Faida Na Changamoto Za Kuuza Viwanja Au Nyumba Bila Kuwa Na Dalali

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Kuuza bila Dalali ni mauzo ya mashamba, viwanja na nyumba ambayo yanafanyika bila kuhusisha dalali kati ya mwenye nyumba na
mnunuzi. Hivyo huwezi kulipia ada ya dalali wa nyumba na ardhi.

Kwa kawaida, mauzo ya aina hii hufanyika kwa wawekezaji ambao wanaanza kuwekeza katika nyumba, viwanja na mashamba. Kuna imani kuwa mwekezaji anayeuza bila dalali hana mtaji wa kutosha, na hayupo makini katika uwekezaji wake.

Hizi ni baadhi ya dhana ambazo hutakiwi kuzipa uzito unapotafuta pesa. Nunua nyumba au kipande cha ardhi bila dalali, ili kuongeza kiasi cha kipato chako na sio kufuatana na dhana za wanaokuzunguka.

Hivyo mmiliki anatakiwa kufanya hatua zote ambazo zilitakiwa kufanywa na wakala au dalali wa mashamba, viwanja na nyumba. Hatua hizo ndizo zinamfanya aweze kutolipia ada ya huduma za
udalali.

Sababu Za Kushindwa Kwa Mauzo Bila Dalali.

Moja.

Wamiliki kutangaza au kuuza kwa bei isiyoendana na thamani ya majengo au ardhi.

Mbili.

Wamiliki kushindwa kuonyesha muelekeo wa kuifikia bei ya
nyumba inayouzwa. Hii huchangia sana kupoteza wanunuzi wengi.

Maandalizi mabaya katika kuuza ardhi na nyumba. Kutofanya usafi, kutosafisha bustani, na kutoweka vivutio vya wapangaji.
Wapangaji ni moja ya vivutio vya wanunuzi wa nyumba.

Hii ni kwa
sababu huanza kuingiza kodi ya pango la nyumba toka mwezi wa
kwanza kwa kumiliki nyumba zao. Kama ni mmoja wapo njia hii
haikufai kutengeneza kipato.

Majengo yanatakiwa kuandaliwa kwa ajili ya kuuza, ikiwemo picha
za matangazo, uwasilishaji wake na kuonyesha katika mtandao wa
intaneti.

Wamiliki kuwa na mbinu duni mno za kufanya mazungumzo. Unahitaji mbinu bora sana ili kukamilisha mauzo bila Dalali na
hatimaye ujipatie faida.

Tatu.

Kushindwa kumlipa mtu ambaye amekutafutia mnunuzi
wako.

Zifuatazo ni hatua za kuuza bila Dalali;-.

Hatua ya kwanza.

Kuandaa ardhi au nyumba.

Hakikisha unakodi mkaguzi kabla hujaanza kutangaza mali yako. Hakikisha kila mbinu muhimu ya mazungumzo bora unaielewa na kuitumia katika mazungumzo yako.

Hakikisha unajiandaa kwa lolote na kuweka subira.Hakikisha hakuna
harufu mbaya ya aina yoyote. Hata Pafyumu usiweke kwa sababu
huwezi fahamu kama itamvutia mnunuzi wako.

Hakikisha sehemu ya
kuingilia inavutia sana. Hakikisha sehemu ya nyuma ya nyumba isiwe
chafu kiasi kwamba linakuwa kama eneo la kuweka kila aina ya takataka.

Hatua Ya Pili.

Kukagua Nyumba yako au ardhi yako.

Kodi mkaguzi aje kuhakikisha kila eneo tayari kwa kuwakaribisha
wanunuzi wa mashamba au viwanja au nyumba unayouza. Unaweza
kukagua wewe mwenyewe kama haiwezekani kukodi mkaguzi wa
nyumba (Professional home Inspector).

Ni vizuri sana ukawaomba watu watano wa karibu yako watakaoweza kukusaidia kukagua nyumba yako. Chukua hatua hii baada ya
kushindwa kumlipa mkaguzi wa majengo.

Hatua Ya Tatu.

Kuhakiki Mtaji Fedha Wa Mnunuzi.

Unahitaji kuhakikisha kuwa mnunuzi wako ana uwezo wa kulipia bei
ya nyumba mtakayoelewana. Ikiwa ni mkopo hakikisha umekuletea
fomu ya ukubali wa mwanzo kutoka benki au taasisi au mtu binafsi au
ushirika anaotaka kushirikiana nayo (Pre-approved loan application
forms).

Hatua Ya Nne.

Kuzungumza Na Mawakala, Wawekezaji
Wengine Na Watu Wanaopenda Kufanya Mambo Yahusuyo Biashara
Ya Nyumba Na Viwanja.

Hapa utahakikisha umepewa uzoefu kutoka kwa hao utakaozungumza
nao. Hufanyi mazungumzo ili uwalipe, lakini unazungumza nao kama sehemu ya maongezi yenu ya kubadilishana mawazo ya kiuwekezaji.

Hatua Ya Tano.

Kupanga Bei Ya Mali.

Panga bei kufuatana na hali ya soko kwa kipindi hicho. Panga bei ya
mali kwa kuangalia bei au gharama ulizotumia katika uwekezaji wako
kwa ujumla.

Hakuna kanuni yoyote bora ya kukuhakikishia kuwa ada
unayoipanga iko vizuri. Unapanga bei ambayo mtaenda kuifanyia
makubaliano na mnunuzi wa mali yako.

Faida Za Kuuza Nyumba Bila Dalali.

Moja.

Ni chanzo cha faida kubwa.

Ada ya kumlipa dalali ni kubwa hasa kama nyumba unayouza
inathamani ya zaidi milioni ishirini. Hivyo kuepuka kumtumia dalali
unakuwa katika nafasi nzuri ya kutengeneza pesa nyingi.

Mbili.

Utapata uzoefu.

Ni lini utaweza kupambana na changamoto za uwekezaji?. Unahitaji
kufanyia kazi maarifa unayoyapata katika vitabu, makala na semina
kuhusu biashara ya kuwekeza katika mashamba, nyumba na viwanja.

Tatu.

Kuwa mzungumzaji bora. Ukitaka kupata mbinu bora za mazungumzo, ingia wewe mwenyewe
kwenye mambo madogo madogo kama vile kuandaa mauzo au hata
kuongea na wanunuzi na mambo mengine mengi kuhusu ardhi na
nyumba.

Hakikisha kila unapopata nafasi jipe muda wa kuboresha
mazungumzo yako. Kama walivyosema, huwezi kujifunza kuogelea
kwenye kitabu. Ingia majini ili uweze kuwa mwogeleaji baada ya
kusoma vitabu.

Nne.

Kuongeza urafiki zaidi.

Kwa sababu kuuza wewe mwenyewe, unajipa nafasi kubwa ya kuwashirikisha watu wa karibu. Ndugu na jamaa watafurahi kama watafanikiwa kununua kwa bei ambayo wote mmeona inafaa.

Changamoto Za Kuuza Bila Dalali.

Moja.

Kuchelewa kuuza.

Unaweza kuchelewa kuuza kwa sababu hauna uzoefu na hutapata
wanunuzi kwa muda. Huwezi kufanana na Dalali ambaye ameamua
kubobea katika mauzo ya ardhi na nyumba.

Hivyo uwezekano wa
kuchelewa kuuza ni mkubwa kuliko kama ungemlipa dalali wa
mashamba, viwanja na nyumba.

Pili.

Unahitaji subira.

Kama huna subira ya kuhakikisha mambo yanaenda kama
ulivyotegemea, hii sio njia inayokufaa rafiki yangu. Kama una haraka
ya kuuza mali yako -mashamba, viwanja na nyumba, hii njia haikufai
kabisa rafiki yangu.

Kama utashindwa kuzungumza na wanunuzi ambao hawana mbinu
bora za mazungumzo, hii sio njia inayokufaa rafiki yangu.

Kama huna
msuli mkubwa wa subira, achana na njia hii au andaa msuli wa subira
ili uitumie njia hii.

Tatu.

Bei sahihi ya mali -mashamba, viwanja na nyumba.

Ni vigumu kuweka kiasi sahihi cha bei ya mali -mashamba, viwanja
au nyumba, unayouza hasa kama hauna uelewa wa kufahamu thamani
ya majengo, viwanja na mashamba.

Kwa kujifunza haya utakuwa umeweza kuona chanagamoto na faida za kumtumia dalali kwenye mauzo ya ardhi au nyumba yako. Mbinu hii ya kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo huitwa FOR-SALE-BY-OWNER (FSBO).

Rafiki yako,

Aliko Musa.

WhatsApp; +255 752 413 711


Google; UWEKEZAJI MAJENGO BLOG
 
Nimejifunza kitu, japo ukitaka kula inabidi ukubali kuliwa.
Ukitaka faida kubwa peke yako mara nyingi huwa haina baraka, ndio maana tunashauriwa kutoa sadaka pia.
Ndio inaongeza mzunguko wa fedha katika jamii na kukua kiuchumi katika nchi na dunia.
 
Dalali ni kazi kwaiyo unatakiwa kujua madalali ndio wanajua wateja na wateja wanajua dalali ndio wanaweza wasaidia kupata wanachotaka so dalali haepukiki ukitaka kuuza kitu chako kwa haraka na kwa faida unayotaka wewe
 
Mi nlijua wamiliki kumbe mnajipa
Promo kwenye mali za watu, mnalipa kodi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom