Tuliowahi kulala Sero/lock up kwa ujinga

Tuliowahi kulala Sero/lock up kwa ujinga

Kumbe ulikuwa hujui!! Wifi mdangaji mzuri tu, hata hapo papya anadanga tu hamna jipya.

Wifi akija mwambie niko sudan.
Mwenza nilikuwa sijui.
Yaani kama wifi tu tumepata.
Wifi mpana, kajaa kuta zote nne.

Ila ndo vizuri atulie na mumewe.
Mambo ya kuanza kugongana macho bar na wifi tukiwa na vi-sponsor vyetu ina huuuuu......
 
Hehehe mnajifanya mnaelewana mnaanza kutusengenya eeh?
Wifi yetu tukuseme wewe tena kipenzi chake toka nitoke na mume wetu!!!
Hizi ni sifa tunakumwagia.
Ushukuru umepata mawifi tunaopatana....hakuna kesi inayokuja kwako
 
Nakumbuka mwaka juzi nililala sero mwaka juzi, kisa wanawake.. Inshu ilikua hivi,, ilikua nyumba ya kupanga tulikua wapangaji wanne kulikua na mwalimu mmoja ameolewa na ana mtoto mmoja uku na uku akashoboka nikamtia mara kibao tu, kuna mpwa wao alikujaga kuwatembelea alikua binti mzuri tu uku na kule nikapita nae ikawa mboga kila nkijisika nakula sa yule dada akajaga akastuka kua namchanganya na mpwa wake (uyu mpwa alikua upande wa mwanaume) Akantukana sana tu nkamtema uyo dada nkaendelea na mpwa wake ilimuuma mno.. Baada ya
siku kadhaa kupita kuna mpangaji mwenzutu akaleta beki tatu mbichi mzuri chuchu yimesimama mwisho wa siku nikaimba nae akaingia king nikamnywa pia,, yule mwalimu alipokuja kujua akaanza kuniponda kwa watu kitaa kua nina ukimwi iliniuma sana, nkamtafutia nafasi na mi nkamtukana kama haitoshi nkamvizia usiku wakati anaoga nkarushia upupu nkasepa zangu nkarudi mda umeenda wakaja kunishitukia kua ni mimi kesho yake wakaenda polisi, ilikua wanidake usiku wakanikosa kesho yake mida ya saa tatu asubui wakanikamata

Kesi ilipokuja kuishia ni baada ya kuweka wazi mambo yote chanzo cha ugomvi nkawaambia askari uyu mi nilikuaga natembea nae na nkatembea na mpwa wake na beki tatu pia sa uyu kinachomsuambua ni wivu mbele ya kaka yangu na kijana wa mwenye nyumba yule dada aliona aibu akasema basi mi naomba aya mambo yaishe yakifika kwa mme wangu ataniua.. Mambo yakaisha na pale nkaama nilikaa polisi toka saa tatu asubui hadi sa kumi na mbili jioni
we nawe itakuwa kweli una UKIMWI sio kwa umalaya huo. na heshima pia huna. mboo unaitembeza kama bakuli. mfyuuu
 
Niliingia mahabusu nusu siku Magomeni Polisi ishu ilikuwa hivi:-
Siku hiyo nilikuwa zangu manispaa Kinondoni nafunga data sheet kwani nilikuwa nahama wilaya kwenda wilaya ingine.
Nilivyomalizana na wadada wa masijala Ile nakata kona kuondoka nje kupitia pale jengo la mkuu wa wilaya Kinondoni nikakutana na mkaka smart tu, simjui.... akaniambia dada mambo, unajua muda mrefu nakufatilia tangu unaingia, yaonekana wewe mstaarabu na blah blah nyingiiiii.....at the end akaniomba tukapate lunch pamoja.
Nami kwa kuwa nilikuwa na njaa nikaona kijana yuko smart afu anaonekana mstaarabu ngoja tu niende ila nikamwambia tusiende mbali sana maana file langu limepelekwa kwa afisa utumishi, akasema sawa.
Basi tukatoka nje akaita teksi tukaingia na kusepa.
Tukaenda mpaka mitaa ya Kigogo cha wote kula.
Dereva taksi baada ya kulipwa alivyotaka kuondoka yule kaka akamwambia kaa na wewe ule.
Dereva akakaa na kuanza kula.
Basi ile tunakaribia kumaliza dereva na yule jamaa wakainuka kwenda msalani, jamaa yule smart nikamuona anarudi kisha akachukua funguo ya gari akaingia kwenye ile taksi peke yake akaiwasha na kusepa.
Mie nikasema kwa kuwa walienda wote msalani itakuwa kamuazima gari.
Dereva anarudi haoni gari wala yule jamaa.
Akaanza kuuliza yule bwana ako yuko wapi?
Nikamwambia mie yule simjui nimekutana nae tu Manispaa.
Afu si mlikuwa wote msalani, nikajua mmeenda kuongea umuazime gari.
Weeeee......yule dereva akasema we dada sikuelewi, utanieleza leo.
Mie yule simjui na wala sijamuona akiingia msalani.
Akaanza kujaza watu....watu walivyojaa akawaeleza kila kitu A to Z.
Mie najitahidi kujitetea ila watu hawaelewi somo.
Wengine wakasema sie majambazi wa magari na nionyeshe yule kaka alikoenda.
Jamani omba yasikukute.
Bili ya chakula haijalipwa, soda hazijalipwa na bado nishaundiwa zengwe.
Kila nikijaribu kujitetea naambiwa wewe dada jambazi, onyesha alipo mwizi mwenzio.
Nikwaambia jamani mie simjui, dereva taksi akaniambia mbona ndani ya gari ulikuwa unaongea nae asi if mnajuana, mie nikamueleza niliamua kumchangamkia tu.
Nikaanza kulia pale....nililia kwa uchungu wa kutuhumiwa jambo ambalo sijafanya.

Baada ya majadiliano ya kama dk 5, ghafla trafiki mmoja akaja mpaka pale, akauliza kulikoni ikabidi wamuelezee maana mie hata nguvu sikuwa nazo.
Baada ya trafiki kusikia vile akasema kuwa kapigiwa simu na trafiki mwenzie kuwa kuna taksi imetelekezwa mitaa ya Magomeni Mapipa baada ya kuishiwa mafuta.
Ikabidi mie, trafiki, wapambe na yule dereva twende Magomeni.
Kufika pale mapipa tukakuta ni ile ile taksi ila ndani hakuna mtu.
Nilipiga magoti na kupiga ishara ya msalaba katikati ya barabara.

Mara akaja mkaka tu akasema vipi mbona mmejaa hapa, tukasema tunamtaka mwenye gari hii, yule kaka akasema huyo dereva kaenda kununua mafuta kasema nimlindie gari yake.
Tukamuuliza yukoje akatutajia, yaani ni yule mwizi kabisa.
Askari akasema tumsubiri ila tutoke hapa barabarani ili hata akija asijue.
Basi tukatoka tukajificha.
Dk 5 yule kaka mwizi akaja na kidumu.
Ila anasogelea gari tu watu wakajitokeza akaachia kidumu akakimbia, akaanza kufukuzwa akaenda kukamatiwa kule mtaa wa Dosi.
Basi alipokamatwa akasema mie siko peke yangu niko na huyu dada.
Weeee.....nililoa sana na kuanza kulia.
Tukabebwa wote tukapelekwa Magomeni polisi.
Kufika pale nikalambwa vibao kama 4 na askari kwa usumbufu kuwa nimewasumbua kumbe najuana na mwizi.
Jamani nilikuwa nalia kama mtoto.

Siku zote mtumaini Mungu hakosi msaada.
Ghafla katika shift za askari pale, aliingia askari ambae namjua na ananijua, baada ya kunikuta pale akaniuliza kulikoni ndipo nikaanza kumueleza yaliyonikuta.
Ndipo yule askari akawasiliana na shemeji yangu ambae ni Afisa uhamiaji airport.

Baada ya kufika pale akasema huyu dada ni shemeji yangu na hana tabia hiyo, huyu kaka mwizi anamsingizia tu.
Basi shemeji wakakaa group na wenzake wakaanza kumuhoji yule mwizi.
At the end ikaja kugundulika kuwa kweli siko nae na wala simjui ila nilikutana nae tu katika harakati zangu za ujana.

Basi kesi ikaisha hapo, yule askari aliyenizaba makofi akanitaka radhi.
Shemeji akanibeba kwenye gari aliyokuja nayo akanishusha nyumbani ye akaelekea ofisini kwake.
Yule dereva akapewa gari yake na mwizi akachapwa makofi na mateke kisha akapelekwa Central.

Tangu siku hiyo:
1. Kama sikujui na ukijifanya kunichangamkia ujue utaishia kutukanwa

2. Ofa za wanaume walio smart, nimekoma tena nimekoma kabisa.

3. Ukinisalimia njiani na nikakuitikia ujue una bahati.
Ila All in All ule ulikuwa ni umalaya tu ambao sitakaa niusahau.
Nilijua nimeopoa mkaka smart kumbe kimeo na kuishia mahabusu.
haaahaaaaaa duh pole sn, simulizi yako inasikitisha. na mwisho imenifurahisha. mwee ukajua umeopoa anaweza kuwa mchumba kumbe jambawazi
 
haaahaaaaaa duh pole sn, simulizi yako inasikitisha. na mwisho imenifurahisha. mwee ukajua umeopoa anaweza kuwa mchumba kumbe jambawazi
Yaani kwa jinsi alivyo wala sikutegemea kabisa kama atakuwa kimeo.
Dah....ila nilipata aibu aisee.
Sitakuja kusahau.
 
Nakumbuka mwaka juzi nililala sero mwaka juzi, kisa wanawake.. Inshu ilikua hivi,, ilikua nyumba ya kupanga tulikua wapangaji wanne kulikua na mwalimu mmoja ameolewa na ana mtoto mmoja uku na uku akashoboka nikamtia mara kibao tu, kuna mpwa wao alikujaga kuwatembelea alikua binti mzuri tu uku na kule nikapita nae ikawa mboga kila nkijisika nakula sa yule dada akajaga akastuka kua namchanganya na mpwa wake (uyu mpwa alikua upande wa mwanaume) Akantukana sana tu nkamtema uyo dada nkaendelea na mpwa wake ilimuuma mno.. Baada ya
siku kadhaa kupita kuna mpangaji mwenzutu akaleta beki tatu mbichi mzuri chuchu yimesimama mwisho wa siku nikaimba nae akaingia king nikamnywa pia,, yule mwalimu alipokuja kujua akaanza kuniponda kwa watu kitaa kua nina ukimwi iliniuma sana, nkamtafutia nafasi na mi nkamtukana kama haitoshi nkamvizia usiku wakati anaoga nkarushia upupu nkasepa zangu nkarudi mda umeenda wakaja kunishitukia kua ni mimi kesho yake wakaenda polisi, ilikua wanidake usiku wakanikosa kesho yake mida ya saa tatu asubui wakanikamata

Kesi ilipokuja kuishia ni baada ya kuweka wazi mambo yote chanzo cha ugomvi nkawaambia askari uyu mi nilikuaga natembea nae na nkatembea na mpwa wake na beki tatu pia sa uyu kinachomsuambua ni wivu mbele ya kaka yangu na kijana wa mwenye nyumba yule dada aliona aibu akasema basi mi naomba aya mambo yaishe yakifika kwa mme wangu ataniua.. Mambo yakaisha na pale nkaama nilikaa polisi toka saa tatu asubui hadi sa kumi na mbili jioni
Hehehehe we jamaa special case
 
Asante mpendwa.
Uso ulikuwa mrefu siku hiyo kama ukuta wa jela

BAK kwa lile tukio aisee....kwanza ungeniona usingeamini.
Wanaosemaga kuwa mwanaume anaweza pigwa vibao na ngumi na mkewe siku ya kufumaniwa kwake alikuwa sahihi.
Nilikuwa mdogo...maana kila ninavyojitetea, naangukia pua.
Weeee....wakaka smart sijui kaulamba mkanda nje, hapana.
Hizi suruali za kadeti naziogopa kinyama
Hahah eti unaogopa suruali za kadeti.
 
Mwaka 2014 niliwekwa ndani polis mwenge kwa kosa LA kupiga konda na dreva nadani ya gari niitokea Bagamoyo aisee masaaa matatu nilihis mwaka Ila niilificha Siri mpaka kesho home hakuna anayejua
 
Duh....hahaha
Umenikumbusha Kuna jamaa Aliwekwa lok up central ndugu zake kila wakimpelekea chakula kizuri polisi walikuwa wanakutia ndani wao juu kwa juu jamaa ndani anambulia kula Mikate tu

Ova
hahaa
noma sanaaaa!
 
Kabisa.
Bora nikutane na jambazi lenzangu mvaa jeans kuliko hawa smart wavaa kadet na vipensi na mashati ya kuchomekea
Hahah.kweli ukingatwa na nyoka hata nyasi zinakushtua.ila sio wote walio smart wako hivyo.
 
Kuna siku nilienda kutoa ushirikiano fulani polisi kwa kesi ya jamaa yangu sasa nikawa namtetea wao wanataka nimkandamize mchizi nikawagomea. Nikawaambia kuanzia sasa sitaki kuongea chochote nimeghairi sasa kuna mmama mmoja akawa jeuri akawaambia wenzie kama hataki kuongea tumeweke mahabusu nikamuambia tunapigana kwanza mukinipiga mnaniweka mahabusu na nikiwapiga nawafi*** nikawaambia hivyohivyo sijui ile kesi iliishaje maana kila mtu aliingia njia yake.
 
Mm nilimzaba makofi mawili Sirro siku nmetoka marekani nikijua ni mshkaji tu...jamaa walinipelemba balaa
 
Niliingia mahabusu nusu siku Magomeni Polisi ishu ilikuwa hivi:-
Siku hiyo nilikuwa zangu manispaa Kinondoni nafunga data sheet kwani nilikuwa nahama wilaya kwenda wilaya ingine.
Nilivyomalizana na wadada wa masijala Ile nakata kona kuondoka nje kupitia pale jengo la mkuu wa wilaya Kinondoni nikakutana na mkaka smart tu, simjui.... akaniambia dada mambo, unajua muda mrefu nakufatilia tangu unaingia, yaonekana wewe mstaarabu na blah blah nyingiiiii.....at the end akaniomba tukapate lunch pamoja.
Nami kwa kuwa nilikuwa na njaa nikaona kijana yuko smart afu anaonekana mstaarabu ngoja tu niende ila nikamwambia tusiende mbali sana maana file langu limepelekwa kwa afisa utumishi, akasema sawa.
Basi tukatoka nje akaita teksi tukaingia na kusepa.
Tukaenda mpaka mitaa ya Kigogo cha wote kula.
Dereva taksi baada ya kulipwa alivyotaka kuondoka yule kaka akamwambia kaa na wewe ule.
Dereva akakaa na kuanza kula.
Basi ile tunakaribia kumaliza dereva na yule jamaa wakainuka kwenda msalani, jamaa yule smart nikamuona anarudi kisha akachukua funguo ya gari akaingia kwenye ile taksi peke yake akaiwasha na kusepa.
Mie nikasema kwa kuwa walienda wote msalani itakuwa kamuazima gari.
Dereva anarudi haoni gari wala yule jamaa.
Akaanza kuuliza yule bwana ako yuko wapi?
Nikamwambia mie yule simjui nimekutana nae tu Manispaa.
Afu si mlikuwa wote msalani, nikajua mmeenda kuongea umuazime gari.
Weeeee......yule dereva akasema we dada sikuelewi, utanieleza leo.
Mie yule simjui na wala sijamuona akiingia msalani.
Akaanza kujaza watu....watu walivyojaa akawaeleza kila kitu A to Z.
Mie najitahidi kujitetea ila watu hawaelewi somo.
Wengine wakasema sie majambazi wa magari na nionyeshe yule kaka alikoenda.
Jamani omba yasikukute.
Bili ya chakula haijalipwa, soda hazijalipwa na bado nishaundiwa zengwe.
Kila nikijaribu kujitetea naambiwa wewe dada jambazi, onyesha alipo mwizi mwenzio.
Nikwaambia jamani mie simjui, dereva taksi akaniambia mbona ndani ya gari ulikuwa unaongea nae asi if mnajuana, mie nikamueleza niliamua kumchangamkia tu.
Nikaanza kulia pale....nililia kwa uchungu wa kutuhumiwa jambo ambalo sijafanya.

Baada ya majadiliano ya kama dk 5, ghafla trafiki mmoja akaja mpaka pale, akauliza kulikoni ikabidi wamuelezee maana mie hata nguvu sikuwa nazo.
Baada ya trafiki kusikia vile akasema kuwa kapigiwa simu na trafiki mwenzie kuwa kuna taksi imetelekezwa mitaa ya Magomeni Mapipa baada ya kuishiwa mafuta.
Ikabidi mie, trafiki, wapambe na yule dereva twende Magomeni.
Kufika pale mapipa tukakuta ni ile ile taksi ila ndani hakuna mtu.
Nilipiga magoti na kupiga ishara ya msalaba katikati ya barabara.

Mara akaja mkaka tu akasema vipi mbona mmejaa hapa, tukasema tunamtaka mwenye gari hii, yule kaka akasema huyo dereva kaenda kununua mafuta kasema nimlindie gari yake.
Tukamuuliza yukoje akatutajia, yaani ni yule mwizi kabisa.
Askari akasema tumsubiri ila tutoke hapa barabarani ili hata akija asijue.
Basi tukatoka tukajificha.
Dk 5 yule kaka mwizi akaja na kidumu.
Ila anasogelea gari tu watu wakajitokeza akaachia kidumu akakimbia, akaanza kufukuzwa akaenda kukamatiwa kule mtaa wa Dosi.
Basi alipokamatwa akasema mie siko peke yangu niko na huyu dada.
Weeee.....nililoa sana na kuanza kulia.
Tukabebwa wote tukapelekwa Magomeni polisi.
Kufika pale nikalambwa vibao kama 4 na askari kwa usumbufu kuwa nimewasumbua kumbe najuana na mwizi.
Jamani nilikuwa nalia kama mtoto.

Siku zote mtumaini Mungu hakosi msaada.
Ghafla katika shift za askari pale, aliingia askari ambae namjua na ananijua, baada ya kunikuta pale akaniuliza kulikoni ndipo nikaanza kumueleza yaliyonikuta.
Ndipo yule askari akawasiliana na shemeji yangu ambae ni Afisa uhamiaji airport.

Baada ya kufika pale akasema huyu dada ni shemeji yangu na hana tabia hiyo, huyu kaka mwizi anamsingizia tu.
Basi shemeji wakakaa group na wenzake wakaanza kumuhoji yule mwizi.
At the end ikaja kugundulika kuwa kweli siko nae na wala simjui ila nilikutana nae tu katika harakati zangu za ujana.

Basi kesi ikaisha hapo, yule askari aliyenizaba makofi akanitaka radhi.
Shemeji akanibeba kwenye gari aliyokuja nayo akanishusha nyumbani ye akaelekea ofisini kwake.
Yule dereva akapewa gari yake na mwizi akachapwa makofi na mateke kisha akapelekwa Central.

Tangu siku hiyo:
1. Kama sikujui na ukijifanya kunichangamkia ujue utaishia kutukanwa

2. Ofa za wanaume walio smart, nimekoma tena nimekoma kabisa.

3. Ukinisalimia njiani na nikakuitikia ujue una bahati.
Ila All in All ule ulikuwa ni umalaya tu ambao sitakaa niusahau.
Nilijua nimeopoa mkaka smart kumbe kimeo na kuishia mahabusu.
Wifi jamanii pole nilikuwa sijaona huu mkasa wako pole sana my wife
 
Daaah! Ebwanaeee Sikuwahi kuwaza kitu kama hiki Komrade. Lakini kwa kutambua nakuthamini hisia zako ngoja nijaribu mkuu! Ila kwakuwa itakuwa ni habari ya kweli basi kuna baadhi ya majina ya mahali na ya wahusika sitaweza kuyataja kwa usalama wangu na wao pia....

◆Nilizaliwa uamishoni takribani miaka thelathini na kitu iliyopita mkoani Arusha. Asili yangu ikiwa moja ya makabila hodari nchini Tanzania. Katika malezi na makuzi nilifanikiwa kuwa na mdogo wangu wakuzaliwa wakike. Pia hatukuwa sisi wenyewe tu kama watoto wa baba na mama mmoja bali tulikuwa na ndugu zetu wengine kadhaa wakiume na wakike ambao baba yetu aliweza kuwazaa kwa mama wengine ambao sisi tuliwaita dada na kaka zetu. Maisha yalikuwa mazuri sana enzi hizo na ilikuwa kama ndio fashion ya kipindi hicho. Baba yetu alikuwa na pesa nyingi ambapo wakati wote sisi hatukuwa na mahitaji yakumshinda hata kidogo. Alihakikisha watoto wake hatupati shida yoyote kwani ni sisi wawili tu ndo tulikuwa tunaishi na baba yetu. Wale ndugu zetu wengine walikuwa wakiishi na mama zao huko walipo. Ila pamoja na upendo mwingi kwa baba yetu hatukuwa tukiishi na mama yetu mzazi bali tulikuwa tunaishi na mama zetu wadogo ambao kwa lugha ya leo tunawaita Mama wa Kambo. Kwetu sisi haikutusumbua kwakuwa kwanza tulikuwa wadogo sana na pia baba alikuwa anafedha hivyo hata kuteswa ilikuwa ni ngumu. Baba yetu alikuwa mkali sana na mkorofi na alikuwa mywapombe lakini si mlevi. Wakati fulani anaetoka safari kalewa hata kama iwe saa ngapi lazima tuamshwe tulenae chakula atuulize maswali ya shule sasa ikitokea tumekosea daaah tunapigwa vibaya mnoo. Hajali ni usiku au ni mchana na hachagui chakukupigia iwe mwiko,mkanda wa suruali,makofi yeye twende kazi hii ilinifanya mnyonge sana hasa ninapokuwa kweli nimekosea. Kuna wakati alishawahi kunipiga mpaka nikashindwa kukaa na hata kwenda shule sababu ya maumivu lakini hii yote pia ilichangiwa na mama yetu mdogo yule mama namkumbuka vizuri sana hakuwa hana hata chembe ya huruma kwa baba yangu naamini alimpendea fedha tu na wala si kitu kingine.
Nikiwa darasa la nne na mdogo wangu akiwa la pili au la kwanza hivi tulifunga shule na likizo yetu ikabidi tuchukuliwe na huyo mama yetu mdogo mpaka kijijini kwao mkoa mwingine kabisa. Tulikaa kule kwa upendo kabisa na baba yetu alikuwa akitutembelea mara moja moja. Familia yao mama yetu mdogo nao walikuwa vizuri tu baadhi ya ndugu zake mmoja alikuwa akifanyakazi benki,mwingine alikuwa mfanyabiashara na mwingine alikuwa ameolewa nje ya nchi ila mtoto wake wa kike alikuwa pale kijijini na kijana wao wa mwisho alikuwa akisoma sekondari....
Baba wa familia hiyo alikuwa mkusanya ushuru katika kampuni moja ya mabasi. Ila huyu mjukuu wao wa kike alionekana ni malaika pale ndani sisi tulikuwa si kitu wala si chochote ila bado tuliheshimu na kutii vyote. Baada ya kukaa kwa muda huko ikabidi twende shule tu kwani zamani hizo hakukuwa na sheria zuizi sana tena kwa shule za msingi hakukuwa na tatizo. Hivyo kiujumla maisha yalikuwa salama tu.
◆Siku moja sikumbuki nilikosa kosa gani jamani ila nakumbuka mama yangu mdogo alinipiga sana na akanambia ngoja baba yako anakuja kesho na lazima nitamwambia. Nilijihisi marehemu wa muda. Nilikaa migombani chini ya mkahawa mmoja nikawaza nakuwazua nikiona vile jinsi kesho nitakavyokuja kupigwa na babangu sijui nitakuwaje Mungu wangu. Maana huyu mamangu mdogo alikuwa akisema jambo kwa baba aisee hauna bahati maana baba hatakuacha na kama ikitokea amekuacha jua umewekwa kiporo.
Baada ya muda mrefu kukaa pale chini ya mkahawa nikapata wazo rahisi sana nikajiuliza hivi sumu si inaua? Sasa kwanini usubiri uje uuliwe na baba yako si bora unywe sumu! Oooh Yes! Nikapata mwanga sasa nini chakufanya. Haraka nikaamka nikaelekea stoo ambayo ilikuwa imejengwa shambani kwa ajili ya kuhifadhi nafaka na mashine ndogondogo za kilimo. Niliingia ndani nakuanza kutafuta dawa ambayo ingenisababishia kifo ili tu nisikutwe. Baada ya kutafuta sana nilipata mfuko ukiwa na dawa ya bluu sikujua ni dawa gani lakini mi niliona tayari nimeshapata ninachokitafuta.
Ilikuwa kama saa 12:45 jioni nilienda kuoga ili nisijekutafutwa. Baada ya kumaliza kuoga nilirudi stoo kwenda kunywa ile dawa (Blue Copper). Kwakuwa ilikuwa ni ya unga nifanya kulamba. Niliilamba yakutosha halafu nikarudi ndani nikijua sitachukua muda mrefu nitakuwa nimeshakufa. Nilikuta chakula mezani nikala haraka haraka kisha nikaenda kulala. Ilikuwa imekaribia saa mbili usiku nilipoanza kutapika. Niliulizwa umekula nini nikasema sijala kitu ila matapishi ni ya rangi ya bluu. Sikukumbuka chochote hadi kesho yake nilipojikuta naruhusiwa kuondoka kurudishwa nyumbani. Mungu wangu sijafa!! Mbona ndo kama nimejiwashia moto tena moto wa mafuta ya petrol!! Nitamwambia nini baba yangu anielewe?? Isitoshe mama jana alisema leo ndio atakuja? Hapo ndio unasikia unatamani ardhi ipasuke utumbukie ndani usikutwe. Nikaomba sala zote nikalia moyoni kwa uchungu sana nikasema haya yote nahisi yasingelitokea kama mama angelikuwepo. Nilichoka akili na mwili huku wasiwasi ukiwa mkubwa sana. Kila nikitafakari ujio wa baba yangu nilichanganyikiwa. Ilipofika usiku na sikumuona baba amani ilirejea kidogo kwani wakati huo magari ya kufika huko kijijini mwisho ilikuwa ni saa 1 jioni. Sasa ikabidi niamue jambo moja kuliko kukutwa na kujitafutia kifo au kilema cha maisha bora nitoroke nyumbani niende kusikojulikana. Asubuhi na mapema niliwahi kuamka nikavaa nguo zangu kawaida kisha nikaondoka. Nikaenda kupanda basi kuelekea mjini. Bahati nzuri watoto hatukuwa tukitozwa nauli hivyo nilifanikiwa kusafiri bure. Nilifika mjini mchana njaa inauma ila kwakuwa nimeshatoka kwenye eneo la mashaka na wasiwasi nilihisi kushiba kila wakati. Ilikuwa siku ngumu sana kwangu kuisha siku hiyo kwani nilizoea kupata kila kitu kwakuletewa na wazazi. Nilijitahidi kuficha aiba yangu na ya watoto wengine pale stendi lakini haikuweza kufichika kwani pamoja na kujifananisha na watoto wa mitaani lakini sikufanania kabisa. Usiku ule nilikaa mahali nikalia kwauchungu sana nikiwaza nitakula nini, nitalala wapi, na kwanini niko hapa!!! Machozi na kilio kilizidi ambapo nikutwa na baadhi ya watu nikilia, waliniuliza kwanini niliwajibu kwamba kuna vijana wamenipiga. Hivyo niliachwa pale. Baridi ilikuwa kali usiku nikiwa nimejikunyata pembezoni mwa mizigo ya abiria wakati wote kukiwa na kelele za magari na watu pia nikajikuta nalala. Nilishtushwa na konda aliekuwa anapakia mizigo saa kumi na mbili kasoro akinitaka niamke ili achukue mizigo. Unaitwa nani? Unaenda wapi? Wazazi wako wako wapi? Ni maswali ambayo wakati wote kila alieniona asubuhi ile aliniuliza wakati huo mimi sikutaka kabisa kuulizwa maswali hayo. Asubuhi kulipambazuka na safari ya mtoto wa mtaani (Chokoraa) ikaanzia hapo.....
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom