Tuliotoka tangu Darhotwire tukutane hapa

Tuliotoka tangu Darhotwire tukutane hapa

....baabake!Zeze DHW;mmenikumbusha mtoto mmoja wa kitanga mtoto wa K'koo blalbasket

...IFM computer lab,
..saa 2 usiku!



.kama umo humu we mtoto njoo chemba
 
Habari wanajamvi. Kabla ya kuanza kwa mtandao wa JF kulikuwa na mtandao wa DHW ambao member wengi tulihama tukahamia huku

Kama ulikuwepo Enzi zile naomba nyoosha mkono juu
Dah....DHW ni kitambo sana ....... nakumbuka vizuri .... ilikuwa chatzone.de ...nilipenda Zaidi Trivia games..tulikuwa na ushindani mkubwa sana na wazee wenzangu wa kijiweni 😀😀😀😀
 
Enzi HIZO nakumbuka Nlikuwa natumia desktop.....ISP yangu ili simply wireles ya csts net kwa mwezi Ilikuwa balaa Malipo...
Dhwire kulikuwa n'a jamaa anajiita hardlife wengine siwakumbi nshawasahau

Ova
 
Nipooooo. Haaaahaaa umenikumbusha mbali sana niliwahi kupata demu coz of DHW
 
miaka ile darhotwire ilikuwa tunaenda kufanya mambo yetu internet cafe!!!!

huku una yahoo messenger au msn messenger......

siku zimesogea sana.
 
Dar hotwire wakati huo nilikuwa sijui kompyuta na smart phone hazikuwepo plus nilikuwa nalima vingamba huko kwetu so nasubiri wa mjini mkomenti nisome historia( historia huwa ni burudani-huwa nafurahi nikisikia tulivaaga pekosi na bugaluu) haya tiririkeni na mjimwage wana dar hotwire.
 
Dah....DHW ni kitambo sana ....... nakumbuka vizuri .... ilikuwa chatzone.de ...nilipenda Zaidi Trivia games..tulikuwa na ushindani mkubwa sana na wazee wenzangu wa kijiweni 😀😀😀😀
Hata Mimi Trivia nilikuwa mdau pigana sana vikumbo na kina Lorenzo, Ccomputer huyu alikuwa anajua majibu yote alafu alikuwa black american anajibu faster mno, Valentinoo, Ggenius Mkuu wewe ndie yule ulijiita Konda?

Mwanzo Mwanzo wa Jambo forums na Jamii Forums ulikuwa ukizungumza neno dhw unakula ban au thread inafutwa hahahaha ilikuwa like adui mkuu
 
Back
Top Bottom