Tuliokuwa tunamkubali Trump tangu akiwa Rais 2016 - 2020

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
2016 hadi 2020 ni kipindi ambacho watu wengi sana walikuwa wahanga wa kuziamini habari za kumchafua Mwamba, hasa hapa kwetu Tz ilikuwa rahisi sana kuwa brainwash wabongo, hata humu JF 98% walikuwa brainwashed kumchukia Trump, ni wachache sana tuliusoma mchezo.

Trump ndie raissi mpenda amani, Hakuona shida kwenda North Korea kwa Kim Jong Un kulegeza bifu, na kweli Kim Jong Un hicho kipindi hakurusha makombora kama alivyoanza sasa,

Trump was a no nonsense man lakini alipenda amani, Jeshi lilikuwa active sana na lilikuwa na baketi kubwa mno, Isis ilifutwa haraka mno hakuna mambo ya siasa, Ni kipindi ambacho hata Putin alitulia kwa kumheshimu Trump, Putin kavamia nchi jirani kipindi cha Bush, Obama na sasa kwa Biden ila alitulia kipindi cha Trump. Peace through strength

Aliweka rekodi kubwa sana za kiuchumi ambazo hata obama anakiri hakuweza kudhani zitakuja kuwepo

Aliweka rekodi kubwa sana za ajira

Aliweka rekodi ya kuweza kudhibiti maharamia wasiingie nchini kiholela na waliowahi kuingia kimagendo kuwa deported, Tangu alivyoondoka hadi sasa maharamia milioni 12 wameingia Marekani.
 
Trump nilimwelewa kwenye vitabu vyake...wakati nasoma mojawapo ya vitabu vyake (Think Big ) nikaanza kupata kauvivu kukimalizia, nilipopata taarifa za jamaa kugombea urais, mzuka ukarudi Tena nikamalizia kitabu chake na nilimpa nafasi kubwa ya kushindwa licha ya mizengwe aliyopambana nayo katika safari yake.

Screenshot_2024-01-16-11-13-39-13_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg

Kinachomponza, yule sio mwanasiasa na anasema mambo jinsi yalivyo, siasa haitaki mambo yaende hivyo.
 
Ni kipindi ambacho watu wengi sana walikuwa wahanga wa fake news za kumchafua Mwamba, kwetu hapa Tz ilikuwa rahisi sana watu wengi kuwa brainwashed na hizi propaganda wachache sana tuliusoma mchezo.

Kama wewe unamsapoti trump tangu 2016 akiwa raisi karibu hapa
Trump nilimkubali tangu 2016. Kiongozi yeyote ambaye hatoki kwenye establishments huwa namkubali, mtu mkongwe anayetoka chama tawala au mpinzani wa muda mrefu huwa siwaamini kirahisi.

Outsiders hasa wafanyabiashara kama Trump huwa wanatumia logic na common sense, sio siasa. Ukitazama interviews za Trump anavyotoa maoni na kujibu utaona anaongea vitu wazi kabisa na vinaeleweka kirahisi. Kuna siku aliuliza kama ISIS na maadui wa Marekani, na Taleban ni maadui wa Marekani. Kwanini Marekani ilienda kupigana na ISIS wakati ISIS inaenda kupigana na Taleban. Logic hapo ni kuwaacha maadui zako wapigane.

Ni watu kama Rais mpya wa Argentina
 
Trump nilimwelewa kwenye vitabu vyake...wakati nasoma mojawapo ya vitabu vyake (Think Big ) nikaanza kupata kauvivu kukimalizia, nilipopata taarifa za jamaa kugombea urais, mzuka ukarudi Tena nikamalizia kitabu chake na nilimpa nafasi kubwa ya kushindwa licha ya mizengwe aliyopambana nayo katika safari yake.

View attachment 2873315

Kinachomponza, yule sio mwanasiasa na anasema mambo jinsi yalivyo, siasa haitaki mambo yaende hivyo.
Siasa inataka watu waongo waongo sana.. mwamba hapo tu ndio anafel. Shida watu pia hatupendi kuambiwa ukweli
 
2016 hadi 2020 ni kipindi ambacho watu wengi sana walikuwa wahanga wa kuziamini habari za kumchafua Mwamba, hasa hapa kwetu Tz ilikuwa rahisi sana kuwa brainwash wabongo, hata humu JF 98% walikuwa brainwashed kumchukia Trump, ni wachache sana tuliusoma mchezo.

Kama wewe unamsapoti trump tangu 2016 akiwa raisi karibu hapa.
Trump ni Trojan horse wa Russia katika siasa za Marekani, Trump ni wale watu wa chama na maslahi binafsi mbele kuliko Taifa. Akishinda Urais tena ataifanya Marekani kuwa dhaifu sana mbele ya maadui/wapinzani wake na kuharibu mahusiano na washirika wengi wa Marekani.
 
Russian hoax trump alishakuwa exonorated na ikaonekana ni Democrats walipika hio propaganda ambayo ilifanikiwa kubrainwash watu wengi ukiwemo wewe.

Kumbuka Kipindi cha Bush, Obama na sasa Ukraine huyo Putin alikuwa anafanya fujo kwa nchi nyingine ila kipindi cha Trump alitulia kabisa, Putin alishaona Trump sio wa mchezo mchezo, Isis aliisafisha ndani ya mda mchache sana,

Trump alichokuwa anataka ni aman, Hakuona shida hata kwenda kwa Kim wa North Korea kulegeza bifu na hicho kipindi Kim hakurusha makombora kama alivyoanza upya kwa sasa.
 
Trump ni Trojan horse wa Russia katika siasa za Marekani, Trump ni wale watu wa chama na maslahi binafsi mbele kuliko Taifa. Akishinda Urais tena ataifanya Marekani kuwa dhaifu sana mbele ya maadui/wapinzani wake na kuharibu mahusiano na washirika wengi wa Marekani.
Ha ha haaa, Wabongo kwa ujuaji hatujambo kabisa ha ha haaaa.

Ndo hatuendelei Kwa sababu ya ujuaji wa kila kitu
 
Russian hoax trump alishakuwa exonorated na ikaonekana ni Democrats walipika hio propaganda ambayo ilifanikiwa kubrainwash watu wengi ukiwemo wewe.

Kumbuka Kipindi cha Bush, Obama na sasa Ukraine huyo Putin alikuwa anafanya fujo kwa nchi nyingine ila kipindi cha Trump alitulia kabisa,

Trump alichokuwa anataka ni aman, Hakuona shida hata kwenda kwa Kim wa North Korea kulegeza bifu na hicho kipindi Kim hakurusha makombora kama alivyoanza upya kwa sasa.
Bila hata hiyo unayoita Russian hoax na hayo madai ya kuwa exonerated ni mara nyingi tu Trump amekuwa akiwasifia watawala madikteta Trump, Xi na Kiduku na kusema wana akili sana au angetamani apate loyalty ya raia wake kama wao au pia angetamani awe dikteta hata kwa siku moja tu.

Putin alitulia kipindi cha Trump kwa sababu Whitehouse katika utawala wa Trump ilikuwa kama dark comedy show, Trump alionyesha kumuamini Putin zaidi kuliko hata CIA na FBI na kubwa zaidi alikuwa akiidhoofisha NATO kiasi kwamba hata ingevunjika kama angeshinda kwa mara ya pili mfululizo.
 
Ni adui wenu mkubwa kwa mnaosapoti mapenzi ya jinsia moja.

Ni shujaa kwetu tunaojua kwamba kuna jinsia mbili pekee
Trump alimteua Richard Grenell ambaye ni shoga kwenye nafasi mbalimbali za juu za serikali ya Marekani.
 
Bila hata hiyo unayoita Russian hoax na hayo madai ya kuwa exonerated ni mara nyingi tu Trump amekuwa akiwasifia watawala madikteta Trump, Xi na Kiduku na kusema wana akili sana au angetamani apate loyalty ya raia wake kama wao au pia angetamani awe dikteta hata kwa siku moja tu.

Putin alitulia kipindi cha Trump kwa sababu Whitehouse katika utawala wa Trump ilikuwa kama dark comedy show, Trump alionyesha kumuamini Putin zaidi kuliko hata CIA na FBI na kubwa zaidi alikuwa akiidhoofisha NATO kiasi kwamba hata ingevunjika kama angeshinda kwa mara ya pili mfululizo.
Labda nikuulize wewe, Mtu kama Xi ni Diktetea lakini yeye na serikali yake walibuni mifumo ambayo iliwaingiza hasara Marekani huku China ikifaidika kupitia International Trade, Huoni kwamba hapo Xi ndie aliewazidi akili kina Obama ?

Putin anawauzia gesi mataifa ya Nato, Anaweza kuwanyima gesi mataifa ya Nato iwe kama silaha ya vita vya kiuchumi, Huoni kwamba hii ni akili ? Trump alikuwa sawa kabisa kumsifia Putin ana akili kwasababu kuna viongozi wapumbavu wanaompa hio chance ya kuwazidi akili, Aliwashauri nchi kama ujerumani watafute chanzo kingine cha gesi.

Trump kwa Xi waliendana sawa, Marekani kwa mara ya kwanza illingiza mabilioni ya dola kutoka China, Kipindi cha Trump mataifa yote ya Nato walichangia bajeti ya ulinzi hakuna alietegea kusubiri Marekani alipie kila kitu ndio maana hata Putin alitulia hicho kipindi kwa kuona Marekani imepata rais mwenye akili,

Kumbuka kiongozi mwema anaweza asijue jibu la 2+2 lakini Dikteta anaweza kujua, Je Dikteta hapa hana akili ? Wakoloni waliokuja hapa Afrika walikuwa hawana akili ?
 
Mimi ni Mrepublican nilifadhaishwa sana na mauaji ya Gadafi na Osama yaliyofanywa na democratic ila kwa nilipata wakati mgumu sana kumkubali Trumph kutokana na ukichaa wake
 
Binafsi nilifurahi sana Trump alivyomnyoosha Hilary Clinton 2016.

Na pamoja na kuwa sio mtaalamu wa mambo ya siasa ama chaguzi naamini hata 2020 alimshinda Joe Biden ni vile tu kila mahali/ taasisi ambako Trump alitakiwa kwenda kudai haki yake aidha walikua completely against him ama walihofia sana hatari ambayo 'demokrasia' ya Marekani na system nzima ya uchaguzi ingepata kama Trump angepewa nafasi ya ku prove for the whole world to see uchakachuaji mkubwa uliofanyika kwenye utaratibu wa kura za posta/ mail-in ballots, maana yake Marekani ingewaambia nini watu??

Trump mwaka 2016 alipata kura milioni 62.9 huku Clinton akipata kura milioni 65.8

Jumla ya kura walau kwa hao wawili ilikua milioni 128.7

Mwaka 2020, miaka minne baadae, Trump aliongeza kura milioni 11.3 kutoka 62.9m alizopata 2016 mpaka kura milioni 74.2

Biden maana yake aliongeza kura za Dems by 15.4m kutoka 65.8m alizopata Clinton mpaka 81.2m alizopata yeye.

Wasiwasi wangu mkubwa ni;
i) Ilikuaje ndani ya miaka minne tu wakaongezeka wapiga kura karibu 27m??

ii) Kwa hesabu za kawaida mtu alieongeza kura 11.3m ndani ya miaka 4 which means base ya wapiga kura wake imeongezeka tena sanaa badala ya kupungua, inawezekana vipi ashindwe uchaguzi?? Kama waliomchukia between 2016 na 2020 waliongezeka, si ilitakiwa walau i reflect kwenye matokeo?

iii) Mbona amekua anamshinda Biden kwenye opinion polls tokea siku ya kwanza Biden ameingia ofsini? Hao wanaompenda Biden wapo wapi?

iv) Ni kwanini miaka minne baadae, Trump amegoma kabisa ku concede uchaguzi? Ni vile tu hapendi kushindwa au anajua kabisa ameibiwa kura?

Binafsi mwaka huu tukijaaliwa uzima nataka niangalie idadi ya wapiga kura itaongezeka kwa kiasi gani ili nipate majibu yangu nikilinganisha na no. (i) above.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni Mrepublican nilifadhaishwa sana na mauaji ya Gadafi na Osama yaliyofanywa na democratic ila kwa nilipata wakati mgumu sana kumkubali Trumph kutokana na ukichaa wake
Trump hakua mwanasiasa, kwake nyeusi ni nyeusi, nyeupe ni nyeupe. Haipo ni haipo, ipo ni ipo, hakuna mambo ya ngoja tutaona cha kufanya. Ungekua basi unafuatilia alivyowanyoosha Wachina kwenye utawala wake.

Binafsi namkubali sana kama navyomkubali JPM kwasababu ya tabia hizo.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni Mrepublican nilifadhaishwa sana na mauaji ya Gadafi na Osama yaliyofanywa na democratic ila kwa nilipata wakati mgumu sana kumkubali Trumph kutokana na ukichaa wake
Gaddafi aliuwawa na Walibya wenzake
 
Back
Top Bottom