Nikilewa mniache
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 19,321
- 52,020
- Thread starter
- #41
Mkuu uliishia standard seven, alafu unaandika vizuri hivi? Kweli shule za mkoa wa kilimanjaro ni hatari sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Daah nimecheka sana mkuu kama mazuri yaani, sema mkuu kuna watu wamepitia mazito ila bado wanaishi.
Pole sana mkuu.
Mzee kwani so ungepanga chumba chako ukaishi mwenyewe tu, ukamwambia bro nataka uhuru wa kukaa mwenyewe nimekuwa mtu mzima, tatizo lingekuwa solved kwa muda, kisha ukaanza kutafuta tiba mwenyewe, maana matatizo Kama hayo yapo common sana usingekosa tiba
Mi nilishafikiria kujiua nikiwa mdogo sana kabla sijaanza hata shule, Sababu nilikuwa napigwa sana na hakuna mtu aliyenijali, nikalamba mfuko uliokuwa umewekewa mahindi ya kupanda yenye sumu ya kuuwa wadudi, sikupatwa hata na jambo lolote nipo hai Hadi leo
Kuna kipindi nakaribia kumaliza chuo nikitafakari sitapata kazi, sijuani hata na watu, pa kuishi Sina zaidi ya kijijini kwa wazazi ambako sikupendi, nikashikwa na depression Ila sikunywa sumu, nilikuwa natamani tu nipate ajali nife, Ila nikaja kupata kazi kimiujiza tu..dah
Sent using Jamii Forums mobile app
''Ukaamua kushuka kwenye mti ili ukifa usidondoke'' Mwisho wa kunukuu.... Ha haa pole sana na hongera kwa zawadi ya uhai mpaka leo
Sent using Jamii Forums mobile app
Huu uzi unaweza ukaonekana hauna maana lakini haya mambo yapo. Mimi kuna muda nilipitia hali ngumu sana kwenye maisha, kuliko niliyonayo sasa. Nilikuwa nawaza kujiua ili nipotee maana hata ndugu wanakuona kituko. Wazo moja tu lilikuwa linafanya nikomae, familia. Nikawaza mimi ndio baba na mume katika familia, kama mimi nimekoswa kazi na hela ilhali nakomaa Je! Itakuwaje kwa mke wangu ambaye ananitegemea 100% katika kutimiza mahitaji ya familia? Vp watoto watakapoona nafukiwa shimoni na wasinione tena? Kwann nisisubiri siku yangu ifike ili angalau nisiihuzunishe familia mara mbili. Wakose chakula najua hapa wanawake hufanya lolote ili waishi na watoto wengine mpaka hufanya mambo haramu, nabado wakose ile faraja yangu ya ngoja nikatafute angalau ya uji. Nilikuwa nikiwaza hayo yote halafu unaenda ndugu anatumbua bia unamuomba hata buku anakunyima anakwambia hana pesa. Umasikini usikieni tu kwa watu. Kiukweli kama isingelikuwa familia huenda ningeshajifia kitaaambo. Mshana Jr aliwahi kuelezea humu kuhusu tiba za kiroho. Nilikuwa nikisoma mada zake nahisi 90% nina shida. Katika kosa sifanyi sasahv nikuwambia mtu mipango yangu ya sasa na baadaye. Nikiulizwa unafanya nn, nawaambia niko nyumbani nasubiri ajira. Maisha ni mtihani mkubwa sana kwa binadamu, ukiona dogo kwa mwenzio ni mateso.
Pole sana mkuu! Yote huwa yana mwisho!hakuna moment mbaya kama uwe huna hela na had marafiki wanakukimbia!inachoma sana!
Twin angu alijiua kwa sumu..ikanisumbua balaa hiyo hali..! Ilinisumbua kwasababu toka tunazaliwa hatujawahi achana naye hata kwa lisaa...pia dada yangu nayemfata zilikua haziivi..nilikua nampiga balaa...bas akaambiwa asicheze na mimi..kwahyo na mimi kwa hasira nikama nikamblock...sikumjali kabs ni dada au ndugu..mdogo wangu wa mwisho nimeachana aye miaka mingi sana naye nikawa namuona mtoto..so mtu niliyeamua kuwa naye benet ni twin wangu sikua mtu wa marafikia
Alipojiua wenyeji wakaanza kusema akifa pacha mmoja mwingine hachukui round! Ile hali ikawa inaniboa sana.alafu hom wakawa kama wamenitenga fulani( walikua wananiogopa maana niligeuka kama kichaa kbs..nilikua natembea na panga naona kila mwanafamilia ndo chanzo cha twin kujiua!) Two months later nikaamua kunywa piriton 20! Nilienda tu dispensary nikasema mama kanituma umpe piriton ..nikanywa zote...lol.niliamka niko hosp! Na drip za kutosha..nakumbuka nililala tu sema tumboni kulikua kunavuruga! Sikufa...! Nikapewa mshauri akaniweka sawa kias chake .since then sijapata mawazo hayo .!Mungu alinipa utashi tena!rip B!
Wanaume Waliotaka kujiua kwa sababu ya mapenzi mnatutia aibu
hahaha
Mangi Shirima, pole sana aisee!!
Sijui hata ni kwa nini nimekuita "shirima"
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu unaandika kwa mtiririko mzuri kuliko hata baadhi ya graduate wa chuo kikuu....
Mkuu hii roho huwa haimwachi mtu ipo siku tu itakuondoa cha kufanya nenda kanisa linaloamini wokovu katubu hiyo dhambi kisha uwekewe mikono ili hilo pepo lifukuzwe lisikufuatilie tena.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna ugonjwa mbaya kama depression, ukipata depression iliyo serious na usipojiuwa wewe ni kidume.
Ndio maana wazungu wanafanya kila namna kupambana na hii kitu, wameanzisha hadi center za kuwasaidia watu walio na depression
Shule zifunguliwe urudi shule
Umetisha sana Mangi,wakati wenzako wanakunywa mbege wewe unajichua!!!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Okay, nimeona comments za baadhi ya members wakinicheka kutokana na historia yangu. Siwalaumu maana pengine kuna changamoto zao walishakumbana nazo wakachukua maamuzi ambayo yaweza kuwa kituko kwangu pia.
Tuendelee na kisa cha pili ambacho ndicho kilichonifundisha kukabiliana na hali yoyote ngumu mbele yangu.
Baada ya mkasa ule wa Dar, ilibidi nirudi kijijini maana hata wazazi walishtuka na kushangaa sana. Pilikapilika za nyumbani sikufurahishwa nazo ikabidi nipande mererani kuajiriwa mahali, ambapo mahali hapo nilikaa tangu mwezi wa 7 mwaka 2011 hadi mwishoni mwa mwaka 2013.
Mahali hapo nilikuwa nacheza na maadili kiasi kwamba nilitoka na kitu kama milioni 5.4, ambayo baada ya kutoka pale nilinunua toyo mpya kwa wakati huo ikiuzwa 1,750,000, nikaitumia mwenyewe mpaka mwishoni mwa mwaka 2014, nikaona mbona hela zangu zinaisha tu badala ya kuongezeka?
Ieleweke nilikuwa sio mzoefu kufanya kazi ya kuendesha Toyo kwa ajili ya kujiingizia kipato, hivyo kazi ile nilijikuta mara nyingi hata hela ya mafuta natoa kwenye akiba. Na wakati huo nilishatoka mererani nikaenda Arusha.
Sasa bwana nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nilimwacha mererani, sasa alikuwa ananisumbua kila siku huku akilia kwamba nimemharibia maisha. Nikakaa nikatafakari wee, nikaamua kuhamishia majeshi tena mererani maana huyu mpenzi wangu mimi ndio nilimtoa usichana wake.
Nilipohamia kule nikagundua kumbe nilikuwa nacheza na maisha. Nikachukua ile milioni nikatafuta fremu nikaweka bidhaa za dukani/duka la vyakula, ila baada ya kuweka bidhaa za ile hela yote, vitu vikaonekana kimojakimoja. Nikaamua kuuza ile pikipiki kwa bei ya Tsh 1,200,000, nikaweka ile hela dukani yote. Kaofisi kangu kakapendeza kiasi maana niliweka na kafriji ka laki mbili mtumba.
Kweli ofisi ilichangamka faster maana nilienda mtaa uleule ambao nilikuwa nimeajiriwa mwaka mmoja nyuma. Nikapiga kazi mara ofisi ikawa kubwa, nikawa naweza hata kuweka laki tatu kwa mwezi huku nimeshatoa matumizi yote na kodi, wakati huo nimeshaweka creti zangu za soda kama 30 na zote zimejaa, nikawa nauza na bia. Mambo yakawa mazuri huku mpenzi wangu kashaanza kuitwa mama kijacho.
Ng'ombe wa masikini hazai
haukuisha hata mwaka yule mwenye nyumba akataka nihamie arekebishe nyumba yake.Ndani ya muda mfupi nikapata fremu jirani na pale lakini nilipohamia hapo mambo yakaanza kusuasua. Wateja wakawa wanaishia duka lililokuwa mbele yangu.
Ofisi ikayumba mpaka kwenye mtaji wa kama milioni 3 huku ukizidi kushuka tu. Wakati kura za Lowasa na Magufuli zikihesabiwa, mke wangu nae kabakiza wiki chache ajifungue. Nikampeleka kwa wazazi wangu huku mimi nikaendelea kupambana.
Kutokana na mke wangu alikuwa na umri mdogo wazazi walinishauri awahi hospitali awe anakaa huko mpaka atakapojifungua maana alikuwa akisumbua uchungu japo alienda kukaa week mbili hospitali ndio akajifungua. Hivyo kipindi yupo kule nikawa natakiwa kutuma hela za matumizi kule, baada ya zile wiki mbili akajifungua akakaa mule wiki zingine 2 kuuguza kidonda. Wakati wa kurudi nyumbani kuna gari iliyoenda kumchukua, sasa kutoka lami hadi nyumbani kuna kama kilomita 2, hivyo kulingana na ubovu wa barabara waliyopita kidonda kikaenda kufungukia nyumbani. Siku ileile ikatakiwa nitumie tena hela ya dharura, na baada ya kurudi kule alikaa zaidi ya mwezi mmoja ndipo akaruhusiwa kurudi nyumbani.
Ndani ya ile miezi miwili nilitumia zaidi ya milioni moja huku ofisi nikaanza kuichukia kutokana na bidhaa nyingi kukosekana na nyingine kuwa zipo lakini hazitoki. Mama watoto aliporudi nyumbani ikabidi nikamuone kwanza maana nilimmiss. Baada ya kurudi kazini nikawa nakunywa pombe ili kupunguza stress, na dukani nikawa nafungua ile asubuhi nauzauza ikifika saa tano naenda kunywa hadi kwenye saa kumi au kumi na moja nafungua tena hadi saa nne.
Marafiki wakaanza kunitenga, kunisema na kuchekelea anguko langu. Nikaamua nihamishe lile duka nipeleke kule wanakochimba madini kabisa ambako kunajulikana kama (opeki), nikaweka na matunda na mbogamboga. Wakati huo kuna jamaa nilicheza nae kamari nikamla kama laki na sitini 160,000 ikabidi aweke pikipiki yake rehani, hivyo nikawa naitumia kufuata matunda na vitu vingine sokoni.
Siku moja nikawa nimeshuka kijiji/mji mdogo wa mererani au sokoni nikalala huko ili kesho yake nipande na vitu vya ofisini/ofisi yenyewe ilikuwa ni ya mabati maana kule hawaruhusu kujenga nyumba za kudumu. Sasa siku hiyo ilikuwa ni Ijumaa, nikashuka kijiji nikalala kesho yake nikanunua vitu nikapanda opeck ili nikafungue ofisi. Lahau lah! Nikakuta kofuli ipo chini na mlango upo wazi. Nilipochungulia ndani kulikuwa hamna hata mizani, wezi wamekomba kila kitu.
Nikafungua vitu nilivyofunga kwenye pikipiki nikatupa kule ndani nikageuza kurudi kijiji, nikaingia geto nikachukua redio yangu nikaiweka dukani kwa demu mmoja aliyekuwa rafikiangu nikaiweka bondi akanipa laki moja.
Saa hiyo sijamwambia yeyote chochote na joto la mwili limepanda. Mke ndio huyo alikuwa na mtoto mchanga, sina kitu ataishije na mimi nitaishije? Marafiki watanionaje? Vipi ndugu zangu ambao wanajua chalii ni mpambanaji?
Hayo ndio yalikuwa mawazo yangu. Nikawaza hapa dawa ni kujiua tu ili niondokane na aibu hizi!.
Ile laki niliyoichukua nikaweka mafuta ya Tsh 15,000 nikaenda Rombo nikajifanya hamna tatizo, nikafurahi na mke wangu huku mtoto akiwa anacheka na mimi mpaka nikawa nawaza kughairi mpango wangu mbaya wa kujiua, lakini nikawa sina pa kutokea.
Nikakaa siku 4, siku ya tano nikatoa elfu tano kwenye chenchi zilizobakia alafu nyingine nikampa mke wangu pamoja na simu niliyokuwa nayo tecno H6, nikamwambia mimi sipendi tena kutumia simu za tachi. Nikawasha pikipiki nikaenda sokoni useri pale Rombo nikanunua viroba viwili vikubwa vya konyagi na sumu ileile iliyokosakosa kuniua kule Dar nikiamini hii nikizama nayo porini siponi.
Nikawasha pikipiki nikaenda nayo mbele ya tarakea huko ambako wanaita Rongai, nikaingia kwenye msitu mnene na pikipiki ya yuleyule jamaa ambaye namdai hela ya kamari kwa lengo la kwenda kujiua.
Msitu ule nilijitahidi kupiga pikipiki mafuta hadi nikafika maeneo ambayo nadhani binadamu hajawahi kukanyaga. Huko ni masokwe makubwa kama Goliath, mangedere ya kila aina na mashimo ya ajabuajabu huku pembeni yake kuna mto wenye maji ya baridi sana kiasi kwamba, kesho yake asubuhi maji ya mto ule kuna baadhi Lea ya juu ilikuwa ina ngozi ya barafu/kama kioo chepesi kwa juu.
Nikajitupa chini nikatafakari kidogo kisha nikabugia ile sumu yote kisha nikakata na vile viroba nikanywa vyote nikawa nasubiria kufa sasa. Muda huo ni kwenye saa kumi na moja kuelekea saa kumi na mbili.
Nikakaa pale zaidi ya lisaa hamna chochote! Nikapandwa na hasira kwanini sifi? Nikaanza kula majani ya kila aina pale ili nife lakini wapi.
Nikawasha pikipiki na ulevi wangu nikaanza kurudi kwa upande mwingine hadi nikatokea kwenye shamba kubwa sana lenye miti ya mbao, ambayo ni mirefu lakini imekatwa matawi yake ya chini yote, ukitazama juu huoni anga sababu ya ile miti ilivyobabana kwa juu, alafu chini baadhi ya maeneo wamelima viazi.
Wakati natembea kwenye lile shamba nikahisi kama naishiwa nguvu, baada ya mwendo tena kidogo nikaanguka puuh na lipikipiki langu. Nikaanza kutapika yale majani niliyokula, baadae kidogo nikawa natapika kila kitu, tumbo likawa linauma, nguvu nikawa sina ila za kujigeuza tu.
Usiku umeshaingia alafu barabara niliiacha mbali kiasi kwamba kwa usiku ule sijui hata ilikuwa upande gani.
Kule ilikuwa hata bundi akilia, mwangwi wake hubaki kwa sekunde kadhaa kutokana na ile miti. Niliteseka sana ila baadae karibia kunakucha ndio Nikawa mzima ila mwepesi kiasi kwamba pikipiki yenyewe ilinipa tabu kuinyanyua pale chini. Nikasubiri mpaka kwenye saa moja kasoro jua lilipochomoza, nikapanda pikipiki nikatafuta ule mto nikaenda kufua nguo nikazivaa zikiwa mbichi nikarudi nyumbani nikadanganya nilivyoaga narudi mererani, kuna namna nilichanganyikiwa nikaja kujikuta Rongai msituni nipo hovyo.
Mama alihuzunika sana pamoja na mke wangu, ila wakawa hawana namna bali ilibidi wanipikie supu kwa siku kadhaa ndio afya yangu ikarudi.
Nilipoamka kule msituni asubuhi nilikuta tairi zote hazina upepo, nikatembea hivo hadi home, tube zikawa zimeharibika kabisa. Kakaangu akanipa Tsh 20,000 nikaenda kuweka mpya ndio nikarudi mererani kuendelea na msoto.
Hiki kisa ndio lilisababisha niwe nakabiliana na hali yoyote inayokuja mbele yangu.
Sent using Jamii Forums mobile app









