Tuliosoma sayansi A-level bila kwenda tuition tukutane hapa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,303
Wakuu leo kuna rafiki yangu wa A-level nilimkumbuka nikajikuta nimekumbuka mambo mengi sana ya enzi hizo miaka zaidi ya 15 iliyopita. Ni kwamba mimi ni mojawapo wa watu tunaojivunia kusoma mchepuo unaoheshimika na kuogopwa kuliko yote nchini yaani PCM (Physics, Chemistry and Pure Mathematics). Ninamshukuru Mungu pia nilivuka salama mitihani ya ACSEE.

Kama ilivyo kwa wengi wetu wenye background za kuhuzunisha ni kwamba nikiwa form V & VI nilikuwa na ufadhili wa ada peke yake Tsh 35000/= kwa muhula. Ila mambo mengine yote nilijisimamia mwenyewe. Wakati wa likizo nilikuwa nafanya sana vibarua vya ujenzi na kazi zote za halali zinazoweza kufanyika ili kujikusanyia hela za kurudi shule. Sikuwahi kusoma Tuition kabisa. Nilikuwa napita tu pale Arusha Sport na kwenye mama wa Mihogo pale mtoni kama unaenda St Theresa kusalimiana na washkaji. Na wale wa Dar tukiwa shule wanatusimulia kuhusu tuition za Mapambano, Mchikichini na kuna nyingine walisema inaitwa Mzumbe Remix ya T.O aitwaye Lusekelo. Nakumbuka form V nilifeli sana kwasababu hiyo.

Wakati naingia form six nikiwa napambania angalau nipate division four ndo nikakutana na rafiki yangu huyu aliyenisaidia kubadil kila kitu. Huyu jamaa yeye alikuwa vizuri hivyo baada ya kumwambia kuwa niko nyuma kimasomo akajitolea kunifundisha kama vile mtoto anayeanza shule. Nakumbuka kwenye Physics tulianzia kwenye mechanics kabisa. Huyu jamaa huwa namchukulia ni malaika tu alitumwa kuniondolea aibu.

Tulikimbizana sana na muda ila hadi tunafanya Mock ya mkoa bado hali ilikuwa tete. Nakumbuka ule mkoa wa Iringa walisema eti div. IV imefutwa kwahiyo matokeo yanatoka NINA ZERO. Hiyo ilikuwa aibu kubwa zaidi kuwahi kunipata. Sikukata tamaa nikaendelea kukomaa na kuongeza juhudi. HAKUKUWA NA KULALA KIZEMBE. Jamaa yangu nae akawa ananisaidia hadi umefika muda wa NECTA. Nikafaulu vizuri II.12

Baada ya chuo jamaa yangu alipata kazi kwenye taasisi moja kubwa ya serikali. Ninamshukuru Mungu kwa kumjalia kazi yenye kipato kikubwa. Nilichojifunza ni kuwa watu kama hawa waliogusa maisha yetu huwa hawana kabisa hata muda wa kukumbuka kuwa nilisaidia mtu fulani. Yaani wao huchukulia poa tu kama hakuna kilichotokea. Pia ni ngumu sana kukutana nae kwenye hali kugombana. Na hata mkigombana hakumbushi chochote. Ila wale waliowahi kukupa kitu kwa roho za kimaskini huwa ndo hukumbusha alivyokusaidia.
 
Daah siongei mengi Lusekelo Kibona msela wangu sana enzi za kipande Cha Iyunga -Nzovwe, acha tuendelee kufaidi maisha na maticulation yetu ya pale mafiati enzi zile dadeki, vichwa tulikutana na kwa wanawake Magdalena Mushi. Acha tuinjoi maisha tule Bata tule Bata. Scholarship raha sana
 
Daah siongei mengi Lusekelo Kibona msela wangu sana enzi za kipande Cha Iyunga -Nzovwe, acha tuendelee kufaidi maisha na maticulation yetu ya pale mafiati enzi zile dadeki, vichwa tulikutana na kwa wanawake Magdalena Mushi. Acha tuinjoi maisha tule Bata tule Bata. Scholarship raha sana
Yuko wapi huyo T.O?
 
nilipiga PCM. Nilikuwa naweza kuchukua notes, nikajisomea, kama ni calculations nikatambaa nazo, nacheki alivyotembea, naanza kupiga mdogo mdogo kisha nahamia kwenye maswali complex na baada ya hapo naweza kumsolvia mtu yoyote akija na swali lake na nitamuuelekeza as if nimekula pindi.
 
Kumbe lilipata div. zero ndio maana halina akili jinga kabisa
Bola-Tinubu-4.gif
 
Hahahaha nilifika advance pcm nikiwa na knowledge ya additional mathematics tu sijui ata kutumia calculator lakini ad natoka msaada pekee wa mwalimu ni kwenye set na hyperbolic function na code two vingne vyote nakula msuri mwenyewe mdogo mdogo tu physics msaada wa mwalimu ni mechanics tu Chand 2 nlisoma mwenyew tu chemia organic nliachana nayo
 
Hahahaha ***** tutafute ela wenetu wakasome st kunani huko Huku serikalini hakuna namna ni shida tu mm nilisoma shule 2yrs namjua head master tu walimu wengine hakuna ila VITU SIO BAD IVOO KA UNAJUA UNAJUA
 
Back
Top Bottom