Tuliotoboa maisha bila kuwa na godfather njooni tujadiliane

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
6,276
21,452
Godfather ni mtu atakayekubeba kukusaidia kupata ajira au mtaji wa kuanzisha maisha, sio rahisi hapa nchini Tz kufanikiwa bila kuwa na 'godfather', anaweza akawa baba yako, mama yako, rafiki au mjomba,

Ila pia tupo wachache tunaojiita "born lucky" tulioweza kupambana (hussle) na kutoboa ili kusimama kimaisha, bila kubebwa na 'godfather'

Kuna siku nilitembea Mkoa wa Dodoma kusalimia rafiki, ilikuwa siku ya Jumapili kama leo, nilikuwa kwenye matembezi ya asubuhi kujionea jiji jipya la Dodoma, nikakuta foleni ya vijana, katika godown ya wachina kule wanakojenga ringroad, ilikuwa ndefu mpaka nje nikauliza kulikoni hapa kijana moja kaniambia waChina wanatoa ajira, mmh!!!!!! nikaguna kwanza hapo ndo nimemaliza chuo ila bado graduation.

Nikaamua kupanga foleni bila hata maombi or application nikajisemea ntajieleza huko huko, kumbe kule wanaandikisha vibarua (cheap labourers) wa kulipwa sh7000 kwa kutwa, nilivyofika kwenye panel ya usahili, nikaanza kujieleza kwamba nilifanya application ila nimekuja kwanza kujua kama na sisi wasomi (graduates) tunahitajika, wakaniuliza ulisoma nini nikajieleza wakaniambia wewe kaa pembeni kwanza, baada wote kumalizika wakanihoji upya tena wakaakajiridhisha kwamba mimi ni graduate japo sina vyeti, to make the long story short nikapewa kazi ya assitant field supervisor, boss wangu alikuwa mchina mimi nikafuatia.

Mshahara na pesa niliokusanya ndo ulikuwa mtaji wangu mpaka leo japo kazi ilidumu kwa miaka miwili tu. Lakini mpaka leo rafiki yangu haamini kwamba sikuwa na appointment ya kazi kwamba sikuenda kwa ajiri yake, nilienda kwa ajiri ya kazi tu.
 
Mimi ni yatima lakini Hapa nilipo nafanya kazi kwenye moja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa. Sikuwa na mtu ninayemfahamu wala aliyenipambania. Kikubwa ni kumcha Mungu, baada ya hapo Mambo yatakuwa yanaenda kwa upesi bila kutarajia.
Sawa mkuu ila uyatima wa mtoto wa kiume mwisho miaka 18, hapo hamna kutegemea mzazi, hapo ndo unafanya hassling yako,
 
Kabla sijachangia nisaidie Tafsiri ya kutoboa kwenye maisha ni ipi? Na una uhakika umetoboa kweli ?
Kutoboa maisha kwa standard life za bongo au kipimo chetu kua na wakika na vifuatavyo hapa Tz tuhitaji mengi

1. Uhakika wa kula milo mitatu.
2. Shelter au nyumba ya uhakika.
3.clothing nguo za uhakika.
4. Akiba ya pesa benki
5. Usafiri wa wakika
6. Amani ya mwoyo na akili
7. Bima ya afya au wakika wakupata matibabu.nk
 
Kutoboa maisha kwa standard life za bongo au kipimo chetu kua na wakika na vifuatavyo hapa Tz tuhitaji mengi

1. Wakika wa kula milo mitatu.
2. Shelter au nyumba ya wakika.
3.clothing nguo za wakika.
4. Akiba ya pesa benki
5. Usafiri wa wakika
6. Amani ya mwoyo na akili
7. Bima ya afya au wakika wakupata matibabu.nk
Akiba kwanzia Shingapi?
 
Wakika ndio nini?
Au unamaanisha UHAKIKA?
 
Mbona hujamnshukuru Mwenyezi Mungu? Hapo ni Mwenyezi Mungu ndio amekusaidia ukapata kazi na mtaji wa biashara. Mshukuru Yeye kwa kutoa sadaka kwa wahitaji.

Na pia uache kujisifu kwamba hapo umepambana mwenyewe na kwamba mafanikio yako yametokana na juhudi zako mwenyewe kwani Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kujisifu na hawapendi wenye viburi. Siku si nyingi utajikuta mikosi inaanza kukuandama na biashara zinafilisika.

Sifa na utukufu vyote ni vya Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na dunia ndio aliyokuwezesha.
 
Mkuu na mshukuru sana Mungu kila siku najua kwamba kudra zake huwezi kufanikisha jambo lolote, ndo maana natumia neno born lucky.
 
Kwa uzoefu wangu, kutoboa kwenye maisha, ukiacha elimu, na kusaidiwa, wakati mwingine, inahitajika "Gods favour" Kufika maeneo Fulani,
Tulikuwa kumi na moja, nafasi ipo moja tu, nono vibaya Sana,
Shirika lenyewe sikuwahi kujua kama linatoa ajira, hiyo post alinitumia jamaa yangu, kwa SMS akaniambia we omba, na mimi naomba,atakae pata, atakua anamtoa mwenzie japo buku la nauri(kama utani vile), usaili tuliitwa wote, ye ye hakutokea, tukawa kumi tu, nilipoingia chumba cha usaili, nikakutana na panel, nikahapa hii nafasi ni yangu! Sitapigika tena na maisha,
Fast forward, niliipata, nipo nakula shushu, huwa namkumbusha Yule jamaa yangu, kila tukikutana, kwamba bila yeye,ningekuwa bado napigika kitaa .
 
Mimi ni yatima lakini Hapa nilipo nafanya kazi kwenye moja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa. Sikuwa na mtu ninayemfahamu wala aliyenipambania. Kikubwa ni kumcha Mungu, baada ya hapo Mambo yatakuwa yanaenda kwa upesi bila kutarajia.
Dah Mzee Niko nahangaika sanaa kutafuta Kazi za UN na TAASISI zake..
Yaani sijawahi itwa hata interview ila bado napambana.
Nishafanya sanaa application.

Hongera sanaa.

#YNWA
 
Watu wanaharibu Uzi, baada ya kuelezea Kama mleta uzi maneno maneno ya nje ya mada, watu tunataka tusome umetoboaje bila kushikwa mkono.
 
Akiba ni akiba ata 500,000 inatosha kwa dhalura za maisha wengine wana akiba mpaka mamillion, ya pesa.
😂😂😂😂.. dogo kma kutoboa ni huku😂😂😂😂😂.. uzi ufutwe tuliojiajiri, walioajiriwa woote tumetoboa😂😂😂😂. Maana njia pekee kundi hizo mbili ishindikane 500 kwenye akiba ni ulevi wa kupindukia😂😂😂.
Dogo jitafakari.. endelea kupambana, bado sana usijipe moyo na viuzi hvi😂😂😂😂. Nimecheka leo
 
Back
Top Bottom