Tuliwaambia lakini Ubishi tu!

Tuliwaambia lakini Ubishi tu!

Anaposema Busara Itumike ana maana gani hasa
 
Pamoja na kwamba wabunge ndio walioipitisha hiyo sheria bungeni bila kuichunguza kwa makini na hii inasababishwa na bunge letu kuendeshwa kimazoea na baazi ya wabunge hasa wa ccm kugeuza pale mjengoni sehemu ya kuuchapa usingizi. Acha sasa iwatoe nyongo. Busara anazozitaka mama Mongela zinamaanisha nini hasa? Kama watunga sheria walishindwa kuzitumia busara ndio, ndio hao watekelezaji wa sheria watakiwe kutumia busara? Naomba radhi kama ninakosea, lakini ninachomaanisha kusema ni kwamba mama Mongela hana uadilifu wa kuweza kuzungumzia suala la rushwa nchini. Huyu mama ndie yule aliechukua mshahara mara mbili katika bunge la Africa na kutakiwa kurejesha us dollar hamsini elfu alizolamba kijanja. Nimemfuatilia kwa kauli zake hasa kuhusu maadili ya uongozi, zina utata mkubwa.
 
wabunge wetu woote sehemu kubwa ni 'shake well be for use' hawana wanalolijua kwa sababu wengi wao ni vilaza, but they are there for their own benefits and prostitusion practices


Bora shake well, hutumika baada ya ku-shake. Vijana wa vyuoni wanawaita 'KUNI MBICHI'. Hata uchochee namna gani moto hauwaki.

Huyo Mongella alikuwa wapi wakati sheria inapita? Naamini siku hiyo pia alichukuwa allowance ya kikao. alijua analipwa kwa sababu gani.

Aina hii ya wabunge ni wengi sana na bahati mbaya waliingia ktk siasa kwa sababu za ki-historia. Mjomba anamuita ktk siasa, anadumu humo na baadaye tunamuita muzoefu. Nonsense!
 
Mimi nazani huyu Mongela hafai kuwa mbunge kabisa hawa ndio wale huwa wanapiga makofi tu bila kupitia miswada halafu dokta silaa ana washushua... wanamkejeli... Ikishapita ikiwabana wanaanza kusingizia kama mama yangu MONGELA...Hapa kachemka!
 
wabunge wetu woote sehemu kubwa ni 'shake well be for use' hawana wanalolijua kwa sababu wengi wao ni vilaza, but they are there for their own benefits and prostitusion practices

Hili zito sana .... Kifupi limenistua sana.....so it means wakiwa Dom kutuwakilisha as the always tell us huwa kazi yao ni hiyo uliyosema???? Kaaaaazi kweli kweli.....Lakini kwa nini wanashinda kama tunayajua yote haya??????
 
Oh, she a doctor now, wow, slow your role homegirl! Which website you got your degrees from
 
binafsi huwa siamini kama Tanzania ina bunge....sema tuna kundi la wezi wa mishahara na posho tu.
 
Mongella: Sheria ya Gharama za Uchaguzi itekelezwe kwa umakini


My Take:
Mmezidi Ubishi, wabunge nyinyi, kulalamika mlalamike nyinyi.. tuliwaimbia na kuwapigia kelele hii sheria mbovu mkaizunguka kwa mbwembwe kama watu wanaomzunguka mganga wa kienyeji.. sasa wacha igeuke iwanyofoe ndio mkome. Inakuwaje mtunga sheria anailalamikia sheria ambayo alikuwa na uwezo wa kuifanyia mabadiliko!

Wabunge wanakaa Bungeni kama misukule tu, badala ya kufanya kazi waliyodhaminiwa na walipa kodi wanakwenda kupiga porojo.

BTW hivi vikao vya CCM vina sehemu gani katika serikali ya Jamhuri? Maana wakikutana wao ndio inakuwa kama serikali, kuna haja kubwa ya kutenganisha haya mambo kwa sababu wanatumia vibaya fweza za walipa kodi kwa mambo ambayo hayaihusu serikali na walipa kodi wake.
 
Wale waliokuwa wakila meza moja na "Yesu" baadaye wakageuka kuwa ma"Yuda Iskarioti" wala hawapaswi kuzungumza lolote. Dhambi ya usaliti utaendelea kuwatafuna tu. Bora wakae kimya tu.
 
Wale waliokuwa wakila meza moja na "Yesu" baadaye wakageuka kuwa ma"Yuda Iskarioti" wala hawapaswi kuzungumza lolote. Dhambi ya usaliti utaendelea kuwatafuna tu. Bora wakae kimya tu.

ni kweli kabisa.. sijui kitu gani kilimuingia huyu mama jamani..
 
usishangae sheria hiyo ilipopitishwa hakuwa macho bungeni.................na hakujua hasa kuwa sheria kama hiyo imepitishwa.

wabunge wetu ni vichekesho kwa kweli

Nadhani ingefaa zaidi ingesomeka "Wabunge wa CCm ...." kwa msingi kwamba walau wale wa kambi ya upinzani walijaribu kuweka angalizo. Na hapa ndipo unapoona kwamba mara nyingi wabunge wa CCM hawajengi hoja kwa maslahi ya Nchi na wananchi wake badala yake huwa hawako tayari kukiangusa chama kwa gharama yoyote, ukosefu wa uzalendo.
 
The bottomline: Bunge letu halitungi sheria, linabariki miswaada ya sheria iliyotungwa na wana CCM waliopo serikalini. Kibaya zaidi wabunge wa CCM huona aibu kupinga kitu kilicholetwa bungeni na wana CCM wanzao waliopo bungeni, hata kama ni madudu kiasi gani. Ukada unawapofusha wawapo bungeni, lakini wakitoka nje wanalalamika kama sisi. Sasa solution ni kuwachangua wabunge wengi kutoka opposition.
 
Mwanakijiji unashangazwa na hilo? nilishasema huko nyuma kuwa wabunge wengi wako pale ila hawajui wako pale kufanya nini zaidi ya sehemu ya mlo. Angalia vikao vinavyoendelea sasa hivi, hawapo ,viti vitupu, katika kikao muhimu kama hiki cha bajeti. Hawa sii wawakilishi wa wananchi,wanajiwakilisha wao na familia zao tuu.

Hawa Wabunge wa Tanzania si wawakilishi wa wananchi bali ni wawakilishi wa matumbo yao. Na hali hii ndiyo inasababisha madudu mengi ndani ya nchi yetu kama ya TRL, ATC, EPA, Richmond, Vitambulisho vya Taifa na mengine chungu nzima miaka nenda miaka rudi.
 
Kwani alikuwaje zamani? Aliwahi kufanya nini chanya, sio cheo, kwenye ma institutions aliyoteuliwa teuliwa?

Yaap! maana hata alipokuwa waziri wa Maliasili miaka ya '80 hakufanya lolote na baadaye aliondolewa kwa kile nilichosikia kama kujimwaga na wageni ktk wizara hiyo. She must be a non-perfomer.

Huko Ukerewe jamani kafanya nini? kuna anayejua jimboni kwake kaonyesha njia yoyote? Ni miaka 10 ktk kiti jamani. Hata hivyo nuko CCM ni wengi. Kilichomponza huyu ni kufungua mdomo.
 
Yaap! maana hata alipokuwa waziri wa Maliasili miaka ya '80 hakufanya lolote na baadaye aliondolewa kwa kile nilichosikia kama kujimwaga na wageni ktk wizara hiyo. She must be a non-perfomer.
Si hapo wizarani tu, unajua alivyoharibu UN New York na AU South Africa?
 
Back
Top Bottom