Tukutane tunaomiliki magofu kwa ajili ya kufarijiana

Kazanazo

JF-Expert Member
Aug 16, 2023
805
1,528
Wakuu habari za muda huu najua mko njema tunaendelea kupata pumzi ya bure na Mungu atubariki

Kama kawaida kuna wakati mtu unapambana na inafika hatua unatamani uwe na kwako uchomoke kwenye mambo za kupanga au tena ukahitaji kujiwekeza kwenye ujenzi kama biashara

Sasa kama ilivyo kawaida kujenga hakujawai kuwa rahisi, baada ya kupiga hesabu zangu nikaona nisimamishe kibanda cha vyumba vitatu na sebure nikiwa na uhakika na biashara yangu kuimarika kiasi kwamba kila mwezi ninaweza kusave 1ml nikaelekeza kwenye ujenzi

Doh! Najuta baada tu ya kuamsha boma upepo wa biashara ukabadirika na nisiweze kunyanyuka mwaka wa pili huu boma limekuwa gofu kila nikipiga ramani hazieleweki.

Je vipi kwako mdau nyumba yako imekamilika au umejiunga katika jumuia ya magofu tz? Unafanyaje kujiondoa katika hali hiyo?

Karibuni
 
Kila jambo na wakati wake, no need to rush
Upo sahihi mkuu lakini kwa kipato chetu wengine tukisubiri perfect time ni miaka buku ndio waweza kujenga

Assume kwa kipato cha lak5 kwa mwezi hapohapo ule uvae pamoja na bill nyingine na usave hadi zifike mill35 au 50 za kusimamisha kibanda umiza sio leo. Kwaiyo wakati mwingine unaanzisha safari ukiamini mbele waweza pata lift
 
Wakuu habari za muda huu najua mko njema tunaendelea kupata pumzi ya bure na Mungu atubariki

Kama kawaida kuna wakati mtu unapambana na inafika hatua unatamani uwe na kwako uchomoke kwenye mambo za kupanga au tena ukahitaji kujiwekeza kwenye ujenzi kama biashara

Sasa kama ilivyo kawaida kujenga hakujawai kuwa rahisi, baada ya kupiga hesabu zangu nikaona nisimamishe kibanda cha vyumba vitatu na sebure nikiwa na uhakika na biashara yangu kuimarika kiasi kwamba kila mwezi ninaweza kusave 1ml nikaelekeza kwenye ujenzi

Doh! Najuta baada tu ya kuamsha boma upepo wa biashara ukabadirika na nisiweze kunyanyuka mwaka wa pili huu boma limekuwa gofu kila nikipiga ramani hazieleweki.

Je vipi kwako mdau nyumba yako imekamilika au umejiunga katika jumuia ya magofu tz? Unafanyaje kujiondoa katika hali hiyo?

Karibuni
Kama upo Dar niuzie hilo boma boss
 
Back
Top Bottom