanya vya kampeni tu; na nafikiri wangeongeza kipengele cha kuzuia "conference calls" miezi mitatu kabla ya uchaguzi.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mtanzania hili ni mojawapo ya tatizo.. "wapo wanakusanya ushahidi manake nini"? Uhalifu unapotendeka au kuhisiwa unatendeka chombo cha sheria hakitakiwi kukaa pembeni "kukusanya ushahidi".. kinatakiwa kuuzuia kwanza usiendelee kutendeka halafu kukusanya ushahidi wa kile kilichotendeka na mara moja kuwatia nguvuni wahusika. Sasa huu mtindo wa TAKUKURU wa kuangalia uhalifu unatendeka hadi "bunge litakapovunjwa" ndiyo jinsi wanavyolea mafisadi.
   
 17. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu hapa ndo umemaliza. Kwani umesahau ya TZ yetu hii. Hiki ni kiini macho tu. Wabunge wa CCM wengi na mambumbumbu. Inaudhi kusikia mtu ambaye alikuwa na nafasi ya kuyasema haya wakati wa kuchangia kutunga hii sheria analalamika sasa!!! Tena ilikwisha rudi kwao mara ya pili!!!

  Inatia uchungu sana bunge la sasa hivi limepoteza mvuto; kikao cha bajeti watu wamejigawia mafao mapema wametokomea majimboni. Nadhani kwa leo hadi jumapili kikao kitapoteza mvuto zaidi kwa ajili ya NEC, kila mtu na kundi lake; ubishi utadhani mtaani manzese!!

  Wacha iwatafune tu, kwani walikuwa hawajui sheria ni msumeno.....aaaargghh:mad:
   
 18. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Labda kwenye makaratasi hawakuielewa sasa ndo wanapata picha kamili, mwe wabunge wetu mwee  FAITH GIVES US SUBSTANCE TO OUR HOPES AND MAKES US CERTAIN OF REALITIES WE DO NOT SEE
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu mama asingojee mpaka Takukuru ndio wamkamate kwa kutoa rushwa ndio wamuengue kugombea kwani hana maadili ya kuwa mbunge; alifukuzwa kuwa Rais wa Afican Union parliament kwa ubadhilifu!! Aliitia aibu nchi yetu kwahiyo kama mwizi hafai kuwa kiongozi.
   
 20. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Wonders will never cease to amaze me! This being one them:A S-eek:!
   
Loading...