Kwakweli GPA kwa upande wangu imenisadia sana. Katika dunia hii ya ushindani, GPA (kutoka vyuo vinavyoheshimika) ndio kigezo kikuu kinachotumika kukutofautisha wewe mwenye GPA kubwa na yule alieye na GPA ndogo kwenye soko la ajira. Endapo wote mna vigezo vinavyifanana, degree zinazofanana, umri unalingana, na wote ni fresh from school, mwajiri anahamia kwenye kuangalia GPA, huu utaratibu ndio umekuwa ukitumika hasa kwenye mashirika makubwa na taasisi zinazojielewa.
Aidha, kutokana na uhaba wa ajira, unapofanikiwa kupata GPA nzuri, unakuwa na uhakika wa kupata ajira kwenye vyuo vikuu, ambayo unaweza kuitumia kama "stepping stone" kuelekea kwenye ajira unayoitaka. Mshahara wa mwalimu wa chuo kikuu si haba kwa kuanzia maisha, kuliko kubaki mtaani. Zipo scholarship, ambazo kutokana na GPA uliopata, unatumiwa tiket ya ndege, unalipiwa ada, na unapewa hela ya kula kila mwezi kwa kipindi chote unachokua huko europe, na pia unapewa tiket ya ndege kurudi nchini utakapomaliza masomo. Fursa hizi zote zinatokana na kiwango chako cha ufaulu.
Nawashauri vijana waliopo vyuoni, watumie muda wao vyema kusoma kwa bidii, kufaulu vizuri sana, maana hio ndio njia pekee itakayokutofautisha wewe na huyo classmate kwenye soko la ajira. Acheni kudanganyana kwamba huku mtaani fursa hazitegemei GPA. Tia mkazo kwenye GPA utaona manufaa yake.