Tulikwenda kupigana msumbiji kama nani!!

Amiliki

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,085
1,004
Mwaka 1975 Baada ya kurudi kutoka katika Vita vilivyomwondoa Mreno Msumbiji tulikusanyika pale Lugalo Jeshini ambapo Mwalimu JK Nyerere alikuja kutupongeza kwa Ushujaa uliomwondoa Mreno .
Katika Hitimisho lake Mwalimu akasema, Mashujaa Mmerejea tunawapokea kwa Shangwe na
HATUNA CHA KUWAPA, CHA KUWAPA NI ASANTE

Nakumbuka yule kijana aliyesimama na kumuuliza Mwalimu akitaka kujua kama tulienda kupigana Msumbiji kama Askari wa Kukodiwa na kama ni Askari wa kukodiwa tulipaswa kulipwa au tulienda kupigana Msumbiji kama ni Sehemu ya Tanzania, basi Tuonyeshwe mipaka ya Tanzania!

Huo ndio ulikuwa mwisho wa kumwona yule kijana mpaka leo na Wanajeshi wengine wakafyata japokuwa hakuwa amepanga peke yake kuuliza maswali yale!
 
Mwalimu alikuwa na ajenda zake za siri, huenda alitaka kuitawala africa. Ndoto zile zile za kuiunganisha africa kama akina Nkwame NKhrumah, akina Patrick Lumumba nk.
 
Mwaka 1975 Baada ya kurudi kutoka katika Vita vilivyomwondoa Mreno Msumbiji tulikusanyika pale Lugalo Jeshini ambapo Mwalimu JK Nyerere alikuja kutupongeza kwa Ushujaa uliomwondoa Mreno .
Katika Hitimisho lake Mwalimu akasema, Mashujaa Mmerejea tunawapokea kwa Shangwe na
HATUNA CHA KUWAPA, CHA KUWAPA NI ASANTE

Nakumbuka yule kijana aliyesimama na kumuuliza Mwalimu akitaka kujua kama tulienda kupigana Msumbiji kama Askari wa Kukodiwa na kama ni Askari wa kukodiwa tulipaswa kulipwa au tulienda kupigana Msumbiji kama ni Sehemu ya Tanzania, basi Tuonyeshwe mipaka ya Tanzania!

Huo ndio ulikuwa mwisho wa kumwona yule kijana mpaka leo na Wanajeshi wengine wakafyata japokuwa hakuwa amepanga peke yake kuuliza maswali yale!

yameandikwa wapi maneno hayo?
 
Bwana mzee hizi ulizoandika ni porojo za kilabuni.
Pengine umehadithiwa habari nusu nusu tu juu ya uwezo wa jeshi letu na kazi kubwa iliyofanya wakati ule.
Kwanza kabisa maneno aliyosema Mwalimu kuwa"HATUNA CHA KUWAPA, CHA KUWAPA NI ASANTE", yalisemwa Kaboya., kambi ya Jeshi kwa Askari waliokuwa wanarudi kishujaa toka Uganda nafikiri 1979/80, na si Lugalo.
Naamini uliyepost hulijui kabisa Jeshi letu na unahadithia mambo uliyodanganywa.
 
quote_icon.png
Originally Posted by Amiliki

Si hayo yameandikwa hapo? Ama kweli wewe Bujibuji. Mwandishi alikuweko kwenye tukio, si kasema "tulikusanyika", "Nyerere kaja kutupongeza", "nakumbuka yule kijana"? Ujinga ni kukataa ukweli ulio dhahiri !
 
TAFUTENI NAMNA NYINGINE YA KUSHUSHA HESHIMA YA MWALIMU........Si KWA VISA VYA KUTUNGA AMBAVYO UKIULIZA SANA NI WAWILI TU WALIOSIMULIANA NDO WANAJUA........!
ZAMA ZILE ZILIKUWA ZA UKOMBOZI WA BARA LA AFRICA...TULIKWENDA KUWAKOMBOA NDUGU ZETU...YEEEEES NDUGU ZETU
 
Wewe Lole Gwakisa, jibu hoja iliyoko, siyo kumzulia aliyepost hoja isiyo yake na kujitia kuijibu. Hoja ni tulienda msumbiji kama nani na siyo uwezo wa jeshi letu. Kama mwaka 1979/80 Kaboya ailtumia maneneo yaliyosemwa na Nyerere mwaka wa 1975 ni nini cha ajabu? Si unakumbuka "zidumu fikra"? Kila mtu alikuwa anamnukuu ili mambo yasimwendee vibaya. Watu wengine bwana! Nyerere ameshafariki miaka 12 sasa lakini wakisikia jina lake tu wanatokwa na jasho jembamba. Huo siyo upendo, ni kuendeleza woga.
 
Asante Mkuu Mahesabu!
Vijana wengi wala hawajui ukombozi wa bara la Afrika ni nini!
Wala hawajui kuwa it was a privilege to serve,nafasi za jeshi zilikuwa zinagombewa na watu hawakwenda Msumbiji tu, bali Zambia,South West Africa(Namibia),Seychelles, Afrika Kusini na sehemu nyingine barani Afrika.
Maswali ati "tulienda kupigania nini" ni maswali ya mgambo wa Jiji na nina uhakika huyu Amiliki amehadithiwa na nduguye ambaye ni mgambo au korokoroni.
 
hata kama huyo kijana hajaonekana mpaka leo hiyo ndiyo zawadi aliyoitaka,huwezi kuuliza swali ambalo majibu yake tayari unayajuwa kuwa daima hautaonekana milele

lakini pia Mwl alimpoteza kijana yule ili kuendelea kudumisha mshikamano uliokuwepo kati ya wanajeshi wenyewe yawezekana huyo kijana alikuwa ni kibaraka wa watu furani

mimi naendelea kumkubali Mwl kwani alikuwa si mtu wa longolongo kama tufanyavyo sasa,watu tulikuwa tukiheshimiana tofauti na sasa,hata kama alikuwa na matatizo yake lakini huwezi kuyalinganisha na sasa
 
Wewe Lole Gwakisa, jibu hoja iliyoko, siyo kumzulia aliyepost hoja isiyo yake na kujitia kuijibu. Hoja ni tulienda msumbiji kama nani na siyo uwezo wa jeshi letu. Kama mwaka 1979/80 Kaboya ailtumia maneneo yaliyosemwa na Nyerere mwaka wa 1975 ni nini cha ajabu? Si unakumbuka "zidumu fikra"? Kila mtu alikuwa anamnukuu ili mambo yasimwendee vibaya. Watu wengine bwana! Nyerere ameshafariki miaka 12 sasa lakini wakisikia jina lake tu wanatokwa na jasho jembamba. Huo siyo upendo, ni kuendeleza woga.
Mkuu Nguchiro kwa kujibu swali lako, kwanza nina observations mbili/tatu,

Kwanza wewe kama Amiliki hajapitia walau JKTkwa jinsi maswali yenu yalivyowekwa
Pili historia ya nji hii bado hamuijui vyema hivyo ktoelewa hali ya nji hii ilkuwaje mara baada ya uhuru
Tatu ndo twende kwenye swali lenyewe.Tanganyika ilipotata uhuru ilikuwa imezungukwa na nchi ambazo zote zilikuwa chini ya utawala wa aidha kikoloni au Waarabu kwa kule Zanzibar.
Malawi -walikuwepo Waingereza
Zambia-Walikuwepo Waingereza
Uganda-Waingereza
Kenya -Waingereza
Mozambique-Wareno
Congo -Wabelgiji
Katika nchi zote hizo , ingallau Waingereza walikuwa wastaarabu na Mtangayika aliweza kuongea naye na akaeleweka.
Mozambique wareno walikuwa wanaua wamakonde(ambao ni ndugu zetu) kama mchezo
Zanzibar-hiyo historia ya utwana na ubwana unaijua vizuri zaid
Kimbilio la mtu mweusi kwa sehemu yote ya kusini mwa Afrika ilikuwa Tanganyika na ndio maana utakuta hata Mandela alihifadhiwa hapa kwetu kabla ya kufungwa kwa miaka 27.
Wengi hawajui kwamba hata CHE GUEVARA alipita mitaa hii ya Dar es salaam kuelekea Congo, kuonyesha jinsi Tanzania ilivyokuwa inaheshika katika masuala ya ukombozi.
Sisemi juu ya watu kama Kaunda,Samora Machel,Mugabe na Nkomo,Zuma na wengine wengi, wote walihifadhiwa sana hapa kwetu.
Wengine mtaona huu ulikuwa upuuzi, lakini hamjui kwamba miaka ya 1966-1970, wareno walipiga sana mikoa ya Mtwara,Lindi na hata Ruvuma kwa mabomu na ndege.
Sasa how do you defend your self, by hiding?
No!
Go after the enemy, na ndicho Mwalimu alichokifanya, Mreno alifuatwa huko huko na kwa kushirikiana na chama cha ukombozi FRELIMO akadundwa huko huko.
Hili ni somo lililotumika vyema vile vile kwa Nduli Idi Amin, alipotuvamia hatumuaga pale Kyaka, akadundwa mpaka mpakani mwa Sudan ili asirudie tena.
Sasa huyo mnayesema alikuliza alienda kufanya nini nafikiri hakuwahi kuwepo mtu kama huyo.
 
Kumbuka kuna watu ambao walikufa kule na wengine ni Vilema mpaka leo. Kama Wazee wa East African Community wanavyoteseka kwa faida ya watu wengine na ndivyo ilivyokuwa kumjengea sifa nyerere kwa damu ya watu wengine.

Dunia nzima inajulikana kwamba unapokwenda kupigana nje ya mipaka ya nchi yako wewe ni kibaraka, na unapaswa kulipwa kama kibaraka yeyote yule ndio maana hata Askari wanaokwenda katika majeshi ya kulinda amani hulipwa handsomely.

Kumbuka hawa pia wana watu nyuma yao wanowategemea.
 
Tanzania ilihusika kwa vita vya ukombozi africa.

Ngoja nijimegee kidogo:mimi nilihusika kupeleka silaha kama mchezaji wa timu ya taifa!
 
Kumbuka kuna watu ambao walikufa kule na wengine ni Vilema mpaka leo. Kama Wazee wa East African Community wanavyoteseka kwa faida ya watu wengine na ndivyo ilivyokuwa kumjengea sifa nyerere kwa damu ya watu wengine.

Dunia nzima inajulikana kwamba unapokwenda kupigana nje ya mipaka ya nchi yako wewe ni kibaraka, na unapaswa kulipwa kama kibaraka yeyote yule ndio maana hata Askari wanaokwenda katika majeshi ya kulinda amani hulipwa handsomely.

Kumbuka hawa pia wana watu nyuma yao wanowategemea.
Hapa ndio nasema tunaongea na mtu ambaye mentality ya Utaifa na kujitoa mhanga kwa nchi haina nafasi kwake.
Hebu tueleze mkuu Amiliki,Chief Mkwawa, Songea, Meli na Sina walilipwa kivipi kutetea hadhi ya mwafrika?
 
Kumbuka kuna watu ambao walikufa kule na wengine ni Vilema mpaka leo. Kama Wazee wa East African Community wanavyoteseka kwa faida ya watu wengine na ndivyo ilivyokuwa kumjengea sifa nyerere kwa damu ya watu wengine.

Dunia nzima inajulikana kwamba unapokwenda kupigana nje ya mipaka ya nchi yako wewe ni kibaraka, na unapaswa kulipwa kama kibaraka yeyote yule ndio maana hata Askari wanaokwenda katika majeshi ya kulinda amani hulipwa handsomely.

Kumbuka hawa pia wana watu nyuma yao wanowategemea.

Unaubinafsi wa kufisha wewe, ukienda kuzima moto kwenye nyumba ya jirani ukajeruhiwa
kwa namna yoyote ile utaomba malipo? unakwenda hata misibani kuwapa pole wafiwa wewe?
Kama kuna mtu anauliza alikwenda kufanya msumbiji nini atakuwa ni mwendawazimu, kwa nini alienda
kama alikuwa hajui anaenda kufanya nini? unaweza kumlazimisha mwanajeshi kwenda vitani?
Nakubali kabisa kwamba hapa kuna mpango wa kumchafua mwalimu ambao unasukumwa na wivu
wa kijinga.

Na kama Mwalimu alikuwa na uwezo wa kuwashawishi watu waende vitani huku hawajui
wanaenda kufanya nini, na wakapigana vita na kushinda kwa kishindo then wakarudi
nyumbani na kuwaambia hakuna cha kuwapa kirahisi rahisi namna hiyo basi hakuwa
mtu wa kawaida.

Kamuambieni Jakaya akawape pole wafiwa wa Nyamongo kwa yale maneno
yake mepesi mepesi kama atakubali, subutu.
 
quote_icon.png
Originally Posted by Amiliki
Mwaka 1975 Baada ya kurudi kutoka katika Vita vilivyomwondoa Mreno Msumbiji tulikusanyika pale Lugalo Jeshini ambapo Mwalimu JK Nyerere alikuja kutupongeza kwa Ushujaa uliomwondoa Mreno .
Katika Hitimisho lake Mwalimu akasema, Mashujaa Mmerejea tunawapokea kwa Shangwe na
HATUNA CHA KUWAPA, CHA KUWAPA NI ASANTE

Nakumbuka yule kijana aliyesimama na kumuuliza Mwalimu akitaka kujua kama tulienda kupigana Msumbiji kama Askari wa Kukodiwa na kama ni Askari wa kukodiwa tulipaswa kulipwa au tulienda kupigana Msumbiji kama ni Sehemu ya Tanzania, basi Tuonyeshwe mipaka ya Tanzania!

Huo ndio ulikuwa mwisho wa kumwona yule kijana mpaka leo na Wanajeshi wengine wakafyata japokuwa hakuwa amepanga peke yake kuuliza maswali yale!

Si hayo yameandikwa hapo? Ama kweli wewe Bujibuji. Mwandishi alikuweko kwenye tukio, si kasema "tulikusanyika", "Nyerere kaja kutupongeza", "nakumbuka yule kijana"? Ujinga ni kukataa ukweli ulio dhahiri !

tatizo jana nimetoka kuangalia snema ya ldd Amin, nkadhani leo ni pati tuu.
 
Asante Mkuu Mahesabu!
Vijana wengi wala hawajui ukombozi wa bara la Afrika ni nini!
Wala hawajui kuwa it was a privilege to serve,nafasi za jeshi zilikuwa zinagombewa na watu hawakwenda Msumbiji tu, bali Zambia,South West Africa(Namibia),Seychelles, Afrika Kusini na sehemu nyingine barani Afrika.
Maswali ati "tulienda kupigania nini" ni maswali ya mgambo wa Jiji na nina uhakika huyu Amiliki amehadithiwa na nduguye ambaye ni mgambo au korokoroni.

akumbuke pia kanali mahfudh nae alikwenda msumbiji kwa hiari yake kwenda kusaidia ukombozi na alifia huko, zamani waafrika walikuwa wa na umoja zaidi kiasi kwamba mtu alijiona hayuko huru kama mwafrika mwenzake ananyanyaswa!
 
Kumbuka kuna watu ambao walikufa kule na wengine ni Vilema mpaka leo. Kama Wazee wa East African Community wanavyoteseka kwa faida ya watu wengine na ndivyo ilivyokuwa kumjengea sifa nyerere kwa damu ya watu wengine.

Dunia nzima inajulikana kwamba unapokwenda kupigana nje ya mipaka ya nchi yako wewe ni kibaraka, na unapaswa kulipwa kama kibaraka yeyote yule ndio maana hata Askari wanaokwenda katika majeshi ya kulinda amani hulipwa handsomely.

Kumbuka hawa pia wana watu nyuma yao wanowategemea.

Kama ni mjinga si lazima kuutangazia ulimwengu!
 
Amiliki,
Jinsi thread yako ulivyoiandika inaleta hisia kuwa ulikuwapo kipindi hicho cha vuguvugu la ukombozi barani Afrika na mimi kama kijana wa leo pia nimepata kusikia nyimbo ktk intaneti (Eastafricantube na Youtube) kuhusu ukombozi wa Afrika toka kwa Afro 70 band na Mbaraka Mwinshehe pia wakiimba kuelezea hisia za kipindi chenu kuhusu ukombozi wa bara la Afrika jukumu lilikuwa lenu nyinyi 'mliokuwa mnaonewa na kunyanyaswa kwa namna mbalimbali kama Waafrika, mfano Tanzania kuvamiwa na majeshi ya Kireno, Majeshi ya kibaraka Ian Smith wa Rhodesia (Zimbabwe) au Majeshi ya Kaburu John Voster.

Ila itakuwa hatulipi uzito suala hili la Ukombozi wa Afrika ikiwa tunazungumza hapa JamiiForum bila kuweka source za kile tunachoandika. Kwa Tanzania historia inatuonyesha Dar-es-Salaam ndiyo ilikuwa makao makuu ya Kamati ya Ukombozi wa Afrika - Organization Of African Union (OAU) - Liberation Commitee. Maana yake kama mdau LoLe Gwakisa alivyotabanaisha ktk mchango wake kuwa '' Tanganyika imezungukwa na nchi ambazo zote zilikuwa chini ya utawala wa aidha kikoloni au Waarabu kwa kule Zanzibar.
Malawi -walikuwepo Waingereza
Zambia-Walikuwepo Waingereza
Uganda-Waingereza
Kenya -Waingereza
Mozambique-Wareno
Congo -Wabelgiji'' mwisho wa nukuu.

Basi Tanganyika na Zanzibar a.k.a Tanzania zilipopata uhuru ziliona umuhimu wa kuzungukwa na mataifa huru ya kiafrika kulikopelekea kuanzishwa East African Community iliyo huru, SADCC n.k. Madhila ya kuzungukwa na nchi ambazo zilikuwa chini ya utawala mkongwe wa Kireno na wa Kikaburu unaelezewa fika kwa ufupi na Nelsona Mandela Foundation -
African countries have played an enormous role in the anti-apartheid struggle. Many countries suffered directly or indirectly from the apartheid regime and felt the consequences of their support to the liberation movements on their own soil. African countries and their organisations have been crucial in pressurising the UN and other international bodies in condemning apartheid and supporting the liberation struggle.
Unfortunately, we have not managed to locate archives witnessing this history and are therefore only able to describe the two organisations below Nelson Mandela Foundation – Anti-Apartheid Movement Archives.

Pia upungufu wa maandiko ya historia ya Ukombozi wa Afrika unapelekea hata watu kama kina Amiliki kupindisha kile kilichokuwapo wakati huo kuhusu vuguvugu la Ukombozi wa mwafrika na kuwa mtumishi wa serikali ambaye ni Mlinzi wa Taifa kama mwajiriwa wa jeshi anajua anapokea mshahara na pensheni kwa kazi yake iwe ndani ya mipaka ya nchi yake au nje ya nchi yake bado anadai 'zawadi kama askari wa kukodiwa. Pia hata madhumuni na nia ya Ukombozi wa mwafrika miaka hiyo ya kina AMILIKI historia yake haijawekwa sawa.

Lakini kutokana na yale maandiko machache juu ya vuguvugu la ukombozi wa Afrika, Tanzania tunaye Brigedia Hashim Mbita ambaye ni Mtanzania alipata kuwa Katibu Mtendaji ya OAU Liberation Commitee, Brigedia Jenerali Hashim Mbita tungemkaribisha aeleze historia hii muhimu ya Kamati ya Ukombozi wa Afrika ambayo ilikuwa na makao makuu yake DSM. Labda Mwanakijiji anaweza kumtafuta namna ya kufanya mahojiano naye na kuwekwa hapa JamiiForum. Maana vyombo vingine vya habari suala hilo halijapewa hata chembe ya kupata nafasi ktk kurasa zake au vituo vya TV.

Pia tuna vijana wa enzi hizo za kina Amiliki ambayo walijitolea kwenda Msumbiji kuisadia FRELIMO wakati wa likizo zao fupi kama wanafunzi wa UDSM kama Jenerali Twaha Ulimwengu na wengine wengi toka hapo UDSM wa miaka hiyo walikubali wenyewe kwenda kusaidia mapambano ya ukombozi kumpiga Mreno ndani ya Msumbiji. Pia hata wale wanamuziki wa enzi hizo za Afro 70 na Mbaraka Mwinshehe wanaweza kuhojiwa juu wa utunzi mzuri wa kuhamashisha ukombozi wa bara la Afrika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom