kutotahiri ndiyo kukosa utii kwa Mungu. Hata Abrahamu baba wa imani aliamriwa atahiri ndipo akawa bestie kindakindaki wa Mungu. Sipora, mke wa kwanza wa Musa alitahiri wanawe kwa jiwe kali-maana kipindi hicho kilikuwa kipindi cha mpito kutoka zama za mawe kwenda zama za chuma. Na alifanya hivyo kwa sababu Musa alijisahau kutotahiri wanawe kutokana na wingi wa shughuli. Mungu alitaka kuwaua, mke akashtuka akawakata magovi kwa jiwe....kuwa na govi si ufahari, ni chukizo.
Waisraeli walipofika tambarare za Moabu kabla ya kuvuka Mto Yordan kuanza kuteka Kanaani, na kabla Musa hajafa, Mungu alimwamuru Musa awatahiri wanaume wote waliozaliwa jangwani ili wasiingie nchi ya ahadi wakiwa wachafu kwa kuwa na magovi.