Tulia na mkeo/mmeo hata kama mna matatizo

ward41

JF-Expert Member
Apr 3, 2022
397
1,394
Ukifanya tendo la ndoa na mke wako, ajabu ni kwamba hata ukitoka hapo unakuwa na Amani tena sana. Unaweza kuamua kufanya maombi kwa Amani kabisa

Tendo hilohilo la ndoa fanya na mtu mwingine asiekuwa mke wako, utaona kimbembe, utakosa Amani, unakosa ujasiri, huwezi hata kuomba, unahukumia moyoni balaa hata kama umefanya sirini. Unakosa kujiamini.

Zinaa ni dhambi mbaya sana, inatukosesha Baraka nyingi kutoka kwa Mungu. Kaa na mke/ mme wako hata kama kuna matatizo.

Uzinzi ni dhambi mbaya mno!
 
Ukifanya tendo la ndoa na mke wako, ajabu ni kwamba hata ukitoka hapo unakuwa na Amani tena sana. Unaweza kuamua kufanya maombi kwa Amani kabis...
Wewe una hofu ya Mungu, ndio maana ukifanya dhambi Roho na Nafsi vinakushitaki

Sasa nikuambie tu ukweli kuwa sio wote wenye hofu ya Mungu au hata kumfahamu Mungu

Chukulia mfano waigizaji wa Porn, Mtu analalana Wanaume au Wanawake karibu 100 huku dunia nzima ikiwashuhudia live na sura zinaonekana

Vipi Mashoga? Wasagaji?
 
maisha ni simple sana! ni simple ukiwa haujajizonganayo.

mmeshikwa kisaikolojia na hizo dini tu na mnatembea humohumo kitu usichoweza wewe kufikiri ni nje ya box!
tendo hilohilo linakupatia mtoto ndio tendo unaloliita dhambi au uzinifu!..

Ni kwa sababu umechagua hivyo ila huyohuyo unaemuamini ndoani ndio anaweza kuwa ndoano yakukulowa na dini yako imekufunganae ya kwamba huwezi kumuacha!.

nafikiri kila mtu aishi kwa uwezo wake,ila nikushauli anza kufikiri nje ya box hivyo vitabu vyenu kulikuwa na wafalme wameoa kitita cha wanawake na walikuwa ni watu wa Mungu huyohuyo unaemuamini..😀
 
Ukifanya tendo la ndoa na mke wako, ajabu ni kwamba hata ukitoka hapo unakuwa na Amani tena sana. Unaweza kuamua kufanya maombi kwa Amani kabis...
Mkuu
Zinaa ni stigma iliyozaliwa kupitia dini.

NA wahuni walioleta hiyo ishu wakabuni na labaratory killer tomatoes ili ukipita na mtu aliyeambukizwa nawe uukwae ufe.

Babu zetu walikuwa na wenza wengi ila sisi tumejifanya wa kisasa tunaishia kuibia mchangani... Oa wake wengi upunguze hiyo stigma kwenye saikolojia yako
 
Ukifuata misingi ya dini utajihukumu mwenyewe kweny nafsi ,ila hawa wazee wa demokrasia wanaona fresh tu .
 
Ukifanya tendo la ndoa na mke wako, ajabu ni kwamba hata ukitoka hapo unakuwa na Amani tena sana. Unaweza kuamua kufanya maombi kwa Amani kabisa...
utamu umekaa sehemu mbaya sana aise, na umezungukwa na vitu vya kuvutia na kuchochea ushawishike uzame kwanza dhambini halafu baadae akili ikukae sawa uanze kujutia 🐒

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Ni kwasababu umekariri hivyo....wenzio wanazini usiku asubuh wanaingia kusali fresh tu
DHAMBI ZOTE NI MBAYA
 
Back
Top Bottom