Msoto wa maisha Dar es Salaam ulivyonifanya nitamani kuwa mwizi na mhujumu uchumi

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Hivi ni visa vya kweli vinavyotokea ili tujifunze graduate na wapambanaji wengine someni hapa. Hakuna cha nitaendelea nitafupisha zaidi iwe fupi.

Ni Mimi pastor prakatatumba abaabaabaabaa etumba etumba.

Ndugu zangu kwanza nikiri jiji la Dar es Salaam watu wanapambana saaana tena saana, kuna variation kubwa Sana kati ya wenye nacho na wasiokua nacho lakini haiondoi wewe kufurahia jiji, kuna bata la pesa ndefu Kama huko kidimbwi (sijawahi kufika), na kuna bata letu sisi wahangaikaji Kama manzese uwanja wa fisi, Sudan temeke n.k.

Nilitokea tabora kuja kuhangaika na maisha baada ya kumaliza chuo na kukaa mtaani takribani mwaka mzima mzee alivyouza pamba akanipatia million mbili, nilipewa husia takribani masaa 7 kwamba nikipoteza huo mtaji nisimwambie kitu nipotee kabisa nisirudi nyumbani maana hiyo ndio ilikua akiba yake na Mimi ndio kijana mkubwa nina wadogo zangu kama 8.

Nilifikia dar tandale kwa tumbo kwa mshikaji wangu tulisoma nae tabora lakini hakufanikiwa kuendelea na masomo, Mara ya kwanza alinichangamkia huku nikimueleza mipango yangu ya biashara n.k, nilikua sijui sehemu yoyote ile dar wala sijui biashara yoyote ile huyo jamaa yangu alikua anafanya kazi kiwandani tegeta wazo ( sina hakika Kama panaitwa hivyo) , akaanza kunitembeza kujua jiji ile kunitembeza tu week Mbili Kama laki 5 ilishakata nikajipa moyo bado hela hipo, mshikaji wangu akawa hachangii chochote nikawa nanunua misosi nikasema fresh jamaa ananisitiri.

Kufupisha story million 1.5 ilikatika ndani ya mwezi na nusu hivi Mimi bila kujua imeenda wapi (usije mjini bila mipango).

nilipobakiza laki tano nikaenda kariakoo nikanunua "sendoz" za kike kwa laki 4 na 80 hivi (nilikua nikipita naona watu wanauza sana hizo sendo wadada wamewazunguka wananunua nikaona fursa) jamaa akanikodisha Eneo lake 10,000 kwa siku pamoja turubai lake (hakunambia Kama migambo wamekataza).

Mimi sikuelewa watu ni wengi nikamwaga chini nikaanza kuuza zile sendoz nikajisemea moyoni biashara si ndio hii? Chap chap nimeshauza kama 70,000 huku nafurahia moyoni ghafla nikaona watu wanakimbia kimbia Mimi sikujali nilikua sielewi kinachoendea kuja kushtuka nimepigwa rungu la kisogo kwa akili yangu ikaanza kuniambia hawa watakua ni majambazi nini?

Hapo network imekata kichwani damu zinavuja ikabidi na Mimi nianze kukimbia kuelekea uelekeo wa wa watu wanapokimbilia, shati langu limeloa damu nikafika sehemu nikanunua maji ya kandoro nikanawa kichwa hapo nimevimba haswa kurudi kwenye mzigo wangu sikuukuta wakanambia migambo wamechukua itabidi niende nikafatilie niandae faini n.k

Nilikuwa na maumivu makali ya kichwa uchungu wa jiji la Dar nikaanza kuuona hapo kumbuka nina mwezi mmoja tu Dar, nikarudi gheto kulala huku nikiwa na mawazo tele hela nimebakiza elfu 80, mzigo wangu umechukuliwa "nikaconfirm" msemo wangu ambao unasema ukizaliwa maskini ni ngumu Sana kutoboa kwenye haya maisha yani ni ngumuuu, nikikaa barabrani nasema hawa walipataje hayo magari? Majumba yalioko mbezi kule, goba nikawa najiuliza nitatoboa kweli? Kwa 80,000?

Mshikaji wangu alikua anapenda kwenda viwanja so alikua ananipeleka maeneo mbali mbali naona vijana wadogo wakiendesha magari wameacha vioo wazi namimi nimetokea bush kuona gari labda la serikali nilikua napata mawazo Sana.

Turudi kwenye story baada ya kupigwa rungu la kichwa nimerudi ghetto mshikaji baada ya kumuelezea yaliyonikuta nikamwambia anitafutie kazi pale kiwandani nadhani kilikua kiwanda cha cement akanambia akirudi kesho yake kutoka job ataniambia.

jioni jamaa kurudi kanambia imeshindikana kupata kazi na anataka kuoa mpenzi wake anakuja so nitafute makao mengine (kumbuka hajawahi kunambia habari za mpenzi wala nini) kwakua Mimi ni mtu mzima nikajiongeza kwamba hapa hela imeisha sitakiwi.

To cut story nikaenda pale tandale kwa wauza mchele nikawa napiga story na wabeba mizigo pale, gari likaingia limetoka mbeya nikaomba kazi ya kupakua mchele kila gunia 500 nikafanya kazi ya kupakua mchele mpaka saa Saba usiku.

1653291133574.jpg

Baada ya kazi nikawa napiga story na mlinzi nikamwambia hali halisi ya maisha yangu nikamwambia natafuta pia chumba cha bei rahisi, akaniambia kuna mtu ataniunganisha hakuna hela ya dalali na chumba ni 30,000 nikasema sawa, usiku mzima nikalala pale akanipatia namba ya mwenye nyumba.

Asubuhi nikarudi kwa jamaa yangu nikavaa nguo zangu za kitanashati kidogo nilizotoka nazo chuo (zilizo survive maana zingine zilishachakaa na kuisha)

Nikatoka nduki mpaka buguruni malapa na begi langu la nguo mgongoni kibembe mwenye nyumba anataka miezi 6, na Mimi ninayo Kama 90,000 pamoja na hela niliyoipata baada ya Kushusha mzigo, nikamwambia mwenye nyumba nimekuja dar kufanya kazi maalumu itakayonifanya nikae mwezi mmoja na nusu sasa nikilipa miezi 6 itakua ni hasara na Mimi sina hata godoro na nguo zangu zipo kwenye ili begi la mgongoni, tena nikamwambia sidhani Kama nitamaliza miezi miwili chukua hii 60,000 baada ya mwezi mmoja na nusu nitakua nimeondoka, nimekuja kufanya kazi za serikali.

Alikua yuko excited kusikia hivyo kusikia kazi za kiserikali tena nilivyomwambia sina vyombo wala kijiko akaniamini akanipatia na godoro la kulalia kumbe muhuni ndio nimekuja kuanza maisha, amna cha kazi ya serikali wala nini sikua tu na kodi target yangu ni kwamba baada ya mwezi nitakua nimempatia kodi yake ya miezi sita.

Nimeandika sana Naendelea kuandika kwa chini sehemu ya mwisho ambalo litakua ni funzo kwa vijana wanaopambana na graduate wasiokua na ramani.

IMG-20220514-WA0008.jpg
 
Hii sehemu nitaongea kwa ufupi saana.

Huwa napenda sehemu zenye mchanganyiko maana huwa naamini pesa zipo.

Nilipita pale Karume nikaona watu wanaosha viatu kuna jamaa rafudhi yake alikua anaongea nikaona huyu wa nyumbani, tuliongea nae haswaa akawa Ananipa kazi ya kuosha viatu pc 1000 ananipa 5000 in short nikapiga kazi pale nikaanza kuzoeleka baada ya mwezi nikawa na hela kidogo ya kuchukua mzigo Kama 80,000 nikawa naingia mule ndani nachukia viatu vya watoto kwa 800 naosha then nauza kuanzia 3000.

Hapo pia msoto wake sio wa mchezo maana tunaanza kuuza viatu saa 8 usiku pale karume kwa nje, tunauza mpaka saa 12 asubuhi ikifika saa 1 asubuhi migambo wanazingua so tunaweka mzigo store mpaka saa 12 jioni ndio tunamwaga barabarani mpaka saa 3 usiku, hebu fikiria hiyo daily routine kwa kijana graduate Kama Mimi na wapo vijana wengi Sana wanaofanya hivyo mahangaiko ni makubwa but kinachopatikana ni kidogo, Mama akinipigia namwambia kila kitu kipo sawa.

Kwenye harakati ya kujichanganya na watu nikapata hili deal ambalo sitalizungumzia sana na ndilo lilinifanya niondoke Dar es Salaam na kusema sitorudi tena

Nilipata deal la kuuza Mafuta ya petrol na diesel kutoka kwa madereva wa mafusso na lorry wakienda huko wanarudi na mafuta tunakubaliana bei then mimi najua nitauzaje

Dah kwa Mara ya kwanza nikashika hela ambazo sikuwahi kushika maana nilikuwa napigiwa simu kila mahali demand ilikuwa kubwa lakini sikuweza ku-play smart nikakamatwa na polisi, huu msala ulikuwa mkubwa saana nahisi nilichomwa sikuwahi kulala polisi hapo kabla nikaambiwa nitapewa kesi ya uhujumu uchumi wakati Mimi nina mwezi tu tokea nianze kuuza mafuta😁😁....kwa ufupi msala uliisha japo haikuwa rahisi sitaongea mambo mengi hapa maana sikuwahi kuwaambia mtu hata mzee hakuwahi kujua Kama nilikamatwa nilipambana mwenyewe nikatoka!...

Nilitoa akiba yoote niliyokusanya kupitia hiyo biashara haramu nikachomoka...

Baada ya hapo nikaenda home Tabora sikukaa muda nikapata ajira, nikasema tokea moyoni sitorudi tena Dar maana kwa jinsi watu wanavyoishi ule ufahari unaweza Kufanya mambo maovu ili u survive. Unashangaa vijana hawana kazi lakini wanamiliki pesa chafu,

Vijana
Usitamani maisha ya mtu always kua wewe, hujui watu wanapatia utajiri.
Usije/usitamani kufanya biashara haramu zina hela sawa lakini ukibananishwa unaweza ukawa ndio mwisho wa ndoto zako humu duniani.

Kijana ukitoka nyumbani kwenda kupambana hakikisha unafikia kwa ndugu yako mtu mzima mwenye familia ili akusitiri kwa vitu vidogo Kama chakula, malazi huku wewe unaendelea kufikiri utafanya nini,

Kwa msoto niliopitia Dar ulinifanya kuwa mgumu na kuwaza kufanya biashara yoyote haramu ili nipate pesa but niliamua kuchomoka na kurudi kwa Mungu.

Tusisahau kupambana huku tukimuomba Mungu maana yeye ndiye mpaji wa vyote.

Lakini bado naamini humu duniani Kama umezaliwa familia maskini kutoboa kufika hatua ya kumiliki pesa sio rahisi kwakweli

Hapa simaanishi pesa ya nyumba na gari namaanisha pesa haswaaaa.
 
Hivi ni visa vya kweli vinavyotokea ili tujifunze graduate na wapambanaji wengine someni hapa. Hakuna cha nitaendelea nitafupisha zaidi iwe fupi.

Ni Mimi pastor prakatatumba abaabaabaabaa etumba etumba.

Ndugu zangu kwanza nikiri jiji la Dar es Salaam watu wanapambana saaana tena saana, kuna variation kubwa Sana kati ya wenye nacho na wasiokua nacho lakini haiondoi wewe kufurahia jiji, kuna bata la pesa ndefu Kama huko kidimbwi (sijawahi kufika), na kuna bata letu sisi wahangaikaji Kama manzese uwanja wa fisi, Sudan temeke n.k.

Nilitokea tabora kuja kuhangaika na maisha baada ya kumaliza chuo na kukaa mtaani takribani mwaka mzima mzee alivyouza pamba akanipatia million mbili, nilipewa husia takribani masaa 7 kwamba nikipoteza huo mtaji nisimwambie kitu nipotee kabisa nisirudi nyumbani maana hiyo ndio ilikua akiba yake na Mimi ndio kijana mkubwa nina wadogo zangu kama 8.

Nilifikia dar tandale kwa tumbo kwa mshikaji wangu tulisoma nae tabora lakini hakufanikiwa kuendelea na masomo, Mara ya kwanza alinichangamkia huku nikimueleza mipango yangu ya biashara n.k, nilikua sijui sehemu yoyote ile dar wala sijui biashara yoyote ile huyo jamaa yangu alikua anafanya kazi kiwandani tegeta wazo ( sina hakika Kama panaitwa hivyo) , akaanza kunitembeza kujua jiji ile kunitembeza tu week Mbili Kama laki 5 ilishakata nikajipa moyo bado hela hipo, mshikaji wangu akawa hachangii chochote nikawa nanunua misosi nikasema fresh jamaa ananisitiri.

Kufupisha story million 1.5 ilikatika ndani ya mwezi na nusu hivi Mimi bila kujua imeenda wapi (usije mjini bila mipango).

nilipobakiza laki tano nikaenda kariakoo nikanunua "sendoz" za kike kwa laki 4 na 80 hivi (nilikua nikipita naona watu wanauza sana hizo sendo wadada wamewazunguka wananunua nikaona fursa) jamaa akanikodisha Eneo lake 10,000 kwa siku pamoja turubai lake (hakunambia Kama migambo wamekataza). Mimi sikuelewa watu ni wengi nikamwaga chini nikaanza kuuza zile sendoz nikajisemea moyoni biashara si ndio hii? Chap chap nimeshauza kama 70,000 huku nafurahia moyoni ghafla nikaona watu wanakimbia kimbia Mimi sikujali nilikua sielewi kinachoendea kuja kushtuka nimepigwa rungu la kisogo kwa akili yangu ikaanza kuniambia hawa watakua ni majambazi nini?

Hapo network imekata kichwani damu zinavuja ikabidi na Mimi nianze kukimbia kuelekea uelekeo wa wa watu wanapokimbilia, shati langu limeloa damu nikafika sehemu nikanunua maji ya kandoro nikanawa kichwa hapo nimevimba haswa kurudi kwenye mzigo wangu sikuukuta wakanambia migambo wamechukua itabidi niende nikafatilie niandae faini n.k nilikua na maumivu makali ya kichwa uchungu wa jiji la Dar nikaanza kuuona hapo kumbuka nina mwezi mmoja tu Dar, nikarudi gheto kulala huku nikiwa na mawazo tele hela nimebakiza elfu 80, mzigo wangu umechukuliwa "nikaconfirm" msemo wangu ambao unasema ukizaliwa maskini ni ngumu Sana kutoboa kwenye haya maisha yani ni ngumuuu, nikikaa barabrani nasema hawa walipataje hayo magari? Majumba yalioko mbezi kule, goba nikawa najiuliza nitatoboa kweli? Kwa 80,000?

Mshikaji wangu alikua anapenda kwenda viwanja so alikua ananipeleka maeneo mbali mbali naona vijana wadogo wakiendesha magari wameacha vioo wazi namimi nimetokea bush kuona gari labda la serikali nilikua napata mawazo Sana.

Turudi kwenye story baada ya kupigwa rungu la kichwa nimerudi ghetto mshikaji baada ya kumuelezea yaliyonikuta nikamwambia anitafutie kazi pale kiwandani nadhani kilikua kiwanda cha cement akanambia akirudi kesho yake kutoka job ataniambia.

jioni jamaa kurudi kanambia imeshindikana kupata kazi na anataka kuoa mpenzi wake anakuja so nitafute makao mengine (kumbuka hajawahi kunambia habari za mpenzi wala nini) kwakua Mimi ni mtu mzima nikajiongeza kwamba hapa hela imeisha sitakiwi.

To cut story nikaenda pale tandale kwa wauza mchele nikawa napiga story na wabeba mizigo pale, gari likaingia limetoka mbeya nikaomba kazi ya kupakua mchele kila gunia 500 nikafanya kazi ya kupakua mchele mpaka saa Saba usiku.

View attachment 2326402

Baada ya kazi nikawa napiga story na mlinzi nikamwambia hali halisi ya maisha yangu nikamwambia natafuta pia chumba cha bei rahisi, akaniambia kuna mtu ataniunganisha hakuna hela ya dalali na chumba ni 30,000 nikasema sawa, usiku mzima nikalala pale akanipatia namba ya mwenye nyumba.

Asubuhi nikarudi kwa jamaa yangu nikavaa nguo zangu za kitanashati kidogo nilizotoka nazo chuo (zilizo survive maana zingine zilishachakaa na kuisha)

Nikatoka nduki mpaka buguruni malapa na begi langu la nguo mgongoni kibembe mwenye nyumba anataka miezi 6, na Mimi ninayo Kama 90,000 pamoja na hela niliyoipata baada ya Kushusha mzigo, nikamwambia mwenye nyumba nimekuja dar kufanya kazi maalumu itakayonifanya nikae mwezi mmoja na nusu sasa nikilipa miezi 6 itakua ni hasara na Mimi sina hata godoro na nguo zangu zipo kwenye ili begi la mgongoni, tena nikamwambia sidhani Kama nitamaliza miezi miwili chukua hii 60,000 baada ya mwezi mmoja na nusu nitakua nimeondoka, nimekuja kufanya kazi za serikali.

Alikua yuko excited kusikia hivyo kusikia kazi za kiserikali tena nilivyomwambia sina vyombo wala kijiko akaniamini akanipatia na godoro la kulalia kumbe muhuni ndio nimekuja kuanza maisha, amna cha kazi ya serikali wala nini sikua tu na kodi target yangu ni kwamba baada ya mwezi nitakua nimempatia kodi yake ya miezi sita.

Nimeandika sana Naendelea kuandika kwa chini sehemu ya mwisho ambalo litakua ni funzo kwa vijana wanaopambana na graduate wasiokua na ramani.

View attachment 2326431
...aiseee
 
Hii sehemu nitaongea kwa ufupi saana.

Huwa napenda sehemu zenye mchanganyiko maana huwa naamini pesa zipo.
Nilipita pale karume nikaona watu wanaosha viatu kuna jamaa rafudhi yake alikua anaongea nikaona huyu wa nyumbani, tuliongea nae haswaa akawa Ananipa kazi ya kuosha viatu pc 1000 ananipa 5000 in short nikapiga kazi pale nikaanza kuzoeleka baada ya mwezi nikawa na hela kidogo ya kuchukua mzigo Kama 80,000 nikawa naingia mule ndani nachukia viatu vya watoto kwa 800 naosha then nauza kuanzia 3000....
Hapo pia msoto wake sio wa mchezo maana tunaanza kuuza viatu saa 8 usiku pale karume kwa nje, tunauza mpaka saa 12 asubuhi ikifika saa 1 asubuhi migambo wanazingua so tunaweka mzigo store mpaka saa 12 jioni ndio tunamwaga barabarani mpaka saa 3 usiku, hebu fikilia hiyo daily routine kwa kijana graduate Kama Mimi na wapo vijana wengi Sana wanaofanya hivyo mahangaiko ni makubwa but kinachopatikana ni kidogo, Mama akinipigia namwambia kila kitu kipo sawa.

Kwenye harakati ya kujichanganya na watu nikapata hili deal ambalo sitalizungumzia sana na ndilo lilinifanya niondoke dar es salaam na kusema sitorudi tena,
Nilipata dea la kuuza Mafuta ya petrol na diesel kutoka kwa madereva wa ma fusso na lorry wakienda huko wanarudi na mafuta tunakubaliana bei then Mimi najua nitauzaje,...

Dah kwa Mara ya kwanza nikashika hela ambazo sikuwahi kushika maana nilikua napigiwa simu kila mahali demand ilikua kubwa lakini sikuweza ku-play smart nikakamatwa na police, huu msala ulikua mkubwa saana nahisi nilichomwa sikuwahi kulala police hapo kabla nikaambiwa nitapewa kesi ya uhujumu uchumi wakati Mimi nina mwezi tu tokea nianze kuuza mafuta....kwa ufupi msala uliisha japo haikua rahisi sitaongea mambo mengi hapa maana sikuwahi kuwaambia mtu hata mzee hakuwahi kujua Kama nilikamatwa nilipambana mwenyewe nikatoka!...
Nilitoa akiba yoote niliyokusanya kupitia hiyo biashara haramu nikachomoka...

Baada ya hapo nikaenda home tabora sikukaa mda nikapata ajira, nika sema tokea moyoni sitorudi tena dar maana kwa jinsi watu wanavyoishi ule ufahari unaweza Kufanya mambo maovu ili u survive. Una shanga vijana hawana kazi lakini wanamiliki pesa chafu,

Vijana
Usitamani maisha ya mtu always kua wewe, hujui watu wanapatia utajiri.
Usije/usitamani kufanya biashara haramu zina hela sawa lakini ukibananishwa unaweza ukawa ndio mwisho wa ndoto zako humu duniani.

Kijana ukitoka nyumbani kwenda kupqmbana hakikisha unafikia kwa ndugu yako mtu mzima mwenye familia ili akusitiri kwa vitu vidogo Kama chakula, malazi huku wewe unaendelea kufikiri utafanya nini,

Kwa msoto niliopitia dar ulinifanya kua mgumu na kuwaza kufanya biashara yoyote haramu ili nipate pesa but niliamua kuchomoka na kurudi kwa Mungu.

Tusisahau kupambana huku tukimuomba Mungu maana yeye ndiye mpaji wa vyote.

Lakini bado naamini humu duniani Kama umezaliwa familia maskini kutoboa kufika hatua ya kumiliki pesa sio rahisi kwakweli
Hapa si maanishi pesa ya nyumba na gari namaanisha pesa haswaaaa.
..biashara haramu zinalipa sana-sema usiue TU.
 
Hapo ndio mwisho ninaomba watu wazima kidogo watoe ushauri kwa vijana wanaopitia kipindi kizito au kigumu au graduate kuishi kwa namna bora ya kufanya taifa letu liwe bora zaidi.
Note mpaka Leo nina alama ya sehemu ya kichwa iliyopasuka nilikia nafuga nywele lakini hiyo sehemu nywele hazioti, nimekua naona huruma kwa wapambanaji Sana maana nakumbuka nilipotokea.
 
Hii sehemu nitaongea kwa ufupi saana.

Huwa napenda sehemu zenye mchanganyiko maana huwa naamini pesa zipo.
Nilipita pale karume nikaona watu wanaosha viatu kuna jamaa rafudhi yake alikua anaongea nikaona huyu wa nyumbani, tuliongea nae haswaa akawa Ananipa kazi ya kuosha viatu pc 1000 ananipa 5000 in short nikapiga kazi pale nikaanza kuzoeleka baada ya mwezi nikawa na hela kidogo ya kuchukua mzigo Kama 80,000 nikawa naingia mule ndani nachukia viatu vya watoto kwa 800 naosha then nauza kuanzia 3000....
Hapo pia msoto wake sio wa mchezo maana tunaanza kuuza viatu saa 8 usiku pale karume kwa nje, tunauza mpaka saa 12 asubuhi ikifika saa 1 asubuhi migambo wanazingua so tunaweka mzigo store mpaka saa 12 jioni ndio tunamwaga barabarani mpaka saa 3 usiku, hebu fikilia hiyo daily routine kwa kijana graduate Kama Mimi na wapo vijana wengi Sana wanaofanya hivyo mahangaiko ni makubwa but kinachopatikana ni kidogo, Mama akinipigia namwambia kila kitu kipo sawa.

Kwenye harakati ya kujichanganya na watu nikapata hili deal ambalo sitalizungumzia sana na ndilo lilinifanya niondoke dar es salaam na kusema sitorudi tena,
Nilipata dea la kuuza Mafuta ya petrol na diesel kutoka kwa madereva wa ma fusso na lorry wakienda huko wanarudi na mafuta tunakubaliana bei then Mimi najua nitauzaje,...

Dah kwa Mara ya kwanza nikashika hela ambazo sikuwahi kushika maana nilikua napigiwa simu kila mahali demand ilikua kubwa lakini sikuweza ku-play smart nikakamatwa na police, huu msala ulikua mkubwa saana nahisi nilichomwa sikuwahi kulala police hapo kabla nikaambiwa nitapewa kesi ya uhujumu uchumi wakati Mimi nina mwezi tu tokea nianze kuuza mafuta....kwa ufupi msala uliisha japo haikua rahisi sitaongea mambo mengi hapa maana sikuwahi kuwaambia mtu hata mzee hakuwahi kujua Kama nilikamatwa nilipambana mwenyewe nikatoka!...
Nilitoa akiba yoote niliyokusanya kupitia hiyo biashara haramu nikachomoka...

Baada ya hapo nikaenda home tabora sikukaa mda nikapata ajira, nika sema tokea moyoni sitorudi tena dar maana kwa jinsi watu wanavyoishi ule ufahari unaweza Kufanya mambo maovu ili u survive. Una shanga vijana hawana kazi lakini wanamiliki pesa chafu,

Vijana
Usitamani maisha ya mtu always kua wewe, hujui watu wanapatia utajiri.
Usije/usitamani kufanya biashara haramu zina hela sawa lakini ukibananishwa unaweza ukawa ndio mwisho wa ndoto zako humu duniani.

Kijana ukitoka nyumbani kwenda kupqmbana hakikisha unafikia kwa ndugu yako mtu mzima mwenye familia ili akusitiri kwa vitu vidogo Kama chakula, malazi huku wewe unaendelea kufikiri utafanya nini,

Kwa msoto niliopitia dar ulinifanya kua mgumu na kuwaza kufanya biashara yoyote haramu ili nipate pesa but niliamua kuchomoka na kurudi kwa Mungu.

Tusisahau kupambana huku tukimuomba Mungu maana yeye ndiye mpaji wa vyote.

Lakini bado naamini humu duniani Kama umezaliwa familia maskini kutoboa kufika hatua ya kumiliki pesa sio rahisi kwakweli
Hapa si maanishi pesa ya nyumba na gari namaanisha pesa haswaaaa.
Dar hakuna tatizo lakini unatakiwa uwe na ramani
 
Mkuu, ndio imeisha au bado inaendelea?

Nadhani wengi tunamatarajio ya kutaka kujua mwishoni hizi harakati zote zimekufikisha hatua gani kimaisha ili somo unalotupa likamilike.
 
Hongera kwa kushare kisa chako na wanajamvi.

Ila una matatizo yafuatayo

Unapenda maisha mazuri ilhali wewe ni maskini, hii ni hatari kwani unaweza kuwekwa jela muda wowote ule.

Unatamaa ukiona biashara ya mtu anafanya unahisi anapata sana hela mwisho wa siku unakimbilia kuanzisha kitu bila kujua A B C . Kifupi hufanyi utafiti kabla.

Ushauri wangu.
Punguza kutamani vya watu yaani, lifestyle,na namna watu wanavyokula Bata zao,

Epuka stori chonganishi, sijui kuzama mamtoni, sijui sauzi kunalipa, Cha msingi kama umegraduate kweli, kaza msuli muda wowote matunda ya Elimu yako utayaona

Dar es salaam mbona inakalika vizuri tu mkuu?

Acha kujiongezea msongo wa mawazo kwa kutamani maghorofa, magari na fahari za wengine.

Duniani Kila mtu Ana talanta na njia zake , wengine huwa hawatumii nguvu kwenye kusaka vipato vyao kwakuwa Wana bahati na ngekewa zao.

Mwenzangu na miye licha ya usomi wako, bado utahaso kiasi Cha kujiona kama umelaaniwa, yote kwa yote ni mipango ya MUNGU, ongeza juhudi zako kwa vitendo na si kwenda kwenye maombi.

Naamini Kila kitu kitakaa poa tu, utapata kadri ya uwezo wako.
 
Back
Top Bottom