Tuliowahi kulala Sero/lock up kwa ujinga

Niliingia mahabusu nusu siku Magomeni Polisi ishu ilikuwa hivi:-
Siku hiyo nilikuwa zangu manispaa Kinondoni nafunga data sheet kwani nilikuwa nahama wilaya kwenda wilaya ingine.
Nilivyomalizana na wadada wa masijala Ile nakata kona kuondoka nje kupitia pale jengo la mkuu wa wilaya Kinondoni nikakutana na mkaka smart tu, simjui.... akaniambia dada mambo, unajua muda mrefu nakufatilia tangu unaingia, yaonekana wewe mstaarabu na blah blah nyingiiiii.....at the end akaniomba tukapate lunch pamoja.
Nami kwa kuwa nilikuwa na njaa nikaona kijana yuko smart afu anaonekana mstaarabu ngoja tu niende ila nikamwambia tusiende mbali sana maana file langu limepelekwa kwa afisa utumishi, akasema sawa.
Basi tukatoka nje akaita teksi tukaingia na kusepa.
Tukaenda mpaka mitaa ya Kigogo cha wote kula.
Dereva taksi baada ya kulipwa alivyotaka kuondoka yule kaka akamwambia kaa na wewe ule.
Dereva akakaa na kuanza kula.
Basi ile tunakaribia kumaliza dereva na yule jamaa wakainuka kwenda msalani, jamaa yule smart nikamuona anarudi kisha akachukua funguo ya gari akaingia kwenye ile taksi peke yake akaiwasha na kusepa.
Mie nikasema kwa kuwa walienda wote msalani itakuwa kamuazima gari.
Dereva anarudi haoni gari wala yule jamaa.
Akaanza kuuliza yule bwana ako yuko wapi?
Nikamwambia mie yule simjui nimekutana nae tu Manispaa.
Afu si mlikuwa wote msalani, nikajua mmeenda kuongea umuazime gari.
Weeeee......yule dereva akasema we dada sikuelewi, utanieleza leo.
Mie yule simjui na wala sijamuona akiingia msalani.
Akaanza kujaza watu....watu walivyojaa akawaeleza kila kitu A to Z.
Mie najitahidi kujitetea ila watu hawaelewi somo.
Wengine wakasema sie majambazi wa magari na nionyeshe yule kaka alikoenda.
Jamani omba yasikukute.
Bili ya chakula haijalipwa, soda hazijalipwa na bado nishaundiwa zengwe.
Kila nikijaribu kujitetea naambiwa wewe dada jambazi, onyesha alipo mwizi mwenzio.
Nikwaambia jamani mie simjui, dereva taksi akaniambia mbona ndani ya gari ulikuwa unaongea nae asi if mnajuana, mie nikamueleza niliamua kumchangamkia tu.
Nikaanza kulia pale....nililia kwa uchungu wa kutuhumiwa jambo ambalo sijafanya.

Baada ya majadiliano ya kama dk 5, ghafla trafiki mmoja akaja mpaka pale, akauliza kulikoni ikabidi wamuelezee maana mie hata nguvu sikuwa nazo.
Baada ya trafiki kusikia vile akasema kuwa kapigiwa simu na trafiki mwenzie kuwa kuna taksi imetelekezwa mitaa ya Magomeni Mapipa baada ya kuishiwa mafuta.
Ikabidi mie, trafiki, wapambe na yule dereva twende Magomeni.
Kufika pale mapipa tukakuta ni ile ile taksi ila ndani hakuna mtu.
Nilipiga magoti na kupiga ishara ya msalaba katikati ya barabara.

Mara akaja mkaka tu akasema vipi mbona mmejaa hapa, tukasema tunamtaka mwenye gari hii, yule kaka akasema huyo dereva kaenda kununua mafuta kasema nimlindie gari yake.
Tukamuuliza yukoje akatutajia, yaani ni yule mwizi kabisa.
Askari akasema tumsubiri ila tutoke hapa barabarani ili hata akija asijue.
Basi tukatoka tukajificha.
Dk 5 yule kaka mwizi akaja na kidumu.
Ila anasogelea gari tu watu wakajitokeza akaachia kidumu akakimbia, akaanza kufukuzwa akaenda kukamatiwa kule mtaa wa Dosi.
Basi alipokamatwa akasema mie siko peke yangu niko na huyu dada.
Weeee.....nililoa sana na kuanza kulia.
Tukabebwa wote tukapelekwa Magomeni polisi.
Kufika pale nikalambwa vibao kama 4 na askari kwa usumbufu kuwa nimewasumbua kumbe najuana na mwizi.
Jamani nilikuwa nalia kama mtoto.

Siku zote mtumaini Mungu hakosi msaada.
Ghafla katika shift za askari pale, aliingia askari ambae namjua na ananijua, baada ya kunikuta pale akaniuliza kulikoni ndipo nikaanza kumueleza yaliyonikuta.
Ndipo yule askari akawasiliana na shemeji yangu ambae ni Afisa uhamiaji airport.

Baada ya kufika pale akasema huyu dada ni shemeji yangu na hana tabia hiyo, huyu kaka mwizi anamsingizia tu.
Basi shemeji wakakaa group na wenzake wakaanza kumuhoji yule mwizi.
At the end ikaja kugundulika kuwa kweli siko nae na wala simjui ila nilikutana nae tu katika harakati zangu za ujana.

Basi kesi ikaisha hapo, yule askari aliyenizaba makofi akanitaka radhi.
Shemeji akanibeba kwenye gari aliyokuja nayo akanishusha nyumbani ye akaelekea ofisini kwake.
Yule dereva akapewa gari yake na mwizi akachapwa makofi na mateke kisha akapelekwa Central.

Tangu siku hiyo:
1. Kama sikujui na ukijifanya kunichangamkia ujue utaishia kutukanwa

2. Ofa za wanaume walio smart, nimekoma tena nimekoma kabisa.

3. Ukinisalimia njiani na nikakuitikia ujue una bahati.
Ila All in All ule ulikuwa ni umalaya tu ambao sitakaa niusahau.
Nilijua nimeopoa mkaka smart kumbe kimeo na kuishia mahabusu.

Pole sana mke mwenza.
 
Nimefurahia story yako
Very good
 
Naomba nisitaje majina,ila nikiwa kidato cha sita(6) mimi na wanangu wa utotoni mmoja alikua mtoto wa mkuu wa mkoa Dar maarufu sana na mwingine baba ake alikua Prof pale UD basi kwa wehu wetu yule swahiba angu mtoto wa Prof akaiba risasi kadhaa ambazo mshua wake alikua anatumia kuwindia tukagawana ili tuuze tupate sarafu za x-mass maana tulikua na mbwembwe za ujana hatari duh balaa likaanza yule mwana kapeleka biashara kwa mshua mmoja ambae ni anawinda sana kumbe mzee alikua cop kitambo na basi swahiba kuulizwa kama ana mzigo wa kutosha akatuunganisha na yule mzee cop ili wote tuuze haraka tukajikuta ubaoni pale O'bay alafu mbaya zaidi mkuu wa mkoa kaibuka akasema tunyooshwe kuliko maelezo maana hata Prof tulimuweka matatizoni ndio nikajua wale wana selo kule chini nashukuru mama zetu wakaja kumwaga chozi baada ya siku 5 ndio washua wakalegeza kamba hapo nimeonana na wahuni wangu mara moja kwenye kutoa maelezo ila tulitengwa ila hii ilikua ni mara yangu ya 3 kuingia nyavuni hizo za mwanzo sijawahi kujilamu mpaka kesho nilienda ngome kishujaa hata mshua alikuja kunitoa uku anatabasamu.
 
Pole sana.
Asante mpendwa.
Uso ulikuwa mrefu siku hiyo kama ukuta wa jela
Mie ni smart pia na si mwizi wa magari LOL! Nikikusalimia kitaa naomba unijibu Madame B 🙂🙂🙂
BAK kwa lile tukio aisee....kwanza ungeniona usingeamini.
Wanaosemaga kuwa mwanaume anaweza pigwa vibao na ngumi na mkewe siku ya kufumaniwa kwake alikuwa sahihi.
Nilikuwa mdogo...maana kila ninavyojitetea, naangukia pua.
Weeee....wakaka smart sijui kaulamba mkanda nje, hapana.
Hizi suruali za kadeti naziogopa kinyama
 
Pole sana mke mwenza.
Asante mwenza.
Mwenza ndio maana namtunishiaga kifua mume wetu maana nishanusa selo na kulala hivo siogopi.
We kama unaogopa ujue atatuongezea mke wa 3
 
Thubutu yakee! Mi mwenyewe ninja vile vile, yaani kama alikuwa na huo mpango aghairi mapemaaaa.
 
Yaani nimekutana nae jukwaani hukoooooo anampongeza dada yake Khantwe kupata mume mpya.
Kumbe wifi alikuwa hajaolewa muda wote huo alikuwa anadanga tu.
Aoe aone cheche za wakeze
 
Kumbe ulikuwa hujui!! Wifi mdangaji mzuri tu, hata hapo papya anadanga tu hamna jipya.

Wifi akija mwambie niko sudan.
Huko Sudan mbona ndo huwa naenda kuchota maji jitahidi tu tusikutane maana ntakachokufanya hata mimi mwenyewe sikijui
 
Back
Top Bottom