Amiliki,
Jinsi thread yako ulivyoiandika inaleta hisia kuwa ulikuwapo kipindi hicho cha vuguvugu la ukombozi barani Afrika na mimi kama kijana wa leo pia nimepata kusikia nyimbo ktk intaneti (
Eastafricantube na Youtube) kuhusu ukombozi wa Afrika toka kwa
Afro 70 band na Mbaraka Mwinshehe pia wakiimba kuelezea hisia za kipindi chenu kuhusu ukombozi wa bara la Afrika jukumu lilikuwa lenu nyinyi 'mliokuwa mnaonewa na kunyanyaswa kwa namna mbalimbali kama Waafrika, mfano Tanzania kuvamiwa na majeshi ya
Kireno, Majeshi ya kibaraka
Ian Smith wa Rhodesia (Zimbabwe) au Majeshi ya Kaburu John Voster.
Ila itakuwa hatulipi uzito suala hili la Ukombozi wa Afrika ikiwa tunazungumza hapa
JamiiForum bila kuweka
source za kile tunachoandika. Kwa Tanzania historia inatuonyesha Dar-es-Salaam ndiyo ilikuwa makao makuu ya
Kamati ya Ukombozi wa Afrika - Organization Of African Union (OAU) - Liberation Commitee. Maana yake kama mdau
LoLe Gwakisa alivyotabanaisha ktk mchango wake kuwa '' Tanganyika imezungukwa na nchi ambazo zote zilikuwa chini ya utawala wa aidha kikoloni au Waarabu kwa kule Zanzibar.
Malawi -walikuwepo Waingereza
Zambia-Walikuwepo Waingereza
Uganda-Waingereza
Kenya -Waingereza
Mozambique-Wareno
Congo -Wabelgiji'' mwisho wa nukuu.
Basi Tanganyika na Zanzibar a.k.a Tanzania zilipopata uhuru ziliona umuhimu wa kuzungukwa na mataifa huru ya kiafrika kulikopelekea kuanzishwa East African Community iliyo huru, SADCC n.k. Madhila ya kuzungukwa na nchi ambazo zilikuwa chini ya utawala mkongwe wa Kireno na wa Kikaburu unaelezewa fika kwa ufupi na
Nelsona Mandela Foundation -
African countries have played an enormous role in the anti-apartheid struggle. Many countries suffered directly or indirectly from the apartheid regime and felt the consequences of their support to the liberation movements on their own soil. African countries and their organisations have been crucial in pressurising the UN and other international bodies in condemning apartheid and supporting the liberation struggle.
Unfortunately, we have not managed to locate archives witnessing this history and are therefore only able to describe the two organisations below Nelson Mandela Foundation – Anti-Apartheid Movement Archives.
Pia upungufu wa maandiko ya historia ya Ukombozi wa Afrika unapelekea hata watu kama kina
Amiliki kupindisha kile kilichokuwapo wakati huo kuhusu vuguvugu la Ukombozi wa mwafrika na kuwa mtumishi wa serikali ambaye ni
Mlinzi wa Taifa kama
mwajiriwa wa jeshi anajua anapokea mshahara na pensheni kwa kazi yake iwe ndani ya mipaka ya nchi yake au nje ya nchi yake bado anadai 'zawadi kama askari wa kukodiwa. Pia hata madhumuni na nia ya Ukombozi wa mwafrika miaka hiyo ya kina
AMILIKI historia yake haijawekwa sawa.
Lakini kutokana na yale maandiko machache juu ya vuguvugu la ukombozi wa Afrika, Tanzania tunaye
Brigedia Hashim Mbita ambaye ni Mtanzania alipata kuwa
Katibu Mtendaji ya OAU Liberation Commitee,
Brigedia Jenerali Hashim Mbita tungemkaribisha aeleze historia hii muhimu ya Kamati ya Ukombozi wa Afrika ambayo ilikuwa na makao makuu yake DSM. Labda Mwanakijiji anaweza kumtafuta namna ya kufanya mahojiano naye na kuwekwa hapa
JamiiForum. Maana vyombo vingine vya habari suala hilo halijapewa hata chembe ya kupata nafasi ktk kurasa zake au vituo vya TV.
Pia tuna vijana wa enzi hizo za kina
Amiliki ambayo walijitolea kwenda Msumbiji kuisadia
FRELIMO wakati wa likizo zao fupi kama wanafunzi wa
UDSM kama
Jenerali Twaha Ulimwengu na wengine wengi toka hapo
UDSM wa miaka hiyo walikubali wenyewe kwenda kusaidia mapambano ya ukombozi kumpiga Mreno ndani ya Msumbiji. Pia hata wale wanamuziki wa enzi hizo za Afro 70 na Mbaraka Mwinshehe wanaweza kuhojiwa juu wa utunzi mzuri wa kuhamashisha ukombozi wa bara la Afrika.