Tulinganishe biashara na ajira hapa

Tulinganishe biashara na ajira hapa

Kabla sijachangia kwanza niseme mleta mada we ni muongo.
Baada ya hapo ndo nichangie sasa.
Mimi nimekosa ajira zaidi ya miaka 10 tangu nihitimu. Ninafanya biashara ndogo ndogo, nimeoa nina familia, nalipa kodi na ada. Nyumba yangu inasubiri kupauliwa. My class mates walioajiriwa wananipiga vibomu vya hapa na pale. Ila mpaka sasa sijaelewa kipi bora kujiajiri au kuajiriwa maana bado naaply
Ndio uhalisia
 
Wakuu hebu tujaribu kulinganisha kati ya biashara na ajira kwa upekee na kwa factor zinazofanana au watu wenye madaraja sawa ya vipato kwa upande wa ajira na mtaji au mapato tuone nani anajilipa/analipwa shingapi na amefanya nini hadi sasa

Nikianza mimi, ki status ni mfanyabiashara mdogo mtaji around 500k-1m return around 300k-500k per month hadi sasa sina nilichofanya zaidi ya kuanza msingi wa nyumba kwa miaka sita toka nianze biashara

Karibuni tushee uzoefu
Huwezi kuwa Bilionea kwa mshahara...lakini waweza kwa biashara..muhimu kuwa na vyanzo zaidi ya viwili vya kipato hata kama ni vidogo kimtazamo,
 
Biashara sio ya kila mtu. Inategemea na uwezo wako wa kuhimilia stress na uvumilivu wa ups and down.
Ukianzisha miradi basi utakua sehemu nzuri kuliko kuanzisha biashara
Kwa maisha yetu yanavyo kwenda ukistaafu napo unakwenda kufungua biashara sasa kwanin usianze mapem kama unawez kufany vyote na muda una ruhusu
 
Muache afanye kinachowezekana kwa wakati husika.
Mitazamo inatofautiana. Mwingine atakuuliza je nikiacha kujenga ili nikuze biashara na bahati mbaya biashara ikafa au malengo ya ukuaji yasifikiwe? Mwingine kipaumbele chake ni kuwa na makazi binafsi kwanza ili awe huru ndo apambane vizuri na biashara.
huyu aliomba ushauri. So maushauri meengi yatatolewa kwa misimamo tofauti. mwisho wa siku yeye ataamua kipi kinamfaa.
 
Mkuu kwa heshma ungefafanua kidogo hapa
Kwa Mwezi Mmoja,
Mwajiliwa kipato chake ni kifupi (yaani Kiko limited)

Ila Kwa mfanyabiashara, Mwezi ni mrefu mno, ana uwezo wa kutengeneza pesa nyingi mno.

Ndo maana utashangaa wafanyabiashara wanakopa pesa za riba kubwa sn (25% plus) na wanarejesha fresh kabisa na hawawazi.

Ila watumishi wanaokopeshwa Kwa riba chee (below 17%) , Bado wanalalamika mabenki yanawanyonya.
 
Hii ni kweli kabisa
 
wafanyabiashara wanakopa pesa za riba kubwa sn (25% plus) na wanarejesha fresh kabisa na hawawazi.
Mifumo ya fedha kibongo bongo inaumiza.

South Africa,Average business loan interest rates at banks range from 6.6% to 11.5% ila bongo inaenda mpk 25-30% hii ni komesha,2025/26 tunahitaji mapinduzi makubwa kwenye financial sector.
 
Mm napokea take home ya 750k kwa mwez......naomben wazo la biashara la kuingiza 20k per day.

Fanya service based business(SBB)

waajiriwa wengi wanafanikiwa zaidi kwny biashara ya kutoa huduma kuliko ya kuuza bidhaa..
Mifano ya SBB
1)ride sharing services ie bolt,Uber,Kama una usafiri wako you can try this after working hours.
2) courier-unaweza kuwa courier wa Amazon au alibaba.
3)Education services -anzisha shule ya nursery,weka matron na mwalimu,mhasibu ww mwenyewe,uko mbeleni ukiwa na mapafu unaanzisha primary school kabisa.

Ongezea na hii idea
4)vending machine-kuna VM za soft drinks,Kuna za snacks,kuna za maziwa,huku mtaani kwetu kuna hadi vending machine ya maji ya kunywa,uwanja ni mpana..mchawi location.

Hizi ni baadhi ya ideas ambazo hazihitaji Sana uwepo wako ,unachohitaji ni upfront cost then after,u keep on downloading money.

Vending machine inafanania hv

Screenshot_20250726-140839.png

Vending machine ya maji
Screenshot_20250726-141509.png
 
Wakuu hebu tujaribu kulinganisha kati ya biashara na ajira kwa upekee na kwa factor zinazofanana au watu wenye madaraja sawa ya vipato kwa upande wa ajira na mtaji au mapato tuone nani anajilipa/analipwa shingapi na amefanya nini hadi sasa

Nikianza mimi, ki status ni mfanyabiashara mdogo mtaji around 500k-1m return around 300k-500k per month hadi sasa sina nilichofanya zaidi ya kuanza msingi wa nyumba kwa miaka sita toka nianze biashara

Karibuni tushee uzoefu
Tusilinganishe ajira na vitu vya hovyo. Labda kama una biashara kama za akina Mwamedi. Sasa biashara ya mtaji milioni 10 mkuu huwezi kulinganisha na ajira. My wife mke wangu naona pale anavyoteseka na biashara zake sitaki hata kufikria. Nilitaka kuacha ajira kwamba tukapambane na biashara alinigomea kabisa!
 
Mtaji wa mkeo ni shingapi na wewe take home yako ni shingapi tuanzie hapo
 
Kabla sijachangia kwanza niseme mleta mada we ni muongo.
Baada ya hapo ndo nichangie sasa.
Mimi nimekosa ajira zaidi ya miaka 10 tangu nihitimu. Ninafanya biashara ndogo ndogo, nimeoa nina familia, nalipa kodi na ada. Nyumba yangu inasubiri kupauliwa. My class mates walioajiriwa wananipiga vibomu vya hapa na pale. Ila mpaka sasa sijaelewa kipi bora kujiajiri au kuajiriwa maana bado naaply
Kwenye biashara hujafanikiwa Kwa sababu bado unamawazo ya kuajiriwa
 
Back
Top Bottom